A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Monday, October 15, 2018

KAMPENI YA DCB DIGITAL YAZIDI KUPASUA ANGA

Mbunge wa Kondoa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kulia), akifurahi na Mkuu wa Masoko wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa (wa pili kushoto), Meneja wa DCB Tawi la Dodoma, Joseph Njile (kushoto) pamoja na Ofisa Mikopo wa DCB Dodoma,  Nuru Ashraf, wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa ambapo benki hiyo ikiwa kama mdau wa maendeleo ilienda kuhamasisha wananchi wa Kondoa kujiunga na huduma yao mpya ya DCB Digital ili kupata  huduma za kibenki kwa kupitia simu ya mkononi katika hafla iliyofanyika katika Kata ya Pahi, wilayani Kondoa, Dodoma juzi. Ndani ya DCB Digital mteja anaweza kujiunga na akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account), huduma ya Malipo ya Nusu Mshahara (Digital Salary advance) na huduma ya ATM bila kutumia kadi ya benki. Wa pili kulia ni mjumbe wa mkutano huo, Shamte Kapesa.
Mbunge wa Kondoa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kulia), akisalimiana na Meneja wa Benki ya Biashara ya DCB Tawi la Dodoma, Joseph Njile huku Mkuu wa Masoko wa DCB, Rahma Ngassa (wa pili kushoto) na Ofisa Mikopo wa DCB Dodoma, Nuru Ashara wakiangalia, wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa ambapo benki hiyo kama mdau wa maendeleo ilienda kuhamasisha wananchi wa Kondoa kujiunga na huduma yao mpya ya  DCB Digital ili kupata  huduma za kibenki kwa kupitia simu ya mkononi katika hafla iliyofanyika wilayani katika Kata ya Pahi, Kondoa mkoani Dodoma juzi. Ndani ya DCB Digital mteja anaweza kujiunga na akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account), huduma ya Malipo ya Nusu Mshahara (Digital Salary advance) na huduma ya ATM bila kutumia kadi ya benki. Wa pili kulia ni mjumbe wa mkutano huo, Shamte Kapesa.
Mbunge wa Kondoa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kulia), akisalimiana na Ofisa Mikopo wa Benki ya Biashara ya DCB Tawi la Dodoma, Nuru Ashraf huku Mkuu wa Masoko wa DCB, Rahma Ngassa (wa pili kushoto) na Meneja Tawi wa DCB Dodoma, Joseph Njile (kushoto) wakiangalia, wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa ambapo benki hiyo kama mdau wa maendeleo ilienda kuhamasisha wananchi wa Kondoa kujiunga na huduma yao mpya ya  DCB Digital ili kupata  huduma za kibenki kwa kupitia simu ya mkononi katika hafla iliyofanyika katika Kata ya Pahi, wilayani Kondoa, Dodoma juzi. Ndani ya DCB Digital mteja anaweza kujiunga na akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account), huduma ya Malipo ya Nusu Mshahara (Digital Salary advance) na huduma ya ATM bila kutumia kadi ya benki. Wa pili kulia ni mjumbe wa mkutano huo, Shamte Kapesa.
Mbunge wa Kondoa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kulia), akisalimiana na Mkuu wa Msoko wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa, huku Meneja Tawi wa DCB Dodoma, Joseph Njile (kushoto) na Nuru Ashraf, Ofisa Mikopo wa DCB  Dodoma  wakiangalia, wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa ambapo benki hiyo kama mdau wa maendeleo ilienda kuhamasisha wananchi wa Kondoa kujiunga na huduma yao mpya ya  DCB Digital ili kupata  huduma za kibenki kwa kupitia simu ya mkononi katika hafla iliyofanyika katika Kata ya Pahi, wilayani Kondoa, Dodoma juzi. Ndani ya DCB Digital mteja anaweza kujiunga na akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account), huduma ya Malipo ya Nusu Mshahara (Digital Salary advance) na huduma ya ATM bila kutumia kadi ya benki.
Mfanyabiashara ndogondogo mkazi wa Kata ya Pahi wilayani Kondoa, Subira Mohamed Ngwata (kulia), akifungua akaunti ya DCB Digital kwa kutumia simu yake ya mkononi huku maofisa wa benki hiyo, Vicent Speratus (kushoto) na Chuki Jarufu wakimpa maelekezo wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa ambapo benki hiyo kama mdau wa maendeleo ilienda kuhamasisha wananchi  kujiunga na huduma yao mpya ya DCB Digital ili kupata  huduma za kibenki kwa kupitia simu za mkononi katika hafla iliyofanyika Pahi, Kondoa, mkoani Dodoma juzi. Ndani ya DCB Digital mteja anaweza kujiunga na akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account), huduma ya Malipo ya Nusu Mshahara (Digital Salary advance) na huduma ya ATM bila kutumia kadi ya benki.
Meneja wa Benki ya Biashara ya DCB Tawi la Dodoma, Joseph Njile (wa pili kulia) akiwaelekeza wakazi wa Kata ya Pahi jinsi ya kujiunga na DCB Digital wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa ambapo benki hiyo kama mdau wa maendeleo ilienda kuhamasisha wananchi  kujiunga na huduma yao mpya ya  DCB Digital ili kupata huduma za kibenki kwa kupitia simu za mkononi katika hafla iliyofanyika Pahi, Kondoa, mkoani Dodoma juzi. Ndani ya DCB Digital mteja anaweza kujiunga na akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account), huduma ya Malipo ya Nusu Mshahara (Digital Salary advance) na huduma ya ATM bila kutumia kadi ya benki.
Mchuuzi wa mbogamboga na mkazi wa Kata ya Pahi wilayani Kondoa, Hadija Iddi (kulia) akipewa maelezo na Ofisa Mahusiano wa DCB Dodoma, Chuki Jarufu jinsi ya kujiunga na huduma ya DCB Digital  wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM Jimbo la Kondoa ambapo benki hiyo kama mdau wa maendeleo ilienda kuhamasisha wananchi  kujiunga na huduma yao mpya ya  DCB Digital ili kupata  huduma za kibenki kwa kupitia simu za mkononi katika hafla iliyofanyika wilayani humo mkoani Dodoma juzi. Ndani ya DCB Digital mteja anaweza kujiunga na akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account), huduma ya Malipo ya Nusu Mshahara (Digital Salary advance) na huduma ya ATM bila kutumia kadi ya benki.
Share:

Monday, October 8, 2018

TAXIFY BODA SASA YAZINDULIWA TANZANIA



Kampuni ya Taxify imezindua huduma ya Taxify Boda jijini Dar es salaam na huduma hii sasa inapatikana katika jiji la Dar es salaam na Mwanza.

Huduma  hii inawezesha watanzania kupata usafiri wa bodaboda kwa kutumia teknologia ya Taxify App inayopatikana katika simu ya kiganja kwa urahisi na bei nafuu.

Tanzania ni nchi ya tatu ambapo huduma hiii imezinduliwa.
Bw. Shivachi Muleji Meneja Mkuu Afrika Mashariki wa Taxify, alisema kuwa kampuni ilibuni huduma hii ya Taxify Boda kutokana na kuongezeko kwa uhitaji wa usafiri wa usalama na uhakika wa pikipiki.

"Tatizo la foleni Dar es salaam umechochea ukuaji wa uhitaji wa usafiri wa pikipiki katika jiji la Dar es salaam, na uhitaji wa usafiri wa usalama na uhakika ni mojawapo ya kipaumbele kwa wasafarishaji na huduma yetu inatoa suluhisho kwa changamoto hizi”* alisema
Bw. Remmy Eseka, Meneja Mkuu Tanzania alisema kuwa  huduma ya Taxify Boda imejikita katika kuhakikisha usalama wa madereva na abiria, na madereva wote ambao wamejisajili na huduma yetu wameelimishwa kuhusiana na hili.

 “Teknologia yetu inatuwezesha kufuatilia tabia ya madereva na huwezesha abiria uwezo wa kutoa maoni kuhusu huduma za dereva na safari yake kila anapotumia huduma zetu”
Kampuni imeweka mwongozo mkamilifu wa kuhakikisha usalama wa abiria. Wateja na madereva watahitajika kuvaa kofia ngumu na jaketi ya reflecta na tabia ya wateja kukaa upande ni marufuku kwa wateja na kuruhusiwa tu, kwa mteja aliye na ulemavu.

Pia, kuhakikisha usalama zaidi kwa wateja na madereva, kampuni inafutiliwa ushirkiano na makmpuni mbalimbali inayotoa huduma ya kwanza baada ya ajali na makampuni ambayo yanaweza kutoa usaidizi kwa dereva au abiria wakati wa dharura au ajali.

Kampuni imewekeza pia na mafunzo ziada ya udereva na huduma ya kwanza na kutoa vyeti kwa wote waliojisajili na huduma. “Tunatamani kupunguza pengo la ufanisi wa madereva kwa kutoa mafundisho na vyeti vya ubora,” alisema Eseka.  Pia kampuni itashirikiana na Jeshi la Polisi  kwa kutelekeza miongozo ya usalama.

Aidha Bw. Eseka alielezea kuwa huduma yao itasaidia madereva bodaboda kujiendeleza kila moja na maendeleo ya kibinafsi kutokana na mfumo wao wa biashara. "Tunataka kusaidia madereva wa pikipiki kufanya biashara zao kwa njia ya kitaaluma zaidi kwa kutoa jukwaa la kufuatilia safari, mapato na hata kupanga mipango ya maendeleo ya kibinafsi kama kujiunga na SACCO. Kwa kuwa sasa hivi madereva boda boda wanajitahidi kuanzisha makundi rasmi, Taxify Boda itatoa elimu kwa vikundi na hatimaye elimu itawasadia kuleta maendeleo kama kununua pipipiki,” alisema.
Eseka alielezea kuwa utoaji wa huduma ya teknologia inayounganisha abiria na madereva boda boda ni njia moja kampuni inachangia kuboresha muundo wa uchumi wa usafirishaji usio rasmi.
Share:

Monday, October 1, 2018

LSF yaweka mikakati ya kujenga uwezo kuboresha huduma za wasaidizi wa kisheria nchini

Msaidizi%2Bwa%2Bkisheria%252C%2BJames%2BSedame%2B%2528kushoto%2529%252C%2Bkutoka%2Bwilaya%2Bya%2BSerengeti%2Bmkoani%2BMara%252Cakitoa%2Belimu%2Bya%2Bhaki%2Bza%2Bbinadamu%2Bna%2Bupatikanaji%2Bwa%2Bhuduma%2Bza%2Bkisheria%2Bkwa%2Bwananchi
Msaidizi wa Kisheria Wilayani Serengeti, Bw. James Sedame (Kushoto) akitoa elimu kuhusu maswala ya kisheria na haki za binadamu kwa wakazi wa Wilaya hiyo. (Mpiga Picha Wetu)Msaidizi wa Kisheria Wilayani Serengeti, Bw. James Sedame (Kushoto) akitoa elimu kuhusu maswala ya kisheria na haki za binadamu kwa wakazi wa Wilaya hiyo. (Mpiga Picha wetu.

Ili kuwafikia watu wengi zaidi  wanaohitaji msaada wa kisheria hadi ngazi ya chini, Shirika la Legal Services Facility (LSF) imeweka mikakati ya kujenga uwezo na kuongeza ufanisi mashirika ya wasaidizi wa kisheria nchi nzima.
“Kujenga uwezo ni muhimu sana kama kweli tunataka vituo vya wasaidizi wa kisheria kutoa huduma kwa ufanisi,” alisema Victoria Mshana, Afisa katika Kitengo cha Kujenga Uwezo-LSF wakati wa mahojiano na gazeti hili hivi karibuni. Kimsingi, LSF—mfuko wa fedha unaofadhiliwa na mashirika ya kimataifa ya Maendeleo--DANIDA) na DFID, inatoa msaada wa fedha kwa mashirika yanayotoa mashirika makubwa ya Kisheria (Regional Mentors Organizations) yaliyoko mikoani yanayowezesha kifedha na kiufundi vituo vya msaada wa kisheria--ambao ndio wadau wakubwa katika kutoa msaada wa kisheria na huduma za wasaidizi wa kisheria hadi ngazi ya chini.
Utoaji wa huduma bora za kisheria na huduma za wasaidizi wa kisheria unategemea uimara wa vituo vya wasaidizi wa kisheria, Mshana alisema na kuongeza kwamba “kuwasaidia watu wenye matatizo ya kisheria ni jambo gumu kama hatuna vituo vya wasaidizi wa kisheria vilivyo imara.”
Baada ya kugundua ukweli swala hili, amesema Bi. Mshana, LSF, kupitia kitengo chake cha kujenga uwezo, imeandaa mpango wa mafunzo ya kujenga uwezo wa mashirika yanayotoa ushauri wa kiufundi kusaidia vituo vya wasaidizi wa kisheria, hivyo kuviwezesha kutoa huduma kitaalamu na kwa mujibu wa sheria za nchi na kanuni zake. Pamoja na mambo mengine, RMOs yanasimamia vituo vya wasaidizi wa kisheria, yakivisaidia viweze kusajiliwa na kuwa na bodi za wakurugenzi.
Kama sehemu ya mkakati wa kujenga uwezo, mashirika yote yanayofadhiliwa na LSF yamepata fursa ya kujua maswala mbalimbali ya kiufundi na ya uendeshaji, kwa mujibu wa Afisa wa LSF.
“Wasaidizi wa kisheria walipata mafunzo kuhusu masuala ya utawala bora, ambapo vituo vyote vya wasaidizi wa kisheria vipatavyo 164 vilianzisha bodi za wakurugenzi, ambazo zitasimamia huduma za wasaidizi wa kisheria. Kati ya vituo 164, vituo 150 (ambavyo ni asilimia 91) vimeanzisha bodi za wakurugenzi,” alisema Afisa huyo wa kujenga cha kujenga uwezo wa LSF.
“Kwa kweli, tunafanya haya yote ili kuhakikisha kwamba vituo vya wasaidizi wa kisheria vinawezeshwa (kiufundi, kiuendeshaji na maeneo mengine muhimu) ili yaweze kutoa msaada wa kisheria na huduma za wasaidizi wa kisheria hadi ngazi ya chini,” aliongeza Mshana.
Kituo cha Wasaidizi wa Msaada wa Kisheria Makete (MAPAO) ni miongoni mwa vituo, ambavyo vimefaidika na mpango wa kujenga uwezo wa LSF. Kituo hiki kimeweza kuanzisha bodi yake ya wakurugenzi inayosimamia na kusaidia uhamasishaji wa rasilimali na utekelezaji wa shughuli muhimu za miradi.
“Bodi ya wakurugenzi imeamua kufadhili MAPAO kwa kujitolea kuchangia na kwa kuwashirikisha wadau wengine kwa njia ya harambee, ambapo kiasi cha Sh1, 917,000 zilikusanywa, kiasi hiki ni sawa na asilimia 23.9 ya fedha zote ambazo MAPAO imepokea kutoka LSF. Haya ni mafanikio makubwa,” alisema Mkurugenzi wa MAPAO, Bw. Denis Sinene.
Ameongeza kuwa “Bodi yetu ya wakurugenzi imekuwa msaada mkubwa sana kwa kituo chetu. Utekelezaji wa miradi yetu yote/shughuli zetu unaenelea vizuri. Pamoja na hayo, tuliweza pia kuanzisha shughuli ambazo zinainufaisha jamii moja kwa moja.”
Kwa mujibu wa Sinene, fedha zilizokusanywa kutokana na harambee, zimesaidia utekelezaji wa shughuli mbalimbali, zikiwemo kutayarisha na kuchapisha vipeperishi 750 vinavyosaidia kutoa elimu ya umma ya namna ya kupata msaada wa kisheria kutoka katika ofisi za MAPAO.
“Sehemu ya fedha zilizotokana na harambee, ilisaidia Shule ya Sekondari ya Mang’oto iliyopo Wilayani Makete, ambayo iliharibiwa na moto,” alisema mkurugenzi.
Mwongozo wa bodi ya wakurugenzi, amesema Bw. Sinene, imeongeza ufanisi wa utekelezaji wa shughuli na  kusaidia kufikiwa kwa kata zilizo mbali, na kuongeza kuwa: “Kwa kweli, kwa sasa kazi zetu zinaonekana, zinapongezwa na zinahitajika zaidi na wanajamii. Harambee imefanya uwepo wa mpango endelevu na kadiri siku zinavyozidi kwenda, kwa kuwa na ujuzi na maarifa kuhusu uhamasishaji wa raslimali, MAPAO wataweza kukusanya asilimia ya 40 ya mapato yake ya mwaka.
Share:

Wednesday, September 26, 2018

TAXIFY YAZINDUA HUDUMA ZAKE JIJINI DODOMA

IMG-20180925-WA0082
Huduma ya teknologia ya teksi inayoongoza Ulaya na Afrika ya Taxify leo imezinduliwa jijini Dodoma na mamia ya madereva teksi ambao wamesajiliwa na Taxify wameanza kutoa huduma kwa wananchi.

Huduma ya Taxify mjini Dodoma itatoa njia salama na ya bei nafuu kwa abiria kupata usafarishaji na usalama wa wateja umeongezeka kwa kutumia teknolojia ya “Share your ETA“ ambayo inampatia mteja fursa ya kutaarifu familia na marafiki safari yake na kuwahakikishia usalama wake.

Menjea Mkuu Tanzania Bw. Remmy Eseka amesema: "Baada ya kuzindua huduma yetu jijini Dar es Salaam na Mwanza, tunaendelea kupanua wigo wa huduma, na mji mkuu wa Dodoma ni mojawapo ya miji ya msingi katika soko letu. Tuna imani ya kwamba watanzania watanufaika na huduma zetu.”

Taxify imetua Dodoma na ofa mbalimbali ambazo zimelengwa kunufaisha madereva ambao wamejisajili na huduma yao. 

Kampuni imetoa mikopo ya simu za kisasa za kiganjani zitakazowawezesha madereva kujiunga na tukutmia teknologia hii katika kutoa huduma kwa wateja.

Katika hili madereva wamepatiwa fursa ya kulipia kwa awamu ya mwezi kwa mwezi kutokana na faida watakayopata kwenye biashara.

Aidha kampuni imeshirikiana na kampuni ya mafuta ya Total na kutoa punguzo la bei ya mafuta na bidhaa za Total kwa madereva wote ambao watajiunga na kadi ya Total.

"Tunafurahia kuwa wa kwanza kutoa huduma ya teknologia ya texsi mjini Dodoma na kuunganisha madereva mbalimbali na huduma yetu. Tuna uhakika teknologia yetu italeta urahisi na kupunguza ucheleshewaji  wa kutoa huduma katika jijini,”* alisema Shivachi Muleji, Meneja Mkuu wa Afrika Mashariki.


Pia, kampuni imelenga kuwanufaisha madereva kwa kutoza ada ndogo ya kutumia teknologia yao kwa asilimia 15 tu,  ambayo ni zaidi ya nusu ya ada wa washindani wao nchini na kote duniani.

"Daima tunatafuta ushirikiano na fursa ambazo zitawezesha madereva kupata faida kubwa zaidi kwa kupunguza gharama za kufanya biashara. Tunaamini  kwamba  madereva watafurahia kazi yao na kutoa huduma bora kwa wasafirishaji.  Madereva tulionao wamefurahishwa na punguzo la gharama ya mafuta kwa kuwa punguzo ni la hapo papo kwenye pampu,"* alisema Remmy Eseka.

Kampuni ya taxify imeweka mipango ya kupanua wigo wa huduma katika Afrika Mashariki na inayomikakati ya kuleta huduma yao kwa madereva bajaji na pikipiki.
Share:

Thursday, September 13, 2018

TAASISI YA LEGAL SERVUCES FACILITY YAENDESHA SEMINA KWA WABUNGE JIJINI DODOMA


Meneja Mradi wa  Legal Services Facility LSF,  Ramadhan Masele (kushoto), akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba wakati wa kikao chakujadili namna watakavyoweza kushirikiana na serikali namna ya kuboresha na kurahisisha upatikanaji wa huduma na msaada wa kisheria kwa wananchi  hafla hiyo imefanyika jana  jijini Dodoma.
Meneja Mradi wa  Legal Services Facility LSF,  Ramadhan Masele, akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Wabunge Tanzania wameombwa kuunga mkono kazi za wasaidizi wa kisheria na watoa huduma za msaada wa kisheria, ambao ni nguzo muhimu katika kuwasaidia mamilioni ya Watanzania kutoka katika vitendo vya kikatili, manyanyaso na udhalimu.
“Ni kweli kwamba wasaidizi wa kisheria na watoa huduma za msaada wa kisheria wengine wamekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaoteswa na kunyayaswa, lakini hawawezi kazi hii kwa ufanisi bila kusaidiwa au kuungwa mkono na watu kama vile wabunge,” Ramadhani Masele, Meneja wa Programu wa Taasisi ya Msaada wa Kisheria (LSF) wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo ya siku mbili kwa wabunge kuhusu wasaidizi wa kisheria na watoa huduma za kisheria nchini, uliofanyika Dodoma jana.
LSF ni shirika lisilokuwa la kiserikali lilioanzishwa Mwaka 2011, linalofadhiliwa na Shirika la Kimataifa  la Maendeleo la Denmark (DANIDA) na Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DfID). LSF inatoa fedha kwa mashirika mbalimbali yanayotoa msaada wa kisheria na huduma za wasaidizi wa kisheria Tanzania Bara na Zanzibar.
Lengo kuu la semina ya wabunge, ni kuwawezesha wabunge kujua masuala mbalimbali, ikiwemo namna wasaidizi wa kisheria wanavyotoa huduma zao, idadi ya wilaya wanazofanya kazi, na aina ya kesi wanazozishughulikia, msaada wa kisheria na huduma za wasaidizi wa kisheria, kazi za LSF na ushiriki wake katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) 17 ya Umoja wa Mataifana
Semina hii ya mafunzo inakuja wakati kuna ongezeko la matukio ya uvunjaji wa haki za binadamu nchini, kama vile watu kuteswa, ukatili wa kijinsia, udhalilishaji wa kijinsia, kuwashambuliwa wanawake kwa kuwapiga, uporaji wa  ardhi na matukio mengine yanayofanana na hayo.
Kwa kupatia ufadhili kutoka LSF, wasaidizi wa kisheria na watoa msaada wa kisheria wameweza kuwasaidia wanawake, wanaume na wasichana maskini na makundi ya watu wengine wananyimwa haki zao, kupata huduma za kisheria kwa gharama nafuu au bila gharama yoyote na huduma bora za msaada wa kisheria na hivyo kupata haki zao, kwa mujibu wa meneja Mpango wa LSF.
“Lakini wasaidizi wa kisheria na watoa msaada wa kisheria wengine wangeweza kutoa huduma na kuwafikia watu wengi zaidi ambao haki zimeminywa au kuvunjwa kama wakiungwa mkono na wabunge,” aliongeza Masele, huku akisema kwamba  “wanawake na wanaume wanaoteswa, kudhalilishwa au kufanyiwa ukatili wa kijinsia, ambao haki zao za ardhi na mirathi zimevunjwa, wanaishi katika majimbo yanayoongozwa na wabunge wenyewe.”
Pamoja na mambo mengine, alisema semina ya mafunzo itawasaidia wabunge kufahamu masuala yanayohusu wasaidizi wa kisheria, jinsi wanavyofanya shughuli zao na jinsi gani wasaidizi wa kisheria wanavyoweza kushirikiana na wabunge kupanua wigo wa huduma za msaada wa kisheria.
“Lengo kuu kuwasaidia watanzania wengi wanaohitaji msaada wa kisheria na kupata haki zao zilizokiukwa. Ni muhimu kwa wabunge kuungana na wasaidizi wa kisheria kwa sababu wananchi wenye matatizo wanatoka katika majimbo yanayoongozwa na wabunge,” alisisitiza Masele.
Kwa mujibu wa maelezo ya LSF, semina hii itawawezesha wa bunge kufahamu huduma mbalimbali zitolewazo na wasaidizi wa kisheria, ambao kwa sasa wanafanya kazi katika wilaya 170 nchini, namna ya kuwasiliana nao, namna ya kupata huduma zao na kueneza taarifa za huduma zao majimboni kwao.
“Taarifa muhimu kama hizi zitarahisha kazi za wabunge na wasaidizi wa kisheria  katika kutatua matatizo/kero mbalimbali za wananchi katika majimbo yao—migogoro ya ardhi, ndoa na mimba za utotoni, mirathi, wanaume kutelekeza familia zao nk,” inasema sehemu ya taarifaya LSF.
Mada za kimkakati zilitolewa na wataalamu wa LSF kwenye semina iliyohudhuriwa na wabunge kutoka Kamati ya Kudumuya Bunge ya Katiba na Sheria na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na Maendeleo ya Jamii.
Share:

Wednesday, September 12, 2018

KWA JAMBO HILI KCB BENKI MUNGU ANAWAONA

 Mkuu wa Walaya ya Temeke, Mh Felix Lyaniva akiongoza mamia ya wakazi wa m
Mbagala pamoja na wafanya kazi wa Benki ya KCB wakati wa hafla yakuazimisha siku ya usafi, hafla hiyo imefanyika maeneo ya viwanja vya Zakhem jijini Dar es Salaam jana.                       
Wafanya kazi wa Benki ya KCB wakiwa katika picha ya pamoja na wakazi wa mbagala baada ya kukamilisha zoezi la kufanya Usafi.
02
Wafanya kazi wa Benki ya KCB wakishirikiana na wakazi wa Mbagala kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ambapo katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Walaya ya Temeke, Mh Felix Lyaniva hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam jana.

Benki ya KCB Tanzania, Jumamosi ya tarehe 8 Septemba imefanya shughuli za usafi ikishirikiana na wakazi wa Mbagala katika eneo la Mbagala Zakhem ambapo benki hiyo imefungua tawi lake la 14 nchini hivi karibuni.

Clouds Media Group, Green WastePro Limited, kampuni ya kazoa na kuchakata taka pamoja na The Creative Company, kampuni kutengeneza matangazo ndiyo walikuwa washirika wakuu wa Benki ya KCB Tanzania katika zoezi hilo liliyopokelewa kipekee na wakazi wa Mbagala ambao pia walishiriki. Zoezi hilo la kufanya usafi pia lilipewa uzito kwa kuwepo kwa ofisi za uongozi za Wilaya ya Temeke ikiwemo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Afisa Mazingira na Watendaji wa Kata na mitaa.

Mkuu wa Walaya ya Temeke, Mh. Felix Lyaniva ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, aliipongeza Benki ya KCB kwa juhudi na kufanikisha kuwaleta wadau mbali mbali pamoja na wananchi wa Mbagala kushiriki katika kufanya usafi. “Mlichokifanikisha leo si kidogo na ninawapongeza lakini pia iwe chachu ya kutaka kufanya zaidi katika jamii yenu, ni mfano  mzuri wa kuigwa hata na makampui mengine.” aliongeza Mh. Felix Lyaniva.

Afisa Mazingira wa Wilaya ya Temeke, Nd. Ally Hatibu aliwashukuru wakazi wa Mbagala kwa kuitikia wito wa Benki ya KCB. Alisema ni ishara njema inayoonyesha kwamba wakazi wa hao wanalipa kipaumbele swala la kutunza mazingira.”Ninawasihi kuendeleza kuukuza ushirikiano huu na kufanya shughuli endelevu za kutunza mazingira.” alisema.

Hafla hiyo pia ilitoa fursa pekee kwa mama ntilie wanaofanya shughuli zao katika maeneo yanayozunguka Tawi la Benki ya KCB Mbagala, kwa kutoa huduma ya chakula kwa washiriki zaidi ya 100 katika hafla hiyo. “Kutoa fursa hii kwa akina mama hawa ilikuwa na jambo la kusudi na tuliwafuata bayana na kuwaomba kushiriki. Tutaendeleza ushirikiano wa aina hii kwa wajasiriamali wote wanaolizunguka tawi letu hasa wakina mama.’’ Alisema Bi. Christine Manyeye, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano ya Umma wa Benki ya KCB Tanzania.

Kwa upande wake, Bi. Jamila Dilunga ambaye alikuwa muwakilishi wa mama ntilie waliohudhulia zoezi hilo, aliishukuru Benki ya KCB kwa fursa waliyotoa kwa wakina mama wa Mbagala.

 Alisisitiza kwamba hakuna sababu ya Mbagala Zakhem kuwa chafu hasa baada ya ujio wa Benki ya KCB inayojali mazingira na usafi wa eneo la biashara zao. Aidha, aliiomba Benki ya KCB kufanya swala la kuhamasisha usafi katika eneo hilo kuwa endelevu.

Kuhusu Benki ya KCB

Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika Mashariki. 

Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation. Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi 14 Tanzania bara na visiwani Zanzibar. Matawi hayo ni Samora, Mlimani, Uhuru, Msimbazi, Lumumba, Buguruni, Oysterbay, Mbagala jijini Dar es Salaam; Moshi, Zanzibar, Arusha Main na TFA, Mwanza na Morogoro. 


Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika Mashariki.
Share:

Tuesday, September 4, 2018

FROM DESPAIR TO TRIUMPH: A WIDOW’S JOURNEY TO HER RIGHTFUL INHERITANCE

Msegena displays the judgement on an inheritance case she had won and recovered her house and other properties left by her deceased husband. Geita paralegals helped her claim her inheritance rights.


Under the Constitution of Tanzania every person is entitled to owning property, a right extended equally to both men and women and governed by the provisions of the Land Act and the Village Land Act. One would therefore rightly assume that this is a straight-forward, clear-cut situation; well, not quite. Incidents of widows losing their inheritance rights after the demise of a husband remain a serious problem in many societies across the country.

In the north-western region of Geita, Ms. Msegena Jeremia lost her husband in 2015 leaving her with the sole responsibility to bring up six children. while still overwhelmed by the pain of losing her husband, members of her clan convened an inheritance distribution meeting, a gathering that would ultimately and without her consent impose the destiny of any valuable assets.

Customarily, the eldest male child is placed in charge of any assets left behind by a deceased father and in Msegena’s case Joshua, a stepson and the eldest of the six children became the overseer of the assets which included a house, money deposited in a bank account and a motorcycle. Joshua was instructed to immediately withdraw TShs.1.9 million from the bank account and after opening an account for each of his siblings deposit an agreed amount into each account. The house and motorcycle would be sold.

This was to be the beginning of what seemed like a series of problems for Msegena. To her utter surprise, Joshua deposited all the money in his bank account and when she confronted him about this breach she said he attacked her physically and threatened to chop her hands off. With relations between the two of them deteriorating her husband’s relatives came together and began forcing her out of her matrimonial home.

“Joshua went so far as to lock me out of the house forcing me to spend two nights outside with no regard for my safety whatsoever. On the third day I couldn’t take it anymore so I went into town to seek any help I could get,” said Msegena with tears welling in her eyes.

In town she knocked on every door she believed would open for her to lay down her tons of burdens – from local community leaders to the police and finally the court. One of her attempts at seeking relief through the court and reclaim the inheritance hit a dead end when Joshua, now loaded with cash, bribed the magistrate who went on to rule in his favor.

Not every member of her late husband’s family wasn’t touched by what she was going through and at this point her sister-in-law, Safi, who apparently knew of a Geita-based paralegal, Bernard Mosira decide to help Msegane by introducing her to Bernard for further assistance. The rescue came to Msegena through Bernard Mosira who took up the case and immediately established communication with her.

“I called Bernard and explained my problem. He advised me to return home and promised me that he would remain in touch with me and that he will pursue my case”, she said.

Upon setting foot home however, the village chairman convened a traditional meeting traditionally known as “Nzengo” to isolate and force her out of the village on the fabricated claim that she engaged in untoward practices and was hence unfit to be part of the village.

On hearing the startling news Bernard travelled to the village the next day and approached the local leaders to at least help Msegena to start settling down again and get on the path to being in full control of her life, while also pointing the leaders to the consequences of their actions.

Seeing an open call to empower Msegena, Bernard used this experience to educate her on relevant provisions of the law, her rights and her responsibilities.

Armed with a new understanding and ripe confidence, she reported the maltreatment Joshua put her through to the local police station and within days he was apprehended and appeared before the primary court.  The court ruled in her favour ordering the clan members and her late husband’s relatives to desist from selling the house as intended, and effectively declared her its legal owner and of the motorcycle.

“During the hearing, I spoke like someone who knew the law, and people, particularly the magistrate and police, were surprised and wondered where I got such knowledge. I surely didn’t look convincing to anyone” stated Msegana.

“we are delighted to know the importance of observing laws and we have gone as far as inviting Bernard and his team and they have come up here twice now to provide legal education during our regular village meetings”, added the elder.

Msegena’s story paints a vivid picture of how effective legal education can be, often drawing two sides that were once polarized closer and closer and ultimately helping them find common ground under the canopy of the law. It makes a strong case for the sensitization of women’s rights and also the banishing of unjust customs and traditions.

Msegena, now a legally-empowered and free woman leads an improved life raising poultry and growing crops on land spreading out at the back of her house. The motorbike she once had no hope of ever seeing again now ferries people between nearby villages earning her extra income and allowing her to provide for her family.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive