A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Monday, January 26, 2026

APeF Yazindua Mfuko wa Ziada Kupanua wigo wa uwekaji Akiba, Uwekezaji na Ulinzi

  

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, (CMSA), CPA Nicodemus Mkama, akikabidhi waraka wa ofa kwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Africa Pension Fund (APeF), Dkt. Hamisi Kibola (wa tatu kushoto), kuashiria uzinduzi rasmi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja wa Ziada Fund, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa APeF, Bw. Mfaume Kimario, pamoja na wadau wengine wa Mfuko wa Ziada; kuanzia kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Alliance Life, Bw. Byford Mutikwasa, Bi. Tupokigwe Mwalwisi kutoka NBC na Bw. Lusungu.

DAR ES SALAAM, 26 Januari 2026. Africa Pension Fund Limited (APeF) leo imezindua rasmi Mfuko wa Ziada, ambao ni mfuko wa kwanza wa uwekezaji wa pamoja katika soko la fedha nchini Tanzania unaojumuisha mafao ya bima ya maisha, hatua inayoweka alama muhimu katika kupanua upatikanaji wa suluhisho za uwekezaji zilizo chini ya udhibiti. Hafla ya uzinduzi imefanyika katika Hoteli ya KingJada, Morocco Square, jijini Dar es Salaam. Kipindi cha awali cha uuzaji wa vipande kupitia mfuko huu kinaanza leo tarehe 26 Januari hadi 25 Februari 2026.

Hafla ya uzinduzi huo ilihudhuriwa na mgeni rasmi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), CPA Nicodemus Mkama, ikihudhuriwa pia na wawakilishi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), mifuko ya hifadhi ya jamii, wasimamizi wa mifuko, madalali, taasisi za kibenki na bima, pamoja na wanahabari.

Mfuko wa Ziada umebuniwa kuwasaidia wawekezaji kuweka akiba na kukuza fedha zao kupitia uwekezaji wenye nidhamu katika soko la fedha, ukiwa na faida ya ziada ya ulinzi wa bima ya maisha kwa wawekezaji binafsi wanaokidhi vigezo. Mfuko huu umerahisishwa kiutendaji, kwa kuwawezesha wawekezaji kuanza kwa urahisi, kuongeza uwekezaji wakati wowote, na kupata fedha zao ndani ya siku tatu za kazi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa APeF, Bw. Mfaume Kimario, alisema, Ziada imeundwa kwa wawekezaji wanaotaka njia rahisi na za kuaminika za kukuza fedha zao bila kupoteza uwezo wa kupata fedha zao pindi zinapohitajika. Huu ni mfuko imara katika soko la fedha unaopatikana kwa urahisi, wenye ulinzi wa bima ya maisha kwa wawekezaji wanaokidhi vigezo ukianzia na thamani halisi ya uwekezaji (vipande), ya chini kabisa ya shilingi 250,000. Bima hiyo hutoa kinga sawa na asilimia 50 ya thamani halisi ya uwekezaji (vipande) hadi kiwango cha juu cha thamani kilichohakikishwa cha shilingi milioni 100, na kiwango cha juu cha malipo ya bima cha shilingi milioni 50.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti na Bodi ya Wakurugenzi, Dkt. Hamisi Kibola, Mjumbe wa Bodi ya APeF, aliipongeza CMSA kwa hatua zilizofikiwa katika kuendeleza masoko ya mitaji nchini Tanzania na kwa kukuza ukuaji na uhai unaoonekana sokoni kwa sasa. Alibainisha kuwa kiwango cha uwekaji akiba nchini Tanzania bado kiko chini ya asilimia 3, na akatoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya wasimamizi na wadau wa sekta ya fedha ili kujenga utamaduni imara wa kujiwekea akiba unaojengwa juu ya taaluma, uaminifu, elimu ya fedha na upatikanaji rahisi wa huduma. Aliongeza kuwa ndiyo sababu APeF ilianzishwa, ubunifu ukiwa kama msingi wake, ili kuongeza wigo kwa vitendo njia za uwekaji akiba na uwekezaji kupitia mifuko ya uwekezaji wa pamoja, mipango binafsi ya pensheni inayounganisha suluhisho za bima na masoko ya mitaji.

Mfuko wa Ziada umeandaliwa kwa ushirikiano na taasisi washirika muhimu, ambapo Alliance Life Assurance Limited ni mtoa bima, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ni Mtunza Dhamana na Mdhamini. Wawekezaji wanaweza kupata huduma za Mfuko wa Ziada kupitia benki wakusanyaji zikiwemo CRDB Bank, NMB Bank, Exim Bank, Azania Bank, COOP Bank, NBC na Mwanga Hakika Bank, pamoja na kupitia mawakala walioidhinishwa na DSE na majukwaa ya kidijitali ya APeF.

Tunaalika Watanzania kufanya suala la kuweka akiba kuwa utamaduni wao kupitia Ziada. Unapoweka akiba kwa uthabiti, unaimarisha familia yako, kuinua jamii yako, na kuunga mkono maendeleo ya taifa. Ziada inakupa mahali rahisi pa kuanzia, kukua hatua kwa hatua, na kulinda kile kilicho muhimu zaidi,” aliongeza Ofisa Mtendaji Mkuu wa APef, Bw. Kimario.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), CPA. Nicodemus Mkama alisema kuidhinishwa kwa mfuko wa ziada kunaendelea kuleta chachu zaidi katika maendeleo ya uwekezaji kwenye mifuko hiyo na kuifanya idadi ya mifuko hiyo ya uwekezaji wa pamoja kufikia 26.

Kuhusu APeF

Africa Pension Fund Limited (APeF) ni msimamizi wa mifuko aliyeidhinishwa, anayetoa huduma za usimamizi wa mifuko, mifuko ya uwekezaji wa pamoja, suluhisho za pensheni binafsi, usimamizi wa mali, na ushauri wa kifedha. APeF imejizatiti kuimarisha usalama wa kifedha kupitia suluhisho za uwekezaji bunifu, zenye uwazi na zinazozingatia misingi bora ya suluhisho za uwekezaji.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Africa Pension Fund (APeF), Bw. Mfaume Kimario, akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja wa Ziada Fund, jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Africa Pension Fund (APeF), Dkt. Hamisi Kibola akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja wa Ziada Fund, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wadau wakihudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja wa Ziada Fund unaoendeshwa na Africa Pension Fund (APeF).
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Africa Pension Fund (APeF), Bw. Mfaume Kimario (kushoto) akizungumza na baadhi ya wadau wa Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja wa Ziada Fund wakati wa hafla ya uzinduzi wa mfuko huo, jijini Dar es Salaam leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, (CMSA), CPA Nicodemus Mkama (katikati), Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Africa Pension Fund (APeF), Dkt. Hamisi Kibola (wa nne kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa APeF, Bw. Mfaume Kimario (wa nne kulia) wakipiga picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo baada uzinduzi rasmi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja wa Ziada Fund, jijini Dar es Salaam leo.
Share:

Wednesday, January 21, 2026

ABSA BANK TANZANIA YAFUNGA KAMPENI YA 'UJANJA NI KUSWIPE NA KADI YA ABSA' KWA DROO YA MWISHO NA KUTANGAZWA KWA MSHINDI WA ZAWADI KUU

Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki yaAbsaTanzania, Bw. Aron Luhanga (kushoto), akifanya droo ya mwisho ya kampeni ya benki ya miezi mitatu ya 'Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa', jijini Dar es Salaam jana. Mteja wa benki hiyo, Bi. Nasreen Karim Abdallah, alijinyakulia zawadi kuu ya Tsh 30,000,000. Kampeni hiyo ililenga kuwahamasisha wateja kuongeza matumizi ya kadi za debit na credit za Absa pamoja na huduma za kibenki kwa njia za kidigitali za benki hiyo.

Benki ya Absa Tanzania imehitimisha rasmi kampeni yake ya 'Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa' iliyodumu Kwa miezi mitatu baada ya kufanyika kwa droo ya tatu na ya mwisho katika hafla Iliyofanyika jijini Dar es Salaam, jana.

Droo ya mwisho imehitimisha kampeni ya miezi mitatu iliyolenga kuwazawadia wateja kwa kufanya miamala na huduma za kibenki kwa njia za kidijitali ikiwa ni pamoja na matumizi ya kadi, huku ikithibitisha dhamira ya Absa ya kuhimiza miamala salama, rahisi na isiyotumia fedha taslimu.

Katika hafla hiyo, Absa ilifanya droo ya mwisho ya kila mwezi na kutoa jumla ya shilingi milioni 18 za Kitanzania (TZS 18 milioni) kwa wateja watatu walioibuka washindi kutokana na ushiriki wao katika mwezi wa mwisho wa kampeni.

Washindi hao ni Bw. Abdulrazak Ali Seif (TZS 10 milioni), Bi. Aysha Mbarak Meghji (TZS 5 milioni), na Bw. Gibbons Samuel Katule (TZS 3 milioni). Droo hiyo ilifanyika kwa kuzingatia Masharti na Vigezo vya kampeni na mbele ya mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, ili kuhakikisha uwazi na haki katika mchakato wa uchaguzi wa washindi.

Katika tukio lililosubiriwa kwa hamu zaidi wakati wa kilele cha kampeni hiyo, Bi. Nasreen Karim Abdallah aliibuka Mshindi wa Zawadi Kuu, akiondoka na shilingi milioni 30 za Kitanzania (TZS 30 milioni). Ushindi huo umetokana na matumizi yake ya mara kwa mara ya huduma za benki za kidijitali na kadi za Absa katika kipindi chote cha kampeni, na unaonesha jinsi miamala ya kila siku inaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga, alisisitiza mchango mkubwa wa wateja katika mafanikio ya kampeni hiyo:

Kampeni hii imekuwa na Manufaa mkubwa kwa wateja wetu tangu mwanzo. Tumehamasishwa kuona jinsi wengi wao wakichangamkia njia rahisi, salama na zisizotumia fedha taslimu katika kufanya miamala. Play Your Cards Right imeonesha kuwa pale wateja wanapochagua benki ya kidijitali, kila mtu hunufaika, kuanzia urahisi wa huduma hadi kuimarika kwa ujumuishaji wa kifedha.

"Tunawashukuru kwa dhati wateja wetu kwa kuendelea kuiamini Absa na kuwa sehemu ya safari hii.

Kwa upande wake, Mkuu wa Usimamizi wa Taarifa na Uchambuzi wa Takwimu (MI & Analytics), Bw. Denis Kessy, alieleza athari pana ya kampeni hiyo:

Absa tunaamini kuwa kila mteja ana Stori yenye thamani. Kampeni hii imetupa fursa ya kusherehekea Stori hizo, kubwa na ndogo, kwa kuwazawadia wateja wetu kwa kutumia tu huduma zetu za benki.

Tunapohitimisha kampeni hii leo, tunajivunia si mshindi wa zawadi kuu pekee, bali kila mteja aliyeshiriki.

Aliendelea kusisitiza ukubwa wa mafanikio ya kampeni hiyo kwa kusema:

Kupitia kampeni hii, Absa iliwazawadia washindi 72 wa kila wiki, washindi tisa wa kila mwezi na mshindi mmoja wa Zawadi Kuu, kwa jumla ya shilingi milioni 120 za Kitanzania (TZS 120 milioni) zilizorejeshwa kwa wateja wetu.

Huu ni uthibitisho dhahiri kuwa kuchagua Absa kunalipa.

Kampeni ya Play Your Cards Right ilikuwa kampeni ya zawadi kwa wateja iliyodumu kwa miezi mitatu kuanzia Oktoba hadi Desemba 2025, ikiwa na lengo la kuhamasisha matumizi ya malipo ya kidijitali na yasiyotumia fedha taslimu. Wateja walipata nafasi ya kushiriki katika droo za kila wiki na kila mwezi kwa kutumia kadi zao za debit au credit za Absa kupitia malipo ya kuswipe, kutap (tap) au ununuzi mtandaoni.

Kwa kukamilika kwa droo ya mwisho, kampeni ya Play Your Cards Right imefikia tamati rasmi. Washindi waliotangazwa katika droo ya mwisho watatambuliwa rasmi katika hafla maalum ya kukabidhi zawadi itakayofanyika mwezi Februari, na hivyo kuhitimisha kampeni hii kwa namna ya kukumbukwa, ikiwa ni uthibitisho wa dhamira ya Absa ya kuwaweka wateja katikati ya kila zawadi na kila hatua ya safari yake.
Mmoja wa washindi wa kila mwezi wa kampeni ya miezi mitatu ya benki ya Absa Tanzania iitwayo 'Ujanja ni Kuswipe na Benki ya Absa' Bw. George Kivaria, akichukua tiketi ya bahati nasibu ili kumpata mshindi wa droo Kuu wakati wa droo ya mwisho iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Mteja wa benki hiyo, Bi. Nasreen Karim Abdallah, alishinda zawadi kuu ya Tsh 30,000,000. Kampeni hiyo ililenga kuwahamasisha wateja kuongeza matumizi ya kadi za debit na credit za Absa pamoja na pamoja na huduma za kibenki kwa njia za kidigitali za benki hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga.
Mkuu wa Usimamizi wa Taarifa na Uchambuzi wa Takwimu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Dennis Kessy (wa tatu kushoto), akikabidhi hundi ya mfano ya Tsh 500,000/- kwa Bw. George Kivaria (wa pili kushoto), mmoja wa washindi wa kampeni ya miezi mitatu ya benki hiyo iitwayo 'Ujanja ni Kuswipe na Benki ya Absa' wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kampeni hiyo ililenga kuwahamasisha wateja kuongeza matumizi ya kadi za debit na credit za Absa pamoja na huduma za kibenki kwa njia za kidigitali za benki hiyo.
Mkuu wa Usimamizi wa Taarifa na Uchambuzi wa Takwimu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Dennis Kessy, akikabidhi hundi ya mfano ya Tsh 500,000/- kwa Bw. Mohammed Zulfikar Hemani (kushoto), mmoja wa washindi wa kampeni ya miezi mitatu ya benki hiyo iitwayo 'Ujanja ni Kuswipe na Benki ya Absa', wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga.
Share:

Tuesday, January 20, 2026

KANISA LA MLIMA WA MOTO LIMEANDAA KONGAMANO LA MAOMBI YA UPONYAJI WATU WOTE MNAKARIBISHWA

‎Kanisa la Mlima wa Moto Tanzania limesema linatarajia kufanya maombezi maalum ya kuliombea Taifa la Tanzania kupitia Kongamano la Neno la Mungu lililopewa jina la Anza Mwaka na Bwana

Akizungumza na waandishi wa habari katika Kanisa la Mlima wa Moto lililopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam, Mchungaji Samwel Hillary, ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya kongamano hilo, alisema lengo lao ni kuhakikisha Taifa linaanza mwaka likiwa karibu na Mungu, jambo lililowasukuma kuandaa kongamano hilo.


‎Mjumbe wa kamati ya Maandalizi ya Kongamano Mchungaji Samwel Hillary akizungumza na Waandishi wa habari katika Kanisa la Mlima wa Moto lililopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam.

‎Alisema kongamano hilo litafanyika kuanzia Januari 25 hadi Februari 1, 2026, na linatarajiwa kuongozwa na Askofu Dastani Maboya, Rose Mgeta, Mchungaji Madoshi pamoja na mchungaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa lengo la kuhubiri Neno la Mungu na kuliombea Taifa ili lipate amani ya kweli pamoja na uponyaji katika maeneo mbalimbali.

‎Kwa upande wake, Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya kongamano hilo, Godfrey Kazinja, alisema wameamua kuliombea Taifa ili kulinusuru na kulirejesha kwa Mungu, pamoja na kuyahamasisha vizazi na jamii kwa ujumla kuishi katika misingi ya kumpendeza Mungu.


‎Katibu wa kamati ya Maandalizi ya Kongamano Godfrey Kazinja akizungumza na Waandishi wa habari katika Kanisa la Mlima wa Moto lililopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam.

‎ 

‎Aidha, Kazinja alisema kutakuwepo na usafiri wa kuwachukua waumini kuanzia eneo la Mwenge hadi kanisani hapo, huku akiwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi ili kupata Neno la Mungu na uponyaji.

‎Naye Sarah Daniel, mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya kongamano hilo, alisema waimbaji mbalimbali wanatarajiwa kushiriki katika tukio hilo, akiwemo John Lissu, Mchungaji Epa, Ashery na wengine wengi, huku akiwaomba Watanzania kuendelea kufuatilia taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini.



‎Mjumbe wa kamati ya Maandalizi ya Kongamano Sarah Danielakizungumza na Waandishi wa habari katika Kanisa la Mlima wa Moto lililopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam.

‎Kongamano hilo ni sehemu ya jitihada za kudumisha amani na upendo miongoni mwa Watanzania, hususan mwanzoni mwa mwaka huu, kwa lengo la kuimarisha mshikamano na maadili ya upendo katika jamii.


‎Mjumbe wa kamati ya Maandalizi ya Kongamano Sarah Danielakizungumza na Waandishi wa habari katika Kanisa la Mlima wa Moto lililopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam.

‎Kongamano hilo ni sehemu ya jitihada za kudumisha amani na upendo miongoni mwa Watanzania, hususan mwanzoni mwa mwaka huu, kwa lengo la kuimarisha mshikamano na maadili ya upendo katika jamii.

Photo by Brian Peter
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive