A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Monday, July 30, 2018

KCB YATOA MILIONI 420 LIGI KUU TANZANIA

 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 420  kwaajili ya udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia (kulia) ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Bi. Fatma Chillo pamoja na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi hiyo  Boniface Wambura.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario (wapili kulia)  na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Wallace Karia wakisaini Mkataba wa  makubaliano ya Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania wenye thamani ya shilingi milioni  420 zilizotolewa na benki hiyo  jijini Dar es Salaam leo. (Kushoto) ni Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi hiyo  Boniface Wambura pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Bi. Fatma Chillo.
 Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania Wallace Karia (katikati),akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  hafla ya makubaliano ya Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania wenye thamani ya shilingi milioni  420 zilizotolewa na benki hiyo  jijini Dar es Salaam leo.  (Kulia) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB  Cosmas Kimario na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi hiyo  Boniface Wambura
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB Tanzania, Cosmas Kimario (kulia),akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  hafla ya makubaliano ya Udhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania wenye thamani ya shilingi milioni  420 zilizotolewa na benki hiyo  jijini Dar es Salaam leo. (katikati) ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Wallace Karia  na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi hiyo  Boniface Wambura
Mkuu wa kitengo cha Masoko na mawasiliano wa benki ya KCB Tanzania Christina Manyenye akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Bi. Fatma Chillo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu  Tanzania Bw. Wallace Karia , wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa KCB Bank na TFF.

KCB Bank Tanzania imengia mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kudhamini Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) kwa msimu wa mwaka 2018/2019. Mkataba huo wenye thamani ya shilingi  za Kitanzania 420,000,000 ulitiwa saini leo na Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank, Nd. Cosmas Kimario na Rais wa TFF Nd. Wallace Karia katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

KCB Bank Tanzania imeongeza thamani ya udhamini wake kwenda ligi hiyo kutoka kiasi cha shilingi za Kitanzania 325,000,000 msimu wa 2017/18 mpaka shilingi 420,000,000 msimu wa 2018/19 ongezeko la ziadi ya milioni 90,000,000, ongezeko linaloashiria dhamira ya benki hiyo kutaka kunyanyua vipaji na kuendeleza ushindani katika mpira wa miguu nchini Tanzania.
Hafla ya kutia saini makubaliano hayo ilihudhuriwa pia na Kaimu Mwenyekiti wa Bodiya KCB Bank Tanzania, Bi.Fatma Chillo, Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Nd. Boniface Wambura, Wakurugenzi wa Bodi na wafanyakazi KCB Bank Tanzania, wawakilishi wa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya soka na waandishi wa habari.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank Tanzania, Nd. Cosmas Kimario alisema kwamba mchango wa kiuchumi unaoletwa na soka ni mmoja sababu  kubwa zilizopelekea KCB Bank Tanzania kutaka kudhamini ligi hiyo kwa Mwaka wa pili mfululizo. “Tunaamini kuwa sekta ya michezo ina mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa nchini kwani ni chanzo cha ajira kwa watanzania hasa vijana.” alisema Nd. Kimario.
Kaimu Menyekiti wa Bodi ya KCB Bank Tanzania, Bi.Fatma Chilloalisema kuwa ni fursa ya kipekee kuweza kudhamini Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu wa pili. “Lengo letu ni kuleta hamasa kwa timu na mashabiki wa mpira wa miguu kwa kuzijengea timu, hata zile ndogo uwezo wa kifedha ili kuziwezesha kushindana kikamilifu hivyo kuongeza ushindani ndani ya ligi.” Alieleza Bi. Chillo.

Rais wa TFF, Ndg. Wallace Karia aliishukuruKCB Bank Tanzania kwa kuidhamini Ligi kuu Tanzania jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu huu wa ligi kuu 2018/19.  Pia alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza kutoa michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.

Kuhusu Benki ya KCB

Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika Mashariki.

Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba,Buguruni, Oysterbay, Mbagala jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro.

Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki.
Share:

Friday, July 27, 2018

AZANIA BANK YAWAKUMBUKA WASTAAFU

Mkurugenzi wa Azania Bank akizungumza na vyombo vya habari kwenye uzinduzi huo.
Mstaafu Hezron Kigondo akielezea faida alizozipata kupitia mkopo wa wastaafu.
Mstaafu Hezron Kigondo pamoja na Mkurugenzi wa Azania Bank Charles Itembe wakati wa Uzinduzi wa Wastaafu Akaunti.

Katika kuendelea kusogeza huduma zake kwa wananchi zaidi na kutoa masuluhisho ya kifedha, Benki ya Azania leo imezindua huduma mbili mpya maalumu kwa ajili ya wastaafu kutoka katika mashirika mbalimbali ya kiserikali na hata ya binafsi. Huduma hizi ni Akaunti maalumu ya wastaafu (Wastaafu Akaunti) ambayo pamoja na faida nyingine za kibenki akaunti hii haitakuwa na makato yoyote na watapata ATM kadi bure huduma nyingine ambayo  Azania Bank imeiletea  kwa wastaafu ni fursa ya kupata mikopo kuweza kujikimu na kuboresha maisha yao.

Akizungumza na vyombo vya habari katika uzinduzi wa huduma hizi Mkurugenzi wa Bank ya Azania Bw. Charles Itembe alisema “Azania Bank inaendea kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha inaendelea kukuza maisha ya watanzania wote kupitia huduma mbalimbali za kifedha inazozitoa. Leo Azania Bank inazindua rasmi Mikopo ya Wastaafu na pia uzinduzi wa kampeni yetu tuliyoibatiza jina la Bega kwa Bega”

Mikopo hii ya wastaafu inalenga wastaafu wote wanaopata pensheni kupitia mifuko ya jamii ambapo kupitia mikopo ya wataafu mteja ataweza kufanya marejesho kwa miezi 72 yaani miaka 6.  Alielezea Zaidi Bw. Charles Itembe.

Mzee Haron L Kigondo ni mmoja wa wanufaika wa huduma hii mpya ya mikopo kwa wastaafu ambapo pamoja na kushuhudia yeye kuupata mkopo wake ndani ya wiki chache tu, alisema “Mikopo hii kweli inakwenda kutupa nafasi sisi Wastaafu kuweza kuendesha maisha yetu na hata kuendesha biashara wakati tukiwa bado tunaendelea kusubiri mafao yetu, Ninaishukuru sana Azania Bank kwa wazo hili kwani litakwenda kusaidia wastaafu wengi sana kuweza kuboresha maisha pamoja na biashara zao”.

Azania Bank kwa sasa ina matawi 17 ambapo ndani ya wiki 3 zijazo inategemea kuwa na matawi 19 baada ya kufungua matawi mapya Dodoma na Morogoro, pamoja na matawi haya Azania Bank inatoa huduma kupitia ATM zaidi ya 270 za Umoja Switch na hii kutoa fursa kwa mtu yoyote popote Tanzania kuweza kupata huduma za kibenki.
Share:

Thursday, July 12, 2018

MORTGAGE FIRM LISTS TSHS 120 BILLION BOND


Tanzania Mortgage Company Limited (TMRC) has listed a Tsh 120 billion bond at the Dar es Salaam Stock exchange (DSE), giving investments another avenue.

The bond will be sold in several trenches, covering a total of five years. The first trench, which was officially listed recently was sold between May 28 and june 8 and registered a subscription of 104 per cent.

"The first trench was sold between May 28 - June 8 2018. Following the awareness from the people, TMRC collected Tsh 12.4 billion, which was 4.3 per cent more than the expected amount of Tsh 12 billion," the Ag. Chief Executive Officer for Capital Markets and Securities Authority (CMSA), Nicodemas Mkama, stated.

According to Mkama, said that the amount to be collected due to this corporate bond sell will be used to provide cheap loans to people and financing other development projects so as to improve the housing industry in the country.

The newly elected TMRC Board of Directors Chairman, Theobald Sabi, said that in seven years, the mortgage firm has managed to increase its loan tenure to an average of 15 to 25 years from 5 - 10 years in 2010.

Sabi said "The number of banks offering mortgage loans has increased to 31 as of March from three in 2010 and mortgage interest has decreased to 16 and 19 per cent from 22 and 24 per cent respectively.

For his part, the Chief Executive Officer for TMRC, Oscar Philemon Mgaya, said they added merely 1.0 per cent on top of the fund sourced through the Tsh12.5 billion bond interest.

"After the Bank of Tanzania lowered treasury bond interest rates, the cost of other instruments may also follow suit and decline," Mgaya said.

The Deputy Minister for Finance and planning, Dr. Ashatu Kijaji, who was the chief guest at the event, hailed TMRC for implementing its role of improving the housing sector in Tanzania by providing loans and stock markets.

Hon. Kijaji, called on the firm to lower interest rates on mortgage loans after sourcing fund at affordable rate.
Share:

Wednesday, July 11, 2018

BENKI YA KCB YAFUNGUA TAWI JIPYA MBAGALA




Dar es Salaam, 9-Julai 2018 – Benki ya KCB Tanzania imefanya uzinduzi wa tawi lake la 14 lililopo Mbagala jijini Dar es salaam. Tawi hilo limezinduliwa rasmi na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mh. Dr. Ashatu Kijaji ambaye aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mh, Felix Lyaniva, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke- Mh. Abdallah Chaurembo, Ndugu Mbunge wa Temeke – Mh Issa Mangungu, Ndugu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke- ACP Emmanuel Lukula, Ndugu Diwani wa kata ya Mbagala- Jumanne Kambangwa, Ndugu Viongozi na maafisa mbalimbali wa Serikali, Wakurugenzi pamoja na wafanyakazi wa KCB Bank.

Katika uzinduzi huu wazungumzaji Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi.Walitoa mafanikio machache ambayo KCB imeweza kufanya kwa jamii. 

KCB Bank imewezesha miradi mikubwa ya maendeleo ya nchi yetu kutokana na rasilimali za KCB Group (strong balance sheet). Miradi hiyo ni kama Barabara ya Msata hadi Bagamoyo, Ujenzi wa Terminal Three (3) JNIA, jengo la One stop Centre TPA na Emergency Laboratory Building (Ofisi ya Raisi, Makumbusho) kwa kutaja tu michache.

Katika hotuba yake mwenyekiti alisema, “Ndugu mgeni rasmi natumaini unakumbuka vizuri mwaka 2017 uliitikia wito wa kuwa mgeni rasmi kwenye warsha ya 2jiajiri iliyokutanisha wanawake zaidi ya 1500 hapa jijini Dar es salaam. Leo nina furaha kurudisha mrejesho kuwa baada ya kutambua mahitaji ya kifedha ya wanawake wajasiriamali, KCB Banki imeshazindua “2jiajiri Women Account” amabayo inawawezesha kuweka akiba na kupata mikopo kwa masharti mepesi na rafiki. Ulitupa changagmoto nasi tukaifanyia kazi.”

Wazungumzaji walisisitizakuwa Tawi hili la Mbagala ni sehemu ya jitihada za kuweza kufikia wateja wao wengi lakini pia kutanua wigo wa huduma za kibenki. Waliendelea kwa kusisitiza kuwa Mbagala ni moja ya maeneo yenye idadi kubwa ya watu jijini Dsm vilevile kuna uwepo wa biashara ndogo, za kati na zile kubwa ambazo zinajumuishwa viwanda, usafirishaji, elimu na kadhalika. Wanaamini kuwa tawi hili litakidhi mahitaji ya kifedha kwa wateja wao wote katika eneo hilo na maeneo ya jirani.

Wazungumzaji waliwakaribishawakazi wote wa Mbagala na wakaribu kutumia huduma zao za kibenki na kufahamu zaidi faida zitokanazo na kuwa mteja wa KCB Bank ikiwemo mikopo, akaunti za akiba zenye faida lukuki, mtandao mkubwa wa ATM zaidi ya 962 Afrika mashariki.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa KCB Bank Bw. Cosmas Kimarioalisema benki hiyo inaunga mkono jitihada za serikali katika kuleta maendeleo kwa wananchi kwa kuboresha huduma zetu ili kuendana na kasi ya mabadiliko na ukuaji wa uchumi.

Vilevile Mkurugenzi Mtendaji aliendelea kusema, kipindi cha kota ya kwanza ya 2018 benki hiyo imeweza kupata faida ya shilingi Bilion 3.6/- benki imeweza kuthibiti madeni chechefu (NPL) kufikia asilimia 7% kiwango ambacho ni kizuri katika utendaji wa kibenki.

Walimaliza kwa kusisitiza kuwa KCB Bankwataendelea kuboresha huduma na kuzisogeza karibu na wateja wao kwa kupitia njia za kidigitali kama vile simu za mkononi, mtandao wa intaneti pamoja na mawakala. Wanaamini kuwa uboreshaji huu sio tu utarahisisha upatikanaji wa huduma zao bali pia utaongeza idadi ya wananchi wanaofikiwa na huduma za kifedha (financial inclusion).

Kuhusu Benki ya KCB

Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 250, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 12,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki katika Afrika Mashariki. Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda. 
KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation.


Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba ,Buguruni, Oysterbay, Pugu jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro.
Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive