Meneja wa NBC Kanda ya Mbeya, Salema Kileo, akikakabidhi funguo ya gari jipya aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ kwa mkazi wa Sumbawanga, Rukwa, Fridiana Tweve (wa pili kushoto), baada ya kuibuka mmoja wa washindi wa kampeni ya akaunti ya Malengo ya benki hiyo iliyodumu kwa muda wa miezi mitatu. Hafla ya makabidhiano ilifanyika mjini Mbeya hivi karibuni. Wengine ni wafanyakazi wa NBC.
Mshindi wa kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC wa Kanda ya Mbeya, Fridiana Tweve, akionyesha ufunguo na kadi ya gari mara baada ya kukabidhiwa na Meneja wa NBC Kanda ya Mbeya, Salema Kileo (kushoto kwake), katika hafla iliyofanyika mjini Mbeya hivi karibuni.
Mshindi wa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya Benki ya NBC, Kelvin Machage mkazi wa Tarime, akijaribu kuwasha gari lake jipya aina ya
Suzuki Carry ‘kirikuu’ muda mfupi baada ya kukabidhiwa alipoibuka
kidedea katika kampeni hiyo iliyodumu kwa mudu wa miezi mitatu.
Hafla hiyo ilifanyika mkoani Mwanza hivi karibuni.
Mshindi wa Kampeni ya Akaunti ya Malengo ya Benki ya NBC, Kelvin Machage (katikati), mkazi wa Tarime, akionyesha kadi ya gari jipya aina ya Suzuki Carry ‘kirikuu’ muda mfupi baada ya kukabidhiwa alipoibuka kidedea katika kampeni hiyo iliyodumu kwa mudu wa miezi mitatu. Hafla hiyo ilifanyika mkoani Mwanza hivi karibuni. Kushoto kwake ni Mkuu wa Idara ya Wateja wa Makampuni, Linley Kapya na Meneja wa Kampeni ya Malengo, Mtenya Cheya, wafanyakazi wa NBC na waalikwa wengine.
0 comments:
Post a Comment