A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Thursday, May 30, 2024

WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI TANGA WAFURAHIA KUJENGEWA VIVUKO VYA WAENDA KWA MIGUU.

  


Na Mwandishi Wetu,Tanga

KATIKA jitihada za kupunguza ajali za barabarani kwa wanafunzi jijini Tanga ,Shirika la Amend kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uswis wamefanikiwa kuweka miundombinu salama barabarani yenye lengo la kuhakikisha wanafunzi wanavuka salama katika safari ya kwenda na kurudi shuleni.

Miundombinu hiyo salama ya barabara imefanyika katika Shule ya Msingi Makorora pamoja na Shule ya Msingi Azimio kwa kuwekewa vivuko vya Pundamilia, njia za watembea kwa miguu pamaja na alama muhimu za usalama barabarani.

Akizungumza kuhusu mradi huo wa miundombinu salama ya barabara, Mkurugenzi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo amefafanua mradi huo umehusisha ujenzi wa njia za watembea kwa miguu, vivuko 4 vya pundamilia, matuta saba ya kupunguza mwendo kasi, alama 15 za barabarani, na michoro 16 ya usalama barabarani.

Pia wametoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi 1,694 na walimu wa shule za msingi Makorora na Azimio ndani ya mwezi tano, 2024 Tanga na Tanzania kwa ujumla.

Kalolo amesema mpango wa kuboresha miundombinu salama ya watembea kwa miguu ni sehemu ya mradi wa mwaka mmoja unaoitwa "Usalama wa Pikipiki kwa Vijana Tanzania".

Amesisitiza mradi huo unaungwa mkono na Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania na una bajeti ya Sh. 424,983,396 huku akifafanua tangu Septemba 2023, shughuli nyingine za mradi zimejumuisha mafunzo ya waendesha pikipiki 300 jijini Tanga, waendesha pikipiki 253 Dodoma.

Pia kampeni a uhamasishaji kuhusu masuala ya usalama wa pikipiki, na kuanzishwa kwa 'Kanuni za Maadili' kwa madereva, Waendesha pikipiki 200 zaidi watapewa mafunzo jijini Tanga ifikapo Juni 2024 na tathmini ya athari za shughuli hizo zote inafanywa hivi sasa.

“Ajali za barabarani ndiyo chanzo kikuu cha vifo vya watoto na vijana wenye umri kati ya miaka 5 na 29 duniani kote nchini Tanzania na kuna zaidi ya majeruhi 330,000 wa ajali za barabarani kwa mwaka ambayo ni ya juu kuliko wastani katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara”amesema.

Amesema mradi huo wa kuokoa maisha unaonesha ajali za barabarani zinaweza kuzuilika kazi hiyo iliyoungwa mkono na Fondation Botnar na sasa Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania, itaendelea kupunguza ajali za barabarani na kuokoa maisha.

Ameongeza kupitia Mpango Kazi wao wa Usafiri Salama na Endelevu kwa Jiji la Tanga, wanalenga kuhakikisha kila mtoto wa Tanga anakuwa na safari salama ya kwenda na kurudi shuleni.

“Hakuna sababu ya kuchelewa kuchukua hatua hili linahitaji kuwa kipaumbele cha juu kwa watunga sera wetu na Tanga ina uwezo wa kuongoza nchi na bara letu katika kukabiliana na chanzo hiki kikibwa cha vifo kwa vijana,”alisema

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Tanga Dalmia Mikaya aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji , amepongeza kutekelezwa kwa mradi huo wa miundombinu ya barabara katika Shule hiyo Makorora na Azimio na matamio yao ni kuona mradi wa usalama barabarani unakwenda katika shule zote za Tanga.

Pia amewaomba wazazi na walezi kuhakikisha wanawalinda wanafunzi dhidi ya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia.Tunafahamu suala la usalama barabarani ni muhimu lakini tuweke nguvu kusimamia usalama dhidi ya ukatili wanaofanyiwa katika jamii zetu.”

Kwa upande wake Mwakilishi wa Ubalozi wa Uswisi Rashid Mbaramula ambaye anashughulikia Miradi amesema nchi Uswis inahistoria kubwa wa kimahusiano na Tanzania na Jiji la Tanga ni miongoni mwao huku akifafanua kuanzia mwaka 1960 Uswis imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo na imekuwa ilishiriki kikamilifu katika kufanikisha Miradi ya maendeleo.

Amesema kupitia mradi huo madereva bodaboda zaidi ya 550 wamepatiwa mafunzo ya usalama barabarani na kufanikiwa kwa mradi huo kunatokana na ushirikiano wa wadau mbalimbali huku akiwapongeza Amend kwa kazi kubwa wanayofanya ya kutoa elimu ya usalama barabarani.

Awali Inspekta wa Jeshi la Polisi Rajab Mhumbi aliyemwakilisha Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga amesema vivuko vya barabarani ambavyo vimewekwa na Amend ni vema vikalindwa na kila mmoja wetau na si jukumu la wanafunzi na walimu peke yao.



Share:

Monday, May 27, 2024

KAMPUNI YA ORYX TANZANIA YAGAWA MITUNGI 800 KWA WANANCHI WA JIOMBO LA BABU TALE MOROGORO.

   

MITUNGI 800 ya gesi ya Kampuni ya Oryx Gas Tanzania ikiwa na makiko yake, imetolewa bure kwa wananchi wa Jimbo Morogoro Kusini Mashariki kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.


Mitungi hiyo imetolewa kwa ushirikiano wa Kampuni ya Oryx na mbunge wa kimbo hilo Hamisi Taletale (Babu Tale) katika mkutano mkuu wa CCM Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki mgeni rasmi akiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana.

Akizungumza kabla ya kukabidhi mitungi hiyo Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulurahman Kinana amempongeza Mbunge Taletale kwa kushirikiana na wadau kugawa mitungi hiyo kwa wananchi hao kwani ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Dk Samia Suluhu Hassan

Amesisitiza Rais Samia ameanzisha kampeni ya nishati safi yenye lengo la kumtua mzigo wa kuni mwanamke na hatimaye kumpa muda mwingi katika kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo hasa kwa kutambua mwanamke ndio nguzo ya familia.

“Kampeni hii ya nishati safi ni matokeo ya sera na ubunifu kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Mwaka jana alianzisha mchakato wa kuwatua akina mama mzigo wa kuni.

"Hivyo katika kufanikisha kampeni hiyo Serikali peke yake haitaweza kwasababu inahitaji fedha nyingi,hivyo nikupongeze Taletale kwa kuunga mkono jitihada za Rais katika kampeni hii,kwani tutakabidhi mitungi ya gesi kwa wananchi,lakini niwapongeze wadau wa gesi kwa kushiriki katika kufanikisha kampeni hii yenye lengo la kumtuamzigo wa kuni mwanamke,"amesema Kinana

Wakati huo huo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Gesi ya Oryx Tanzania, Benoite Araman, Meneja wa Mifumo ya Gesi yenye Matumizi Makubwa Oryx Gas Tanzania LTD, Richard Sawere amesema hatua ya kushirikiana na Mbunge Taletale kugawa mitungi hiyo ni hatua hiyo ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk. Samia.

Amesema Rais Dk.Samia amedhamiria ifikapo mwaka 2030 asilimia 80 ya Watanzania wawe wananatumia nishati safi ya kupikia huku akifafanua Kampuni ya Oryx pia umeamua kunusuru uharibifu wa mazingira na kulinda afya za wananchi kwa kutumia nishati safi na rafiki kwa afya za wananchi.

"Nchini Tanzania, wananchi 33,000) wanapoteza maisha kila mwaka kwa kuvuta moshi na chembe chembe zinazotokana na mkaa na kuni. Kupika na gesi ya Oryx itatatua jambo hili," amesema.

Awali akitoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitungi na majiko hayo, Meneja Masoko wa kampuni hiyo Peter Ndomba amesema sera ya kampuni hiyo ni kuhakikisha nchi nzima inatambua umuhimu wa kutumia gesi.

 "Hii ni kampeni ya kitaifa ambayo Rais Samia Suluhu Hassan aliizindua kwa lengo la kuhakikisha kwamba miaka 10 ijayo zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi".

 Katika hatua nyingine Mbunge wa amesema kuwa Rais Samia ameelekeza kutekelezwa kwa kampeni ya nishati safi,hivyo Wana Morogoro Kusini Mashariki wameona Kuna kila sababu ya kumuunga mkono Rais Samia kwa vitendo kwa kutumia nishati safi ya kupikia inayotokana na gesi ili kuachana na kuni na mkaa.










Share:

Wednesday, May 15, 2024

Absa Dar City Marathon 2024 donates hospital equipment to Mnazi Mmoja Hospital

Absa Bank Tanzania Head of Marketing and Corporate Affairs, Mr. Aron Luhanga hands over a part of hospital equipment to Mnazi Mmoja Hospital In-charge, Dr. Delila Moshi (centre), at a function in Dar es Salaam yesterday. Looking on is the bank's Digital Marketing Manager, Mr. Albert Longfellow.

Absa Dar City Marathon donated hospital equipment to Mnazi Mmoja Hospital’s reproductive and child health (RCH) clinic in Dar es Salaam to support the government efforts to provide quality health services to all Tanzanians.

This follows from the successful event that was held on 5 May 2024 in Dar es Salaam. The occasion was running in parallel with a blood donation campaign organized by The Runners Club with the support of the marathon sponsors, partners, vendors, services providers and the general public.

The handover of the hospital equipment was attended by In-charge of Mnazi Mmoja Hospital, Dr. Delila Moshi, Ilala Municipal RCH Coordinator, Dr. Milka Mathania, leaders and members of The Runners Club and representatives of the sponsors of the marathon, Absa Bank Tanzania Limited, Hill Water, Alliance Life Assurance Limited and Gardaworld Security Services Limited.

Speaking at the occasion, Dr. Delila expressed her gratitude to Absa Dar City Marathon for choosing Mnazi Mmoja Hospital for the second consecutive year as their preferred institution for their charitable donation and urged them to continue supporting the hospital in the coming marathons.

She also praised The Runners Club blood donation campaign, informing that lack of adequate blood is one of the major challenges of the hospital which admits more than 200 expecting mothers in the maternity ward and attends to more than 400 children daily in the RCH clinic.

On her side, the Ilala Municipal RCH Coordinator, Dr. Milka advised that RCH is one of the major challenges of public health in Dar es Salaam and urged The Runners Club to continue with this initiative for the greater benefit of the community.

The spokesperson of The Runners Club, Mr. Godphrey Mwangungulu informed the audience that Absa Dar City Marathon that was held on Sunday, 5 May 2024 at Mnazi Mmoja Grounds, Dar es Salaam was the 4th edition and attracted more than 2,500 runners in the 21.1km, 10km and 5km race categories.

Theme of the marathon was aligned with the Club’s vision of healthy lifestyles and the donation of hospital equipment to Mnazi Mmoja Hospital RCH Clinic was to fulfil that vision.

The selection of Mnazi Mmoja Hospital was in line with the saying that charity begins at home given the close proximity of the hospital to Mnazi Mmoja Grounds, the venue of the marathon for the past four events.

The representative of Absa Bank Tanzania Limited, the main sponsors of the marathon, Mr. Aron Luhanga, who is the bank’s Head of Marketing and Corporate Relations said that Absa supports The Runners Club’s vision of healthy lifestyles through running, and this was one of the main reasons for sponsoring the marathon, which included this charitable donation of hospital equipment. In addition, Absa motivates and promotes healthy lifestyles amongst its staff members and clients through the Absa Health Club.

This donation is also aligned with our Citizenship agenda of being a force for good to our communities and play a major role in the society”, said Mr. Luhanga.

The representative of Hill Water, the sponsors of the 10km corporate run said that supporting the RCH Clinic is aligned with the company objectives particularly in the provision of quality drinking water to the community.

The company is delighted to support the community that has supported them over the years by providing by providing hospital equipment to Mnazi Mmoja Hospital and advocates for the community to live a healthy lifestyle."

This is for the sake of having and a strong and healthy generation for the growth of our country, our company will continue to support deserving charitable activities through its CSR initiatives”.

The representative of Alliance Life Assurance Limited, the sponsors of the 5km family fun run, Ms. Josephine Mfikwa said that the company supports The Runners Club vision of healthy lifestyles and this donation is a demonstration of their commitment to support the health needs of the society.

As a life assurance provider, healthy lifestyles are likely to prevent untimely deaths leading to long and happy lives”, said Ms. Josephine.
Absa Bank Tanzania Chief Internal Auditor, George Binde (second left), hands over medical equipment for Mnazi Mmoja Hospital to Dar es Salaam City Council non-communicable diseases cordinator, Dr Milka Mathania, donated by Absa to support the government efforts to provide quality health services in the country.
Share:

Wednesday, May 8, 2024

Gateway to growth: Absa opens new office in China

Absa Bank Tanzania Acting Corporate Director, Nellyana Mmanyi (right), addresses a media conference about the official opening of the bank's China office during a brief occasion in Dar es Salaam today. She was flanked by Absa Bank Tanzania's Head of Marketing and Corporate Affairs, Mr. Aron Luhanga.

BEIJING, China: 08 May 2024 - Absa Group marks a historic milestone with the official launch of a non-banking subsidiary in the People’s Republic of China, fortifying the vital economic bridge between Africa and China.

The African continent is endowed with talent, mineral wealth and a young population – and is poised to play an increasingly influential role in global trade, as investors recognise its status as the last true frontier in global growth. Through this expansion, Absa Group isn't merely acquiring a new location; we're affirming our dedication to expanding our global presence and playing our part in facilitating growth on the continent,” says Arrie Rautenbach, Group Chief Executive Officer of Absa Group.

The China-Africa investment relationship has flourished over the past few decades, with China emerging as the continent’s largest bilateral trade partner. This has been fuelled by Chinese investment in Africa’s vast natural resources and infrastructure projects, creating huge commercial opportunities for both regions.

Our decision to establish a presence in China was driven by our ambition to better connect trade, investment flows and clients into Africa, where we will serve them across our extensive continental footprint. Absa Group intimately understands the continent and seeks to be a partner of choice for organisations looking to access opportunities on the continent,” Rautenbach continues.

Absa Group’s expansion into China highlights Absa’s client-centric approach, in being able to innately understand their client’s needs. Its office in China will operate under a wholly foreign owned enterprise licence which permits the financial institution to provide general advisory services to clients based in China for concluding transactions across the African continent, as a non-banking subsidiary of Absa Group Limited.

This office allows the Absa Group to provide general advisory services to clients based in China for concluding transactions across the African continent, as well as distribute economic or general securities research reports permitted by Chinese regulation to corporate and institutional clients in China and across the African markets.

The new office will enable Absa Group to offer local support to Chinese clients and stakeholders to conclude transactions across the African continent, helping to support clients’ needs, goals, and ambitions. This is part of a wider commitment from Absa to expand its operations with an international presence in strategic markets and offer deep expertise in African markets to its overseas clients,” says Charles Russon, CE of Absa Corporate & Investment Bank.

He goes on to say, “Our presence in China will help to firmly establish Absa’s capability to provide general advisory services to clients based in China for concluding transactions across the African continent. This will not only give us a physical presence in the region but also help us to meet the needs of our clients operating in this rapidly growing market.

Being present in China allows us to be close to clients who see trade and investment in Africa as key to their strategic ambitions”, concludes Russon.

About Absa Group Limited

Absa Group Limited (‘Absa Group’) is listed on the Johannesburg Stock Exchange and is one of Africa’s largest diversified financial services groups. Absa Group offers an integrated set of products and services across personal and business banking, corporate and investment banking, wealth and investment management and insurance. Absa Group owns majority stakes in banks in Botswana, Ghana, Kenya, Mauritius, Mozambique, Seychelles, South Africa, Tanzania (Absa Bank Tanzania and National Bank of Commerce), Uganda and Zambia and has insurance operations in Botswana, Kenya, Mozambique, South Africa and Zambia. Absa also has representative offices in China, Namibia, Nigeria and the United States, as well as securities entities in the United Kingdom and the United States, along with technology support colleagues in the Czech Republic.

For further information about Absa Group Limited, visit www.absa.africa.

For further information about Absa Corporate and Investment Banking (CIB), visit www.cib.absa.africa.

Media enquiries or to request interviews: PRmedia@absa.africa
Share:

Sunday, May 5, 2024

Absa Dar City Marathon 2024 zatimua vumbi jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Aron Luhanga (kushoto), akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za nusu marathon (Km 21) za Absa Dar City Marathon kwa upande wa wanaume, Dickson Paul kutoka Mwanza, mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Absa, Bi. Ndabu Lilian Swere.

*Benki ya Absa yaahidi kuendeleza udhamini wake

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MBIO za Absa Dar City Marathon 2024 zimetimua vumbi lake jijini Dar es Salaam jana katika hali ya hewa ya utulivu mara baada ya tishio la kimbunga Hidaya kupoteza uwezo wake Kwa mujibu wa taarifa kutoka mamlaka husika hivyo kuwafanya wakimbiaji kufurahia mandhari nzuri za jiji mashuhuri la Tanzania.

Ikiwa ni mara ya nne kufanya mbio hizi chini ya udhamini mkuu wa Benki ya Absa Tanzania, mtifuano huo ulishuhudia wanariadha zaidi ya 3000 wakifukuza upepo katika mitaa ya katikati ya Jiji hilo katika mbio hizo ambazo licha ya lengo lake kuu kuwa ni kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba kwa ajili ya Wodi ya wanawake ya Hospitali ya Mnazi Mmoja, lakini lingine ilikuwa ni kutangaza vivutio vya utalii vipatikanavyo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kufanyika mbio hizo, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Aron Luhanga alisema kutokana na mafanikio ya mbio hizo, Benki Yao itaendelea kuwepo kwa kipindi kirefu katika kudhamini mbio hizo.

Kama ahadi ya chapa yetu isemayo Tunadhamini Story Yako, Benki ya Absa itaendelea kuthamini story za maisha ya watanzania, kwani sehemu ya mapato ya mbio hizi yatakwenda kusaidia jamii kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba kwa ajili ya wanawake na watoto.

Absa tunaamini kuwa mtu yoyote anaweza kuandika story yake kutokana na mazoezi na kukimbia ni moja ya mazoezi, lakini pia tunaamini utajiri upo kwenye afya, na kukimbia kunaleta afya, hivyo jamii na nchini itapiga hatua kubwa ya kimaendeleo kukiwa na watu wenye afya Bora,Absa tupo kihakikisha Story hizo zinaandikwa kwa ufanisi” alisema Bwana Luhanga.

Akizungumza kuhusu huduma zao za kibenki Bwana Luhanga alisema benki yao imesheheni bidhaa na huduma mbalimbali zenye ubora wa kamataifa ikiwa ni pamoja na akaunti za watoto, mikopo ya nyumba, magari pamoja huduma ya kadi ya mkopo (credit card) ya kipekee nchini kabisa inayomwezesha mteja kupata kadi huyo ikiwa tayari imewekewa kiasi cha pesa cha kuanzia.

Naye Mwenyekiti wa The Runners Club, waandaaji wa Absa Dar City Marathon, Godfrey Mindu aliishukuru Benki ya Absa pamoja na wadhamini wengine kwani kujitoa kwao kunaenda kuleta mabadiliko makubwa kwa maisha ya watanzania.

Dar City Marathon 2024 ilishirikisha mbio za KM 5, 10 na 21 huku kwa upande wa KM 10 wanawake mshindi wa kwanza alikuwa Anastasia Dolomongo kutoka Arusha akitumia muda wa DK 34:04:31, kwa upande wa wanaume mshindi alikuwa Emanuel Shahanga kutoka Hanang akitumia muda wa Dk 29:00:03.

Kwa upande wa mbio za KM 21 za nusu marathon upande wa wanawake, ushindi wa kwanza ulienda kwa Sara Ramadhani kutoka Arusha pia akitumia muda wa Saa 1:13:21:08, huku kwa upande wa wanaume, Dikson Paul kutoka Mwanza akiibuka kidedea kwa kutumia muda wa Saa 1:02:58:04.

Mbali na Benki ya Absa kama mdhamini mkuu, wadhamini wengine ni Kampuni ya Alliance Life Assurance, Hill Water, Kilimanjaro Milk na Kampuni ya Garda Security.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (kushoto), akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za nusu marathon (Km 21) za Absa Dar City Marathon kwa upande wa wanawake, Sara Ramadhani kutoka Arusha, mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki wa Absa, Bwana Aron Luhanga.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (kushoto), akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza wa mbio za KM 10 za Absa Dar City Marathon kwa upande wa wanawake, Anastasia Dolomongo kutoka Arusha, mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki wa Absa, Bwana Aron Luhanga.
Share:

Saturday, May 4, 2024

Uzinduzi wa Sinza Kwa Wajanja Marathon watikisa Dar

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge (katikati), Diwani wa Kata ya Kijitonyama, Dama Lusangija, Mkuu wa Kituo cha Polisi Mabatini, ASP Soty Mtaki na mhamasishaji maarufu wa mtandaoni, Dotto Magari (kushoto), wakikata utepe kuzindua Sinza Kwa Wajanja Marathon 2024, jijini Dar es Salaam jana.

*Kusaidia wodi ya wazazi ya Hospitali ya Palestina

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.

Uzinduzi wa mbio za Sinza Kwa Wajanja Marathon umefanyika jijini Dar es Salaam jana katika hafla iliyopambwa na shamrashamra mbalimbali huku mgeni rasmi akiwa ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge.

Sinza Kwa Wajanja Marathon inatarajiwa kufanyika Juni 16 mwaka huu katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama, wilayani Kinondoni huku wanariadha wakichuana katika mbio zenye umbali wa kilomita tano, 10 na 21 (nusu marathon), kulingana na mwenyekiti wa Klabu ya Marafiki wa Sinza, Bwana Geofrey Mhando.

Bwana Mhando alisema kwamba usajili wa Sinza Kwa Wajanja Marathon tayari umeshaanza na aliwasihi wadau wa michezo kujisajili ili kushiriki katika tukio hili la kihistoria.

Alisisitiza kwamba mbali ya kukuza maendeleo ya michezo, tukio hilo linalenga kukusanya fedha kusaidia wodi ya uzazi ya Hospitali ya Palestina.

"Tumejitolea kukuza afya njema nchini, ndio maana tumefanya uamuzi wa kuandaa tukio hili, sehemu ya fedha zitakazopatikana zitatumiwa kununua vifaa tiba kwa ajili ya wodi ya uzazi ya hospitali ya Palestina.

Tunatambua umuhimu wa Hospitali ya Palestina ya Sinza katika Wilaya ya Kinondoni, ikiwa msaada mkubwa si tu kwa wakazi wa Sinza bali pia kwa maeneo jirani, ni muhimu kuisaidia," alisema Bwana Mhando.

Aidha alisema mbio hizo zitashirikisha wanariadha wote wa kitaifa na wengineo kwani lengo kubwa hasa si kupata washindi bali ni kusaidia maendeleo ya watanzania wenzetu hususan wanawake na watoto wanaopata huduma za afya katika Hospitali ya Palestina.

"Mbio hizi zinatumika si tu kuunganisha wakazi wa Sinza kutoka maeneo tofauti bali pia kurahisisha kubadilishana mawazo, hivyo, wakazi wa zamani wa Sinza na wengine kutoka ndani na nje ya Sinza wanakaribishwa," aliongeza.

Bwana Mhando pia aliongeza kuwa kabla ya mbio kuanza, tarehe 15 Juni, kutakuwa na hafla ambayo wajasiriamali wataonyesha bidhaa zao kwenye viwanja vya Posta, ikiambatana na shamrashamra mbalimbali za burudani.

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, alipongeza waandaaji wa Sinza kwa Wajanja Marathon kwa tukio hilo litakalochangia kuhamasisha maendeleo ya michezo na afya njema kwa wakazi wa Sinza na maeneo jirani huku akihamasisha wadau wa michezo nchini kushirikiana na waandaaji kufikia malengo yao.

"Hii ni wazo zuri sana, hasa kwa Sinza Kwa Wajanja Marathon, ambayo inafanyika mara ya kwanza, nawasihi wadau wote kusaidia waandaaji na kushiriki kwenye tukio huli," alisema Mstahiki Meya akizindua rasmi tukio hilo.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Kijitonyama, Bwana Dama Lusangija, alisema kwamba mbio hizo zitaongeza hamasa kwa wakazi wa maeneo hayo na maeneo jirani ili kujenga tabia ya kufanya mazoezi na kudumisha afya njema.

"Tunashukuru waandaaji kwa kuandaa mbio hizi, zinazofanyika kwa mara ya kwanza kwa wakazi wa Sinza na maeneo jirani, hili ni tukio la kihistoria ambalo litakuza si tu afya njema bali pia kukuza maendeleo ya michezo," alisema Bwana Lusangija.

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Kituo cha Polisi Mabatini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ASP) Soty Mtaki alisema kuwa wamejiandaa kutoa usalama kwa washiriki wote kabla na wakati wa mashindano.

Baadhi ya wadhamini wa Sinza Kwa Wajanja Marathon ni, Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, Kampuni ya ulinzi ya SGA, IceDrop, Switch, Kuambiana Investment, Azam Media, Mapembelo Cargo na Gentlemen Club.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge (katikati), Diwani wa Kata ya Kijitonyama, Dama Lusangija, Mkuu wa Kituo cha Polisi Mabatini, ASP Soty Mtaki na mhamasishaji maarufu wa mtandaoni, Dotto Magari (kushoto), wakionyesha fulana zitakazovaliwa wakati mbio za Sinza Kwa Wajanja Marathon 2024, zinazotarajiwa kutimua vumbi katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama, Dar es Salaam Juni 16 mwaka huu.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive