A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Wednesday, July 16, 2025

Akiba Commercial Bank Plc Yazungumza na Wateja Wake Mjini Moshi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Akiba Commercial  Bank PLC Bw. Silvest Arumasi akifungua Mkutano wa wateja wa Benki hiyo mkoa wa Moshi wenye lengo la kusikiliza maoni yao, kushirikishana maendeleo ya Beni na kutoa elimu ya fedha. Pia ulikuwa ni jukwaa la kutoa shukrani kwa uaminifu wao tangu Benki ilipoanza kutoa huduma zake katika mkoa hu
wateja wa Benki hiyo wakifuatilia mkutano huo.

Akiba Commercial Bank Plc imeendelea kuimarisha dhamira yake ya kuwa benki inayosikiliza wateja kwa kufanya mkutano maalum na wateja wake jijini Moshi, tarehe 16 Julai 2025. Tukio hilo lilihudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki, Bw. Silvest Arumasi, kama mgeni rasmi.

Mkutano huo uliwaleta pamoja wateja wa eneo la Moshi kwa lengo la kusikiliza maoni yao, kushirikishana maendeleo ya Benki na kutoa elimu ya fedha. Pia ulikuwa ni jukwaa la kutoa shukrani kwa uaminifu wao tangu Benki ilipoanza kutoa huduma zake katika mkoa huo.

Bw. Arumasi aliwahimiza wateja kutumia majukwaa kama haya kama sauti yao ya moja kwa moja kwa Benki kwa kusema . "Kwetu ACB, kuwa karibu na mteja si kauli tu,  ni utamaduni tunaouishi. Tunathamini maoni yenu na tumejizatiti kuyawekea kazi kwa vitendo," alisisitiza.

Wateja walieleza mafanikio kadhaa ya ushirikiano wao na Benki na kutoa mapendekezo mbali mbali kwa lengo la kunufaisha pande zote mbili.  
Aidha, wateja walionesha kufurahishwa kwa kiasi kikubwa na ushiriki wa moja kwa moja wa Mkurugenzi Mtendaji katika tukio hilo, hususan kwa kujibu hoja mbalimbali papo kwa papo na kutoa maamuzi ya moja kwa moja kwa baadhi ya changamoto zilizowasilishwa. Walimtaja kuwa kiongozi wa mfano mwenye upeo mpana wa kibiashara na uwezo wa kufikiri kimkakati, kipaji na uwezo  unaosaidia  kuharakisha maamuzi muhimu kwa maendeleo ya Benki na ustawi wa wateja.

Katika hitimisho la mkutano, Akiba Commercial Bank iliahidi kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na kuendeleza utamaduni wa kusikiliza wateja kama sehemu ya mkakati wake wa kuwa Benki inayosikiliza, inayojali  na inayoleta matokeo chanya katika jamii.
Share:

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA YA ‘AIRTEL CHAPAKAZI’ MAALUM KWA WAJASIRIAMALI



Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Bw. Joseph Muhere (katikati), akizungumza na waadishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya Airtel Chapakazi jijini Dar es Salaam leo. Airtel Chapakazi inalenga kuinua biashara ndogo ndogo kwa kuwawezesha wajasiriamali kote nchini kutumia teknolojia kama daraja la kufikia masoko mapya, wateja wapya na fursa zaidi za kukuza kipato. Kushoto ni Mkuu wa Huduma za Wajasiriamali, Bw. Charles Banduka na Meneja Mahusiano wa Kampuni hiyo, Bw. Jackson Mmbando.

Airtel Tanzania leo imezindua rasmi huduma ya Airtel Chapakazi, suluhusho jipya lililoundwa kuchochea ukuaji wa wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo kote nchini. Uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika Makao makuu ya Airtel Tanzania jijini Dar es Salaam, ulionyesha dhamira ya Airtel katika kukuza maendeleo jumuishi ya kidijitali na kuunga mkono ajenda ya kukuza uchumi wa Tanzania.

Airtel Chapakazi inalenga kuinua biashara ndogo ndogo kwa kuwawezesha wajasiriamali kote nchini kutumia teknolojia kama daraja la kufikia masoko mapya, wateja wapya na fursa zaidi za kukuza kipato. Kulingana na takwimu za kitaifa, asilimia 15 tu ya biashara ndogo ndogo na za kati nchini Tanzania kwa sasa zinapata zana rasmi za masoko ya kidijitali, pengo ambalo Airtel Chapakazi inalenga kuziba. Airtel Chapakazi ni suluhisho la kibunifu linaloenda kuwapa wafanyabiashara wadogo uwezo sawa wa kidijitali unaotumiwa na makampuni makubwa.

Huduma ya Airtel Chapakazi inapatikana katika vifurushi vitano (05) vilivyoundwa kulingana na ukubwa na mahitaji na utofauti wa biashara:

● SME chap pack (TZS 100,000): Inajumuisha laini 2 za simu, kila moja ikiwa na GB10 ya data, SMS 1,000, na dakika 1,000 kwa mitandao yote. Pia kifurushi hiki kinajumuisha router ya intaneti ya bure kwa ajili ya matumizi ya ofisi yenye kasi ya 10 Mbps

 Kifurushi cha SME Bomba (TZS 150,000): Inajumuisha laini 3 za simu, kila moja ikiwa na 10GB ya data, SMS 1,000, na dakika 1,000 kwa mitandao yote. Pia kifurushi hiki kinajumuisha router ya intaneti ya bure kwa ajili ya matumizi ya ofisi yenye kasi ya 20 Mbps.

 Fahari Pack (TZS 200,000): Inajumuisha laini 5 za simu, kila moja ikiwa na 10GB ya data, SMS 1,000, na dakika 1,000 kwa mitandao yote. Pia kifurushi hiki kinajumuisha router ya intaneti ya bure kwa ajili ya matumizi ya ofisi yenye kasi ya Mbps 30 na SMS 5,000.

 Supa Pack (TZS 300,000): Inatoa laini 9 za simu zenye data sawa, SMS, na manufaa ya sauti, router ya ofisi ya bure ya Mbps 30, na SMS 10,000 kwa wingi.

● Max Pack (TZS 400,000): Inatoa laini 14 za simu, router ya ofisi ya bure yenye kasi ya Mbps 50, na SMS 15,000 — zinazofaa kwa timu kubwa yenye watu wengi au yenye ukuaji wa kasi ya juu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel Tanzania, Joseph Muhere, alisema Airtel Chapakazi inadhihirisha dhamira ya Airtel kusaidia biashara ndogo ndogo na za kati kupitia huduma suluhishi za kidijitali.

"Kwa kutumia Airtel Chapakazi, wateja watapata msaada wa karibu kutoka kwa mawakala wetu kuanzia hatua ya mwanzo hadi kupakua programu kutoka Play Store. Baada ya taarifa hizo kuthibitishwa, mteja atapokea ujumbe mfupi wa kiunganishi wa kupakua programu ya Airtel Chapakazi kutoka Play Store, mteja atapakua programu hiyo, kuchagua kifurushi: Fahari, Supa, au Max, na kukamilisha malipo ili kuwezesha huduma.” Alieleza Muhere.

Muhere alisisitiza juu ya umuhimu wa biashara ndogo ndogo na za kati katika uchumi wa Tanzania, akibainisha kuwa kundi hilo la wafanyabiashara wajasiriamali linashikilia zaidi ya asilimia 95 ya biashara zote, limeajiri zaidi ya watu milioni 8, na linachangia takriban asilimia 35 kwenye Pato la Taifa, ilhali wengi bado hawajafikiwa na zana za kijiditali ambazo zinaweza kukuza biashara zao kwa kiasi kikubwa.

"Kwa kipindi kirefu, Airtel Tanzania ilikuwa na dhamira ya kuanzisha suluhisho la kidijitali ambalo litaboresha sekta ya biashara na kuchangia katika kukuza uchumi wa nchi na sasa ndoto hiyo imetimia kwa kupitia Airtel Chapakazi," aliongeza Muhere.

Uzinduzi wa Airtel Chapakazi ni sehemu ya dhamira kubwa ya Airtel Tanzania katika kukuza maendeleo jumuishi, yanayoendeshwa na teknolojia nchini kote kwa kuwapa wafanyabiashara wanazohitaji ili kustawi katika zama za kidijitali.
Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Airtel Tanzani, Bw. Jackson Mmbando (kulia), akizungumza na waadishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma ya Airtel Chapakazi jijini Dar es Salaam leo. Airtel Chapakazi inalenga kuinua biashara ndogo ndogo kwa kuwawezesha wajasiriamali kote nchini kutumia teknolojia kama daraja la kufikia masoko mapya, wateja wapya na fursa zaidi za kukuza kipato. Kushoto ni Mkuu wa Huduma za Wajasiriamali, Bw. Charles Banduka na Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel, Bw. Joseph Muhere.
Mkuu wa Huduma za Wajasiriamali wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Bw. Charles Banduka (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa huduma ya Airtel Chapakazi jijini Dar es Salaam leo. Airtel Chapakazi inalenga kuinua biashara ndogo ndogo kwa kuwawezesha wajasiriamali kote nchini kutumia teknolojia kama daraja la kufikia masoko mapya, wateja wapya na fursa zaidi za kukuza kipato. Kushoto kwake Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel, Bw. Joseph Muhere na Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo, Bw. Jackson Mbando.
Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel Tanzania, Bw. Joseph Muhere (katikati), pamoja na baadhi ya wafanyakazi wengine wa Airtel, wakipiga picha nyuma ya bango lililoandaikwa 'Chapakazi' kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Chapakazi, jijini Dar es Salaam leo. Airtel Chapakazi ni suluhusho jipya lililoundwa kuchochea ukuaji wa wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo nchini kote.
Share:

Thursday, July 10, 2025

Airtel Tanzania Yawapa Walimu Mafunzo ya Ujuzi wa Kidijitali Kupitia Mpango wa SmartWASOMI

Mkurugenzi wa Machapisho na Utafiti kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Bw. Kwangu Zabron Masalu (Katikati), akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati wa warsha iliyoandaliwa kwa walimu wa IT, iliyoandaliwa na Airtel Tanzania kupitia Airtel Africa Foundation, kwa kushirikiana na UNICEF na Wizara ya Elimu, chini ya mpango wa Airtel SmartWASOMI, unaolenga kuboresha elimu ya kidigitali kwa kuwawezesha walimu na wanafunzi kupata maudhui ya kielimu kupitia maktaba mtandao ya Taasisi ya Elimu Tanzania na Shule Direct bila gharama ya vifurushi vya data. Kushoto ni Bw. Audax Tibuhinda kutoka Unicef na kulia Bw. Jackson Mmbando, Meneja Mahusiano wa Airtel Tanzania.

Airtel Tanzania kupitia Airtel Africa Foundation, kwa kushirikiana na UNICEF na Wizara ya Elimu, imeandaa warsha ya mafunzo kwa walimu wa IT chini ya mpango wa Airtel SmartWASOMI, mradi wa kisasa wa ujifunzaji wa kidijitali unaolenga kuboresha upatikanaji wa elimu bora kupitia teknolojia.

Warsha hiyo imewakutanisha walimu 60 kutoka shule za msingi na sekondari ambazo tayari zimeunganishwa na mpango wa Airtel SmartWASOMI. Mpango huu ulizinduliwa mwezi Mei 2024 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ikiwa ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania kupitia Airtel Africa Foundation, UNICEF na Serikali ya Tanzania. Zaidi ya shule 400 kote nchini zimeunganishwa na jukwaa hili, likiwa na huduma ya bure ya mtandao (zero-rated) kwa majukwaa ya mitaala ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Shule Direct, hivyo kuwapa maelfu ya wanafunzi na walimu fursa ya kupata rasilimali za ujifunzaji wa kidijitali bila gharama za data.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni wa Airtel Tanzania, Bi. Beatrice Singano, alisisitiza umuhimu wa walimu katika mafanikio ya mpango huo.

Walimu ndio msingi wa mfumo wetu wa elimu, lengo la warsha hii ya mafunzo ni kuongeza uwezo wa walimu katika kufundisha kwa njia ya kidijitali na kuboresha matokeo ya elimu kwa wanafunzi wa shule za sekondari. Tunawekeza kikamilifu katika kuboresha elimu kupitia kuwaandaa walimu kutoa elimu bora inayojumuisha matumizi ya teknolojia,” alifafanua.

Bi. Singano aliongeza kuwa Airtel SmartWASOMI imeondoa kikwazo kikubwa cha ujifunzaji wa kidijitali kwa kutoa huduma ya kuingia kwenye maudhui ya elimu bila gharama ya data kupitia mtandao wa Airtel, hivyo kuwapa wanafunzi na walimu njia rahisi na ya uhakika ya kufikia vifaa vya kujifunzia vilivyokubaliwa na serikali.

Katika mafunzo ya leo, walimu walipata uzoefu wa moja kwa moja wa kutumia zana za ujifunzaji wa kidijitali kupitia jukwaa la Airtel SmartWASOMI, ikiwa ni pamoja na kufikia maudhui ya mitaala, rasilimali shirikishi, na mbinu za kuingiza zana hizi kwenye ufundishaji wa kila siku darasani. Hii itasaidia walimu kurahisisha upangaji wa masomo, kuboresha ufundishaji kwa kutumia maudhui ya kidijitali, kutoa kazi shirikishi, na kufuatilia maendeleo ya wanafunzi kwa ufanisi zaidi, hivyo kuongeza ushirikiano na ubora wa ufundishaji darasani,” alisema.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Machapisho na Utafiti kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Bw. Kwangu Zabron Masalu, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Dk. Aneth Komba, alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye amesisitiza sana matumizi ya teknolojia ya mawasiliano. Matokeo yake, masomo ya teknolojia sasa yanafundishwa kuanzia elimu ya awali hadi ngazi ya chuo kikuu.

Lengo ni kuhakikisha kuwa fursa hii inaleta mapinduzi katika mfumo wa elimu wa Tanzania, tukizingatia kuwa elimu yetu kwa sasa inalenga zaidi kuzalisha wahitimu wenye ujuzi na umahiri katika kila ngazi,” alisema Bw. Masalu.

Walimu walioshiriki warsha hiyo waliupokea mpango huo kwa furaha kubwa, kwa wengi, ilikuwa mara yao ya kwanza kushiriki kwenye jukwaa kubwa la kidijitali linalolenga shule za sekondari nchini Tanzania.

Bi. Neema Avumba, mwalimu kutoka Shule ya Msingi TEGETA A, jijini Dar es Salaam alisema: “Ningependa kutoa shukrani zangu kwa Airtel Tanzania, UNICEF na serikali kwa kuandaa mafunzo haya leo, kabla ya warsha hii, wengi wetu hatukujua uwezo wa zana za kidijitali, sasa najihisi nimewezeshwa kuleta mbinu mpya darasani, tayari naona jinsi zitakavyowavutia na kuwashirikisha wanafunzi kwa njia ambayo hatukuweza hapo awali.

Kwa upande wake, Bw. Nassoro Shamsi, mwalimu kutoka Shule ya Msingi Mji Mwema, Kigamboni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, aliongeza kwa kusema: “SmartWASOMI imefungua fursa mpya. Sasa tunapata maudhui ya mtaala yaliyowezeshwa na nyenzo za kufundishia bila gharama za data kwa kutumia mtandao wa Airtel. Nimefurahi sana kuanza kutumia ipasavyo jukwaa hili baada ya mafunzo haya.

Mbali na mafunzo ya kiteknolojia, warsha hiyo pia iliwawezesha walimu kushirikiana, kuuliza maswali na kubadilishana uzoefu. Lengo si kuongeza ujuzi tu, bali pia kuunda mtandao wa mabalozi wa ujifunzaji wa kidijitali kote nchini.

Mpango wa Airtel Tanzania ni kufikia zaidi ya shule 1,000 ifikapo mwisho wa mwaka 2025, kwa kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya kidijitali, ushirikiano madhubuti na jamii pamoja na msaada kutoka kwa wadau muhimu. Juhudi hizi zinaendana na ajenda ya kitaifa ya kukuza upatikanaji jumuishi wa elimu bora ya kidijitali na kuchangia malengo mapana ya kukabiliana na upungufu wa walimu wenye sifa, kuongeza uelewa wa kidijitali kwa wanafunzi, na kuhakikisha usawa katika upatikanaji wa rasilimali za elimu katika mikoa yote.
Ofisa Vifaa vya Intaneti wa Mradi wa SmartWASOMI, Bw. Harrison Isdory (kulia), akitoa mafunzo kuhusu matumizi ya baadhi ya vifaa hivyo katika wakati wa warsha iliyoandaliwa kwa walimu wa IT, iliyoandaliwa na Airtel Tanzania kupitia Airtel Africa Foundation, kwa kushirikiana na UNICEF na Wizara ya Elimu, chini ya mpango wa Airtel SmartWASOMI, unaolenga kuboresha elimu ya kidigitali kwa kuwawezesha walimu na wanafunzi kupata maudhui ya kielimu kupitia maktaba mtandao ya Taasisi ya Elimu Tanzania na Shule Direct bila gharama ya vifurushi vya data. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive