A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Friday, March 28, 2025

AKIBA COMMERCIAL BANK YAWAKUMBUKA WATOTO WENYE UHITAJI DAR ES SALAAM.

 

Akiba Commercial Bank Plc Yapeleka Tabasamu Kituo cha Kulea Watoto- Chakuwama Sinza Dar es Salaam, 28/03/2025 – Katika kuendelea kujitoa kwa jamii, Akiba Commercial Bank Plc imetoa msaada kituo cha kulea Watoto cha Chakuwama, ikilenga kuboresha ustawi wa watoto na kuleta tabasamu kwenye nyuso zao.

Msaada huu, ambao unajumuisha mahitaji muhimu, unaonesha dhamira ya Benki hiyo ya kusaidia wenye uhitaji na kujenga matumaini kwa mustakabali mwema.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Bi. Dora Saria, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Akiba Commercial Bank, alieleza kuwa Benki hiyo inaamini katika kuunga mkono jamii na kuleta mabadiliko chanya ya kudumu.

"Akiba Commercial Bank, tunaamini katika nguvu ya mshikamano katika kubadili maisha. Msaada huu ni hatua muhimu ya kuhakikisha ustawi wa watoto hawa na kuleta matumaini kwa wenye uhitaji kwa maisha bora yajayo," alisema Bi. Saria.
Kwa upande wake, Bw. Hassan Tabu, mwakilishi wa Kituo cha Chakuwama, aliishukuru Akiba Commercial Bank kwa ukarimu wake, akibainisha kuwa msaada huo utakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya watoto hao.

"Tunaishukuru sana Akiba Commercial Bank kwa kusimama nasi. Msaada huu utasaidia kwa kiasi kikubwa kukidhi mahitaji ya watoto na kuwapatia sababu ya kutabasamu," alisema.
Kupitia juhudi hizi, Akiba Commercial Bank Plc inathibitisha tena dhamira yake ya kuwajibika kwa jamii kwa vitendo, ikilenga kuleta mabadiliko chanya na ya kudumu kwa jamii inayoihudumia.
Share:

Friday, March 21, 2025

Taasisi za Ulinzi wa Mlaji zimetakiwa kushirikiana na FCC

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Suleimani Jafo, amezitaka taasisi zote za serikali zinazohusika na ulinzi wa mlaji kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha haki za watumiaji zinalindwa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Haki za Watumiaji Duniani, Dkt. Jafo amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya mamlaka mbalimbali za udhibiti ili kuhakikisha bidhaa na huduma zinazopatikana zinakidhi viwango vya ubora na zinauzwa kwa bei nafuu.

Dkt. Jafo amezihimiza taasisi kama Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Vipimo (WMA), Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na taasisi nyingine muhimu kushirikiana kwa karibu ili kuimarisha ulinzi wa walaji.

Haki za watumiaji ni nguzo muhimu kwa ustawi wa uchumi wetu. Serikali ina jukumu la kuhakikisha kuwa watumiaji wanalindwa dhidi ya unyonyaji, hasa katika mazingira ya mabadiliko ya soko la kimataifa,” alisema Dkt. Jafo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), William Erio, amesema kuwa FCC inaendelea kuchukua hatua madhubuti kulinda maslahi ya watumiaji na kuimarisha ushindani wa haki katika soko.

Tunajivunia juhudi za kimataifa zinazolenga kulinda haki za walaji, na hapa Tanzania, tunahakikisha soko letu linakuwa la haki, uwazi na lenye ushindani wa kweli,” alisema Erio.

Aidha, alibainisha kuwa FCC imepata cheti cha Shirika la Uthibitisho la Kimataifa (ICO), hatua inayothibitisha jitihada za tume hiyo katika kupata utambuzi wa kimataifa na kujenga imani katika soko la Tanzania.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga, amepongeza FCC kwa juhudi zake katika kuimarisha ushindani mzuri kwenye sekta ya viwanda.

Ni muhimu kwa viwanda vyetu kuendelea kuboresha bidhaa na huduma zao ili kukidhi matarajio ya watumiaji. Ushindani wa haki unaleta mazingira mazuri kwa biashara kukua huku tukihakikisha haki za watumiaji zinalindwa,” alisema Tenga.

Maadhimisho haya ya Siku ya Haki za Watumiaji Duniani yamekuwa jukwaa muhimu la kutathmini maendeleo yaliyofikiwa katika kulinda walaji na kutoa wito wa ushirikiano madhubuti kati ya serikali, wadau wa sekta binafsi na mashirika ya watumiaji ili kuimarisha mazingira ya soko la Tanzania.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Suleimani Jafo, akizugumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Haki za Watumiaji Duniani.
Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani FCC Dkt. Aggrey Kalimwage Mlimuka.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), William Erio
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Suleimani Jafo,akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (F. CC), William Erio.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga.
Share:

Wednesday, March 19, 2025

Benki ya Absa Tanzania na World Vision Tanzania Washirikiana Kuboresha Upatikanaji wa Maji katika Kijiji cha Kwedizinga

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la World Vision Tanzania, Bi. Nesserian Mollel, wakisaini hati ya makubaliano jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya ushirikiano kwenye Mradi wa Maji katika Kijiji cha Kwedizinga, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Benki ya Absa imetoa mchango wa TZS milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa kisima katika kijiji hicho kitakachowanufaisha wakazi zaidi ya 3,000, ambapo watoto wanawakilisha 55% ya idadi ya wakazi wa kijiji hicho.

Absa Bank Tanzania imetangaza ushirikiano wa kimkakati na Shirika la World Vision Tanzania ili kuboresha upatikanaji wa maji safi, usafi wa mazingira na watu katika kijiji cha Kwedizinga, Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga. Mpango huu unaonyesha dhamira ya Absa ya kuwawezesha jamii na kuwa chachu ya maendeleo chanya.

Kijiji cha Kwedizinga, ambacho kina vijiji vidogo saba na idadi ya watu takriban 4,000, kimekuwa kikikabiliwa na changamoto za kupata maji safi na salama. Hivi sasa, wakazi wanategemea mabwawa na mito ya msimu, hali inayosababisha ongezeko la magonjwa yanayotokana na maji na kuweka mzigo mkubwa kwa wanawake na watoto ambao mara nyingi husafiri zaidi ya kilomita 2 kila siku kutafuta maji.

Mradi huu unalenga kushughulikia changamoto hizi kupitia hatua kuu zifuatazo:

Uchunguzi wa Kihidrolojia na Uchimbaji wa Visima: Kufanya uchunguzi wa kina wa maji chini ya ardhi ili kubaini eneo linalofaa zaidi kwa ajili ya kisima chenye mavuno mengi, ikifuatiwa na uchimbaji hadi kina cha mita 180.

Mfumo wa Kusukuma Maji kwa Nguvu za Jua: Kufunga mfumo rafiki wa mazingira wa kusukuma maji kwa kutumia nishati ya jua ili kusafirisha maji kutoka kisimani hadi kwenye tanki la kuhifadhi lililoinuliwa.

Uhifadhi na Usambazaji wa Maji: Kujenga tanki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita 50,000 na kuanzisha mtandao wa usambazaji maji wenye vituo vingi vya ukusanyaji, kuhakikisha kwamba vijiji vidogo vyote saba vinapata maji safi ndani ya mita 400, sambamba na viwango vya sera ya maji ya Tanzania.

Ushirikishwaji wa Jamii na Mafunzo: Kuunda na kutoa mafunzo kwa kamati ya watumiaji wa maji ili kusimamia mfumo wa usambazaji maji, kukuza mbinu endelevu, na kufanya uhamasishaji wa jamii kuhusu usafi wa mazingira na usafi binafsi.

Mpango huu unalingana na Malengo kadhaa ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, ikiwemo SDG 3 (Afya Bora na Ustawi), SDG 4 (Elimu Bora), na SDG 6 (Maji Safi na Usafi wa Mazingira). Pia unaunga mkono Awamu ya 3 ya Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Maji ya Tanzania (2022/2025), ambao unalenga kuwaunganisha mamilioni ya watu na vyanzo vipya na vilivyoboreshwa vya maji.

Absa Bank Tanzania imejitolea TZS 50,000,000 kuwezesha mradi huu, ikionyesha dhamira ya benki ya kuiwezesha Afrika ya Kesho, pamojaz, hatua moja baada ya nyingine.

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini, Bw. Obedi Laiser, Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Bank Tanzania, alisisitiza dhamira ya benki ya kuwa chachu ya maendeleo chanya katika jamii wanazofanya kazi: "Katika Absa, tunaamini kwamba kila story ina umuhimu. Ushirikiano huu ni ushahidi wa lengo letu la kuiwezesha Afrika ya Kesho, pamoja, hatua moja baada ya nyingine. Kwa kutoa upatikanaji endelevu wa maji safi katika kijiji cha Kwedizinga, hatuboreshi tu afya na usafi wa mazingira, bali pia tunashughulikia masuala ya utofauti na ujumuishaji, fursa za kielimu, na kuwezesha ukuaji wa kiuchumi."

Bi. Nesserian Mollel, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa World Vision Tanzania, pia alitoa maoni kuhusu ushirikiano huo: "World Vision imejitolea kufanya kazi na jamii kuleta maendeleo. Ushirikiano huu na Absa Bank Tanzania unaonyesha dhamira yetu ya kukuza mabadiliko ya kibinadamu. Pamoja, tunahakikisha kwamba watoto na familia katika kijiji cha Kwedizinga wanapata moja ya mahitaji ya msingi ya maisha - maji safi."

Mradi unatarajiwa kunufaisha moja kwa moja wakazi wote 3,890 wa kijiji cha Kwedizinga na kuwanufaisha kwa namna tofauti watu wengine 596 kutoka vijiji jirani, hatua muhimu kuelekea kuboresha afya, elimu, na matokeo ya kiuchumi katika eneo hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa tatu kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya ushirikiano na Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la World Vision Tanzania, Bi. Nesserian Mollel, jijini Dar es Salaam leo, ambapo kupitia makubaliano hayo Benki ya Absa imetoa mchango wa TZS milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa kisima cha maji kitakachowanufaisha wakazi zaidi ya 3,000 wa Kijiji cha Kwedizinga, Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga ambapo watoto wanawakilisha 55% ya idadi ya wakazi wa kijiji hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (katikati), Mkurugenzi wa Wateja wa Makampuni wa Absa Tanzania, Bi. Nellyana Mmanyi na Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la World Vision Tanzania, Bi. Nesserian Mollel wakifurahi jijini Dar es Salaam leo, muda mfupi mara baada ya kusaini hati ya makubaliano, kwa ajili ya ushirikiano katika Mradi wa Maji kwenye Kijiji cha Kwedizinga, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Share:

Wednesday, March 12, 2025

"Stori za Afya za Wanawake wa Tanzania zina thamani kwetu", Absa Bank

Baadhi ya Wafanyakazi Wanawake wa Benki ya Absa Tanzania kupitua umoja wao uitwao ‘Red Skirts’ wakiwa katika picha ya pamoja na madaktari pamoja na wagonjwa katika Hospitali ya CCBRT, baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya wagonjwa wa fistula kama sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, hospitalini hapo mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Absa wakibeba msaada wa vifaa vitakavyosaidia huduma za watoto wanaozaliwa kabla ya muda (Njiti), kab;la hawajavikabidhi katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Meneja Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Anna Chacha (wa saba kushoto) akikabidhi msaada wa vifaa tiba na vifaa muhimu vitakavyosaidia huduma za watoto wanaozaliwa kabla ya muda (Njiti) katika Hospitali ya Muhimbili kwa Mkuu wa Kitengo cha Watoto Wachanga, Dk. Martha Mkony, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (kulia) akikabidhi msaada wa vifaa tiba kwa Mkuu wa Ubora na Huduma kwa Wateja wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Emelda Lwena, kwa ajili ya wagonjwa wa fistula, kwenye jengo la mama na mtoto la hospitali hiyo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

WATOTO wanaozaliwa na changamoto mbalimbali katika Hospitali ya Muhimbili, sasa wanaweza kupata ahueni zaidi mara baada ya wafanyakazi wanawake wa Benki ya Absa Tanzania, kukabidhi msaada wa vifaa tiba na vifaa muhimu vya kusaidia watoto hao wanazaliwa kabla ya kufika wakati wa kujifungua.

Akizungumza wakati akipokea vifaa hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Watoto Wachanga katika hospitali hiyo, Dk. Martha Mkony alitoa shukrani kwa wafanyakzi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanwake Duniani alisema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka kwani utasaidia sana watoto wanaozaliwa kila siku katika hospitali hiyo.

Nipende kuwashukuru sana wanawake wa Benki ya Absa kwenye kundi lao wanalojiita ‘Red Skirts’ kwa tendo hili la kijamii, na tunajua hii ni mwanzo wa mahusiano marefu kati ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha watoto wachanga pamoja na Benki ya Absa na tunaahidi kushikiriana kwa pamoja katika kuwahudumia watoto wachanga”, alisema Dr. Marha.

Akizumgumza wakati akibidhi vifaa hivyo, Meneja katika Kitengo cha Rasilimali Watu wa Benki ya Absa, Bi. Martha Chacha alisema, kwa kuthamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya Taifa, pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili, wanawake wa Benki ya Absa Tanzania, kupitia umoja wao wa ‘Red Skirt’ walikwenda kutoa misaada kwa wagonjwa wa fistula katika Hospitali ya CCBRT pamoja na kitengo cha Watoto Njiti katika Hospitali ya Muhimbili.

Kwa niaba ya wanawake wenzangu tupo mahali hapa tukiwakisha benki yetu kutoa misaada hii, Benki ya Absa inajali Story za Wanawake wa Tanzania, Story za mafanikio ya kiafya na kiuchumi kwa wanawake zina umuhimu sana kwetu”, aliongeza Bi. Anna
Share:

Tuesday, March 11, 2025

Absa Group Reports 10% Increase in 2024 Earnings after Material Second-Half Recovery

 

Salient points
  • Revenue increased 5% to R109.9 billion
  • Operating costs rose 5% to R58.5 billion
  • Cost-to-income ratio unchanged at 53.2%
  • Pre-provision profit increased 5% to R51.4 billion
  • Impairments decreased 8% to R14.3 billion
  • Credit loss ratio improved to 103 basis points from 118 basis points
  • Headline earnings increased 10% to R22.1 billion
  • Return on equity grew to 14.8% (from 14.4%)
  • Group CET 1 ratio improved to 12.6% (from 12.5%)
  • Dividend per share increased 7% to R14.60 per share
Absa Group earnings increased 10% in 2024, underpinned by a material improvement in the second half, demonstrating meaningful progress after a disappointing first half. Earnings were driven by both a more supportive operating environment as well as deliberate steps taken to support performance.

Our organisation rallied in the second half, refining our focus areas to ensure that our actions are targeted and precise in generating value and earnings uplift,” said Charles Russon, Interim Chief Executive Officer at Absa Group. “We are confident in our strategic direction and our ability to continue delivering value to our stakeholders while expanding access to innovative financial solutions across our markets.”

Absa Group’s financial performance in 2024 signals recovery and demonstrates improving franchise health. The Group made progress with recent strategic execution changes introduced to set the Group on a path to delivering appropriate returns.

Revenue increased by 5% and headline earnings increased 10%, bolstered by a reduction in retail impairments in South Africa. Non-interest revenue saw growth of 6%, reinforcing the strength of the Group’s underlying business and diversified income streams.

Enhanced risk management practices and improving customer financial health drove an 8% decline in impairment charges. Consequently, Absa reported a decline in the credit loss ratio (CLR) to end the year at 103 basis points, which remains slightly above the upper end of the group’s target range. CLR in the second half was 85 basis points.

The balance sheet remains strong, with a Common Equity Tier 1 (CET1) ratio of 12.6% which is at the top-end of our target range and liquidity metrics are healthy.

While return on equity (RoE) remains below medium-term ambitions, the Group has made clear year-on-year progress, with a visible pathway toward achieving its 16% RoE target by 2026.

Key structural improvements, including disciplined risk management, cost efficiencies, and optimised capital allocation, are starting to translate into improved results. Our stronger second-half performance gives us confidence that we are taking the right action to support delivery of a 16% RoE by 2026,” said Deon Raju, Absa Group Financial Director.

A key driver of the Group’s strong recovery in the second of the year was a strategic pivot towards prioritising sustainable growth over market share expansion. This ensured more disciplined capital allocation to higher-value sectors, refined pricing strategies to better reflect risk, and a shift from product profitability to customer franchise profitability, enabling better decision-making and performance tracking.

Growing customer numbers and digital adoption and improving customer experience remain a key priority for Absa. The Group expanded its total customer base by 4% to 12.7 million, with digitally active customers up 14% across the Group. Absa’s customer experience index improved to a weighted score of 101, from 96 in 2023, with improvements noted across all businesses. The Corporate and Investment Banking unit increased primacy to 42% from 40% as new clients leveraged our broader product set.

Enhanced customer experiences, supported by digital innovation and service enhancements, have contributed to increased engagement and stronger client relationships.

The organisation also made significant progress on its non-financial performance metrics, particularly in sustainability and ESG initiatives, advancing its commitment to financial inclusion, youth and women empowerment, small and medium enterprise development, and climate change mitigation on the continent. The Group achieved its goal of facilitating R100 billion in sustainable financing a year ahead of schedule.

We are making strategic investments where they have the greatest impact—delivering meaningful value to our customers while ensuring sustainable, long-term growth. By optimising our operations and enhancing efficiency, we are improving affordability, expanding access to financial services, and strengthening the customer experience at every touchpoint,” said Russon.

Business Unit Performance
  • Product Solutions Cluster (PSC) headline earnings increased 38% to R3.3 billion.
  • Everyday Banking (EB) increased 18% to R4.0 billion.
  • Relationship Banking (RB) increased 4% to R4.3 billion.
  • Absa Regional Operations - Retail and Business Banking (ARO RBB) increased 12% to R1.8 billion.
  • Corporate and Investment Banking (CIB) increased 6% to R11.7 billion.
Outlook

Building on the second-half momentum, Absa Group will continue to focus on driving earnings growth and generating shareholder value. While the external environment is uncertain and may affect earnings, the Group remains confident in its ability to manage these effectively. RoE is expected to continue improving, supported by disciplined capital allocation and the ongoing benefits of the Group’s strategic initiatives. Credit loss ratios are expected to improve further, into the top end of the Group’s target range, largely driven by further recovery in South Africa’s retail portfolio. Additionally, the impact of substantial items is expected to ease, particularly regarding hyperinflationary accounting for the Ghanaian operations.

Absa is in the process of reviewing its retail operations in South Africa, to better serve its customers and clients and strengthen its position in a highly competitive market. The programme is on track to deliver a retail bank in the first half of this year. The primary aim of the review is to reinforce Absa’s foundational strengths in retail and fortify the company’s market-differentiating products and services. The outcome of the design phase will determine how Absa integrates various capabilities for maximum efficiency and improved customer experience, while achieving minimal disruption.

The execution of our strategy remains clear and disciplined, anchored in enhancing user experiences, maintaining primacy, driving digital innovation, and acting as an active force for good in everything we do,” said Russon. “As we build on the momentum of our recovery, we are focused on sustained, profitable growth—ensuring we continue to create meaningful value for our customers, colleagues, and shareholders across the continent.
Share:

Sunday, March 2, 2025

MAWAKALA WA SIMTANK WAFURAHIA MIAKA 35 YA KAMPUNI HIYO.

  Mwanzilishi wa Kampuni ya Silafrika Tanzania inayozalisha bidhaa za Simtank, Gulab Shah (wapili kushoto), akikabidhi cheti na zawadi ya mfano wa ufunguo wa Gari kwa mlliki wa Kampuni ya Ravi Group, Ravindra Chadarana baada ya kuibuka washindi wa kwanza katika hafla ya kusheherkrea miaka 35 ya utoaji huduma iliyoambanana na kuwapongeza Mawakala wa bidhaa za SIMTANK nchini. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Silafrika, Alpesh Patel na Sachin Dawda mwakilishi wa Kampuni ya Ravi Group.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Silafrika, Alpesh Patel akizungumza na wanahabari wakati wa hafla ya kusheherkrea miaka 35 ya utoaji huduma iliyoambanana na kuwapongeza Mawakala wa bidhaa za SIMTANK nchini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Silafrika, Alpesh Patel Akikabidhi cheti na zawadi maalum Kwa mmoja ya mawakala wanafanya vizuri wakati wa hafla ya kusheherkrea miaka 35 ya utoaji huduma iliyoambanana na kuwapongeza Mawakala wa bidhaa za SIMTANK nchini.





Kampuni ya Simtanki imekutana na mawakala zaidi ya 60 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ilikurudisha shukurani kwao kutokana na kile wanachokifanya ikiwa ni maadhimisho ya miaka 35 tangu kuanzishwa kwa Kampuni hiyo.


Maadhimisho hayo yamefanyika Februari 29,2025 katika hoteli ya Hayyt legency jijini Dar es salaam.

Meneja Mauzo kutoka Kampuni hiyo Salman Khan amesema mawakala hao ni chanzo cha mafanikio makubwa kwani wamesaidia kupatika mauzo ya zaidi ya Lita bilioni 26 tangu wameanza na hiyo nizaidi ya pisi laki 6.

"Sisi ni waanzilishi na wabobezi wa hii biashara hasa katika uzalisha wa haya matenki na tumekuja na teknolojia tofauti ikiwemo unbreakable tanki ikiwa na garantee ya miaka 25,"amesema...


Naye Wakala kutoka Mbezi Beach Suleiman Seif amesema Simtank haina mashindani kwani imekuwa ikipendwa na watu wengi na ndani ya mwenzi mmoja unaweza uza tanki zaidi ya 50 za lita 1000 na hiyo nikutokana na uhitaji wa watu.
Share:

MIXX BY YAS YATOA ZAWADI YA MILIONI 20 MTWARA.

Hatimaye kampeni ya Magift inayofanywa na kampuni ya Yas Tanzania ,kupitia kitengo cha Mixx by Yas imeweza  kuwazawadia, wateja na washindi wake wa mkoa wa mtwara zawadi mbalimbali, ikiwemo fedha na gari Moja.
Akizungumza mara baada ya kuibuka mshindi wa kampeni ya Mixx by Yas, Zena Ponera ambaye ni mkazi wa manispaa ya Mikindani mjini mtwara ameelezea  MIKINDANI Siri ya ushindi huo, ambapo mbali na mambo mengine amesishukuru Yas kwa kufanikisha kuchezesha Droo za Magift ya KUGIFT 2024-25.

Kwa upande wake Meneja wa Yas Kanda ya Mtwara, Eric Munuku,ameelezea namna kampeni hiyo ilivyoweza kuwanufaisha watanzania wengi ambao wameweza kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha magari  na zawadi za simu za mkononi Kutoka Yas na Mixx by Yas.

Kampuni ya mtandao wa Mawasiliano ya Yas Tanzania kwa kipindi cha miezi miwili na nusu iliyopita iliendesha kampeni hiyo nchi ambapo jumla ya washindi Zaidi 300 walifanikiwa kujinyakulia zawadi mbalimbali Kutoka Kampuni ya Yas Tanzania.
Share:

MIXX BY YAS YAPIGA JEKI MAWAKALA WAKE.

Kampuni ya mtandao wa Mawasiliano ya YAS Tanzania,imesem inamikakati kabambe katika kuhakikisha inaendelea kutoa huduma Bora salama na uhakika kwa wateja wake ndani ya mwaka huu wa 2025.

Akizungumza wakati wa hafla fupi iliyowakutanisha baina ya viongozi wa Yas na Mixx by Yas, na baadhi ya Mawakala na Mawakala Wa kuu Yas iliyofanyika usiku wa kuamkia Leo March Moshi 2025 jijini dar es salaam Afisa mkuu wa Mixx by Yas Angelika Pesha, amesema wao kama Mixx by Yas wanaanmini ili kufika mbali wanaihitaji kuwa na wadau ikiwemo Mawakala na Mawakala wakuu.

Pesha amesema kuwa wao wameamua kukukutana na wadau wao kwa namba Moja au nyingine ilikubadirishana mawazo lakini ni Imani yake kuwa siku zote wanaamini kuwa  sherehekea kidogo kwa kila kinachopatikana hiyo ni njia sahihi kufanikiwa.

aidha Pesha Amesema kuwahuu ni mwaka WA 15 kufanya tukio la namna hiyo ambapo mwanzoni waalianza na mawakala wapatao 2300 mwaka 2010, ambapo lengo kubwa ni kuwa na Mawakala wengi Zaidi na kuwafikia wateja wengi zaidi Nchini kwani Yas ni mtandao ulioenea nchi nzima.

Vilevile Bi Pesha amechukua fursa hiyo kujipongeza kwani hadi sasa Yas Tanzania ina Mawakala Zaidi ya 200000 nchi nzima ambapo amesema kama itakumbukwa Yas imefanya uwekezaji mkubwa hivyo Moja ya Malengo yao ni kuwafikia wateja wengi kwenye miji mikubwa nchini,lakini pia kujitanua Zaidi kidigitali

katika hatua nyingine Peshaa hakuacha kufanya kuwa lengo jingine ni kuendelea kuwapa uwezo and Mawakala wao kwani kama unavyojua kwa sasa watanzania wengi wamekuwa wakifanya miamala hivyo kupitia mifumuo Yao ya kidigitali itasidia kutoa huduma Bora Zaidi na ndio maana wamekuwa wakiwekezaa kwenye Teknolojia ambapo kwa sasa wamefikia kwenye Teknolojia ya 4 na 5G kwenye maeneo mengi hapa nchini lakini pia mikakati Yao ni kuvuka mipaka ya Tanzania
Kampuni ya Yas ambayo mwishoni mwa mwaka Jana ilibadili chapa yake Kutoka TIGO Tanzania ambapo sasa inajulikana kama YAS, imekuwa ikifanya vizuri sokoni na kujizolea Tuzo mbalimbali ikiwemo ile ya OOKLA ambayo umenifanya kampuni hiyo kuwa kinara barani Afrika ukilinganiaha na kampuni nyingine za mtandao hapa nchini, na Afrika kwa ujumla.
Aidha Yas ndio mtandao unaoongoza Nchini kwa kuwa umeenda Nchini nzima mijini na vijijini,huku ikiwa imewekeza kiasi kikubwa cha fedha na mitaji katika miundombini na teknolojia hususani ile ya kimkakati ambapo sasa inakuja na mfumo mpya 5G, na kwenye miji mikubwa nchini na kwengineko
Share:

Saturday, March 1, 2025

Smallholder farmers get support to adopt modern mechanization

By Our Reporter

AGRICULTURAL mechanization has the potential to transform Tanzania's agricultural sector, driving increased productivity, reducing labor intensity, and fostering economic growth.

Despite its benefits, mechanization remains underdeveloped and inequitably adopted. Increasing agricultural operating income is not only an important step in improving agricultural work for farmers in the new era, but is also a powerful way to promote rural revitalization.

According to reports, for every 1 percent increase in the level of mechanization, the yields of all crops, grain crops, and cash crops increase by 1.2151, 1.5941, and 0.4351 percent, respectively.

For that reason, the Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) under the Youth Entrepreneurship for Food and Agriculture (YEFFA) in partnership with Sahara Accelerator has sought to launch the Kilimotech Accelerator.

The idea is to provide innovative solutions to help in the adoption of mechanization, especially among smallholder farmers in various regions of Tanzania.
The focus is on scaling agricultural innovations that help smallholder farmers towards increased incomes, better livelihoods, and improved food security.

African farmers need uniquely African solutions to the environmental and agricultural challenges they face, enabling them to sustainably boost production and gain access to rapidly growing agricultural markets. In short, AGRA’s mission is to transform the lives of smallholder farmers from that of a solitary struggle for survival to a business that thrives,” AGRA says.

A report commissioned by AGRA and prepared by Sahara Accelerator states that large-scale farms benefit disproportionately, while smallholder farmers—who represent the majority—face significant barriers.

These include high machinery costs, limited access to financing, inadequate infrastructure, and fragmented policy frameworks. Smallholder farmers rely on basic mechanization methods, including hand-tool technologies and draft animal power,” the report states.

The report includes findings from stakeholder mapping exercises conducted in Singida, Manyara, Njombe, and Mbeya, focusing on sunflower, maize, horticulture, and rice value chains.
Sahara Accelerator Chief Strategist, Adam Mbyallu, says that the study identifies systemic challenges and highlights opportunities to promote inclusive mechanization.

Innovations such as digital platforms (e.g., Hello Tractor), pay-as-you-go financing, leasing systems, and local manufacturing initiatives are critical tools for democratizing mechanization and making it more accessible to smallholder farmers,” says Mbyallu.

Drawing from global success stories, including Asia's Green Revolution, this report outlines strategic pathways to promote mechanization adoption in Tanzania.

Mbyallu says that Tanzania can establish a resilient and inclusive mechanization ecosystem by fostering public-private partnerships and integrating sustainable practices.

The report concludes with targeted recommendations and a strategic roadmap for enhancing the efficiency and sustainability of agricultural mechanization,” he adds.

Among the recommendations in the report include developing innovative financing models tailored to the specific needs of agriculture value chain stakeholders. These models should address the unique operational conditions of smallholder farmers, processors, and distributors to facilitate access to modern equipment and tools.

The report also suggests practical training and capacity-building initiatives to enhance financial knowledge, record-keeping practices, and stakeholder awareness. This would enable smallholders and other actors to meet financial institutions' requirements for mechanization loans and capital.

It also calls for the establishment of a coordinated financing framework to connect key stakeholders in the mechanization financing ecosystem, including beneficiaries, financial institutions, manufacturers, and equipment dealers.

This would streamline financing processes, reduce delays, and enhance accessibility for smallholder farmers,” the report notes.

Furthermore, the report recommends the adoption of accessible and affordable digital and automation technologies to address inefficiencies in agricultural mechanization.

Emerging tools, such as smartphone applications for crop disease identification and digital platforms for farm management, can significantly advance the sector towards agriculture 4.0, leveraging technologies like IoT, cloud computing, big data, AI, and decision support systems.
There is also the need to develop programs to improve digital literacy, technical skills, and readiness among stakeholders, particularly small and medium-scale farmers, processors, and distributors. Increased capacity in these areas will drive the adoption and effective utilization of digital and automation technologies.

Local agricultural equipment manufacturers need support in improving the quality and competitiveness of their products. This includes addressing challenges such as limited access to capital, high operational costs, outdated manufacturing methods, and insufficient skills and capacity-building opportunities,” the report adds.

The report recommends the fostering of a conducive ecosystem to enhance support structures and systems for local manufacturers through organizations like the Small Industries Development Organization (SIDO) and the Centre for Agricultural Mechanization and Rural Technology (CAMARTEC).

This includes providing access to modern tools, skills training, and policy incentives to stimulate innovation and growth in local equipment manufacturing,” the report says.

Engineer Victor Byanjweli is a horticulture farmer based in Iringa and the Regional Coordinator for Irrigation and Mechanization who believes the idea behind Kilimotech Accelerator being implemented by AGRA in collaboration with Sahara Accelerator is a huge investment in smallholder farmers’ future.

First I commend the whole idea of promoting mechanization amongst smallholder farmers, empowering the farmers and people with innovative ideas at the grassroots is huge in itself because it will do more than increase productivity,” he says.

He added that the problem is not only in the use of modern implements and machinery but also there is a serious shortage of operators and workshops.

As such my first impression of what Sahara Accelerator wants to bring to the table is a great leap forward by any stretch and we are looking forward to working with them,” he adds.

AGRA is an African-led institution with the vision to contribute to a food system-inspired inclusive agricultural transformation across Africa, to reduce hunger, improve nutrition, and adapt to climate change.

The institution’s mission is to transform the lives of smallholder farmers from that of a solitary struggle for survival to a business that thrives.

Since 2006, it has worked with our partners, governments, non-governmental organizations, private sector businesses, and more; to deliver a set of proven solutions to smallholder farmers and indigenous African agricultural enterprises.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive