A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Monday, June 24, 2024

ACI Financial Markets Association of Tanzania Strengthens Stakeholder Engagement and Collaboration

ACI FMA Tanzania President, Ms. Naomi Mafwiri (second from left), exchanges ideas with some of the leaders of the ACI FMA in Dar es Salaam recently, shortly after concluding their meeting which discussed the achievements of the association over the 100 days since their leadership came into power. This included setting various strategies to ensure the institution fulfills its set goals. Ms. Naomi affirmed the association’s commitment to strengthening stakeholder engagements and fostering a collaborative environment within the financial markets arena. From left are Mr. Lawrence Mlaki, Treasurer, Mr. Nicholas Mkisi, Vice President, and Ms. Catherine Mwita, Secretary of ACI FMA Tanzania.

By special correspondent, Dar es Salaam

The ACI Financial Markets Association of Tanzania has affirmed its commitment to strengthening stakeholder engagement and fostering a collaborative environment within the financial markets arena.

Speaking in Dar es Salaam during the association’s leadership team strategic meeting at the weekend, marking the charter’s first 100 days in office, ACI FMA Tanzania charter President Ms. Naomi Mafwiri Rhubera highlighted the substantial strides the new team has made in supporting financial market players while upholding rigorous ethical standards.

"One of the key initiatives we have undertaken during our first 100 days includes proactive engagement with the Bank of Tanzania (BoT) to ensure strict adherence to the 'FX Code of Conduct 2024'. Through a series of physical and virtual meetings, all stakeholders have been sensitized and briefed on this critical framework. Amid challenges such as the scarcity of the greenback, ACI FMA Tanzania has collaborated closely with stakeholders to enhance forex liquidity by implementing crucial measures," said Ms. Naomi.

Ms. Naomi also mentioned several impactful training sessions, notably a comprehensive exploration into the derivatives space led by market expert Brian Onyino, the Senior Financial Services Executive from Nairobi, Kenya. Additionally, the ACI Dealing Certificate training, facilitated by essential partner Petter Skerritt & Associates from Johannesburg, South Africa, has equipped market participants with essential skills for global market operations.

"Going forward, plans include further training sessions, panel discussions, and social gatherings aimed at promoting networking and addressing ongoing challenges," Ms. Naomi added.

She also emphasized the leadership team's 'open door policy', encouraging feedback and collaboration from financial market players to achieve shared goals and enhance ACI FMA Tanzania.

ACI FMA Tanzania is a non-profit organization under the umbrella of ACI FMA. The aim of ACI FMA Tanzania is to influence industry behavior and support best market practices by providing access to relevant training, engagements, and professional certifications in the attempt of creating ethical and professional financial markets practitioners.
ACI FMA Tanzania President, Ms. Naomi Mafwiri (second from left), shakes hands with ACI FMA Tanzania Treasurer, Mr. Lawrence Mlaki, in Dar es Salaam recently, shortly after concluding their meeting which discussed the achievements of the association over the 100 days since their leadership came into power. This included setting various strategies to ensure the institution fulfills its set goals. Ms. Naomi affirmed the association’s commitment to strengthening stakeholder engagements and fostering a collaborative environment within the financial markets arena. Looking on are the Association’s Vice President, Mr. Nicholas Mkisi, and Ms. Catherine Mwita, Secretary of ACI FMA Tanzania.
ACI FMA Tanzania President, Ms. Naomi Mafwiri (second from left), shakes hands with ACI FMA Tanzania Secretary, Ms. Catherine Mwita, in Dar es Salaam recently, shortly after concluding their meeting which discussed the achievements of the association over the 100 days since their leadership came into power. This included setting various strategies to ensure the institution fulfills its set goals. Ms. Naomi affirmed the association’s commitment to strengthening stakeholder engagements and fostering a collaborative environment within the financial markets arena. Looking on are the Association’s Treasurer, Mr. Lawrence Mlaki (left), and Mr. Nicholas Mkisi, ACI FMA Tanzania Vice President
Share:

Sunday, June 16, 2024

WAZIRI WA AFYA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA KIDO BALOZI WA KAMPENI YA HOLELA-HOLELA ITAKUKOSTI

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akipokea Zawadi kutoka kwa KIDO ambaye ni balozi wa kampeini ya Holela-Holela itakukosti mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo leo Jijini Dodoma. Kampeni ya Holela-Holela Itakukosti inazingatia udhibiti kuhusu usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa (UVIDA) na magonjwa ya kipaumbele ya zuonotiki (magonjwa ambayo yanaweza kuambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa wanadamu) na inaratibiwa na ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Wizara ya Mazingira, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID). Kampeni ya Holela-Holea Itakukosti inasisitiza mbinu kamilifu ya “Afya Moja" kushughulikia tatizo la UVIDA na magonjwa ya zuonotiki. Holela-Holela ilizinduliwa mwishoni mwa mwezi uliopita ikiwa ni ushirikiano ya Ofisi ya Waziri Mkuu Wizara ya Afya, Wizara ya Mazingira, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).

Dodoma Jumamosi 15 Juni 2024

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanyia mazungumzo na KIDO ambaye ni balozi wa kampeni ya Holela-Holela itakukosti. Kampeni ya Holela-Holela itakukosti inasisitiza mbinu kamilifu ya "Afya Moja" kushughulikia tatizo la UVIDA na magonjwa ya zuonotiki na ilizinduliwa Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi uliopita kwa uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana Wizara ya Afya, Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Wizara ya Mazingira huku ikifadhaliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kupitia mradi wa Breakthrough ACTION.

Akizungumza leo Jijini Dodoma baada ya kufanyia mazungumzo na balozi KIDO, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alisisitiza juu ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa (UVIDA) na magonjwa ya kipaumbele ya zuonotiki (magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu) ambayo kampeini ya Holela-Holela Itakukosti imelenga. ‘Naomba nichukue fursa hii nitoe wito kwa jamii kuwa Mtanzania anaweza kufanya mambo machache tu kukabiliana na UVIDA, kama vile kupata na kufuata ushauri wa mtaalamu wa afya kabla ya kutumia dawa, kutumia dozi ya dawa kikamilifu kama unavyoshauriwa na mtaalam wa afya, kufuata maelekezo ya mtaalam wa mifugo/kilimo juu ya matumizi sahihi ya dawa kwa mifugo/mimea, na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na usafi wa mazingiria kwa ujumla’.

Waziri Ummy aliongeza, ‘Suala la UVIDA ni tatizo kubwa sana, na athari zake ni kama vile ugonjwa kujirudia rudia na kuchukua muda mrefu kupona, kuenea na kusambaa kwa vimelea sugu vya magonjwa dhidi ya dawa, ulemavu na hata kifo. Mbali na hapo kuna athari za kiuchumi kama vile kutumia gharama kubwa kwenye matibabu, hivyo kupungua kwa pato binafsi, la familia na taifa’.

Waziri Ummy alisema kuwa Serikali inafanya jitihada kabambe za kukabiliana na UVIDA, ikiwemo kuzindua kampeni ya “Holela Holela itakukosti”, inayolenga kuongeza uelewa juu ya UVIDA na kuleta mabadiliko chanya ya tabia ili kukabiliana na UVIDA katika jamii. Pamoja na kampeni hiyo upo mpango kazi wa mapambano ya UVIDA (NAP AMR 2023-2028), na kamati ya Taifa ya Mapambano ya UVIDA (AMR MCC) inayofanya kazi chini ya mwamvuli wa Afya moja. Vilevile kuna miongozo mbalimbali ya Kisekta inayosaidia katika mapamabano ya UVIDA

Kwa Upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa USAID nchini Tanzania Alex Klaits alisisitiza umuhimu wa juhudi za pamoja, akisema, "Kampeni inaonyesha jukumu muhimu la ushirikiano katika kuleta athari chanya na kuhakikisha uendelevu wa muda mrefu, ikiwaleta pamoja wadau wa Afya moja kutoka sekta mbalimbali kupambana na UVIDA na magonjwa ya zuonotiki.
Share:

Wednesday, June 12, 2024

Absa Bank Tanzania yazindua Huduma ya Mikopo ya Magari Ili Kusaidia Wateja Kununua Magari Mapya na yaliyotumika

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere (katikati), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya mikopo ya magari ya benki hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Absa, Bwana Beda Biswalo na Mkuu wa Kitengo cha Mikopo, Bi. Patricia Nguma.

Absa Bank Tanzania imeendelea kuthibitisha kuwa mstari wa mbele katika uvumbuzi wa bidhaa na huduma kwa kuzindua Huduma ya Mikopo ya Magari (VAF) kwa lengo la kufanya umiliki wa magari kuwa rahisi na nafuu zaidi kwa wateja wake.

Huduma ya Mikopo ya Magari ya Absa (VAF) ni suluhisho la kifedha la muda wa kati lililobuniwa kusaidia wateja wa benki kununua magari mapya na yaliyotumika kutoka kwa wauzaji wa ndani bila hitaji la kuwa na fedha zote za malipo mkononi. Suluhisho hili linaakisi mkakati wa benki wa kutoa suluhisho za kifedha zinazowiana na maisha na matarajio ya wateja wake.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Absa VAF, Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Bank Tanzania, Bi Ndabu Swere, alisema, “Tunafurahia sana kuzindua huduma ya Mikopo ya Magari. Hii ni ishara ya kujitolea kwetu kusikiliza wateja wetu na kutatua changamoto na mahitaji yao. Tunaelewa kwamba kununua gari si rahisi kwa sababu magari si rahisi, na kwa kuwa watu hawana fedha taslimu wakati wote, wanaweza kuhitaji msaada kutoka mahali pengine hasa wakati wauzaji wa magari wanahitaji malipo mapema. Hapa ndipo Mpango wa Mikopo ya Magari wa Absa unapoingia.

Kupitia Absa VAF, wateja wetu watafurahia ufadhili wa hadi 90% kwa magari mapya, na hadi 80% kwa magari yaliyotumika ambapo gari lililonunuliwa kwa mkopo linatumika kama dhamana. Bidhaa hii inatoa faida nyingi kwa wateja wetu, ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wateja kupata fedha za kununua gari la chaguo lao wakati ambapo hawana fedha zote mapema. Inawaachia wateja uhuru wa kutumia fedha zao kwa uwekezaji au kwa gharama zisizotarajiwa zinazoweza kujitokeza wakati wa mwaka. Inampa mteja kupata gari lake mara tu benki inapokamilisha mchakato wa mkopo wa VAF. Inapunguza mzigo wa kifedha kwa mteja kwa kumruhusu kulipia gharama kwa awamu ndogo ndogo za kawaida na mteja anahitajika tu kutoa kiasi kidogo cha malipo ya awali.”

Kwa upande wake, Bw. Beda Biswalo, Meneja wa Masoko na Mawasiliano wa benki, alisema, “Suluhisho letu la Mikopo ya Magari sio tu nyongeza ya kimkakati ya kibiashara kwa huduma zetu, lakini pia lina uhusiano wa kina na Ahadi yetu ya Chapa inayosema, ‘Story Yako ina Thamani’. Katika Absa tunajali sana Story za wateja wetu na maendeleo wanayopata katika maisha. Tunavutiwa na safari za wateja wetu na tunataka kuwa sehemu ya maandiko yao, sehemu ya Story za kweli watakazopaswa kuhadithia kwa miaka mingi ijayo wanaposimulia safari zao za mafanikio. Tunaamini kwamba tunapowasaidia wateja wetu kupata vitu wanavyohitaji ili kuboresha ubora wa maisha yao, tunaishi lengo letu la kuiwezesha Afrika ya kesho, pamoja, hatua moja baada ya nyingine.

Katika hitimisho lake, Bi Swere aliwashukuru wateja wote wa benki na kuwataka Watanzania wote kuchukua fursa hii nzuri, akisisitiza kuwa upatikanaji wa huduma hii ni rahisi sana na haina usumbufu. Inaanza na mteja kuchagua gari analopenda kununua kutoka kwa moja ya wauzaji wetu wa magari walioteuliwa kwa makini, kisha kuomba huduma ya VAF kupitia maafisa wetu wa mikopo, tunapopitia ombi la mteja, kama mteja amekidhi vigezo ataombwa kufanya malipo ya awali katika akaunti ya Absa, Absa italipa malipo kamili (malipo ya awali + salio lililobaki) kwa muuzaji wa gari, mteja atapewa gari lake kufurahia safari yake mpya.

Mchakato wetu wa maombi ni wa haraka, rahisi, na wa gharama nafuu, unampa mteja utulivu wa akili, kwani tunasimamia kila kipengele, kuanzia kutambua wauzaji wa magari wanaoaminika hadi kuhakikisha magari yaliyokusudiwa yanakidhi viwango vya juu kupitia mpango madhubuti wa ukaguzi. Tumeingia makubaliano na wasambazaji na wauzaji wa magari wanaoaminika, ambao watakuwa wasambazaji wakuu wa magari mapya na yaliyotumika yaliyochaguliwa kwa wateja wetu. Pia tunahakikisha usimamizi wa mwanzo hadi mwisho, ikiwa ni pamoja na malipo ya kodi husika za serikali, ada za uhamisho, na bima kwa niaba ya mteja, ikimruhusu mteja kuzingatia mambo muhimu zaidi anapoendelea kuandika kurasa ya safari yake ya mafanikio.” alihitimisha.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Patricia Nguma (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya mikopo ya magari ya benki hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wengine kulia kwake ni, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Swere na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Absa, Bwana Beda Biswalo.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Beda Biswalo (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya mikopo ya magari ya benki hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wengine kushoto kwake ni, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Swere na Mkuu wa Kitengo cha Mikopo, Bi. Patricia Nguma.
Share:

Saturday, June 8, 2024

WABUNGE WANAWAKE NA KAMPUNI YA ORYX TANZANIA WAMPONGEZA RAIS SAMIA.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Gas kama Benoit Araman (wanne kushoto), akisoma ujumbe uliondikwa katika Tuzo ya Rais Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Kampuni hiyo kwa ajili ya kutambua mchango wa Rais katika kuhimiza matumizi ya Nishati Safi ya kupikia.Tuzo hiyo imepokelewa na Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson leo wakati wa Mashindano ya Siku ya Nishati Safi ya Kupikia Duniani ambapo kwa Tanzania Oryx wameshikiana na Wabunge wanawake kuadhimimisha siku hiyo

WABUNGE wanawake nchini kwa kushirikiana na Kampuni ya Oryx Gas Tanzania wametoa tuzo kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kutambua mchango wake katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Tuzo hiyo kwa Rais Dk. Samia imetolewa leo Juni 7, 2024 Mjini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Nishati Safi ya Kupikia Duniani ambapo Oryx, wabunge wanawake, wabunge vinara katika nishati safi wametumia maadhimisho hayo kujadili kwa kina mchango wa Rais Dk. Samia katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia Afrika, hususan Tanzania.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson aliyekuwa mgeni rasmi, amesema kuna kila sababu kwa wabunge na Oryx kumpa tuzo Rais Dk. Samia kwa kuwa amekuwa kinara wa nishati safi ya kupikia na juhudi zake zinashuhudiwa na Watanzania, Afrika na dunia kwa ujumla.

Amesema Rais Samia alipokuwa nchini Dubai na hivi karibuni aliposhiriki mkutano kuhusu nishati safi ya kupikia Paris, Ufaransa ametambuliwa kuwa kinara wa nishati hiyo.
Hivyo wanaendelea kusisitiza Dk. Rais Samia ndiye kinara wa nishati safi ya kupikia.

Amesema katika Bara la Afrika kunachangamoto ya nishati ya kupikia na takwimu zinaonesha asilimia 80 ya wananchi barani humo wanatumia nishati isiyo safi ya kupikia na kwamba kutoka katika nishati hiyo itachukua muda. 

“Hivyo Rais Dk. Samia anasaidia kupunguza muda kwa kuendelea kutafuta fursa kubadilisha upikaji kwa kuacha kutumia nishati chafu na kuhamia katika nishati safi ya kupikia kama gesi.

“Juhudi hizo za Rais zimeanza Tanzania na takwimu nchini zinaonesha asilimia 90 ya wananchi hadi sasa wanatumia nishati isiyo safi ya kupikia.

“Hivyo juhudi za Rais zinatusogeza angalau kutoka asilimia 90 na kusogea hadi 25 ili wawe wachache wanaotumia nishati chafu ya kupikia,” amesema.

Akifafanua zaidi Dk. Tulia amesema wanafahamu nishati isiyo safi ina madhara kwa binadamu na kwa nchini takwimu zinaonesha vifo takribani 33,000 hutokea kila mwaka kutokana na athari za kutumia nishati isiyofaa, hivyo kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Amesema mbali na vifo, kutumia nishati chafu kumekuwa kukisababisha athari za mazingira na kijamii huku akitumia nafasi hiyo kueleza namna ambavyo wanawake na mabinti wamekuwa wakitumia muda mwingi kutafuta kuni na mkaa badala ya kufanya shughuli za maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman amesema kwa kutambua mchango wa Rais Samia katika nishati safi wameamua kumpa tuzo kumuunga mkono juhudi zake za kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo.

Benoit amesema tuzo hiyo ina ujumbe usemao “Kampuni ya Oryx Energies inatoa tuzo hii kwa Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutambua uongozi wake wa kipekee katika kushinda na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini Tanzania na Afrika.”

Akitoa ahadi ya kampuni hiyo, amesema hadi sasa wameshatoa mitungi ya gesi na majiko yake 35,000 kwa makundi mbalimbali nchini na wataendelea na mkakati wao kwani dhamira yao ni kuona asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2032 inafikiwa kama ambavyo Rais Samia ameelekeza.

Awali Mwenyekiti wa Wabunge Wanawake nchini Shally Raymond, amesema wabunge wanawake pamoja na wabunge vinara wa nishati kwa kushirikiana na Oryx wameamua kutoa tuzo kwa Rais huku akitumia nafasi hiyo kupongeza jitihada zinazochukuliwa na Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia nchini.
Share:

Saturday, June 1, 2024

KAMPUNI YA ORXY TANZANIA YAWAPELEKA WASAMBAZAJI WA VILAINISHI VYA KAMPUNI HIYO DUBAI

 


Na Mwandishi Wetu

WASHINDI wawili wa Shindano la Wauzaji na Wasambazaji wa vilainishi vya Oryx wamejishindia safari ya kwenda Dubai ambapo wamekabidhiwa tiketi zao leo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi tiketi kwa washindi wawili wa shindano hilo Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania Kalpesh Mehta amesema Kampuni ya Oryx Services and Specialties Ltd iliendesha shindano la wauzaji (mawakala) bora wa vilainishi vya Oryx Energies kati ya Maduka ya Oryx na wasambazaji wa Vilainishi vya Oryx.

Amesema shindano hilo lilianza Januari na kumalizika Desemba 2023 na kwamba leo Mei 31, 2024 wametangaza washindi wa shindano hilo ambao ni Mbise Oil Shop iliyopo Arusha (Oryx Shop) na Lwimba Investment Company Ltd iliyopo Dar es salaam (Msambazaji).

Amesema kuwa zawadi wa shindano hilo ni Safari ya kwenda Dubai ambapo leo washindi wao wamekabidhiwa tiketi zao tayari kwa safari huku akifafanua gharama zote za safari hiyo ya siku nne Dubai zimelipiwa na kampuni ya Oryx Services and Specialities Limited. Kila mshindi amepata tiketi mbili kwa ajili ya safari ya Dubai.

"Tunatarajia kutangaza mashindano yafuatayo hivi karibuni ambayo yatakuwa ya kusisimua zaidi kuliko shindano lililopita.Ni matumaini yetu wauzaji wetu wote watashiriki tena vyema kama mwaka uliopita.

"Oryx Energies ni kampuni kubwa na ya muda mrefu ya kimataifa inayotoa huduma za nishati barani Afrika. Oryx Energies huagiza, kuchakata, huhifadhi na kusambaza bidhaa za mafuta ya magari, machine na mitambo (Dizeli, Petroli, Vilainishi) na gesi za kupikia (LPG) zitumikazo katika sekta mbalimbali za uchumi.

"Ni msambazaji namba moja wa bidhaa za mafuta na vilainishi katika sekta ya uchimbaji madini (migodi). Pia Oryx Energies inaongoza kusambaza vilainishi katika sekta zingine za kiuchumi kama usafirishaji wa nchi kavu (pikipiki, magari, treni) na majini, viwandani, ujenzi na kilimo.

Pia Oryx Energies huzalisha na kusambaza vilainishi mbalimbali kuanzia vya magari, mitambo ya migodini na viwandani, uzalishaji wa umeme nk ambavyo vimeidhinishwa na Watengenezaji wakubwa wa Vifaa Halisi (Original Equipment Manufacturers) na vinakidhi au kuzidi viwango vya kimataifa.

Ameongeza katika kuhakikisha bidhaa na huduma zinapatikana kwa watumiaji kote nchini, Oryx Energies inaendelea kuboresha njia zake za usambazaji kwa kupitia Maduka ya Kipekee ya Kampuni (CODOs), Wasambazaji na vituo vya mafuta vya Oryx.

Akizungumza kwa niaba ya washindi , Vaileth Cilwimba kutoka Lwimba Investment Company Ltd jijini Dar es salaam (Msambazaji) amesema ushindani ulikuwa mkubwa lakini anashukuru kituo chao kuibuka washindi kutokana na juhudi wanayofanya katika kukuza bidhaa za Oryx pamoja na kutafuta masoko.

"Tunashukuru kwa kushinda na kupata tiketi kwa ajili ya kwenda Dubai ambapo tumelipiwa kila kitu kwa maana ya gharama zote, kwetu hii inatufanya tuongezee bidii zaidi kwa kuuza zaidi bidhaa bora za Oryx zikiwemo za Vilainishi vya magari,bodaboda na bajaji."

Awali Arthur Awet ambaye ni B2C Key Account Manager Kampuni ya Oryx Services and Specialties Ltd amesema Oryx Services and Specialties LTD iliendesha shindano ya CODO na wasambazaji wao 50 ya kutafuta mtendaji bora wa mauzo katika bidhaa zao zote za vilainishi.

"Leo ni siku ya makabidhiano ya tikiti kwa washindi, ambapo kila duka iliyoshinda imejishindia tiketi mbili ya Kwenda na kurudi Dubai ambayo gharama zote za safari zimelipwa. Safari ya washindi hawa itakua baada ya mwezi wa Ramadhan."
Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania Kalpesh Mehta akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa shindano la wauzaji (mawakala) bora wa vilainishi vya Oryx Energies kati ya Maduka ya Oryx na wasambazaji wa Vilainishi vya Oryx ambapo washindi hao wamezawadiwa tiketi ya kwenda Dubai. Hafla hiyo imefanyika leo Mei 31,2024 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania Kalpesh Mehta akimkabidhi mfano wa zawadi ya tiketi ya Safari ya kwenda Dubai Mwakilishi wa Kampuni ya Mbise Oil Shop iliyopo Arusha (Oryx Shop)(Msambazaji) ambaye ni mshindi wa shindano la wauzaji (mawakala) bora wa vilainishi vya Oryx Energies kati ya Maduka ya Oryx na wasambazaji wa Vilainishi vya Oryx. Zozi la ugawaji wa tiketi hizo limefanyika leo Mei 31,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania Kalpesh Mehta akimkabidhi mfano wa zawadi ya tiketi ya Safari ya kwenda Dubai Vaileth Cilwimba kutoka Lwimba Investment Company Ltd jijini Dar es salaam (Msambazaji) ambaye ni mshindi wa shindano la wauzaji (mawakala) bora wa vilainishi vya Oryx Energies kati ya Maduka ya Oryx na wasambazaji wa Vilainishi vya Oryx. Zozi la ugawaji wa tiketi hizo limefanyika leo Mei 31,2024 Jijini Dar es Salaam.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive