Friday, March 29, 2024
KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA TANZANIA WAYAKUMBUKA WATEJA WAKE
BancABC Tanzania yatoa msaada pamoja na kufuturisha kituo cha watoto yatima cha New Faraja
Baadhi ya watoto wanaolelewa kwenye kituo cha watoto yatima cha New Faraja kilichopo Mburahati Jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba pamoja na nasaha kutoka kwa viongozi wa BancABC Tanzania mara baada ya benki hiyo kutoa msaada wa vyakula mbali mbali pamoja na kuwaandalia futari watoto hao ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo kwenye kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadan.
Mkuu wa kitengo cha Udhibiti wa BancABC Tanzania (kushoto), akimkabidhi msaada wa vyakula mbali mbali Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto yatima cha New Faraja kilichopo Mburahati Jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam Ijumaa 29 Marchi 2024 BancABC Tanzania, ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara imetoa msaada wa vyakula mbali mbali pamoja na kuandaa futari kwa watoto wanaolelewa kwenye kituo cha watoto yatima cha New Faraja kilicho Mburahati Jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo kwenye kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadan.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam mara ya kukabidhi msaada huo, Mkuu wa Idara ya Udhibiti BancABC Tanzania Saleh Geva alisema benki hiyo imetoa msaada pamoja na kufuturisha kituo cha Watoto yatima cha New Faraja kama ishara ya kuonyesha upendo pamoja na kuwapa tabasamu na hasa kwenye kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadan. ‘Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wanahitaji kuonyesha upendo. Sisi BancABC Tanzania na hasa wafanyakazi tumefarajika sana kujumuika nao pamoja na kupata wasaa wa kufuturu na watoto wanaolelewa kwenye kituo hiki. Kilikuwa ni kipindi faraja sana kwao lakini furaha kwetu kuona watoto hawa wakitabasamu. Lengo letu ilikuwa ni kufanikiwa kuona watoto hawa wajisikia kama sehemu ya Jamii ya Watanzania’, alisema Geva.
Geva aliongeza ‘Kuwafanya watoto hawa watabasamu na kufurai kunawapa matumaini yao ya maisha ya baadae. Kuja kwetu kufuturu na watoto hawa kumetuonyesha kwa nini BancABC Tanzania imekuwa ikijikita sana kwenye kusaidia Jamii ambayo inayotuzunguka. Tutaendelea na utamanduni huu wa kusaidia Jamii ambayo inaishi kwenye mazingira mangumu kwa sababu tunaamini ni moja Kati ya nguzo ya sisi kuendelea kukua kibiashara’,
‘Furaha yetu sisi BancABC Tanzania ni kuona tukibadilisha maisha ya Watanzania. Tunaamini kwenye Jamii yenye usawa na ndio sababu mwaka huu tuliamua kuja kufuturu na watoto hawa ambao wanaishi kwenye mazingira magumu ’, alisema Geva.
‘BancABC Tanzania, ikiwa ni taasisi ya kutoa huduma za kifedha imekuwa ikifanya kazi kubwa sana kuwafikia Watanzania na hasa wale ambao bado hawafikiwa na huduma za kibenki. Kwa sasa, BancABC Tanzania tunao mawakala zaidi ya 700 nchini kote’, alisema Geva huku akiongeza kuwa benki hiyo inayo akaunti maalum kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na wa kati kwa ajili ya kutoa mikopo ya kuimarisha biashara zao’.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kituo cha New Faraja Zamda Idrisa alisema kuwa wamefarijika kwa kuona taasisi binafsi kama BancABC Tanzania ikiunga mkono Jamii ambayo inaishi kwenye mazingira mangumu.
Aliongeza ‘Msaada wenu umekuja kwenye muda muafaka kwani watoto hawa wanahitaji kuonyesha upendo kama watoto wengine. Tunawashukuru kwa msaada wenu na tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu azidi kuwafungulia riziki kwenye maisha yenu ya kila siku’.
‘Tunatoa rai kwa taasisi zingine pamoja na watu binafsi wazidi kutusaidia kwani watoto hawa wanahitaji kuvaa, kusoma, chakula pamoja na matibabu na kituo chetu hakina wadhamini bali tunatengemea misaada kutoka kwa wadau mbali mbali kama BancABC Tanzania walivyokuja hapa kutusaidia kwa siku ya leo.
Wednesday, March 27, 2024
BODABODA TANGA WAPATA MAFUNZO MAALUM YA UTOAJI WA HUDUMA YA KWANZA
Na Mwandishi Wetu,Tanga
MADEREVA bodaboda katika Jiji la Tanga wamepatiwa mafunzo ya huduma ya kwanza kwa lengo la kuwawezesha madereva hao kutoa msaada wa huduma ya kwanza inapotokea ajali
Mafunzo hayo ya huduma ya kwanza kwa madereva wa bodaboda inakwenda sambamba na elimu ya Usalama barabarani inayotolewa na Taasisi ya AMEND kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uswisi ambao ndio wanaofadhili mradi wa utolewaji wa mafunzo hayo kwa madereva bodaboda.
Baadhi ya wadau ambao wanashirikishwa katika kutekeleza mradi huo wameeleza kwa kina kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo kwa sababu yanakwenda kupunguza changamoto ya ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikisababisha vifo na ulemavu kwa madereva wengi wa bodaboda na watumiaji wengine wa usafiri huo.
Akieleza zaidi kuhusu mafunzo hayo CPL Hamisi anayetoka Kitengo cha Elimu Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tanga amesema wanaushukuru AMEND na Ubalozi wa Uswisi kwa kuona haja ya kutekeleza mradi huo kwani unakwenda kuongeza uelewa kwa madereva bodaboda kujiepusha na ajali pamoja na kutoa huduma ya kwanza inapotokea ajali.
Amesema ni muhimu kutolewa kwa huduma ya kwanza pale ajali inapotokea huku akisisitiza anapaswa kutoa hiyo ni mtu aliyepata elimu ya mafunzo ya jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyepata ajali
"Mafunzo haya yatasaidia kuokoa maisha kwa mtu aliyepata ajali ya bodaboda,"amesema na kutoa mwito kwa baadhi ya bodaboda kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu zinapotokea ajali na badala yake watumie elimu waliyoipata kuokoa maisha ya waliopatwa na ajali barabarani.
Kwa upande wake Ofisa Miradi kutoka AMEND Scolastica Mbilinyi ameeleza kwamba lengo la kutoa elimu ya huduma ya kwanza kwa bodaboda ni kusaidia kuokoa maisha ya watu pindi ajali zinapotokea.
Ameongeza wamekuwa na mradi huo wa kutoa mafunzo ya usalama barabarani kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Jeshi la Polisi na Msalaba Mwekundu pamoja na wadau wote muhimu.
Aidha amesema AMEND miongoni mwa mambo wanayofanya ni pamoja na kutoa elimu ya usalama barabarani, ujenzi wa miundombinu ya barabara kwenye shule zilizopo maeneo hatarishi na kwa wakati huu huo wanatoa mafunzo ya huduma ya kwanza kwa madereva.
Pamoja na hayo amesema mpaka sasa AMEND kwa ufadhili wa ubalozi wa Uswiswi wameshatoa elimu ya usalama barabarani katika mikoa ya Tanga na Dodoma na lengo ni kuwafikia madereva wa bodaboda 750.
Wakati huo huo Diana Kashmiry kutoka Kikosi kazi cha huduma ya kwanza- Shirika la Msalaba Mwekundu amesema elimu wanayoitoa inamuwezesha dereva bodaboda kufahamu changamoto aliyoipata mtu ajalini na jinsi ya kumsaidia kwa kumpa huduma ya kwanza
Aidha ametoa angalizo kutokana na mazingira hatarishi yanayokuwepo katika ajali, ni vema kwa mtu asiye na vifaa vya kutoa huduma ya kwanza asiye huduma hiyo ili kumuepusha na madhara yanayoweza kujitokeza yakiwemo ya magonjwa ya kuambukiza.
Tuesday, March 26, 2024
BENKI YA DCB YAZINDUA PROGRAMU YA VICOBA KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA
Monday, March 25, 2024
BENKI YA EQUITY TANZANIA YAFUTURISHA WATEJA WAKE ZANZIBAR
Akiongea kwenye hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Bw. Rojas Mdoe amesema kwamba Benki ya Equity Tanzania inathamini mchango wa wateja wakekatika ukuwaji wa amana za benki na kwa kutumia huduma za benki. Akaendelea kusema, dhumuni kubwa la kuandaa Futari hii ni kuwashukuru wateja wake kwa kuwa bega kwa bega kuhakikisha tunabadilisha maisha ya kila Mtanzania.
Aliendelea na kusema kuwa benki yetu inaendelea kuboresha huduma zake na kuhakikisha kuwa inatanua wigo wake wa upatikanaji nchini ili kuweza kuwafikia wateja wote Tanzania na kuhakikisha kuwa inatimiza dhamira yake ya kubadilisha maisha ya kila Mtanzania.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Afisi ya Raisi Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mh. Sharif A. Sharif alisema, nawapongeza sana benki ya Equity kwa kuunga mkono juhudi za serikali kwa kukuza uchumi wa taifa letu kwa kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anatumia mifumo rasmi ya kifedha (financial inclusion). Vilevile kwa ubunifumkubwa wa kutoa huduma bora za kibenki za kidijitali.
Kuhusu Benki ya Equity
Equity Bank (T) ni Benki yenye matawi 16 nchini, mawakala zaidi ya 2,000 ikiwa na zaidi ya wafanyakazi zaidi ya 400 ikiwa ni moja ya uwekezaji mkubwa zaidi ulioanzia nchini Kenya na baadaye kusambaa katika nchi nyingine 5 za Afrika Mashariki, ikiwemo Tanzania, Uganda, Congo-DRC, Rwanda na Sudan ya Kusini.
Saturday, March 23, 2024
KAMPUNI YA ORYX TANZANIA YAWAKOMBOA WAKAANGA SAMAKI FERI YAKABIDHI MITUNGI 700 YA GAS BURE
KAMPUNI ya Oryx Gas Tanzania imeahidi kufunga mtambo mkubwa wa nshati safi ya kupikia katika Soko la Samaki la Kimataifa Feri jijini Dar es Salaam ambapo wajasiriamali wa soko hilo watakuwa na urahisi wa kuipata nishati hiyo na kwa gharama nafuu kwa ajili ya kukaanga samaki.
Hatua hiyo imekuja baada ya wajasiriamali wa soko hilo kutoa ombi kwa Kampuni ya Oryx Gas pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ilala ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge Muss Zungu baada ya kupokea ombi kutoka kwa wajasiriamali wa soko hilo walioomba kufungiwa mtungi mkubwa wa gesi wakiamini utawasaidia katika shughuli zao.
Ahadi ya kufungwa kwa mtungi mkubwa wa gesi imetolewa wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi 700 ya gesi ya Oryx kwa Baba na Mama Lishe wa soko la Samaki la Kimataifa Feri jijini Dar es Salaam leo Machi 22,2024.
Wakati anazungumza mbele ya wajasiriamali hao,Zungu amewahakikishia Mama Lishi na Baba lishe katika Soko la Samaki la Kimataifa Feri kuwa watafungiwa mtambo wa nishati safi ya kupikia ili kuwaepusha kutumia fedha nyingi kununua gesi kupitia mitungi midogo.
Amesema hatua hiyo ni utekelezaji wa mkakati wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa lengo la kulinda mazingira kuwaweka wanawake katika nafasi nzuri ya kujiendeleza kiuchumi.
Zungu kabla ya kueleza hayo alipokea maombi ya wafanyabiashara hao kupitia kwa kiongozi Zone Namba 7 katika soko hilo, Said Mpinji aliyelalamika kuwa wanalazimika kutumia sh. 110,000 kila siku kujaza gesi ya kuendeshea shughuli za baba na mama lishe.
Hivyo Zungu amesema tayari amezungumza na kampuni ya Gesi ya Oryx Tanzania kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wake, Benoit Araman na amekubali kufunga mifumo ya gesi ya kisasa kasha kusambaza huduma hiyo kwa wafanyabiashara hao kwa gharama nafuu.
“Mkombozi wetu ni Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye ameanzisha kampeni ya nishati safi ya kupikia, kuhakikisha Watanzania wanaishi maisha mazuri.
“Oryx wamekubali kuweka mtungi mmoja mkubwa na mifumo ya usambazaji, kasha watasambaza huduma kwa mama na baba lishe waliopo hapa na kuwafungia mita halafu watakuwa wakilipia huduma kama wanavyofanya katika umeme,” amefafanua.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Benoit Araman amesema Oryx wamewafikia wajasiriamali hao kwa lengo la kutekeleza mkakati wa Rais Dk. Samia wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kulinda mazingira na afya za wananchi.
"Tangu Julai mwaka 2021, tulianza mkakati huu baada ya Rais Dk Samia kutangaza kuwa Serikali yake inataka kuona hadi mwaka 2030 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia."
Wakati huo huo Mwenykiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abbasi Mtemvu aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, ameeleza kuwa ugawaji wa mitungi kwa baba na Mama Lishe hao ni utekelezaji wa Ilani huku akitumia nafasi hiyo kumpongeza Zungu kwa namna anavyowatetea wananchi wa jimbo lake.
Aidha ameipongeza Serikali kwa kuendelea kupeleka maendeleo kwa wananchi.Pia amewataka mama na baba lishe wa sokoni hapo kujiandaa kupokea mitaji kutoka serikali ili kunua biashara zao.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ( wa pili kulia),Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ( wa kwanza kulia), Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle ( wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya Gasi ya Orxy, Benoite Araman ( wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi mama lishe na mfanyabiashara katika soko la Samaki la Kimataifa Feri, Happy Kiondo wakati wa makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa mama lishe na baba lishe wa soko hilo leo Machi 22, 2024.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu (katikati) akiwa na Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle ( wa kwanza kushoto), Meneja Mauzo wa Kampuni ya Gasi ya Orxy , Shaban Fundi (wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia ya Oryx Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Zone no.7 wa Soko la Samaki la Kimataifa Feri Jijini Dar es Salaam, Saidi Mpinji wakati wa makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa mama lishe na baba lishe wa soko hilo leo Machi 22, 2024. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (kulia).
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ( wa pili kulia),Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ( wa kwanza kulia), Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle ( wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya Gasi ya Orxy, Benoite Araman ( wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi mama lishe na mfanyabiashara katika soko la Samaki la Kimataifa Feri, Happy Kiondo wakati wa makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa mama lishe na baba lishe wa soko hilo leo Machi 22, 2024.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ( wa pili kulia),Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ( wa kwanza kulia), Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle ( wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya Gasi ya Orxy, Benoite Araman ( wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi mmoja wa mama lishe na mfanyabiashara katika soko la Samaki la Kimataifa Feri wakati wa makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa mama lishe na baba lishe wa soko hilo leo Machi 22, 2024.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ( wa pili kulia),Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ( wa kwanza kulia), Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle ( wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya Gasi ya Orxy, Benoite Araman ( wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi mama lishe na mfanyabiashara katika soko la Samaki la Kimataifa Feri, Salma Mohammed wakati wa makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa mama lishe na baba lishe wa soko hilo leo Machi 22, 2024.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Gesi ya Orxy, Benoite Araman wakiwasikiliza wafanyabiashara wa samaki katika soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu ( kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Gesi ya Orxy, Benoite Araman katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Gasi ya Orxy, Benoite Araman akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.Baadhi ya wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali hao, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.Meneja Masoko wa Kampuni ya Gesi ya Orxy Peter Ndomba akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mtungi wa kupikia wa gesi ya Orxy katika hafla ya makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.