Kampeni ya ufadhili wa matibabu ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto 60 kwa muda wa miezi sita iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda mevuka malengo kutoka Watoto 60 hadi kufikia watoto 90 ikiwa ni ongezeko la watoto 30 jambo linalokwenda kurejesha uhai kwa watoto hao ambao tayari wazazi wao walikuwa wamekata tamaa kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu.
RC Makonda amesema ongezeko hilo la Watoto 30 limetokana na Kampeni ya uchangishaji wa fedha iliyofanywa na Kituo cha Utangazaji cha Wasafi Media ambao wamefanikiwa kuchangisha kiasi cha Shilingi milioni 60 ambapo kati ya fedha hizo Shilingi Milioni 20 zimetolewa na msanii Diamond na nyingeni zimetolewa na wadau na wasanii mbalimbali wakiwemo Mbosso, Rayvany, Lavalava, Irine Uwoya, Queen Darling, Babutale, Jux, Star Times, DSTV na wadau wengine walioguswa na jambo hilo.
Aidha RC Makonda amemshukuru msanii Diamond kwa kujitolea 20% ya mapato yote yatakayopatikana kupitia tamasha la Wasafi Festival 2019 yatumike kugharamia matibabu ya moyo kwa Watoto waliolazwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Kwa upande wake Msanii Nasib Abdul almaarufu Kama Diamond Plutnumz amempongeza RC Makonda kwa kuwa kiongozi mwenye Moyo wa Kujali na kubeba changamoto za wananchi anaowaongoza.
0 comments:
Post a Comment