A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Saturday, April 4, 2020

RC MAKONDA AWATAKA WANANCHI WASIJIFUNGIE NDANI KUSUBIRI CORONA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na wakazi wa Kinondoni alipokwenda kukagua ujenzi wa barabara inayojengwa kwa maagizo ya Rais John Pombe Magufuli.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, akikagua barabara za mitaa zilizoko mtaa wa Kariakoo karibu na Ofisi za CCM Lumumba. (Picha na Brian Peter)Na Mwandishi wetu,

Wananchi wanaingia hasara kwa kukwepa majukumu yao huku mambo yakienda tofauti wanaanza kuilalamikia serikali ili iweze kupatia msaada.

Amesema hayo leo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaaam Mh Paul Makonda wakati akikagua mradi wa TARURA katika eneo la Kinondoni shamba ambapo kumekuwa na mgogoro baina ya TARURA na wananchi wa eneo hilo.

Pia amewataka wananchi kuacha kujifanya wajuaji wakati tatizo linapokuwa kubwa kwasababu wakati watu wanaingia katika eneo la mradi ambalo hawatakiwi kuvamia.

Vilevile amewataka wananchi kufanya kazi huku wakichukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona wasikae ndani watafute hela ili wasije wakafa na njaa.

“Tokeni ndani mkafanye kazi Corona isiwe kigezo cha kujifungia ndani tumepambana na magonjwa mengi ikiwemo kipindupindu na magonjwa mengine tufanye kazi huku tukichukua tahadhari’amesema Makonda.

Aidha  Makonda amekukagua miradi ya barabara inayotekelezwa na TARURA katika wilaya ya Ilala na Kinondoni kujua maendeleo ya miradi hiyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive