A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Monday, April 19, 2021

BENKI YA EXIM YAPANIA KUNUFAISHA WATEJA WAKE HUDUMA ZA KIDIGITAL

Benki Ya Exim Yajizatiti na  'Mteja Kwanza' Utoaji Huduma Za Kidigitali.


Dar es Salaam: Aprili 18, 2021: Benki ya Exim imesisitiza kuhusu mkakati wake wa kuwekeza na kutanguliza zaidi maslahi ya wateja wake hususani katika mipango yake muhimu ikiwemo ile ya  uvumbuzi na utoaji wa huduma kwa wateja.


Akizungumza kuhusiana na mkakati huo jijini Dar es Salaam mwishoni nwa wiki, Ofisa Mtandaji Mkuu wa Benki hiyo Bw Jaffari Matundu alisisitiza kuwa benki hiyo imejizatiti kuhakikisha kwamba wateja wake wananufaika zaidi na ukuaji wa technolojia katika utoaji wa huduma za kibenki.


"Lengo ni kuhakikisha kwamba benki ya Exim tunatumia vyema huu ukuaji wa kidigitali katika utoaji wa huduma za kibenki kwa wateja wetu…lengo ni kuona wanaridhishwa na huduma zetu na wanazifurahia. Tunaamini kwamba furaha na ukuaji wao ndio biashara yetu,'' alisema.


Aliongeza kuwa agenda ya uvumbuzi imebaki kuwa kipaumbele cha benki hiyo katika kuelekea kwenye lengo lake la msingi ambalo ni kuifanya benki hiyo kuwa ya kidigitali zaidi huku kipaumbele kikibaki kuwa ni 'mteja kwanza'.


Katika kabiliana na changamoto ya COVID 19 benki hiyo mapema mwaka jana ilizindua kampeni ya "Maliza Kirahisi Kidigitali' iliyodumu katika kipindi cha mwaka mmoja ikilenga kubadilisha tabia ya wateja na kuongeza kasi ya mabadiliko yanayoendelea ya nchi kutoka katika kutumia pesa taslimu kwenda malipo ya dijiti.


"Kampeni hiyo pia inakwenda sambamba na kuunga mkono mkakati wa Serikali wa kuhamasisha matumizi ya kidigitali katika kufanya miamala uchumi pamoja na  kuhakikisha wateja wetu wanahudumiwa bila kwenda kwenye matawi" aliongezea.


Ili kurahisisha zaidi miamala na kuifanya bora zaidi na rahisi kwa wateja, benki ina chaguzi kadhaa za huduma kupitia simu na kidigitali ambazo wateja wanaweza kuzitumia kupata huduma na kufanya miamala muda wowowte katika siku saba za wiki Katika kuhakikisha kwamba huduma za benki hiyo zinakuwa jumuishi, huduma ya USSD ndio ilihusika katika kuipamba kampeni hiyo.


''Kila mwingiliano na mteja ni nafasi kwetu kuwaelewa vizuri wateja wetu na namna ya kuwahudimia kulingana na mahitaji yao. Tunapoendelea kupanua huduma zetu, tunaweza kuona jinsi kila huduma inatimiza mahitaji ya watumiaji. Ni suala la kuendelea kujifunza na uvumbuzi. ’


"Zaidi, kusikiliza kwa karibu maoni ya wateja hutusaidia kupata mrejesho unaotuwezesha kufanya maboresho na uvumbuzi ili kuimarisha huduma tunazowapatia. Lengo ni kufanya maisha yao yawe rahisi. Tunazingatia urahisi wa matumizi, na kufanya huduma zetu kuwa thabiti, salama, na haraka.'' alisema.

Share:

Sunday, April 18, 2021

NBC YAUNGA MKONO SERIKALI SEKTA YA ELIMU YATOA MSAA VIFAA VYA ELIMU KIBITI

  nbc%2B1

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Bw Gullamhussein Kifu (watatukushoto) akipokea msaada wa madawati  viti pamoja na meza 500 kwa ajili ya shule za wilaya hiyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Wateja wa wadogo wa Benki ya NBC Bw Elibariki Masuke(wa pili kulia) msaada huo ukilenga kuboresha sekta ya elimu  Wengine pichani ni Mbunge wa jimbo la Kibiti Bw Twaha Mpembenwe (kushoto),Mkurugenzi wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Bi Neema Singo (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kibiti Bw Abduljabir Marombwa hafla hiyo imefanyika hivi karibuni wilayani kibiti.nbc%2B3

Mkurugenzi wa Wateja wa wadogo wa benki ya NBC Bw Elibariki Masuke akizungumza na wajasiriamali wanawake wilayani Kibiti wakati wa mafunzo ya kibiashara na ujasiriamali kwa  wanawake wajasiriamali 150 wilayani humo ili kuwajengea uwezo wa kuemdesha biashara zao kwa ufanisi huku wakizingatia nidhamu ya fedha kabla hawajapatiwa mikopokwa ajili ya kukuza mitaji yao na benki hiyo.
NBC%2B5
M
eneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya NBC Bw Jonathan Bitababaje akitoa mafunzo kwa wajasiriamali hao.

Kibiti, Pwani:  April 17, 2021: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetoa msaada wa madawati 250, viti viti pamoja na meza 250 wilayani Kibiti mkoni Pwani ikiwa ni sehemu ya Mpango wa kipekee wa uwajibikaji wa Jamii (CSR) ambao unaplenga kuchangia utoaji wa elimu bora nchini.

 

Zaidi, benki hiyo pia imetoa mafunzo ya kibiashara na ujasiriamali kwa  wanawake wajasiriamali 150 wilayani humo ili kuwajengea uwezo wa kuemdesha biashara zao kwa ufanisi huku wakizingatia nidhamu ya fedha kabla hawajapatiwa mikopokwa ajili ya kukuza mitaji yao.

 

Madawati hayo yalikabidhiwa na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya Hiyo Bw Gullamhussein Kifu . Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mbunge wa jimbo la Kibiti Bw Twaha Mpembenwe pamoja na maafisa wengine wa wilaya hiyo akiwemo  Mkurugenzi Mtendaji.

 

Bwana Masuke alisema kuwa benki hiyo imejitolea kusaidia katika kuboresha ustawi wa jamii kupitia misaada ya kijamii ikiwemo elimu na kwamba wameguswa sana na suala la changamoto ya madawatikwenye baadhi ya maeneo hapa nchini sababu iliyosababisha wao kuchukua hatua hiyo ili kuboresha  zaidi sekta hiyomuhimu.

 

"Ni furaha kwetu kuwa sehemu ya kutatua changamoto kwenye sekta muhimu kama hii. Kupitia ushirikiano na ushawishi tunaoupata kutoka kwa Mbunge wa Kibiti na ofisi ya Mkuu wa wilaya tunaahidi kuendelea kushirikiana na jamii ya wana Kibiti huku pia tukifikiria namna kufungua tawi letu wilayani  Kibiti kufuatia fursa mbalimbali tunazoziona ikiwemo kilimo na mradi wa kituo cha kupozea umeme wa Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere,’’ alisema.

 

Alishauri pia wanafunzi na walimu watakaonufaika na msaada huo kutunza madawati na meza hizo ili viweze kutumika kwa muda mrefu na hivyo kusaidia walengwa wengi zaidi.

 

Kuhusu mafunzo kwa wajasiriamali wanawake  Bwana Masuke alisema kuwa miongoni mwa sababu zinazokwamisha utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali wengi ni pamoja na wao kuendesha biashara zao bila kuzingatia misingi ya kifedha ikiwemo kutunza kumbukumbu za mahesabu ikiwemo mapato na matumizi.

 

Kwa mujibu wa Bw Masuke ni kutokana na uwepo wa changamoto hiyo ndio sababu benki hiyo imekuwa ikishirikiana na taasisi nyingine ikiwemo TanTrade, SIDO, VETA na washauri binafsi kuelimisha wajasiriamali kuhusu namna bora ya kusimamia na kuendesha biashara zao ili kuwajengea uwezo kabla ya kuwapatia mikopo.

 

"Tumekuwa tukishirikiana na washirika wengine kutoa mafunzo kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kwenye maeneo kama usimamizi wa hesabu, utunzaji wa vitabu na uongozi, ili tuwaweke vizuri kwa ufikiaji rahisi wa mikopo", Masuke alisema.

 

Akizungumza mara tu baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Bw Gullamhussein Kifu pamoja na kuishukuru benki ya NBC kwa kutoa msaada kwa wakati haswa unaohitajika, aliiomba benki hiyo ifungue tawi lake wilayani humo mapema iwezeknavyo ili iweze kuwasaidia wakulima na wafanyabiashara husani wadogo.

 

"Msaada huu utasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa madawati katika baadhi ya shule zetu…tunashukuru sana NBC tunaomba muendelee kusaidia kwenye maeneo mengine pia ikiwemo sekta ya afya ." Alisema.

 

Akizungumzia mafunzo kwa wajasiriamali wanawake wilayani humo Bw Kifu alitoa wito kwa washiriki kuhakikisha wanayatumia vyema kwa kuwa yanalenga kuwasaidia katika upatikanaji wa mikopo sambamba na kuendesha biashara zao kwa ufanisi na kwa faida

 

“Kibiti ni wilaya  changa inayohitaji watu wake ili kuendelea. Kabla hatujapokea wawekezaji kutoka nje ni lazima tuanze sisi wenyewe humu ndani. Kupitia mafunzo haya tunakwenda kupata wajasiriamali na wafanyabaishara wenye weledi wa kutosha kutambua fursa zilizopo na kuzitumia,’’ alisema.


Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Bw Twaha Mpembenwe aliiomba benki hiyo iendelee kuwekeza zaidi wilayani humo kwa kufungua tawi lake sambamba na kuwasaidia wajasiriamali na wakulima hususani wa zao la ufuta pamoja na vijana ambao kwasasa wanakibiliwa na changamoto ya huduma za kifedhaikiwemo mikopo na elimu ya biashara na kilimo cha kisasa.

Share:

Thursday, April 15, 2021

TADB na NBC kuwawezesha maelfu ya wakulima kupata mikopo nafuu

 _E1A1886Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Elvis Ndunguru  (katikati), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutia saini mikataba kwaajili kuingia makubaliano yakufanya kazi pamoja na Benki ya Taifa ya Biashara NBC yenyelengo la  kuwawezesha maelfu ya wakulima wadogo katika minyororo ya thamani ya kilimo wengine pichani kulia ni  maofisa wa Benki ya TADB._E1A1889Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC ElvisNdunguru (kulia), akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  hafla yakuingia makubaliano  yakufanya kazi pamoja na Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB yenyelengo la  kuwawezesha maelfu ya wakulima wadogo katika minyororo ya thamani ya kilimo kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB, Derick Lugemala.

_E1A1922

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC ElvisNdunguru wapili (kushoto waliokaa) pamoja na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB, Derick Lugemala wakitia saini Mkataba wa makubaliano wa kufanya kazi pamoja kwaajili ya kuwawezesha wakulima wadogo katika minyororo ya dhamani ya kilimo wanaoshuhudia kulia ni Meneja wa Mfuko maalum wa dhamana kwa wakulima wadodo kutoka TADB  Asha Tarimo pamoja na Mkurugenzi wa sheria wa TADB Edson Rwechungura Picha na Brian Peterdownloaddownload




TADB na NBC kuwawezesha maelfu ya wakulima kupata mikopo nafuu

·         Zadhamiria kukuza mitaji na kuleta mageuzi katika kilimo, uvuvi na ufugaji

Dar es Salaam. Jumanne, 13 April, 2021. Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeingia katika makubaliano na benki ya biashara NBC kuwawezesha maelfu ya wakulima wadogo wadogo nchini kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuweza kukuza biashara zao na kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji.


Makubaliano haya, yaliyosainiwa leo katika makao makuu ya TADB jijini Dar es Salaam, yataiwezesha benki hiyo kutoa dhamana kwa wakulima watakaoenda kuomba mikopo NBC kufanya shughuli za kilimo, ufugaji pamoja na uvuvi kwa riba nafuu ya asilimia kumi na nne (14%) tu. Dhamana hii inaratibiwa na TADB chini ya mfuko maalum wa dhamana kwa wakulima wadogo nchini ‘SCGS’.  


“Kwa muda mrefu tumeona wakulima wetu nchini wakipata changamoto ya mitaji. Wengi wakilazimika kukopa kwa riba za kibiashara ambapo wengi wao wamekuwa wakipata changamoto ya kuhimili riba hizo kubwa. Hivyo, kama taasisi ya maendeleo ya kifedha, kupitia mfuko wa dhamana kwa wakulima wadogo, tumeona umuhimu wa kutoa mikopo hii nafuu kwa kushirikiana na NBC ili kuwawezesha wakulima wengi zaidi kupata mitaji,” alieleza Derick Lugemala, Mkurugenzi wa Fedha kutoka TADB.


Kwa upande wake, Elvis Ndunguru, Mkuu wa Biashara za Kibenki kutoka NBC, alisema kwamba mikopo hiyo watakayokuwa wanatoa kwa dhamana ya TADB itawawezesha kuwakopesha wakulima wadogo mikopo ya mtaji hadi kiwango cha shilingi 50 milioni kwa mkulima mmoja mmoja, shilingi 500 milioni kwa vikundi na vyama vya wakulima, na hadi shilingi 1 bilioni kwa kampuni ambazo miradi yake inawaunganisha na kuwanufaisha wakulima wadogo wengi.


Akieleza vigezo vya kupata mikopo hiyo, Ndunguru alisema:

“Ili kukidhi vigezo vya kupata mikopo hii, mkulima anahitajika kuwa amefanya biashara ya kilimo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu, awe na leseni ya biashara. Awe na kumbukumbu ya taarifa za kifedha. Mikopo hii inapatikana katika matawi yote ya arobaini na saba (47) ya NBC yaliyopo Tanzania bara na Zanzibar. Tunatoa rai kwa wakulima wote wadogo kuchangamkia fursa hii.”

 

Hapo awali, Lugemala alisema, lengo la mikopo hii yenye masharti nafuu ni kuchagiza benki za kibiashara na taasisi za kifedha kutoa mikopo zaidi kwa wakulima na kuwezesha ukuaji wa minyororo yote ya thamani yanayohusiana na kilimo, uvuvi na ufugaji nchini.


“Mpaka Desemba 2020, mfuko huu wa dhamana ulikwisha toa mikopo katika miradi ya kilimo, uvuvi na ufugaji yenye thamani ya shilingi bilioni 66 na kuwafikia wanufaikaji zaidi ya 9000 moja kwa moja na wasionufaika moja kwa moja 750,000. Baadhi ya miradi tuliyowezesha ni pamoja na kwenye korosho, mpunga, kahawa, miwa, mahindi, mihogo, pamba na ufugaji wa kuku,” alifafanua Lugemala.


Kutokana na taarifa kutoka TADB, mfuko huu wa dhamana ulianzishwa Februari 2018. Na katika kipindi cha miaka mitatu sasa, TADB imeshashirikiana na benki na taasisi za kifedha kama NMB, CRDB, Azania, Benki ya Posta (TPB), Stanbic, FINCA Microfinance, UCHUMI Commercial Bank, Tandahimba Community Bank (TACOBA), Mufindi Community Bank (MUCOBA) na NBC.


“TADB inaamini kwamba kupitia mtandao huu wa ushirikiano wa kimkakati, idadi kubwa ya wakulima wadogo watafikiwa na kuwezeshwa,” alisisitiza Lugemala.

xxxx Mwisho xxxx

Kuhusu TADB:

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ni benki ya umma yenye malengo ya kuongoza mikakati ya kujenga uwezo na mipango ya kuimarisha mnyororo wa thamani wa kilimo na kuunga mkono Serikali ya Tanzania katika kuunda na kutekeleza sera za kilimo na mikopo ya vijijini. Mpaka Desemba 2020, TADB imekwisha nufaisha wakulima 1,788,202 na kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 300 katika mikoa 26 ya Tanzania Bara na Zanzibar. Mikopo hii imewezesha kukua kwa minyororo ya thamani kwenye sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.

 

Kuhusu NBC:

Benki ya NBC ni benki pekee ya kimataifa inayopatikana katika mikoa na maeneo mbalimbali nchini ikiwa na matawi 47 na mashine za ATM zaidi ya 180, pamoja na Mawaka zaidi ya 3,000. Benki ya NBC inatoa huduma mbalimbali za ukusanyaji fedha za huduma nyingine za kibenki kwa wateja mbalimbali kwa zaidi ya miaka 54 nchini . Benki ya NBC sasa imeajiri wafanyakazi takriban 1,100 nchi nzima.

 

Kwa maelezo zaidi au msaada tupigie +255 76 898 4000/4011 | +255 22 219 3000 | +255 22 551 1000 or email us NBC_Marketingdepartment@nbc.co.tz

Kwa taarifa zaidi:

Amani Nkurlu, Meneja Mahusiano na Masoko – TADB

Barua pepe: amani.nkurlu@tadb.co.tz                                                                                                                                Simu: +255 754 878 385 au +255 712 223 839

 

David Raymond, Meneja Mwandamizi-Chapa na Mawasiliano

National Bank of Commerce Limited (NBC)

Barua pepe: david.raymond@nbc.co.tz

Simu: +255 717 742832

Share:

Monday, March 8, 2021

AKIBA COMMERCIAL BANK YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KUCHAGUA CHANGAMOTO KULETA FIKRA MPYA KWA MAENDELEO

 
Meneja wa Benki ya Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Tawi la Kijitonyama Joachim Mowo (kulia), akikata keki pamoja na wateja wake kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambapo benki hiyo iliandaa hafla fupi kwaajili ya kuwashukuru wateja wake.
Meneja wa Benki ya Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Tawi la Kijitonyama Joachim Mowo (kulia), akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya futa vicoba endelevu ambae pia ni mteja wa Benki hiyo Hanipha Tarimo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo benki hiyo iliandaa hafla fupi kwaajili ya kuwashukuru wateja wake hafla hiyo imefanyika katika ofisi za benki ya ACB Tawi la Kijitonyama leo Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Dora Siria.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Dora Siria akimlisha keki Afisa wa Benki hiyo Tawi la Kijitonyama, Amani Mwakitalima wakati wa maadhimisho wa siku ya wanawake duniani ambapo Benki hiyo iliandaa hafla fupi kwaajili ya wateja wake.
Meneja wa Benki ya Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Tawi la Kijitonyama Joachim Mowo (katikati), akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani taasisi mbalimbali zimetakiwa kuhakikisha wanatoa huduma katika hali ya usawa bila kubagua jinsia.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Akiba commercial (ACB), Dora Siria Kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Hayo yamesemwa wakati wa Benki ya ACB kuwashukuru wateja wao waliokuwa nao kwa kipindi cha muda kirefu.

Amesema, kauli mbiu ya mwaka huu ni “Choose to Challenge" yaani Chagua Changamoto zaidi kwa maana kuwa changamoto maranyingi zinaleta fikrampya, mitazamomipya na mabadiliko.

Siria amesema, wanatambua mchango wa wanawake katika kujenga jamii bora ndio maana zaidi ya asilimia 50 ya wateja wanaopata huduma kwenye benki yao ni wanawake.

"Asilimia 50 ya wateja wetu ni wanawake ambao wamewezeshwa kwa kupewa huduma mbalimbali ambazo zimewasaidia kubadilisha hali zao za maisha kwa kuwa na maisha bora," amesema Dora.

Akiba Commercial Bank kama sehemu ya jamii pia inalichukulia swala hili kwa umakini na uzito wake tunaelewa na tunatambua na kuheshimu nafasi ya Mwanamke katika jamii.

Nae Mwenyekiti wa Taasisi ya Fata Vicoba Endelevu ambae pia ni mteja wa benki hiyo Hanipha Tarimo amesema amekuwa mteja wa ACB kwa kipindi cha muda wa miaka mitano na ameweza kujiendeleza kiuchumi kwa kufanya biashara yake ya kuuza nywele origino za kike, maduka ya Nguo yaliyopo karioo mtaa wa msimbazi, na ameendesha maisha yake vizuri tokea aanze kutumia Benki hiyo.

Amesema, anawasihi wanawake wengine wasisite kuchukua kuitumia Benki ya Akiba Commercial bank kwani inasaidia kuinua wanawake kiuchumi na pia ACB wamekuwa ni moja ya taasisi wasikivu hususani pale mteja anapokua amekwama.
Share:

Benki ya NBC Yawafunda Wanawake Kuhusu Ubora wa Bidhaa na Mikopo

 PIC%2B1.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TABWA) Bi Noreen Mawala (kushoto), akikabidhi zawadi kwa niamba ya wanawake wajasiliamali nchini kwenda kwa Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi Consolatha Shayo (Kulia) na Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya hiyo Bw Jonathan Bitababaje (katikati) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa benki hiyo katika kuwasaidia na kuwawezesha wanawake wajasiliamali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika jana wakati wa kufunga Maonesho ya Wafanyabiashara wanawake Tanzania yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.PIC%2B2.Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi Consolatha Shayo akizungumza WANAWAKE WAFANYA BIASHARA  na washiriki wa maonesho hayo waliohudhulia mafunzo ya ujasiliamali yaliyodhaminiwa na benki ya NBC kwa kushirikiana na TABWA pamoja na wadau wengine ili kuwatia shime wanawake katika ujasiliamaliPIC%2B9.

Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi Consolatha Shayo (kushoto), akikabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo hayo kwa mmoja kati ya washiriki  waliohudhuria semina hiyo.


Dar es Salaam: Machi 8, 2021: Wanawake wajasiliamali na wafanyabiashara nchini wameshauriwa kuongeza jitiahada zao zaidi katika kuboresha zaidi mawazo ya biashara sambamba na kuongeza ubora za wa bidhaa zao ili kuongeza ushawishi kwa taasisi za kifedha nchini ziweze kuwakopesha kwa urahisi.


Akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya Wafanyabiashara wanawake Tanzania yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku nne, Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi Consolatha Shayo alisema taasisi za kifedha zinashawishika zaidi kutoa mikopo kwa kuzingatia ubora wa wazo la biashara na sio jina au jinsia ya mkopaji.


Alisema hiyo ndio sababu benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inaendelea kuwaongezea ujuzi wajasiliamali hao ili kuboresha mawazo na bidhaa zao ili kuwajengea uwezo utakaowezesha kufanya biashara zao kwa weledi na kutengeneza faida itayowawezesha kurejesha mikopo yao.


“Ndio maana kupitia wataalamu ambao tunawatumia kutoa elimu kwa wajasiliamali kupitia maonesho kama haya, tumekuwa tukifundisha na kusisitiza sana juu ya umuhimu wa kujenga zaidi majina ya bidhaa zao kuliko majina yao binafsi kwa kuwa taasisi za kifedha zinatazama zaidi biashara zao na sio jinsia wala majina yao binafsi,’’ alisema  Consolatha.


Pamoja na kudhamini maonesho hayo, benki hiyo pia iliandaa programu kadhaa za mafunzo kwa wajasiliamali ikiwemo kliniki ya biashara kwa kushirikisha taasisi na mamlaka mbalimbali ikiwemo Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).


Zaidi benki hiyo ilitumia fursa hiyo kutangaza huduma zake mahususi kwa ajili ya wanawake na wajasiliamali zikiwemo akaunti za NBC kua Nasi na akaunti mpya ya Johari.


“NBC Kua nasi ni akaunti maalum kabisa kwa wote wanaojihusisha na biashara ndogo ndogo kama vile mama na baba lishe, wenye maduka ya reja reja, wasindikaji wa vyakula na mazao, bodaboda, wazabuni wa taasisi mbalimbali wakati akaunti ya Johari ni mahususi kwa ajili ya wanawake na inawezesha kuweka akiba kidogo kidogo kwa kianzio cha shilingi 10,000 tu. Akaunti zote hizi hazina makato ya mwezi,’’ alisema.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TABWA) Bi Noreen Mawala ambae taasisi yake ndio iliratibu maonesho hayo pamoja na kuipongeza benki ya NBC pamoja na wadau wengine kwa kufanikisha maonesho hayo, alisema taasisi hiyo kwasasa inaandaa safari ya mafunzo na maonesho ya biashara katika nchi za Oman na Comoro ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara hao kutangaza biashara zao katika mataifa hayo.


“Baada ya mafanikio kupitia maonesho haya yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya mwanamke Duniani  tunatarajia kuwa na safari za maonesho ya biashara zetu katika nchi za Oman na Comoro ili kufungua milango zaidi ya kutangaza biashara zetu nje nchi,’’ alisema.

Share:

Saturday, March 6, 2021

BENKI YA NBC YADHAMINI MAONESHO YA WAFANYA BIASHARA WANAWAKE TANZANIA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi (Uwekezaji) Kitila Mkumbo (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa wafanya biashara wanawake yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC yenye kauli mbiu MWANAMKE MILIKI KIWANDA KWA UCHUMI ENDELEVU, maonesho yaliyozinduliwa na waziri huyo katika viwanja vya mlimani city jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho.
Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonesho ya wafanya biashara wanawake Tanzania yaliyodhaminiwa na Benki hiyo ambapo katika uzinguzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi (Uwekezaji) Kitila Mkumbo halfla ya uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya mlimani city jijini Dar es Saalam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi (Uwekezaji) Kitila Mkumbo (katikati) akipokea zawadi ya kifungashio kilichotengenezwa na wajasiliamali wakitanzania wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonesho ya wafanya bishara wanawakeTanzania yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC kutoka kwa Mkurugenzi wa Chama cha Wafanyabiashara Tanzania (Tabwa), Noreen Mawalla (kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho
Baadhi ya wanawake waliohudhulia hafla ya uzinduzi huo wakifurahia jambo kutoka kwa mgeni rasmi.
Picha ya pamoja waziri pamoja na wadhamini wa maonesho hayo.

Serikali imewataka wanawake kuchangamkia fursa zinazotolewa katika mikoa wanayoishi ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili hasa kwenye swala zima la mitaji.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubumgo wakati alipoalikwa kuwa Mgeni rasmi na kuzindua maonyesho ya biashara za wanawake Tanzania yaliyodhaminiwa na Benki ya Taifa ya bishara NBC,kwa lengo mahususi la kuwainua wanawake kiuchumi yanayofanyika Mlimani City kwa siku tatu mfurulizo.

Waziri Mkumbo amesema Serikali kwa kutambua umuhimu na mchango wa maendeleo kwa wanawake kwa Taifa, letu na Serikali inayoongozwa na jemedali wetu Rais John Pombe Magufuli wameanzisha dirisha maalumu la mikopo kwa halmashauri zote nchini kwa ajili ya kuwainua wanawake na vijana.

"Tunatambua jitihada zenu na malengo yenu lakini Serikali tunatoa wito kwa wanawake wote nchini kuchangamkia fursa zinazotolewa kupitia mikoa yao ziweze kuwasaidia kwenye changamoto zinazowakabili,” amesema Waziri Mkumbo.

Waziri huyo pia ameishukuru Benki ya Taifa ya Biashara NBC ambayo ndio mdhamini mkuu wa maonesho hayo kwa uzalendo walioufanya kutambua kuwa hakuna maendeleo bila wanawake na kulibeba hili ili wanawake waweze na vijana waweze kwenda sawa na spidi ya uchumi wa kati na kuzitaka Taasisi nyengine kuiga mfano huo kwani utaleta matokeo nyanya katika sekta ya uwekezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chama cha Wafanyabiashara Tanzania (Tabwa), Noreen Mawalla aliiomba Serikali kuwasaidia majengo ya wazi ili wanawake wafanyie biashara zao katika mazingira mazuri na salama yatakayowawezesha kulipa kodi kwa wakati.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho katika uzinduzi huo leo, amemwambia Waziri kuwa lengo kuu la udha mini wa benki hiyo kwa maoneso ya wanawake wafanya biashara tanzania ni kuwawezesha wajasiliamari wadogo na wa kati ambao ndiyo walengwa wakuu wa maonesho haya.

NBC ni Benki inayo wajali wateja wake na watanzania wote kwa ujumla hivyo ili waweze kuwa wafanyabiashara bora nilazima wapate elimu ya kifedha hivyo tunawakaribisha NBC waje wapate elimu pia kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo alisema mwinyidaho.
Share:

AKIBA COMMERCIAL BANK RECEIVES TSHS 17 BILLION IN STRATEGIC INVESTMENTS FROM THE NATIONAL BANK OF MALAWI

01
Akiba Comercial Bank's Acting Managing Director, Juliana Swai (right) speaks to reporters at a press conference in Dar es Salaam yesterday. She is flanked by the Bank's Head of Marketing & Communications, Dora Saria.

Dar es Salaam - Akiba Commercial Bank (ACB) has received Sh17 billion in strategic investments from the National Bank of Malawi (NBM) in a merger that was concluded February 2021.

Through the investment, Akiba Commercial Bank has strengthened its capital base to meet requirements of the Bank of Tanzania required for operations of commercial banks in the country.

Addressing reporters at a press conference yesterday, Akiba Comercial Bank's Acting Managing Director, Juliana Swai said the merger aimed at strengthening the bank’s capital as required by the Bank of Tanzania.

“Akiba Commercial Bank has been looking at the market demands as well as a strategic investor or shareholder in order to strengthen the bank and improve its services as well as starting more other services required in the country’s market,” she said.

She pledged major and positive changes in services delivery as well as systems of services delivery, saying customers will be serviced with the highest integrity and professionalism based on the experience from both institutions.

“We also understand the bilateral relations between the two countries in various areas including trade and creating an enabling environment for trade prosperity through easy access of financial services.

Share:

Thursday, February 4, 2021

MAENDELEO BENKI YAZINDUA KAMPENI YA UPENDO WOTE KWAKO

  
Meneja wa Huduma kwa wataja wa Maendeleo Benki, Syvia Chaula (katikati), akizungumza na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO itakayoanza siku ya leo tarehe 04/02/2021 hadi tarehe 13/02/2021 ikihamasisha wateja wote wa Maendeleo Bank kutumia huduma ya MB Mobile (*150*50#) pamoja na huduma za mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao za Maendeleo Bank. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Kampeni ya Upendo wote kwako wa Maendeleo Benki Eliupendo Mziray pamoja na Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Teknohama wa Benki hiyo George Wandwalo.
Meneja wa Huduma kwa wataja wa Maendeleo Benki, Syvia Chaula (katikati), akionesha maandishi kuashiria uzinduzi rasmi i wa Kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO itakayoanza siku ya leo tarehe 04/02/2021 hadi tarehe 13/02/2021 ikihamasisha wateja wote wa Maendeleo Bank kutumia huduma ya MB Mobile (*150*50#) pamoja na huduma za mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao za Maendeleo Bank. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Kampeni ya Upendo wote kwako wa Maendeleo Benki Eliupendo Mziray pamoja na Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Teknohama wa Benki hiyo George Wandwalo.
Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Teknohama wa Maendeleo Benki George Wandwalo (katikati), akizungumza na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO itakayoanza siku ya leo tarehe 04/02/2021 hadi tarehe 13/02/2021 ikihamasisha wateja wote wa Maendeleo Bank kutumia huduma ya MB Mobile (*150*50#) pamoja na huduma za mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao za Maendeleo Bank. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Kampeni ya Upendo wote kwako wa Maendeleo Benki Eliupendo Mziray pamoja Meneja wa Huduma kwa wataja wa Maendeleo Benki, Syvia Chaula.

Na Mwandishi Wetu | Dar es Salaam | Leo tarehe 04/02/2021 katika ukumbi wa Mikutano wa Maendeleo Bank iliyopo Posta jijini Dar es Salaam, Meneja wa huduma kwa Wateja wa Maendeleo Bank Sylvia Chaula, amezindua rasmi kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO itakayoanza siku ya leo tarehe 04/02/2021 hadi tarehe 13/02/2021 ikihamasisha wateja wote wa Maendeleo Bank kutumia huduma ya MB Mobile (*150*50#) pamoja na huduma za mitandao ya simu kuweka fedha katika akaunti zao za Maendeleo Bank.

Sylvia Chaula ameeleza kuwa kilele cha kampeni ya UPENDO WOTE KWAKO kitakuwa ni siku ya wapendanao (Valentine’s day) yaani tarehe 14/02/2021 ambapo washindi watatu watakaoshinda watapata zawadi mbalimbali kama vile Laptop, Simu Janja, Saa pamoja na kupata chakula cha usiku na Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Dr Ibrahim Mwangalaba pamoja na jopo la wafanyakazi wa Maendeleo Bank katika Hotel ya Holiday Inn iliyopo Posta.

“Washindi wote watatu wapata nafasi adhimu ya kuwaalika wapendwa wao katika chakula cha usiku, yaani kila mshindi atakuja na +plus one wake katika siku hiyo ambapo pamoja na chakula cha usiku pia kutakuwa na tukio la washindi kupokea zawadi zao kutoka Maendeleo Bank.” Aliongeza Sylvia Chaula.

“Unajua maneno matupu hayanogeshi shughuli, siku hiyo ya wapendanao sisi kama Maendeleo Bank tunapenda kutumia muda wetu kuwaonyesha wateja wetu kuwa tunawapenda, tunawajali na kuwathamii ndio mana tumechagua siku hiyo kuwaonyesha wateja wetu upendo tulio nao kwao kwa vitendo na sio maneno.” Aliongeza Mkuu wa Kitengo cha Uendeshaji wa Bank na Tehama Ndg. George Wandwalo.

Maendeleo Bank imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inatoa huduma na kuja na majawabu mbalimbali yanayoweza kuwakwamua watu kiuchumi na hivyo kutoka kwenye hali moja ya maisha na kwenda kwenye hatua nyingine.

Maendeleo Bank imekuwa ikifanya hivi kwa kuja na huduma mbalimbali kama vile Huduma za Mikopo kwa Wajasiriamali wadogo wadogo, Wafanyakazi, Taasisi, Vikundi, na huduma nyingine nyingi za kibenki.

Kwa mawasiliano zaidi;
Eliupendo Mziray,
Mratibu wa Kampeni ya Upendo Wote Kwako
Maendeleo Bank
0758698022
Share:

Sunday, January 24, 2021

KILA JAMBO JIPYA MAISHANI LINA VITA VIPYA

       
Na Mwandishi Wetu | Arusha | Wakristo kote ulimwenguni wametakiwa kujiandaa na kutambua kuwa kila jambo jipya linalotokea katika maisha ya Mtu linakuwa na vita vipya.

Wito huo umetolewa na Askofu Joseph Lai Laizer wakati akihubiri neno la Mungu lililokuwa na kichwa cha somo kisemacho “Jambo Jipya na Vita vipya” katika Kanisa la Christian Life Church Sinai Mlima wa Washindi lililopo Kiranyi Mkoani Arusha.

Askofu Laizer amesema kuwa kila jambo jipya linalotokea katika maisha ya Wakristo lazima yawe na vita vipya hivyo Wakristo wanapaswa kujiandaa kupambana na vita hivyo kwa silaha ya maombi pamoja na kumtolea Mungu sadaka.

“Lazima uombe maombi ya vita huku ukiambatanisha na sadaka, sadaka ni kitu cha muhimu sana”

“Jambo jengine katika kuvishinda vita hivi, yakupasa kumpata Kuhani atakayesema na kutoa matamshi juu ya hivyo vita vyako”

"Wakati Mfalme wa Israel alipoingia vitani na vita kuwa vikali alilikumbuka hili umuhimu wa kuwa na Kuhani katika vita vyako vipya ......Lakini Yehoshafati akasema, Je! Hapana hapa nabii wa Bwana, ili tumwulize Bwana kwa yeye? Akajibu mtumishi mmoja wa mfalme wa Israeli, akasema, Yupo hapa Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akimimina maji juu ya mikono yake Eliya..... 2Wafalme 3:11"

“Napenda kuwaasa watu wa Mungu, kuwa usifurahi sana kuwa kuna jambo jipya linakwenda kutokea kwasababu Unabii umetoka, au kwasababu Mungu amesema kupitia watumishi wake yakupasa kujiandaa na vita vipya”

“Hata mwaka kuna mambo Mungu anakwenda kufanya kwako lakini lazima ujiandae kwasababu kila jambo jipya lina vita yake” alisema Askofu.

Laiton Deo Shinze mmoja wa Waumini wa Kanisa hilo waliohudhuria Ibada hiyo alitoa maoni yake kuhusu somo hili na kusema “Kwa kweli neno la Mungu alilotufundisha leo Askofu Lai, limetufundisha kwakila jambo yatupasa tumtegemee Mungu”

Nae Bi Flomena Fredrick aliongeza kuhusu neno alilofundisha Askofu Lai “Neno la leo limenibariki sana. Mtumishi wa Mungu alikuwa anatufundisha jinsi ya kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine, yakwamba kila unapotoka hatua moja kwenda nyingine unajenga kitu kipya na kila kitu kipya huja na changamoto mpya, hivyo kuelekea hatua nyingine hupaswi kulegea, unahitajika kupambana ili kuyafikia yale mafanikio yaliyokusudiwa”

Ibada hiyo iliitimishwa kwa maombi maalumu kwaajili ya Wakristo wote Ulimwenguni. Kanisa la ‘Christian Life Church’ Sinai Mlima wa Washindi ni huduma inayopatikana katika jiji la vArusha maeneo ya Kiranyi, Sakina. Engi wanapokea na kushuhudia ukuu wa Mungu kupitia Mtumishi wake Askofu Joseph Lai Laizer.
Share:

Sunday, January 17, 2021

MWANADAMU UMEUMBWA KUSHINDA

Na Mwandishi Wetu | Arusha | Askofu wa Kanisa la ‘Christian Life Church’ Sinai Mlima wa Washindi lililopo Sakina jijini Arusha, Joseph Laizer amewaasa vijana waliohitimu katika vyuo mbalimbali nchini kuwa mwanadamu ameumbwa kushinda.
Askofu Laizer, Baba wa Washindi ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum aliyoyafanya na mwandishi wetu jijini humo.

“Vijana wengi huishia kulalama na kuiona serikali kama sio msaada kwao kisa kukosa namna ya kupata ajira mara tu ya wao kuhitimu elimu yao, huku wakisahau ile nafasi ya kupata elimu bure na ya mkopo vyuoni ni njia tosha ya kuwapelekea kwenye mafanikio wayatakayo”

“Wanadamu tumeumbwa washindi, sasa ili kufikia lengo la ushindi kuna vitu vya kufanya na sio kulalamika, na kubweteka, unahitajika kufanya mambo kwa zaidi ya vile ilivyozoeleka”

“Mchezaji bora kwenye mashindano ni Yule anayejituma na kufanya jambo la ziada ambalo litapelekea timu yake kushinda, na sio kulalama kutegemea huruma za mwamuzi wa mchezo” alisema Askofu Laizer.

“Vijana wanasahau kuwa thamani ya maisha yao yapo ndani yao wenyewe, hakuna atakayekuthamini usipojithamini wewe mwenyewe”

“Wewe ni msomi leo, hakikisha hautembei jinsi ile wengine walitembea, maana unachokifanya leo ndio matokeo ya kesho yako, ukipanda malalamiko utavuna hay ohayo malalamiko, hakikisha unafanya kile wengine hawafanyi”

“Unataka kufanya biashara sawa, hakikisha unafanya zaidi na vile wengine wanafanya hapo ndipo utakapoona ushindi, siku zote tumeumbwa kushinda, hatukuumbwa kushindwa”

“Biblia mara kadhaa inatufundisha kuwa Mkono wa mwenye bidii Utatawala, ni waase vijana na watanzania kwa ujumla, serikali imetutengenezea jukwaa tayari la mafanikio, ni sisi ndio tunatakiwa kujipanga vizuri ni namba gani tunaiweza kuicheza kiufasaha na kwa ubora huku tukiongeza bidii na ubora kwenye kile tunachokitakakukifanya” aliongeza Askofu Laizer.

Kanisa la ‘Christian Life Church’ Sinai Mlima wa Washindi ni huduma inayopatikana katika jiji la Arusha maeneo ya Sakina, wengi wanapokea na kushuhudia ukuu wa kiungu kupitia Roho wake Mtakatifu.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive