A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Sunday, January 19, 2025

Benki ya Akiba yakabidhi zawadi kwa washindi wa kampeni ya 'Twende Kidigitali'


Benki ya Akiba imewashukuru wateja wake kwa kushiriki katika kampeni 'Twende Kidigitali' na kuwahimiza kuendelea kutumia huduma zake za kidijitali kama vile ACB Mobile, Internet Banking, ACB VISA Card na ACB Wakala ili kufurahia uzoefu wa kipekee wa huduma za kibenki.


Shukrani hizo zimetolewa jijini Dar es salaam Januari 2025 na Mkuu wa Kitendo cha Biashara wa benki hiyo, Dkt. Danford Muyango wakati wa hafla ya kuwazawadia washindi wa droo ya kwanza ya kampeni ya hiyo ambapo wateja kadhaa kutoka Dar es Salaam na mikoani wamekabidhiwa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha zilizowekwa moja kwa moja kwenye akaunti zao kupitia Benki ya Akiba.


"Kampeni ya 'Twende Kidijitali' ilizinduliwa mwezi Desemba 2024 kwa lengo la kuboresha mazingira ya kibenki kwa wateja wakati wa msimu wa sikukuu na pia kuwasaidia wateja kushinda changamoto za kifedha mwezi huu wa Januari kupitia zawadi mbalimbali" amesema Danford.
Wateja walionyesha furaha na shukrani kwa Benki ya Akiba kwa jitihada zake za kuimarisha huduma za kidijitali ambazo zimeboresha uzoefu wao wa kibenki kwa kuwapatia urahisi na wepesi wa kupata huduma za kifedha wakiwa mahali popote na wakati wowote.


Mmoja wa wateja wa waliokabidhiwa zawadi na Benki ya Akiba ni Alfayo Zephania ambaye alieleza jinsi alivyopokea furaha habari njema za kuibuka mshindi wa kampeni hiyo.


"Nilifurahishwa sana na tarifa ya ushindi wangu na ninaishukuru Benki ya Akiba kwa kujali wateja wake na kutoa huduma bora. Natoa rai kwa wateja wengine kujiunga na Benki ya Akiba ili kunufaika na huduma bora ikiwemo mikopo ambayo imenivusha pakubwa katika biashara zangu” alisema Zephania.


Mteja mwingine, Ezekiel Willium alielezea furaha yake kwa zawadi aliyoshinda, akisema ushindi huo umempa hamasa zaidi ya kushiriki kwa bidii ili kupata zawadi kubwa zaidi katika droo kuu ya mwisho wa kampeni hiyo ya 'Twende Kidigitali'.


Pia Benki ya Akiba imewashukuru wateja wake kwa kushiriki katika kampeni hiyo na kuwasihi waendelee kutumia huduma za kidijitali za benki hiyo ili kunufaika zaidi.


Meneja Mwandamizi Benki ya Akiba, Magreth Mwasumbi (kulia) akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wateja wa benki hiyo walioibuka washindi wa kampeni ya 'Twende Kidigitali'.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive