A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Tuesday, August 29, 2023

Airtel, Pesapal venture to ease mobile transactions in Tanzania

Airtel Money’s Director, Mr. Andrew Rugamba (right), and Ms. Bupe Mwakalunda, Pesapal Country Manager, exchange documents that symbolize their newfound partnership during a brief yet impactful meeting held in Dar es Salaam today. Through this strategic alliance, both entities are poised to revolutionize online payments, offering merchants and customers unparalleled convenience and speed.
  • Customers and Merchants to reap more
  • Pesapal, Airtel Money service geared to boost financial inclusion
Dar es Salaam. 29th August 2023: Pesapal Tanzania, among the leading POS payment and online payments company in Tanzania, providing affordable payment services to several merchants including hotels, restaurants, hospitals, pharmacies, to mention but a few, has partnered with Airtel Money to provide Airtel Money as an additional payment option to all its merchants, on Pesapal POS machines.

This innovation will allow Airtel Money customers to make payments conveniently, secured at any Pesapal merchant using Airtel Money while all Pesapal merchants can now receive payments directly from Airtel money users.

Pesapal has also extended Airtel Money payment option to the Pesapal online payments gateway, enabling more than 300 merchants supported by Pesapal to accept payments via Airtel Money, thus providing a convenient payment option to all Airtel Money customers. The Airtel Money option for online payments is more affordable than most means used to make online payments.

Under the partnership, all businesses that use Pesapal payment machines will receive payments with Airtel Money, in addition to Visa and Mastercard payments.

Speaking at the launch of the Airtel Money payment option, at Wood Berry Café, a Pesapal merchant in Dar es Salaam today, Pesapal country Manager Ms. Bupe Mwakalunda said that “the breadth and size of the partnership will bring convenient, affordable and secure payment solutions, better service delivery to all Airtel Money customers to experience a simple payment solution”.

"Tanzania is rapidly changing towards a cashless economy, and we look forward to working with Airtel Money to support merchants in this transition period by enabling them to serve their customers better at all times be it online merchant payments, home delivery services, or at their favorite retail store."

We are determined to provide our customers with the best and most innovative solutions in receiving payments. This partnership is one step forward towards achieving digital lifestyle, bringing innovative financial services closer to our customers in Tanzania," said Ms. Bupe.

On his part, Airtel Money Director, Andrew Rugamba said that “Airtel Money is pleased to partner with Pesapal to launch yet another innovative service that will increase convenience to Airtel Money customers by enabling seamless, affordable payments for goods and services for all Airtel Money customers. The service will be available in several merchant locations throughout Tanzania expanding the Airtel Money touch points. The service is robust and has gone further to provide Airtel Money customers with a receipt for each payment’’.

Businesses and online merchants will now serve all their customers conveniently through Airtel Money. All money collected through Pesapal merchants on behalf of the merchant will be settled at the merchant’s bank account, we encourage all merchants that want a secure, affordable, and convenient payment method to use Pesapal and Airtel payment option.", said Rugamba.

Pesapal and Airtel Money partnership is another step in enhancing digital payments supporting the GoT financial inclusion agenda.

According to the Global System for Mobile Communications Association (GSMA), in 2021, Africa accounted for 70 percent of the USD 1 trillion in mobile phone transactions.

It increased 39 percent to USD 701.4 billion in 2021 from USD 495 billion in 2020, indicating the future of African banking is mobile phones.

In addition to Airtel Money merchants’ partnership launched today, the company has over 200,000 wakalas and 4,000 Airtel Money Branches across the country making Airtel Money service available to all 24 hrs /7 days a week.

About Airtel Africa

Airtel Africa is a leading provider of telecommunications and mobile money services, with a presence in 14 countries in Africa, primarily in East Africa and Central and West Africa.

Airtel Africa offers an integrated suite of telecommunications solutions to its subscribers, including mobile voice and data services as well as mobile money services both nationally and internationally.

The Group aims to continue providing a simple and intuitive customer experience through streamlined customer journeys.

www.airtel.africa

About Pesapal Ltd:

Thousands of businesses and customers trust us to simplify and secure their payments.

Founded in 2009, we are the leading payments services company with the in-house expertise in building payments and commerce in Africa. Pesapal has more than 300 employees in 5 African countries - and we are adding more.

We are on track to connect one million entrepreneurs and consumers in Africa to e-commerce, digital payments, and the global financial system by 2030.

Pesapal is under the supervision of the Central Bank of Tanzania, the Central Bank of Uganda, the Central Bank of Kenya, and the National Bank of Rwanda.
Share:

Sunday, August 27, 2023

Rais wa Zanzibar aipongeza Benki ya Absa Tanzania kusaidia juhudi za kupunguza na kuepusha vifo vya mama wajawazito na watoto.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk Hussein Ali Mwinyi (katikati), akishiriki matembezi na mbio fupi za Amref Wogging Marathon 2023 mjini Zanzibar jana zilizofanyika kwa udhamini mkuu wa Benki ya Absa Tanzania. Wengine kutoka kushoto ni, Mke wa Rais, mama Mariam Mwinyi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa, Obedi Laiser, Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Zanzibar, Mhe. Hassan Khamis Hafidh na Mkurugenzi wa Shirika la Amref, Dk. Florence Temu. Hafla hiyo ilikuwa na lengo la kuchangisha fedha kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba kwa uzazi salama na afya ya mama na mtoto.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto), akipata maelekezo kuhusu huduma za kibenki za Benki ya Absa, kutoka Kwa Meneja Mahusiano wa Wateja Maalumu wa benki hiyo, Salim Khamis Salum wakati akiwasili katika viwanja vya Maisara mara baada ya kushiriki matembezi na mbio fupi za Amref Wogging Marathon 2023 zilizofanyika kwa udhamini wa Benki ya Absa, mjini Zanzibar jana. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa, Obedi Laiser. Hafla hiyo ilikuwa na lengo la kuchangisha fedha kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba kwa uzazi salama na afya ya mama na mtoto.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk Hussein Ali Mwinyi (kushoto), akizungumza katika hafla ya matembezi na mbio fupi za Amref Wogging Marathon 2023 zilizofanyika Kwa udhamini wa Benki ya Absa mjini Zanzibar jana. Hafla hiyo ilikuwa na lengo la kuchangisha fedha kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba kwa uzazi salama na afya ya mama na mtoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser (kulia), akitoa hotuba yake katika hafla ya matembezi na mbio fupi za Amref Wogging Marathon zilizofanyika Kwa udhamini wa Benki ya Absa mjini Zanzibar jana. Mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi (kushoto). Hafla hiyo ilikuwa na lengo la kuchangisha fedha kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba kwa uzazi salama na afya ya mama na mtoto.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa nne kushoto) akikabidhi cheti cha shukurani Kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser, Kwa kutambua udhamini mkuu wa Benki hiyo katika mbio fupi na matembezi ya Amref Wogging Marathon zilizofanyika visiwani Zanzibar jana. Hafla hiyo ilikuwa na lengo la kuchangisha fedha kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba kwa uzazi salama na afya ya mama na mtoto.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa tatu kushoto), akikataa utepe kuashiria makabidhiano rasmi ya gari la kliniki inayotembea lilolilotokewa na Shirika la Amref kwenda Wizara ya Afya ya visiwani humo. Ilikuwa ni wakati wa hitimisho la matembezi na mbio fupi za Amref Wogging Marathon zilizofanyika mjini Zanzibar chini ya udhamini mkuu wa Benki ya Absa Tanzania.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa nne kushoto), viongozi kutoka jukwaa kuu, wakipozi Kwa picha ya kumbukumbu pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Absa, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wao, Obedi Laiser muda mfupi baada ya kukamilika kwa matembezi na mbio fupi za Amref Wogging Marathon zilizofanyika mjini Zanzibar jana chini ya udhamini mkuu wa benki hiyo.

Na mwandishi wetu, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Benki ya Absa Tanzania, kwa kudhamini matembezi na mbio fupi zenye lengo la kuchangia vifaa tiba kwa uzazi salama wa mama na mtoto.

Akizungumza mara baada ya matembezi hayo yaliyoitwa ‘Wogging Marathon 2023’ yaliyoandaliwa na Shirika la Amref Health Afrika kwa kushirikiana na Serikali ya Zanzibar chini ya udhamini wa Absa katika Viwanja vya Maisara, mjini Zanzibar jana, Rais Mwinyi alisema anatambua na kuthamini udhamini mkubwa wa Benki ya Absa pamoja na waandaaji wa matembezi hayo.

Kwa niaba ya serikali natoa shukurani kwa Benki ya Absa Tanzania na kuwataka waendelee kutupa ushirikiano katika kuhakikisha tunafanikiwa katika malengo yetu ya kupunguza idadi ya vifo vya mama wajawazito na watoto vinavyotokana na uzazi".

Nimefurahi kusikia kuwa kampeni hii ni ya miaka mitatu na ilianza tokea mwaka jana ikiwa na lengo la kukusanya shilingi bilioni moja huku taarifa nilizonazo zikionyesha kuwa hadi sasa ahadi za jumla ya shs milioni 792 zimetolewa huku kilichopatikana ni shs milioni 557”, alisema mheshimiwa rais.

Akizungumza mara baada ya matembezi hayo yaliyokuwa ya umbali wa kilomita tano na kumi, ambapo pia alishiriki matembezi hayo akiwa na mkewe Mama Mariam Mwinyi, viongozi kisiasa, kiserikali, taasisi za umma na binafsi na wananchi ndani ya kisiwa hicho na wageni wengine kutoka nje ya Zanzibar alisema, kampeni ya Uzazi Salama inaunga mkono juhudi za serikali katika kupunguza na kuepusha vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga kutokana na ukweli kuwa bado takwimu za vifo hivyo bado vipo juu.

Takwimu zinaonyesha vifo vya kina mama 134 kati ya vizazi hai 100 kwa mwaka na vifo 28 vya watoto wachanga kati ya vizazi hai 1,000 kwa mujibu wa takwimu za Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania (TDHS) za mwaka 2017”, alisema Rais Mwinyi akiongeza kuwa kiwango hicho kinasababishwa na changamoto mbalimbali zikiwemo upungufu wa vifaa tiba, uhaba wa wahudumu pamoja na kukosekana kwa dawa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa, Bwana Obedi Laiser alisema kampeni hii inaenda sambamba na dhumuni kuu la benki ya Absa ambalo ni kuiwezesha Afrika ya kesho, pamoja, mtu mmoja baada ya mwengine katika kuiwezesha jamii yenye afya bora na mustakabali mzuri.

Sisi kama Absa tunatambua juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya pamoja na mashirika kama Amref katika kuleta mabadiliko katika jamii hususani katika suala zima la afya ya mama wajawazito na mtoto kwani afya ya mtoto ni msingi wa Taifa la watu wa sasa na wa kesho".

Tutaendelea kushirikiana na serikali za Zanzibar katika jitihada zake za kuwaletea wananchi wake maendeleo, tuna malengo makubwa ya kibiashara hapa Zanzibar katika kutanua huduma zetu za kibenki, na tutaendelea pia kushirikiana na Amref katika jitihada hizi za kuokoa maisha ya mama na mtoto japo hii ni mara yetu ya kwanza”, alisema Bwana Laiser.

Matembezi na mbio fupi za Amref wogging ni hafla la kila mwaka inayoandaliwa na shirika hilo kwa ushirikiano na serikali huku yakiwezeshwa kwa udhamini wa taasisi mbalimbali, wananchi pamoja na wadau wengine yakiwa na lengo kutafutu suluhu za changamoto zinazosababisha vifo vya wamama wajawazito na watoto wachanga nchini.
Share:

Friday, August 25, 2023

Mchengerwa Awakaribisha Wawekezaji Rufiji Benki Ya CRDB Ikizindua Tawi Lake Ikwiriri

Rufiji. Tarehe 25 Agosti 2023: Baada ya Benki ya CRDB kufungua tawi, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohammed Mchengerwa amewakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya Tanzania kuja kuwekeza kwenye fursa tele zilizopo wilayani Rufiji.

Mchengerwa amesema Rufiji ambayo ni kati ya wilaya kongwe nchini inazidi kukua kila siku kwa kuimarisha miundombinu ya huduma za jamii kwani tayari serikali imejenga zahanati 24, shule za msingi 45 na sekondari 9 ndani ya vijiji 38 ilivyonavyo zinazotoa nafasi kwa wananchi kutibiwa na watoto kupata elimu itakayowasaidia kujikomboa katika maisha yao hivyo ujio wa Benki ya CRDB inawaongezea fursa za kujiimarisha kiuchumi.
Uamuzi wa serikali kujenga Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) umeleta neema nyingi zitakazowanufaisha wananchi na halmashauri hii yenye utajiri mkubwa wa ardhi, maliasili na utamaduni. Ukiacha bwawa hili, kuna hekta 300,000 limetengwa kwa ajili ya kilimo kitakachoendeshwa kwa mfumo wa umwagiliaji. Ni wakati sahihi sasa kwa wawekezaji kutoka ndani na nje ya Tanzania kuja kuwekeza wilayani Rufiji kwani kuna usalama wa kutosha kuanzia namna ya kuhifadhi fedha zao mpaka kutekeleza miradi watakayoianzisha,” amesema Mchengerwa.

Ili kutoachwa nyuma, Mchengerwa ambaye ni mbunge wa Rufiji tangu mwaka 2015 amewahimiza wananchi wenzake kulitumia tawi hilo la Benki ya CRDB hivyo kunufaika na huduma zinazotolewa na kujihakikishia usalama wa fedha, kukopa kwa ajili ya miradi na mipango binafsi hata kufanya uwekezaji.
Rufiji ni kati ya wilaya kongwe nchini lakini kwa muda mrefu haikuwa imefunguka ila leo hii Benki ya CRDB imeonyesha njia. Ili kuwa wilaya ya sita wakati wa mkoloni na ya 13 baada ya uhuru. Mimi ni mteja wa siku nyingi wa Benki ya CRDB hivyo nawasihi wananchi wenzangu nanyi mjiunge kutumia huduma za benki hii."

"Benki hii ya CRDB inayo huduma ya imbeju ambayo ni programu maalumu ya kuwawezesha vijana na wanawake. Makundi haya muhimu kwa jamii yetu yapo wilayani Rufiji na kwa kufika kwenye tawi hili ndivyo yataweza kunufaika na programu hii inayotoa mtaji wezeshi kwao. Kwa kuwa Rufiji ina kila kitu kinachohitajika kwa mjasiriamali kujikwamua kiuchumi, mtaji huu unaotolewa na Benki ya CRDB na mikopo ya aina tofauti iliyopo ni msingi mkubwa wa kuwakomboa wananchi kiuchumi,” amesema Mchengerwa.

Mchengerwa amezitaja fursa nyingine zilizopo wilayani humo kuwa ni pamoja na kilomita za mraba 6,500 ambazo ni hifadhi na misitu zinazofaa kwa utalii. Nyingine amesema ni uvuvi, huduma za kijamii na ukarimu zikiwamo hoteli. Kwenye kilimo, amesema ufuta, korosho na mazao mengine mengi ya biashara yanastawi vyema wilayani humo na hivi karibuni kiwanda kikubwa cha sukari kitajengwa wilayani humu.
Kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa alisema wamejipanga vyema kukidhi mahitaji ya mtaji kwa ajili ya wateja wao wakiwamo wawekezaji wanaohitaji shilingi hata fedha za kigeni.

Jana benki yetu imepata kibali za kuorodhesha hatifungani ya kijani yenye thamani ya dola milioni 300 za Marekani ambazo ni sawa na shilingi bilioni 780. Fedha zitakazokusanywa kutokana na mauzo ya hatifungani hii zitaelekezwa kwenye miradi inayolinda na kujali mazingira. Rufiji ni kati ya maeneo yanayostahili kuzitumia hivyo nawakaribisha mje tuwahudumie,” amesema Raballa.
Afisa huyo amesema kupitia tawi hilo, wananchi wa wilaya nzima ya Rufiji wanafunguliwa milango kunufaika na mtandao mpana wa matawi 260 yanayoifanya Benki ya CRDB kuwa na idadi kubwa zaidi ikilinganishwa na benki nyingine nchini.

Licha ya huduma matawini, kupitia mawakala wa benki, mashine za kutolea fedha na zile zinazopokea malipo ya kadi au kupitia simu ya mkononi, amesema Benki ya CRDB inatoa ushauri na elimu kuhusu masuala ya fedha, uwekezaji na namna bora ya uendeshaji wa biashara.
Watu wengi hudhani benki ni kuweka, kutoa pesa au kuomba mkopo tu lakini ukweli wasioujua ni kuwa tunatoa elimu na ushauri na tumekuwa tukifanya hivyo kwa wateja wetu ingawa wengi hawaitumii huduma hii. Hivyo niwakaribishe katika Benki yenu ya CRDB kupata ushauri".

"Na kupitia taasisi yetu ya CRDB Bank Foundation, tunafanya uwezeshaji kwa wanawake na vijana kwa kuwapa mitaji wezeshi kwa masharti nafuu ili kuwapa nafasi ya kuimarisha kipato chao na kushiriki kujenga uchumi wa taifa,” amesema Raballa.

Benki ya CRDB ndio taasisi pekee ya kizalendo yenye matawi nje ya mipaka ya Tanzania ikitoa huduma nchini Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Share:

Saturday, August 12, 2023

Thamani ya uwekezaji mfuko wa PSSSF kufikia sh. trilioni 7.98-Majaliwa

 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kiwango cha thamani ya uwekezaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) imeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 7.98 kwa mwaka 2022/2023 kutoka shilingi trilioni 7.5 kwa hesabu za mwaka wa fedha ulioishia Juni, 2022.

Amesema hayo leo (Jumamosi, Agosti 12, 2023) wakati wa maadhimisho ya miaka mitano ya mfuko huo na uzinduzi wa huduma za wanachama kidijitali, kwenye ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma.

Thamani hii ipo katika soko la hisa ambalo ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa mitaji nchini ambapo mfuko huo ni muwekezaji mkubwa wa ndani mwenye hisa katika makampuni makubwa kama CRDB Bank Plc, NMB Bank Plc, Tanzania Breweries Limited, na Vodacom Tanzania Plc.

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Mifuko ya Hifadhi ya jamii kufanya uwekezaji wenye tija kwa wanachama na jamii inayolingana na thamani ya fedha za wanachama “Fanyeni utafiti wa kina kubaini masoko ili uwekezaji unaofanywa usilete hasara kwa mifuko.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza mifuko yote ya Hifadhi ya Jamii kuendelea kulipa mafao kwa wakati ili kuleta utulivu kwa wanachama. “Wazee wastaafu wasisumbuliwe, kumbukeni kuwa sisi sote ni wastaafu watarajiwa.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ameziagiza taasisi za Serikali kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati uzinduzi wa mkongo wa mawasiliano wa 2Afrika na matumizi ya teknolojia ya 5G la kutaka taasisi zote za Serikali ziwe zinasomana ili kurahisisha na kuboresha utoaji wa huduma kwa Watanzania.

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof Joyce Ndalichako amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa maono na dhamira ya dhati ya kuimarisha sekta ya hifadhi ya jamii “lengo la Rais Samia ni kuona inafanya kazi kwa tija, ufanisi na kutoa huduma bora."

Tunampongeza pia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia kwa uthubutu wa kutoa fedha kwa mfumo wa hati fungani shilingi trilioni 2.17 za kulipa deni ambalo lilimedumu kwa muda mrefu, mfumo huu umewezesha PSSSF kulipa wastaafu kwa wakati.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) CPA Hosea Kashimba amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano, hadi kufikia Juni, 2023 mfuko huo umelipa kiasi cha shilingi trilioni 8.88 kwa wanufaika 262,095.

Amesema kuwa kati ya Julai, 2018 na Juni, 2023 mfuko huo umeweza kulinda na kuongeza thamani yake kwa asilimia 27.76 kutoka trilioni 5.83 hadi trilioni 8.07 Juni, 2023. “Ongezeko hili ni sawa na wastani wa asilimia 6.72 kwa kila mwaka”.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea zawadi kutoka kwa Waziri Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako (wa tatu kushoto) wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka mitano ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja uzinduzi wa huduma za kidigitali za PSSSF Pamoja jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Huduma zinazopatikana kupitia ‘PSSSF Pamoja’ ni utaratibu wa wanachama wapya kujiunga kwenye mfuko, mfumo wa kidigitali wa kuanzisha madai ya mafao na uhakiki wa wastaafu kupitia simu janja popote walipo bila kufika kwenye ofisi za mfuko. Wengine kutoka kulia ni, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo, CPA. Hosea Kashimba na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSF, Mhandisi Musa Iyombe.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa huduma za kidigitali ya PSSSF Pamoja, wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka mitano ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa huduma za kidigitali za mfuko huo jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Huduma zinazopatikana kupitia PSSSF Pamoja ni utaratibu wa wanachama wapya kujiunga kwenye mfuko, mfumo wa kidigitali wa kuanzisha madai ya mafao na uhakiki wa wastaafu kupitia simu janja popote walipo bila kufika kwenye ofisi za mfuko. Kulia kwa mheshimiwa waziri mkuu kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu), Prof. Joyce Ndalichako na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSF, Mhandisi Musa Iyombe na Mkurugenzi Mkuu wa mfuko huo, CPA. Hosea Kashimba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishikana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), CPA. Hosea Kashimba wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka mitano ya mfuko pamoja na uzinduzi wa PSSSF Pamoja jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa PSSSF, Mhandisi Musa Iyombe na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule. Waziri mkuu Majaliwa ameagiza mifuko yote ya hifadhi ya jamii kulipa mafao kwa wakati.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa nne kulia), akikabidhi zawadi kwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PSSSF, Dk. Aggrey Mlimuka wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka mitano ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa huduma za kidigitali za PSSSF Pamoja jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wahudhuriaji wakishiriki maadhimisho ya miaka mitano ya miaka mitano ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa huduma za kidigitali za PSSSF Pamoja jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Wapiga ngoma wakionesha umahiri wao kunogesha sherehe za maadhimisho ya miaka mitano ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, viongozi wa Mfuko wa PSSF, viongozi wa kiserikali wa mkoa wa Dodoma pamoja na wahuduriaji wengine mashuhuri wakipozi kwa picha ya kumbukumnbu mara baada ya maadhimisho ya miaka mitano ya PSSSF mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Share:

Wednesday, August 2, 2023

Airtel yazindua Airtel Vikoba Kidigitali

    
*Inapatikana kwa wateja wote wa Airtel Money

*ni kwa kushirikiana na Benki ya TCB kupitia kauli mbiu isemayo ‘Tubebane Pamoja’.

Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kulia), akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya Airtel Vikoba kwa kutumia njia ya Airtel Money kwa kushirikiana na Benki ya TCB kupitia kauli mbiu yao ya ‘Tubebane Pamoja’ jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Masoko wa TCB, Deo Kwiyukwa, Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba na Mkuu wa Tehema na Uendeshaji wa TCB, Jema Msuya.
Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba (wa pili kushoto), akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya Airtel Vikoba kwa kutumia njia ya Airtel Money kwa kushirikiana na Benki ya TCB kupitia kauli mbiu yao ya ‘Tubebane Pamoja’ jijini Dar es Salaam leo. Pamoja naye kutoka kushoto ni, Mkuu wa Tehama na Uendeshaji wa TCB, Jema Msuya, Mkuu wa Masoko wa TCB, Deo Kwiyukwa na Meneja Mahusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.
Mkuu wa Tehama na Uendeshaji wa Benki ya TCB, Jema Msuya (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba na Mkurugenzi wa Masoko wa TCB, Deo Kwiyukwa.
Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba (kulia), na Mkuu wa Tehama na Uendeshaji wa Benki ya TCB, Jema Msuya wakionesha mfano wa kadi ikiwa ni ishara ya ushirikiano kati yao wakati wa uzinduzi wa huduma ya Airtel Vikoba kwa kutumia njia ya Airtel Money kwa kushirikiana na Benki ya TCB kupitia kauli mbiu yao ya ‘Tubebane Pamoja’ jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni, Mkuu wa Masoko wa TCB, Deo Kwiyukwa na Meneja Huduma za Airtel Money, Hellen Lyimo.
Share:

Tuesday, August 1, 2023

Benki ya Absa Tanzania kuziwezesha biashara ndogo na za kati kupitia mikopo yenye dhamana kutoka Mfuko wa Dhamana Afrika (AGF)

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Obedi Laiser (wa pili kushoto), akizungumza jijini Dar es Salaam leo, katika hafla ya utiaji saini makubaliano na Mfuko wa Dhamana Afrika (AGF), ambapo kupitia makubaliano hayo Absa itatoa mikopo maalumu kwa dhamana kutoka mfuko huo. Mikopo hiyo itawalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati. Kutoka kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la AGF, Bwana Jules Ngankam, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Absa, Bwana Melvin Saprapasen Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Absa Tanzania, Bwana Aron Luhanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Obedi Laiser (kulia), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Dhamana Afrika (AGF), Bwana Jules Ngankam wakitia saini hati za makubaliano yatakayoiwezesha Benki ya Absa kutoa mikopo kwa dhamana kutoka mfuko huo. Mikopo hiyo itawalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati hususan wanawake na vijana. Wanaoshuhudia ni maofisa kutoka AGF na Absa. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Obedi Laiser (kulia), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Dhamana Afrika (AGF), Bwana Jules Ngankam wakibadilishana hati za makubaliano yatakayoiwezesha Benki ya Absa kutoa mikopo kwa dhamana kutoka mfuko huo. Mikopo hiyo itawalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati hususan wanawake na vijana. Wanaoshuhudia ni maofisa kutoka AGF na Absa. Ilikuwa ni katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam leo. Wanaoshuhudia ni maofisa kutoka Absa na AGF.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Bwana Melvin Saprapasen (wa pili kulia), akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Obedi Laiser (wanne kushoto), na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Dhamana Afrika (AGF), Bwana Jules Ngankam (wa tatu kushoto), wakipiga picha ya kumbumbuku muda mfupi baada ya kutia saini makubaliano yatakayoiwezesha Benki ya Absa kutoa mikopo kwa dhamana kutoka mfuko huo. Mikopo hiyo itawalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati hususan wanawake na vijana. Wanaoshuhudia ni maofisa kutoka AGF na Absa. Ilikuwa ni katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam leo.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive