Katibu Kata wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Buyuni Chanika, Juma Mnambiya akikabidhi fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Udiwani kata ya buyuni kwa bi Jessica Motto, wakati wa siku maalum zilizotangazwa na mamlaka husika kuchukua fomu kwaajili yakugombea nafasi mbalimbali makabidhiani hayo yamefanyika leo katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo chanika Dar es Salaam anaeshuhudia (kulia), ni mume wa Jessica, Bw Meckson Motto.
Kada kindakindaki wa CCM Jessica Motto leo Jumanne Julai 14, akichukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kumteuwa kugombea nafasi ya Udiwani katika kata ya Buyuni Chanika Dar es Salaam.
Jessica Motto akitia saini kwenye daftari la wageni
Kada kindakindaki wa CCM Jessica Motto akionesha fomu yake mara baada yakukabidhiwa
Katibu Kata wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Buyuni Chanika, Juma Mnambiya akitoa maelekezo ya jinsi yakujaza fomu hiyo.
0 comments:
Post a Comment