A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Thursday, April 13, 2023

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAFUTURISHA WATEJA WAKE JIJINI DAR ES SALAAM

   

Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercia Bank Sabasaba Moshingi (watatu kushoto), wakiwaongoza wateja wa  pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo kupata mlo wa futari uliyoandaliwa na Tanzania Commercia Bank kwa ajili ya wateja wake  jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la millenium towerMkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercia Bank Sabasaba Moshingi (kushoto), akiongozana pamoja na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,  Sheikh Walid Alhad Omar na viongozi mbalimbali wa kidiniwa mkoa wa Dar es Salaam wakati wa hafla yakushiriki mlo wa futari uliyoandaliwa na Tanzania Commercia Bank kwa ajili ya wateja wake  jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la millenium towerMkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Commercia Bank Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa hafla yakushiriki mlo wa futari uliyoandaliwa na TCB kwa ajili ya wateja wake  jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la millenium tower

Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,  Sheikh Walid Alhad Omar akitoa neno la shukrani kwa Mkurungenzi Mtendaji waTanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, kwakujali na kuona umuhimu wa mfungo wa Ramadani na kuandaa mlo wa futari kwaajili ya wateja wake wa Dar es Salaam.hafla hiyo imefanyika makao makuu ya Benki hiyo jengo la milenium tower.Maofisa wa Tanzania Commercial Bank (TCB) pamoja na wateja wa benki hiyo wakishiriki mlo huo.

wafanya kazi wa TCB pamoja na wageni waalikwa wakiendelea kupata mlo 

Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhusiano wa Tanzania Commercial Bank TCB,  Bi Chichi Banda (kushoto), akiwa kwenye picha ya pozi na Meneja Mawasiliano na Uhusiano  wa Benki hiyo Bi Gloria Mutta wakati wa hafla yakupata mlo wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo ambapo katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally
Share:

Sunday, April 2, 2023

TANZANIA COMMERCIA BANK YATOA MSAADA WA MADAWATI MKOANI TABORA


IMG-20230402-WA0001
Mkuu wa wilaya ya Nzega Mh Naitapwaki Tukai akizungumza wakati wa hafla yakupokea msaada wa madawati 70 kwa shule ya msingi Nyasa iliyopo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora yaliyotolewa na Tanzania Commercial Bank ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Benki hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Raia Dk Samia Suluhu Hassani katika sekta ya elimu. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika shuleni hapo
IMG-20230402-WA0000
Meneja wa Tanzania Commercia Bank Tawi la Nzega Shomari Shabani, (kushoto mwenyekoti jeusi), Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bi Veronica Ng'waru kushoto kwake na Maofisa kutoka TCB pamoja na wanafunzi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Benki ya TCB kukabidhi msaada wa madawati 70 kwa shule ya msingi Nyasa iliyopo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya kampeni Benki hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Raia Dk Samia Suluhu Hassani katika sekta ya elimu. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika shuleni hapo.

Tanzania Commercia Bank imetoa msaada wa madawati 70 kwa shule ya msingi Nyasa iliyopo Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, ikiwa ni muendelezo wa mpango wa benki hiyo katika kusaidia Serikali kuboresha ubora wa elimu hapa nchini.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi madawati hayo iliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja wa benki ya TCB tawi la Nzega Bw. Shomari Shabani alisema msaada huo ni sehemu ya jitihada ambazo benki hiyo imekuwa ikifanya kusaidia jamii inayoizunguka.

Alisema kuwa benki hiyo imekuwa ikijiweka mstari wa mbele kushirikiana na serikali kufanikisha mipango mbalimbali katika kuboresha sekta ya elimu, afya hapa nchini hatua inayopelekea kuwa ndio chachu ya maendeleo kwa sekta zote ikiwemo ya benki pia.

“Mchango uliotolewa na Tanzania Commercia Bank wa kuchangia katika elimu unatokana na matumaini yetu kuwa bila kuwa na jamii iliyoelimika hata huduma za kibenki tunazozitoa zitadhoofika kutokana na ukweli kwamba biashara yetu hii inategemea sana mafanikio ya jamii inayotuzunguuka mafanikio ambayo tunaamini yataletwa na elimu,’’ alisema.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, mkuu wa Wilaya ya Nzega Mh. Naitapwaki Tukai pamoja na kuishukuru Tanzania Commercia Bank kwa msaada huo alisema msaada huo umepatikana kwa wakati muafaka kwa kuwa shule hiyo ipo kwenye mkakati wa kutafuta madawati zaidi kutokana na uhaba wa madawati unaoikabili shule hiyo.

Alisema shule hiyo sasa bado inakabiliwa na uhaba wa madawati zaidi na hivyo kutoa wito kwa taasisi na mashirika mengine kuiga mfano kwa Tanzania.
Share:

Monday, March 27, 2023

Absa Bank Tanzania bids farewell to its Managing Director during a special Iftar Gala

Outgoing Managing Director of Absa Bank Tanzania, Abdi Mohamed (left), serves Iftar dish to the Director of the Human Resources of the bank, Parick Foya, during a special iftar gala organized by the bank for its employees during the Holy Month of Ramadhan, an event that doubled as farewell platform for Abdi. The event took place in Dar es Salaam over the weekend. Third left is Absa’s Chief Internal Auditor, George Binde, and the Head of Business Banking, Melvin Saprapasen.
Outgoing Managing Director of Absa Bank Tanzania, Abdi Mohamed (centre) receives a prize from the bank’s Finance Director (CFO), Obedi Laiser, during a special Iftar party organized by the bank for its employees to spice the Holy Month of Ramadhan in Dar es Salam over the weekend. Left is the Director of Human Resources of Absa Bank Tanzania, Patrick Foya.
The outgoing Managing Director of Absa bank Tanzania, Abdi Mohamed (second left), enjoys the company of the Head of the Marketing and Corporate Relations, Aron Lubanga (left), during a special Iftar dinner organized by the bank for its workers, in Dar es Salam over the weekend.
Head of the Business Banking of Absa Bank Tanzania (Melvin Saprapasen (left), Chief Operating Officer of the bank, Oscar Mwamfwagasi, and the Director of Corporate and Investment Banking, Hugo Chilufya, serves food during a special Iftar set up by the bank for its employees and also to bid farewell to out-going Managing Director, Abdi Mohamed in Dar es Salaam over the weekend.
A cross- section of Absa Bank Tanzania employees enjoy their meal during an Iftar gala organized by the bank, in Dar es Salaam over the weekend. The function doubled as farewell arena for out-going Managing Director, Abdi Mohamed.
Some Absa Bank Tanzania workers ready to serve their meal during a special Iftar party organized by the bank in Dar es Salaam over the weekend. The function doubled as farewell venue for out-going Managing Director, Abdi Mohamed.
Share:

Wednesday, March 22, 2023

FREIGHT MANAGEMENT YAJA NA MPANGO KUBORESHA HUDUMA ZA USAFIRISHAJI NCHINI

 


Meneja Operation wa Freight Management Ltd, Dorine Gibson akifafanua jambo wakati wa semina fupi ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Kampuni hiyo mbinu za kisasa za kuboresha huduma wa usafirishaji nchini.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KAMPUNI inayotoa huduma za anga za ugavi na usafirishaji nchini, Freight Management Company Ltd (FMCL), imetangaza mpango wake mpya wa kutoa huduma bora za anga za ugavi na usafirishaji kama sehemu ya mchango wake katika kukuza uchumi wa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa FMCL Witness Panga amesema wantaka huduma za anga za ugavi na usafirishaji ziwe kwenye kiwango bora ndani ya nchi na kimataifa.

Akirejea jitihada na marekebisho yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuchochea uwekezaji wa sekta binafsi, Witness amesema kampuni yake imejipanga vizuri kusaidia mipango ya Serikali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma kwenye ugavi na usafirishaji na huduma zingine nchini Tanzania.

Alielezea huduma za ugavi na usafirishaji kama nguzo muhimu katika kuchechemua ukuaji wa biashara na uwekezaji na hivyo kukuza uchumi wa taifa na kuleta maendeleo kwa watanzania.

“Matokeo chanya katika uchumi wetu yatainua na kuboresha hali ya maisha ya Watanzania wa kawaida,” amesema na kuongeza kwamba: “Kwa vile sisi ni sehemu ya jamii hii, mchango wetu kwa maendeleo haya ni muhimu na haukwepeki.”

Amesema kampuni yake ina wabia wenye mtandao mkubwa na ulioimarika, unaoiruhusu kampuni kutoa huduma zinazoaminika na zenye gharama nafuu kwa wateja wake (wa ndani na kimataifa).

Pamoja na huduma zingine, kampuni ya FMCL inatoa huduma za anga za ugavi na usafirishaji, ambazo ni pamoja na usafirishaji wa mizigo kwa njia ya anga, usafirishaji wa kuunganisha kwa njia ya anga, kubadili meli/kuhamisha shehena na huduma za kukodisha.

“Tunatoa huduma mbalimbali za ugavi na usafirishaji baharini, ikiwa ni pamoja na usafiri wa kuunganisha kwa njia ya anga, kubadili meli/kuhamisha shehena na huduma za kukodisha, ukaguzi wa mizigo na kutoa hati ya utakaso wa ushuru,” amesema.

Kampuni inatoa pia huduma za ushauri na uchanganuzi. “Wafanyakazi wetu wana uzoefu wa kuweza kutoa suluhisho lililo bora zaidi kwa mchororo wa mahitaji ya ugavi na usafirishaji.”

Katika kufanya kazi zake, Freight Management inatoa huduma za usafirishaji wa kimataifa kwa njia ya anga na baharini kutoka huduma za usafirishaji wa kawaida hadi huduma changamani.

Kimsingi, FMCL ina uwezo wa kutoa huduma yoyote ya usafirishaji, kutoka vifurushi vidogo hadi makontena makubwa. Wafanyakazi wetu wazoefu wanajituma kuhakikisha shehena za wateja wetu zinafika muda wake, salama na ndani ya bajeti.

“Tunajivunia pia huduma ya usafirishaji wa mizigo baina ya nchi na nchi, tukitoa kwa wateja wetu fursa za uchaguzi wa njia ya kutumia, kwa viwango nafuu zaidi na kwa huduma bora.

Huduma za utaratibu wa ugavi na usafirishaji ni pamoja na utakaso wa ushuru, kufunga mizigo, kuhifadhi mizigo ghalani, usambazaji, usimamizi wa orodha/hesabu ya vitu/bidhaa na usafirishaji.
Share:

WAKAZI WA NYAMIKOMA WAISHUKURU TANZANIA COMMERCIAL BANK KWA UJENZI WA ZAHANATI

  Meneja wa Tanzania commercial Bank (TCB), Tawi la Musoma Hagai Gilbert (kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa mabati 135 yaliyotolewa na Benki hiyo kwa Diwani wa kata ya Kyanyari kijiji cha Nyamikoma wilaya ya Butiama  Mkoa wa Mara, Mkingi Itagata, kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nyamikoma wilayani humo.


Maofisa wa Tanzania Commercial Bank wakiongozwa na Meneja Benki hiyo tawi la Musoma Hagai Gilbert pamoja na uongozi wa kijiji cha Nyamikoma wakikagua ujenzi wa kituo cha Afya kinachojengwa kwa nguvu za wananchi ambapo TCB imeguswana kuchangia kwa kutoa msaada wa mabati 135 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huo


Wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Butiama wakisaidia kushusha mabati 135 yaliyotolewa na Tanzania Commercial Bank (TCB) kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi wa zahanati.



Tanzania commercial bank imekabidhi mabati 135 katika kijiji cha Nyamkoma kilichopo wilaya ya Butiama mkoani Mara kwa dhamira ya kuunga mkono juhudi za serikali katika juhudi zake za kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma ya afya.

Msaada huo ulitolewa leo katika kijiji cha Nyamkoma kilichopo wilaya ya Butihama mkoani mara na kupokelewa na Diwani wa kata ya kinyare Mh. Mkingi Itagata. 



Pamoja ya kuishukuru Benki ya TCB wakati akipokea msaada huo, Diwani wa kata ya Kinyare Mh Mkingi Itagata amesema kuwa bado kuna uhitaji ili ujamilisha ujenzi wa kituo cha afya kwani gharama ya ujenzi ni milioni 150 lakini hadi sasa kiasi walichokusanya ni milioni 47.



“Serikali pamoja na wazazi tutaongeza nguvu kwenye ujenzi  huu maana wananchi wamekuwa wakifuata huduma ya afya mbali kidogo na kijijini hapo.” Amesema Mingi


Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo, Meneja wa Benki ya TCB Tawi la Musoma Gilbert Hagai   aliwasihi wananchi wa kijiji hicho kuwa TCB itaendelea kuunga mkono juhudi za wananchi wapenda maendeleo na kuhakikisha kuwa benki hiyo inasogea huduma zake karibu.


Aidha  pia amewapongeza wazazi na uongozi wa kijiji kwa jitihada zao za kuchangia na kuanza ujenzi wa zahanati hiyo toka mwaka 2017 hii inaonesha kuwa ni kwa namna gani kumekuwa na uhitaji.


“Benki yetu ya Tanzania Commercial Bank ni mdau mkubwa wa  Maendeleo, kwa kawaida kila mwaka tunatenga fungu kutoka katika faida yetu kwa ajili ya kurudisha katika jamii na tunaipa kipaumbele kwani Kuwekeza kwenye Elimu, Afya  na maeneo mbalimbali tukiwa kama benki tunaamini vitu hivi vyote vinatusiaida kupata wateja na wafanyakazi wa benki yetu wa baadaye.


 Tutaendelea kuchangia na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassani katika kuboresha sekta ya afya kwa kadri tunavyoweza na tunaahidi kwamba huu si mwisho.” Ameongeza gilbert.

Share:

Tuesday, March 14, 2023

DCB Elimu Mpango Mzima Na Mama Samia Yazidi Kuchanja Mbuga

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge (wa pili kushoto) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Isidori Msaki kilichotolewa na Uongozi wa Shule ya Mtakuja kwa kutambua mchango wa DCB kwa maendeleo ya shule hiyo. Ilikuwa ni baada ya kupokea msaada wa madawati 30 shuleni hapo, Kunduchi, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni .Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Hanifa Suleimani Hamza na Kaimu Ofisa Elimu wa Manispaa hiyo, Msingwa Ibrahimu.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Mtakuja baada ya kuwakabidhi msaada wa madawati 30 ikiwa ni muendelezo wa kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo “Elimu Mpango Mzima na Mama Samia” jijini leo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa wakijitambulisha ambapo wakipata nafasi ya kuelezea huduma mbalimbali za kibenki zinazotolewa na benki hiyo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge akizungumza kabla ya kupokea msaada wa madawati 30 kwa ajili ya shule ya msingi Mtakuja yaliyotolewa na Benki ya Biashara ya DCB.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro akizungumza katika hafla hiyo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria makabidhiano ya msaada wa Madawati 30 kutoka Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro (katikati) kwa ajili ya Shule ya Msingi Mtakuja shuleni hapo, Kunduchi, Dar es Salaam leo. Wanaoshangilia kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Hanifa Suleimani Hamza, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Isidori Msaki, Kaimu Ofisa Elimu wa Manispaa hiyo, Msingwa Ibrahimu na Mkuu wa Shule ya Msingi Mtakuja, Anna Nyomeye.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro, akishikana mikono na wanafunzi wa Shule ya msingi Mtakuja muda mfupi baada ya kukabidhi msaada wa madawati 30 ikiwa ni muendelezo wa kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo “Elimu Mpango Mzima na Mama Samia” shuleni hapo Leo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge (kushoto), akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro huku Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Isidori Msaki (wa tatu kushoto akiangalia), katika hafla ya makabidhiano ya msaada wa madawati 30 kwa ajili ya Shule ya Msingi Mtakuja ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake inayoendelea ya ‘ Elimu Mpango Mzima na Mama Samia ’ shuleni hapo, Kunduchi, Dar es Salaam leo.
Share:

Thursday, March 9, 2023

Halmashauri ya Jiji la Dar yaishukuru Benki ya Biashara ya DCB kusaidia sekta ya elimu

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki (kulia), Diwani wa Kata ya Bonyokwa, Tumika Malilo (wa pili kushoto) na Ofisa Elimu wa jiji, Spora Tenga wakishangilia baada ya Benki ya DCB kukabidhi msaada wa madawati 30 kwa shule ya msingi Kifuru ikiwa ni sehemu ya kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo “Elimu Mpango Mzima na Mama Samia”, shuleni hapo, Kinyerezi, nje kidogo kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam leo.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (DCC) imeishukuru Benki ya Biashara ya DCB katika kusaidia uboreshaji wa elimu kwa kuchangia madawati 30 katika shule ya msingi Kifuru iliyopo Kinyerezi, Ilala nje kidogo kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa DCC Eng. Aman Mafuru amesema hayo katika hafla ya kukabidhi madawati shuleni hapo ambapo amesema tayari serikali ipo katika mchakato wa kuhakikisha shule zote za msingi zinazokabiliwa na changamoto ya madawati zinapatiwa madawati hayo.

"Tutahakikisha kwamba ushirikiano wetu na benki ya DCB Commercial Bank unasonga mbele katika kuhakikisha kuwa tunatatua changamoto nyingi za huduma za kijamii zinazoikabili manispaa na jamii kwa ujumla," alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki, alisema katika jitihada za kuisaidia Serikali ya Tanzania kuboresha sekta ya elimu nchini, benki ya Biashara ya DCB ina mpango wa kuchangia angalau madawati 1,000 katika shule mbalimbali za msingi nchini kati ya mwaka 2023/2025.

Msaki alisema madawati 30 yanayotolewa katika Shule ya Msingi Kifuru iliyopo Kinyerezi, Ilala, Dar es Salaam ni miongoni mwa madawati 150 ambayo benki hiyo itasaidia shule mbalimbali za msingi za Manispaa ya jiji hilo.

Alisema pamoja na kuboresha sekta ya elimu, madawati hayo pia yatahakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira mazuri, hivyo kusaidia kuboresha ufaulu wa wanafunzi katika shule za sekondari.

"Tunaunga mkono kampeni yetu iliyopewa jina la 'Elimu Mpango mzima na Mama Samia' inayotambua umuhimu wa elimu katika maendeleo ya taifa," alisema.

Msaki alisema kupitia Bodi ya wakurugenzi ya Benki ya DCB inayoongozwa na Bi Zawadia Nanyaro inalenga kuhakikisha kuwa wanafunzi wa shule za msingi wanakuwa na mazingira mazuri ya kujifunzia.

Alisema benki hiyo pia inaunga mkono mipango ya manispaa katika kuboresha sekta ya elimu mkoani humo na nchi nzima kwa ujumla ambapo katika hafla hiyo benki inakabidhi madawati 30 kati ya 150 yaliyopangwa kukabidhiwa kwa halmashauri za manispaa ya Dar es Salaam.

"Tunaamini serikali kupitia kwa Rais Samia Suluhu Hassan inafanya kazi kubwa kuboresha sekta ya elimu, lakini serikali pekee haiwezi kumudu gharama zote za elimu kwa wanafunzi nchini," alisema.

Alisema benki hiyo itaendelea kusaidia mipango mbalimbali ya maendeleo ya serikali katika sekta ya elimu katika shule hiyo inayokabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo majengo ya madarasa, vyoo, madawati pamoja na huduma nyingine za kijamii katika shule hiyo na nchi nzima kwa ujumla.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru ( kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki wakikata utepe kuashiria makabidhiano ya msaada wa madawati 30 kwa shule ya msingi Kifuru yaliyotolewa na DCB ikiwa ni sehemu ya kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo “Elimu Mpango Mzima na Mama Samia” jijini leo. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Elimu kata ya Bonyokwa, Sylvia Lyimo, Ofisa Elimu wa jiji, Spora Tenga, Diwani wa Kata ya Bonyokwa, Tumika Malilo na Mkuu wa Shule ya Kifuru, Wilfred Lwagaza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki akishikana mikono na wanafunzi wa shule ya msingi Kifuru baada ya kuwakabidhi msaada wa madawati 30 kama sehemu ya kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo “Elimu Mpango Mzima na Mama Samia” jijini leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 30 kwa shule ya msingi Kifuru shuleni hapo, Kinyerezi nje kidogo kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru akizungumza kabla hajapokea msaada wa madawati 30 yaliyotolewa na Benki YA DCB, shuleni hapo, Kinyerezi, Dar es Salaam leo.
Diwani wa Kata ya Bonyokwa, Tumika Malilo akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa akipiga picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Kifuru mara baada ya hafla hiyo, shuleni hapo leo. DCB ilikabidhi msaada wa madawati 30 yakipokewa na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru.
Mkuu wa Shule ya Msingi Kifuru akitoa neno la shukrani baada ya Benki ya Biashara ya DCB kukabidhi madawati 30 kwa shule yake kupitia kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo “Elimu Mpango Mzima na Mama Samia”. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Isidori Msaki, Ofisa Elimu wa jiji, Spora Tenga, Diwani wa Kata ya Bonyokwa, Tumika Malilo na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru.
Share:

Wafanyakazi wa Freight Forwarders Tanzania Ltd watoa msaada Hospitali ya Mloganzila katika kusherehekea Siku ya Wanawake duniani 2023

 


Naibu Mkurugenzi Mtendaji MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi (wa pili kushoto) akipokeza msaada wa msaada wa kabati la kuhifadhia dawa za dharula (Trolley) lenye thamani ya shilingi milioni 2 kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya Freight Forwarders Tanzania Ltd, Veronica Chilunda, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani.








KAMPUNI ya Freight Forwarders Tanzania Limited imekabidhi msaada wa kabati la kuhifadhia dawa za dharula (Trolley) kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila lenye thamani ya shilingi milioni 2  ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 8 kila mwaka.


Akikabidhi msaada huo Mwakilishi wa Kampuni ya Freight Forwarders Tanzania, Veronica Chilunda amesema kampuni imeguswa na huduma nzuri zinazotolewa Mloganzila hivyo wameona watoe msaada huo kama sehemu ya kurejesha kwa jamii.


Akipokea msaada huo Naibu Mkurugenzi Mtendaji MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji, amewashukuru watumishi wanawake wa kampuni hiyo kwa msaada  waliotoa kwani umekuja wakati muafaka wakati hospitali ikiwa katika maboresho hususani katika  maeneo ya kutolea huduma na vifaa tiba.


Aidha Bi. Veronica ametoa wito kwa watu na makampuni mbalimbali kujitokeza kusaidia mahitaji katika hospitali hiyo ambayo kwa sasa imepanua wigo wa utoaji huduma.

Share:

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAWAFIKIA WANAWAKE WENYE UHITAJI HOSPITAL YA OCEAN ROAD WAKISHEREHEKEA SIKUKUU YA WANAWAKE DUNIANI

 

Meneja Mawasiliano na Uhusiano Tanzanian Commercial bank (TCB), Gloria Mutta (watatu kulia)  akikabidhi misaada wa vitu mbalimbali kwa  Afisa Ustawi wa jamii wa Hospitali ya Ocean Road Cancer Institute (ORCI) Devotha Kibanga Kwaajili ya kusaidia wagonjwa wanawake wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya Ocean road jijini Dar es Salaam Ukiwa ni kusherehekea siku kuu ya wanawake inayofanyika kila tarehe 8 ya mwezi wa tatu kila mwaka wengine pichani ni wafanyakazi ya hospital hiyo Hafla hiyo imefanyika jana.


Katika kusherehekea sikukuu ya mwanamke duniani, Tanzania Commercial Bank (TCB) imeendelea kuwa karibu na wateja wake katika kuzingatia usawa wa kijinsia kwa maisha endelevu. 

Tanzania Commercial Bank (TCB) imetumia sikukuu hiyo kuwakumbuka na kuwatembelea wagonjwa wanawake wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya Ocen Road na kutoa misaada mbalimbali.

Akizungumza wakati alipotembelea wagonjwa hao Meneja mawasiliano na uhusiano wa Benki hiyo Bi. Gloria Mutta ameeleza kuwa "Tanzania Commercial Bank(TCB) imeendelea kuwa karibu na jamii kwa kutoa misaada mbalimbali hususani kwa wenye mahitaji maalum".

Ameeleza kuwa " Tanzania Commercial Bank (TCB) imetambua mchango wa mwanamke katika kuleta maendeleo"

Aliwahamasisha wanawake hao kuendelea kuiamini na kuitumia Benki hiyo kwani tumekuwa tukitoa misaada mbalimbali pale tunapohitajika.

mutta aliongeza kuwa benki ya TCB  inatoa huduma nchi nzima ina matawi ambayo yanafanya kazi masaa 24 yote hayo ni kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma  muda wowote.

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii Ocean Road Cancer Institute (ORCI) Devotha Kibanga ameishukuru benki hiyo na kusema kuwa imekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada kwa jamii inayotuzunguka hususani sekta ya afya

Share:

Wednesday, March 8, 2023

Benki Ya Absa Yawataka Wanawake Kujiamini

Wito umetolewa kwa wanawake wafanyakazi pamoja na wengine nchini kujiamini wenyewe na kuwa imara ili waweze kutimiza malengo yao bila kusubiri kusukumwa kwani wanawake wamepewa uwezo mkubwa ndani yao.

Wito huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Sheria na Udhibiti wa Sera na Kanuni wa Benki ya Absa Tanzania, Irene Sengati Giattas wakati wakifanya matembezi maalumu kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani akihimiza wanawake mahali pa kazi kuacha woga pale wanapopata nafasi za juu za uongozi na wasisubiri kutiwa moyo bali wao wenyewe wajitie moyo na kusonga mbele.

Akitoa mfano alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan ni mfano bora wa mwanamke mchapa kazi anayefanya mambo makubwa, wapo mawaziri wengi wanawake bora, wapo wabunge wengi wanawake na wapo pia viongozi wa taasisi mbalimbali wanawake wanaofanya vizuri katika utumishi wao.

Mmoja wa wafanyakazi wa Absa aliyeshiriki matembezi hayo, Aikande Kimaro alisema wameanza maadhimisho kwa kutembea kilomita nane wakisindikizwa na wafanyakazi wanaume kwa kuonyesha kuwa ushirikiano kutoka kwa wanaume ni muhimu katika kufanikisha majukumu yao mahali pa kazi na pia umuhimu wa mazoezi katika kuleta afya ya mwili na akili

Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio la matembezi hayo
Share:

Thursday, March 2, 2023

TANGA CEMENT NA MIAKA 20 UDHAMINI WA KILIMARATHON

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement PLC, Reinhardt Swart (kulia) akigawa maji kwa baadhi ya wakimbiaji wa kilomita 42 na 21 waliokuwa wakipita kwenye kituo cha maji na soda cha Simba Cement wakati wa mbio za Kili Marathon zilizofanyika mkoani Moshi mwishoni mwa wiki ambapo kampuni hiyo imetumia nafasi hiyo kusherehekea miaka 20 ya udhamini wa mbio hizo tokea zilipoanzishwa.

Meneja Mkuu wa Biashara wa Tanga Cement PLC, Peet Brits akigawa maji kwa baadhi ya wakimbiaji wa kilomita 42 na 21 waliokuwa wakipita kwenye kituo cha maji na soda cha Simba Cement wakati wa mbio za Kili Marathon zilizofanyika mkoani Moshi mwishoni mwa wiki ambapo kampuni hiyo imetumia nafasi hiyo kusherehekea miaka 20 ya udhamini wa mbio hizo tokea zilipoanzishwa.

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Tanga Cement PLC, Mtanga Noor (kulia), akihudumia vinywaji kwa baadhi ya wakimbiaji wa kilomita 42 na 21 waliokuwa wakipita kwenye kituo cha maji na soda cha Simba Cement wakati wa mbio za Kili Marathon zilizofanyika Moshi mwishoni mwa wiki ambapo kampuni hiyo imetumia nafasi hiyo kusherehekea miaka 20 ya udhamini wa mbio hizo tokea zilipoanzishwa.

Simba Cement imeendelea kuwa kinara wa ufadhili wa mbio za Kili Marathon kwa miaka 20 sasa huku ikielezwa kuwa mbio hizo za kimataifa zimezidi kuboreka zaidi kila mwaka.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kwa mbio hizo zilizofanyika 26 Februari 2023, katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Meneja wa Biashara wa Tanga Cement PLC, Peet Brits amesema, huu ni mwaka wa 20 wa ushiriki wao wakiwa wadhamini wakongwe na wakimbiaji kupitia timu za Simba katika mbio hizo ambazo Simba Cement na waandaaji wa Kili Marathon wamekuwa wakiziboresha hadi kufikia miaka 20 kwa mwaka 2023.

Amesema, udhamini wa mbio hizo ni kutokana na umuhimu wa michezo hasa Kili Marathoni ambayo huwakutanisha wafanyakazi wa Simba Cement na kufanya shughuli hii kwa umoja kama wanavyofanya viwandani pamoja kukutana na wadau pamoja na wateja wao.

"Katika ushiriki wetu hatukuangalia vyeo au nafasi zetu za kazi tuliona, Mkurugenzi Mtendaji akigawa maji kwa wakimbiaji, tulizungumza lugha moja kutoka langoni hadi kileleni kwa ushirikiano na wafanyakazi ambao ni wakimbiaji (Timu Simba) kwa pamoja na wakimbiaji wengine, wadau na wateja," alisema.

Pia alisema, wakati wa baada ya mbio hizo wafanyakazi ambao ni wakimbiaji wamekutana na wateja na wadau wao Kanda ya Kaskazini na kubadilishana mawazo ya uboreshaji katika huduma.

Kuhusiana na mafanikio kupitia mbio za Kili Marathon Peet amesema, wamefurahi kushirikiana katika mbio hizo zilizofanyika kwa mara ya 20 sasa na kufanya vizuri katika mbio hizo pamoja na kutoa huduma ya kugawa maji kwa wakimbiaji wa Kilometa 42 na 21 waliopita katika kituo chao cha kugawa maji.

"Tuna uhakika wakimbiaji wamefurahi kupita katika kituo chetu cha Point 8 wakati wa mbio hizi na kupata huduma, tutaendelea kushiriki katika tukio hili kila mwaka. Tunaipenda na kuithamini Kili Marathon na tunafurahi kudhamini kwa kugawa maji kwa wateja wetu na wadau wote waliopita katika 'Water Point' yetu na hawa ni kutoka katika mikoa ya Kaskazini ikiwemo Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na mikoa mingine," alieleza.

Aidha amesema, kwa mwaka huu walijipanga kufanya vyema zaidi ikilinganishwa na mwaka uliopita kwa kuongeza idadi ya wakimbiaji kwa timu Simba pamoja na kuongeza nguvu baina yao kwa kuwapa moyo wakimbiaji na kumaliza kwa ushindi.

Vilevile amesema, wamekuwa na Timu hiyo inayojumuisha wafanyakazi si kwa mashindano ya Kili Marathon pekee na kampuni ilihakikisha gharama zote ikiwemo vifaa, malazi, usafiri na burudani zinatolewa kwa kila mshiriki ili waweze kupata ushindi na kueleza kuwa wamekuwa na mashindano mbalimbali katika idara ambayo yameleta chachu kwa kampuni kudhamini timu hiyo ya Simba.

Peet amesema kwa mwaka huu, wamevunja rekodi kwa kuwa na jumla ya washiriki 28 na kupitia Kili Marathon, wamesherehekea kwa upekee mafanikio ya mwaka 2022 wakiwa washindi wa jumla wa tuzo ya Rais kwa mzalishaji bora wa mwaka na mshindi wa jumla wa tuzo ya taarifa ya fedha iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA.)
Share:

Tuesday, February 21, 2023

RC SERUKAMBA AWATAKA WARATIBU KUONGEZA BIDII UTOAJI ELIMU YA VVU

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba akizungumza na waratibu wa UKIMWI wa Wizara,Mikoa na Halmashauri wakati wa kikao cha usambazaji wa taarifa ya mapitio ya fedha za UKIMWI kwenye sekta za umma na sekta binafsi ya mwaka 2022. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa fedha na Utawala wa TACAIDS, Yasin Abasi na kushoto ni Mratibu wa UKIMWI Mkoa wa Singida, Patrick Kasango.

Na Mwandishi Wetu, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba amewaagiza waratibu wa UKIMWI nchini kuzungumza na jamii kwa uwazi kuhusu mabadiliko ya tabia katika kujikinga na maambukizi ya VVU ifikapo 2030 kuwe na Tanzania isiyokuwa na UKIMWI.

Akizungumza leo Februari 20,2023 wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa taarifa ya mapitio ya fedha za UKIMWI kwenye sekta za umma na sekta binafsi ya mwaka 2022 iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana aalisema iwapo jamii itaelewa vizuri na ikakubali kubadili tabia Tanzania itafikia malengo ya Dunia ya 2030 ya kumaliza UKIMWI.

Serukamba alisema kuwa Serikali imekua ikipambana kudhibiti maambukizi ya VVU pamoja na madhara yake kwa zaidi ya miaka thelathini, ambapo kwa kiasi kikubwa mapambano haya yanategemea fedha kwa ajili ya utekelezaji wa afua za UKIMWi,ambapo amefafanua kuwa kwa mahitaji kwa mwaka ni takribani Sh. Trilini 1.3.

Aidha, aliongeza kuwa utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI umekua ukipata fedha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali hivyo ni muhimu kufanya mapitio ya fedha zinazotumika kwenye afua hizo ili kubaini mchango wa taasisi za sekta ya umma na mchango wa taasisi za sekta binafsi ikiwa ni pamoja na kutambua Maeneo ambayo mchango huo unapelekwa kulingana na afua za VVU na UKIMWI lakini muhimu zaidi kutambua upungufu uliopo wa fedha katika kutekeleza afua za VVU na UKIMWI hapa ili Kuhakikisha utekelezaji wenye tija kwa Taifa, Jamii na mtu mmoja mmoja.

Akifafanua umuhimu wa kufanyika kwa zoezi la Mapitio ya Fedha za UKIMWI kwenye Sekta ya Umma na Binafsi (Public and Private Expenditure Review) ni kuwa zinaisaidia serikali kufahamu kiwango cha matumizi ya fedha za UKIMWI kinachopangwa na Sekta ya Umma na Binafsi.

Pia kufahamu maeneo ambayo fedha hizo zinaelekezwa, kujua kiwango cha utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI ili kubaini mchango wa sekta ya umma na binafsi katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI. Aidha, mapitio ya fedha za UKIMWI husaidia kubaini changamoto katika utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI nchini na kuweka mikakati ya kuzitatua.

Serukamba ameyataja mafanikio ya mafanikio yaliyotakana na zoezi hilo kuwa ni pamoja na kuboresha ugawaji wa rasilimali fedha za UKIMWI kulingana na afua zinazotekelezwa hapa nchini, kuimarisha mikakati ya kuhamasisha sekta binafsi na sekta za umma kupanga na kutekeleza shughuli za VVU na UKIMWI kwenye maeneo yao pamoja na kukuza mchango wa sekta ya umma na sekta binafsi katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI hapa nchini.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TACAIDS, Yasini Abasi alisema kuwa uhitaji wa fedha za UKIMWI bado ni mkubwa kwani kwa sasa wafadhili wanaendelea kupungua na hivyo kuitaka jamii kuendelea kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI ili hata pale itakapo tokea waansitisha basi Mfuko uwe na fedha za kutosha kwa ajili ya huduma za UKIMWI.

Kikao hicho kiliwashirikisha waratibu wa UKIMWI kutoka baadhi ya Wizarani,Halmashauri na Mikoa.
Waratibu wa UKIMWI kutoka Wizarani, Halmashauri na Mikoa walioshiriki Kikao cha usambazaji wa taarifa ya mapitio ya fedha za UKIMWI kwenye sekta za umma na sekta binafsi ya mwaka 2022 kilichoandaliwa na Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) wakiwa katika kikaohicho.
Mkuu wa MKoa wa Singida Peter Serukamba (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wawezeshaji wa zoezi la kukusanya taarifa za fedha za UKIMWI kwenye sekta ya umma na sekta binafsi pamoja na waratibu wa UKIMWI (aliyekaa kulia kwake) ni Mkurugenzi wa fedha na Utawala wa TACAIDS, Yasin Abasi na kushoto ni Mratibu wa wa UKIMWI MKoa wa Singida, Patrick Kasengo. Picha hii imepigwa mara baada ya uzinduzi wa kikao cha usambazaji wa taarifa ya mapitio ya fedha za UKIMWI kwenye sekta za umma na sekta binafsi ya mwaka 2022.
Mkuu wa MKoa wa Singida, Peter Serukamba ambaye alikuwa mgeni rasmi (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa UKIMWI kutoka wizarani na baadhi ya Waratibu wa Halmashauri nchini mara baada ya ufunguzi wa kikao cha uzinduzi wa kikao cha usambazaji wa taarifa ya mapitio ya fedha za UKIMWI kwenye sekta za umma na sekta binafsi ya mwaka 2022 kilichofanyika leo Februari 20,2023 mkoani Singida. Kulia kwake Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TACAIDS, Yasin Abasi na kushoto ni Mratibu wa UKIMWI Mkoa wa Singida, Patrick Kasango.
Mkuu wa MKoa wa Singida, Peter Serukamba ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa UKIMWI kutoka wizarani na baadhi ya Waratibu wa Halmashauri nchini mara baada ya ufunguzi wa kikao cha uzinduzi wa kikao cha usambazaji wa taarifa ya mapitio ya fedha za UKIMWI kwenye sekta za umma na sekta binafsi ya mwaka 2022 kilichofanyika leo Februari 20,2023 mkoani Singida. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TACAIDS, Yasin Abasi na kushoto ni Mratibu wa UKIMWI Mkoa wa Singida, Patrick Kasango.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive