A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Wednesday, July 12, 2023

ACB BANK YAJIKITA KULETA MAPINDUZI YA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA WAKE

  

Na Mwandishi wetu

Akiba Commercial Bank Plc( ACB) imesema itahakikisha inaendelea kujikita kuleta mapinduzi ya utoaji huduma bora za kibenki hapa nchini kwa kuboresha huduma zake ikiwemo kuweka fedha na kutoa fedha pia kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu kwa .

Akizungumaza Jijini Dar es salaam na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Silvest Arumasi wakati katika banda la benki hiyo katoka maonyesho ya ya 47 ya Sabasaba ndani ya amesema kuwa benki ya Akiba imeboresha huduma zake ambazo zitakuwa chachu ya kukidhi matarajio ya wateja waliopo pamoja na wateja watarajiwa katika kujipatia huduma.

Hata hivyo amebainisha kuwa Maboresho makubwa yamefanywa kwa huduma za wateja binafsi,(Personal banking) ambayo inawalenga Waajiriwa wa sekta za Umma na sekta binafsi ambapo mteja anaweza kupata mikopo ya aina mbalimbali kuendana na mahitaji yake mathalani huduma za mikopo ya kujenga na kuboresha makazi, pia mikopo ya muda mfupi (Salary advance) kwa ajili ya kutatua dharura za kifedha kwa muda mfupi.


" Benki imezidi kuboresha huduma za mikopo kwa wateja wakubwa ,w (Corporate customers) wakati,na wadogo kuendana na mahitaji ya soko na tunatoa huduma za bima kwa wajasiriamali pamoja na vikundi mbalimbali ikiwemo mikopo ya bima –IPF (Insurance Premium Financing)" amesema Mkurugenzi

Sambamba na hayo Mkurugenzi amebainisha kuwa benki imeboresha huduma zake kwa kupitia Mawakala wake (Akiba Wakala) na simu ya mkononi (Akiba Mobile) pia imeboresha mifumo ya utumaji pesa kwenda nje ya nchi.

Aidha wito umetolewa kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo na amewashukuru kuchagua benki ACB hiyo kutumia huduma zake ikiwemo wafanyakazi ,Wajasriamali hivyo amewasisitiza waendelee kupata huduma bora kwani ni benki sahihi na bora inayolenga kutimiza malengo ya Wateja wake.
Share:

Monday, July 10, 2023

DAR COMPANY UNVEILS PLAN TO IMPROVE HOSPITALITY SERVICES IN TANZANIA.


By Correspondent

A Dar es Salaam-based catering and hospitality firm, FOODEX yesterday unveiled its new national plan to improve services delivery in the country’s hospitality industry.

“We want to transform catering and hospitality industry services in this country and provide high quality and standard services to domestic and international customers,” said FOODEX Chief Executive Officer, Safa Erzurumlugil during a press briefing on the company’s new strategy in Dar es Salaam.

The company’s plan intends to complement the sixth government initiatives to improve catering and the hospitality industry, which is a key to ongoing national economic and business growth and development strategies.

 “We are determined and committed to supporting government strategies aimed at transforming the hospitality industry,” said Safa Erzurumlugil, adding that “the move will attract investors and tourists from different parts of the world to come to Tanzania.”

He said as the government took long-term strategic steps to boost the business and investment environment, the provision of high quality and up to standard catering and hospitality services was inevitable.

“Business and investment growth will definitely need high quality food, catering and other related services. That is why FOODEX has come up with a new strategic plan that will ensure Tanzanians and foreigners doing business in the country are provided with standard food and catering services.”

Expounding on food and catering service delivery, the company top official said his company would provide catering services that embraced all types of events and occasions, delivering outstanding culinary experience to its esteemed clients and guests.

“We have a team of experienced chefs, event planners and service members of staff who work closely with each client to create customised menus that reflect their unique tastes and preferences. We use the freshest and high quality ingredients, sourced locally whenever possible, to create delicious and visually stunning dishes,” he said.

He explained that their extensive menu offers included a range of international cuisines such as Italian, Indian, Chinese, as well as special dietary options such as vegetable, vegan, gluten-free, halal, hot and cold buffets, plated meals, and snack platters.”

As regards corporate services, FOODEX catering services have been designed to provide business with high quality, delicious food for different types of corporate events, board meetings, training sessions, office parties and so on with the main goal of providing customers with stress-free event experience and high-quality services, according to CEO.

In fact, FOODEX is a modern catering firm that innovates with modern gastronomy and commercial services that integrate customer relationships. “FOODEX has a rapid development team, feedback collection units with large customer base, providing full food and services management and prefers to investment in this geographic area because of the welcoming environment.”
Share:

Saturday, July 8, 2023

Benki ya Absa yatambulisha Mpango wake mpya uitwao 'Tunaiwezesha Afrika ya kesho pamoja, hatua moja baada ya nyengine' ni katika kuiwezesha Afrika kutatua changamoto zake za kiuchumi na kijamii

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser akizungumza wakati wa hafla ya kuutambulisha Mpango mpya ya benki hiyo uitwao 'Tunaiwezesha Afrika ya kesho pamoja, hatua moja baada ya nyengine' jijini Dar es Salaam jana ukiwa na lengo la kuliona Bara la Afrika likipata uwezo wa kutatua changamoto za kiuchumi na kijamii.
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa Benki ya Absa, Patrick Foya akizungumza wakati wa hafla ya kutambulisha Mpango mpya wa benki uitwao 'Tunaiwezesha Afrika ya kesho pamoja, hatua moja baada ya nyengine' jijini Dar es Salaam jana Ukiwa na lengo la kuliona Bara la Afrika likipata uwezo wa kutatua changamoto zake za kiuchumi na kijamii.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mwasiliano wa wa Benki ya Absa, Aron Luhanga akizungumza wakati wa hafla ya kutambulisha mpango mpya wa benki hiyo uitwao ' Tunaiwezesha Afrika ya kesho pamoja, hatua moja baada ya nyengine' jijini Dar es Salaam jana, ukiwa na lengo la kuliona Bara la Afrika likipata uwezo wa kutatua changamoto zake za kiuchumi na kijamii.
Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya Absa, Genade Mzee akizungumza wakati wa hafla ya kuutambulisha mpango mpya wa benki uitwao 'Tunaiwezesha Afrika ya kesho pamoja, hatua moja baada ya nyengine' jijini Dar es Salaam jana, ukiwa na lengo la kuliona Bara la Afrika likipata uwezo wa kutatua changamoto zake za kiuchumi na kijamii.
Mkuu wa Uendeshaji wa Matawi ya Benki ya Absa, Mwilongo Irene Msungu akizungumza wakati wa hafla ya kuutambulisha mpango mpya wa benki hiyo uitwao ' Tunaiwezesha Afrika ya kesho pamoja, hatua moja baada ya nyengine' jijini Dar es Salaam jana, ukiwa na lengo la kuliona Bara la Afrika likipata uwezo wa kutatua changamoto zake za kiuchumi na kijamii.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Absa Tanzania wakihudhuria hafla hiyo jijini Dar es Salaam Jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Absa Tanzania kutoka jijini na mikoani wakiwa katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam Jana.
Share:

Friday, July 7, 2023

MAKAMU WA RAIS DKT MPANGO APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA ELIMU KUTOKA TANZANIA COMMERCIAL BANK MKOANI KIGOMA

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Muyama mara baada ya gafla ya kupokea vyumba vitatu vya madarasani ofisi mbili za walimu na Samani mbalimbali za maofisini yaliokabidhiwa na Tanzania commercial Bank (TCB), katika Shule ya Msingi Muyama iliyopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango (wapili kulia), akikata utepe kuashiria kupokea Madarasa, Samani mbalimbali na Ofisi za Walimu yaliokarabatiwa na Tanzania Commercial Bank (TCB) katika Shule ya Msingi Muyama iliopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ikiwa ni utaratibu wa Benki hiyo kurudisha kwa kutoa msaada kwa jamii (CSR).

Hafla hiyo imefanyika katika shule hiyo hivi karibuni wengine pichani ni kutoka (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Sabasaba Moshingi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof Joyce Ndalichako na viongozi wengine wa serikalini pamoja na Maafisa wa Benki

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Philip Mpango, ameishukuru Tanzania Commercial Bank kwa kutoa msaada wa ukarabati wa Vyumba Vitatu vya Madarasa, Ofisi Mbili za Walimu madawati 50 pamoja na printer na vitu mbalimbali vya ofisini katika Shule ya Msingi Muyama iliopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma

Akipokea msaada huo aliushukuru ongozi mzima wa Benki ya TCB kwa kuendelea kusaidia jamii katika suala zima la Elimu Mkoa wa Kigoma na maeneo mengine hapa nchini.

Makamu wa Rais Philip Mpango alipokea msaada huo alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani humo na kutaka taasisi nyengine kuiga mfano mzuri unaofanywa na Tanzania commercial bank

Ameeleza kuwa Benk ya TCB imeonesha ukomavu wake hasa kwenye swala la elimu ya kifedha maana bila elimu hakuna chochote kwenye maendeleo ya nchi yetu.

Dkt Mpango ameongeza kuwa hata yeye amesoma katika shule hiyo ambayo leo Tanzania commercial bank wametoa msaada wa vitu hivi kwaajili ya kukuza elimu na maeneo mengine alisema mpango.

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw Sabasaba Moshingi alitoa shukrani za dhati kwa Mhe Mpango kwa kuweza kufika kwenye hafla fupi ya makabidhiano na kuhaidi kuwa benki itaendelea kusaidia jamii katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu. Vile vile alitoa rai kwa wananchi wa Buhigwe na maeneo ya karibu kuweza kujiunga na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka benki ya TCB mara baada ya hafla ya kupokea vyumba vitatu vya madarasa na ofisi mbili za walimu na Samani mbalimbali za maofisini yaliokabidhiwa na Tanzania commercial Bank (TCB), katika Shule ya Msingi Muyama iliyopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive