Monday, March 27, 2023
Absa Bank Tanzania bids farewell to its Managing Director during a special Iftar Gala
Wednesday, March 22, 2023
FREIGHT MANAGEMENT YAJA NA MPANGO KUBORESHA HUDUMA ZA USAFIRISHAJI NCHINI
Meneja Operation wa Freight Management Ltd, Dorine Gibson akifafanua jambo wakati wa semina fupi ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Kampuni hiyo mbinu za kisasa za kuboresha huduma wa usafirishaji nchini.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI inayotoa huduma za anga za ugavi na usafirishaji nchini, Freight Management Company Ltd (FMCL), imetangaza mpango wake mpya wa kutoa huduma bora za anga za ugavi na usafirishaji kama sehemu ya mchango wake katika kukuza uchumi wa Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa FMCL Witness Panga amesema wantaka huduma za anga za ugavi na usafirishaji ziwe kwenye kiwango bora ndani ya nchi na kimataifa.
Akirejea jitihada na marekebisho yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuchochea uwekezaji wa sekta binafsi, Witness amesema kampuni yake imejipanga vizuri kusaidia mipango ya Serikali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma kwenye ugavi na usafirishaji na huduma zingine nchini Tanzania.
Alielezea huduma za ugavi na usafirishaji kama nguzo muhimu katika kuchechemua ukuaji wa biashara na uwekezaji na hivyo kukuza uchumi wa taifa na kuleta maendeleo kwa watanzania.
“Matokeo chanya katika uchumi wetu yatainua na kuboresha hali ya maisha ya Watanzania wa kawaida,” amesema na kuongeza kwamba: “Kwa vile sisi ni sehemu ya jamii hii, mchango wetu kwa maendeleo haya ni muhimu na haukwepeki.”
Amesema kampuni yake ina wabia wenye mtandao mkubwa na ulioimarika, unaoiruhusu kampuni kutoa huduma zinazoaminika na zenye gharama nafuu kwa wateja wake (wa ndani na kimataifa).
Pamoja na huduma zingine, kampuni ya FMCL inatoa huduma za anga za ugavi na usafirishaji, ambazo ni pamoja na usafirishaji wa mizigo kwa njia ya anga, usafirishaji wa kuunganisha kwa njia ya anga, kubadili meli/kuhamisha shehena na huduma za kukodisha.
“Tunatoa huduma mbalimbali za ugavi na usafirishaji baharini, ikiwa ni pamoja na usafiri wa kuunganisha kwa njia ya anga, kubadili meli/kuhamisha shehena na huduma za kukodisha, ukaguzi wa mizigo na kutoa hati ya utakaso wa ushuru,” amesema.
Kampuni inatoa pia huduma za ushauri na uchanganuzi. “Wafanyakazi wetu wana uzoefu wa kuweza kutoa suluhisho lililo bora zaidi kwa mchororo wa mahitaji ya ugavi na usafirishaji.”
Katika kufanya kazi zake, Freight Management inatoa huduma za usafirishaji wa kimataifa kwa njia ya anga na baharini kutoka huduma za usafirishaji wa kawaida hadi huduma changamani.
Kimsingi, FMCL ina uwezo wa kutoa huduma yoyote ya usafirishaji, kutoka vifurushi vidogo hadi makontena makubwa. Wafanyakazi wetu wazoefu wanajituma kuhakikisha shehena za wateja wetu zinafika muda wake, salama na ndani ya bajeti.
“Tunajivunia pia huduma ya usafirishaji wa mizigo baina ya nchi na nchi, tukitoa kwa wateja wetu fursa za uchaguzi wa njia ya kutumia, kwa viwango nafuu zaidi na kwa huduma bora.
Huduma za utaratibu wa ugavi na usafirishaji ni pamoja na utakaso wa ushuru, kufunga mizigo, kuhifadhi mizigo ghalani, usambazaji, usimamizi wa orodha/hesabu ya vitu/bidhaa na usafirishaji.
WAKAZI WA NYAMIKOMA WAISHUKURU TANZANIA COMMERCIAL BANK KWA UJENZI WA ZAHANATI
Meneja wa Tanzania commercial Bank (TCB), Tawi la Musoma Hagai Gilbert (kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa mabati 135 yaliyotolewa na Benki hiyo kwa Diwani wa kata ya Kyanyari kijiji cha Nyamikoma wilaya ya Butiama Mkoa wa Mara, Mkingi Itagata, kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nyamikoma wilayani humo.
Maofisa wa Tanzania Commercial Bank wakiongozwa na Meneja Benki hiyo tawi la Musoma Hagai Gilbert pamoja na uongozi wa kijiji cha Nyamikoma wakikagua ujenzi wa kituo cha Afya kinachojengwa kwa nguvu za wananchi ambapo TCB imeguswana kuchangia kwa kutoa msaada wa mabati 135 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huo
Wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Butiama wakisaidia kushusha mabati 135 yaliyotolewa na Tanzania Commercial Bank (TCB) kwa ajili ya kusaidia kuendeleza ujenzi wa zahanati.
Tanzania commercial bank imekabidhi mabati 135 katika kijiji cha Nyamkoma kilichopo wilaya ya Butiama mkoani Mara kwa dhamira ya kuunga mkono juhudi za serikali katika juhudi zake za kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma ya afya.
Msaada huo ulitolewa leo katika kijiji cha Nyamkoma kilichopo wilaya ya Butihama mkoani mara na kupokelewa na Diwani wa kata ya kinyare Mh. Mkingi Itagata.
Pamoja ya kuishukuru Benki ya TCB wakati akipokea msaada huo, Diwani wa kata ya Kinyare Mh Mkingi Itagata amesema kuwa bado kuna uhitaji ili ujamilisha ujenzi wa kituo cha afya kwani gharama ya ujenzi ni milioni 150 lakini hadi sasa kiasi walichokusanya ni milioni 47.
“Serikali pamoja na wazazi tutaongeza nguvu kwenye ujenzi huu maana wananchi wamekuwa wakifuata huduma ya afya mbali kidogo na kijijini hapo.” Amesema Mingi
Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo, Meneja wa Benki ya TCB Tawi la Musoma Gilbert Hagai aliwasihi wananchi wa kijiji hicho kuwa TCB itaendelea kuunga mkono juhudi za wananchi wapenda maendeleo na kuhakikisha kuwa benki hiyo inasogea huduma zake karibu.
Aidha pia amewapongeza wazazi na uongozi wa kijiji kwa jitihada zao za kuchangia na kuanza ujenzi wa zahanati hiyo toka mwaka 2017 hii inaonesha kuwa ni kwa namna gani kumekuwa na uhitaji.
“Benki yetu ya Tanzania Commercial Bank ni mdau mkubwa wa Maendeleo, kwa kawaida kila mwaka tunatenga fungu kutoka katika faida yetu kwa ajili ya kurudisha katika jamii na tunaipa kipaumbele kwani Kuwekeza kwenye Elimu, Afya na maeneo mbalimbali tukiwa kama benki tunaamini vitu hivi vyote vinatusiaida kupata wateja na wafanyakazi wa benki yetu wa baadaye.
Tutaendelea kuchangia na kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassani katika kuboresha sekta ya afya kwa kadri tunavyoweza na tunaahidi kwamba huu si mwisho.” Ameongeza gilbert.
Tuesday, March 14, 2023
DCB Elimu Mpango Mzima Na Mama Samia Yazidi Kuchanja Mbuga
Thursday, March 9, 2023
Halmashauri ya Jiji la Dar yaishukuru Benki ya Biashara ya DCB kusaidia sekta ya elimu
Wafanyakazi wa Freight Forwarders Tanzania Ltd watoa msaada Hospitali ya Mloganzila katika kusherehekea Siku ya Wanawake duniani 2023
Naibu Mkurugenzi Mtendaji MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi (wa pili kushoto) akipokeza msaada wa msaada wa kabati la kuhifadhia dawa za dharula (Trolley) lenye thamani ya shilingi milioni 2 kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya Freight Forwarders Tanzania Ltd, Veronica Chilunda, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani.
KAMPUNI ya Freight Forwarders Tanzania Limited imekabidhi msaada wa kabati la kuhifadhia dawa za dharula (Trolley) kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila lenye thamani ya shilingi milioni 2 ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayoadhimishwa Machi 8 kila mwaka.
Akikabidhi msaada huo Mwakilishi wa Kampuni ya Freight Forwarders Tanzania, Veronica Chilunda amesema kampuni imeguswa na huduma nzuri zinazotolewa Mloganzila hivyo wameona watoe msaada huo kama sehemu ya kurejesha kwa jamii.
Akipokea msaada huo Naibu Mkurugenzi Mtendaji MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji, amewashukuru watumishi wanawake wa kampuni hiyo kwa msaada waliotoa kwani umekuja wakati muafaka wakati hospitali ikiwa katika maboresho hususani katika maeneo ya kutolea huduma na vifaa tiba.
Aidha Bi. Veronica ametoa wito kwa watu na makampuni mbalimbali kujitokeza kusaidia mahitaji katika hospitali hiyo ambayo kwa sasa imepanua wigo wa utoaji huduma.
TANZANIA COMMERCIAL BANK YAWAFIKIA WANAWAKE WENYE UHITAJI HOSPITAL YA OCEAN ROAD WAKISHEREHEKEA SIKUKUU YA WANAWAKE DUNIANI
Meneja Mawasiliano na Uhusiano Tanzanian Commercial bank (TCB), Gloria Mutta (watatu kulia) akikabidhi misaada wa vitu mbalimbali kwa Afisa Ustawi wa jamii wa Hospitali ya Ocean Road Cancer Institute (ORCI) Devotha Kibanga Kwaajili ya kusaidia wagonjwa wanawake wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya Ocean road jijini Dar es Salaam Ukiwa ni kusherehekea siku kuu ya wanawake inayofanyika kila tarehe 8 ya mwezi wa tatu kila mwaka wengine pichani ni wafanyakazi ya hospital hiyo Hafla hiyo imefanyika jana.
Katika kusherehekea sikukuu ya mwanamke duniani, Tanzania Commercial Bank (TCB) imeendelea kuwa karibu na wateja wake katika kuzingatia usawa wa kijinsia kwa maisha endelevu.
Tanzania Commercial Bank (TCB) imetumia sikukuu hiyo kuwakumbuka na kuwatembelea wagonjwa wanawake wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya Ocen Road na kutoa misaada mbalimbali.
Akizungumza wakati alipotembelea wagonjwa hao Meneja mawasiliano na uhusiano wa Benki hiyo Bi. Gloria Mutta ameeleza kuwa "Tanzania Commercial Bank(TCB) imeendelea kuwa karibu na jamii kwa kutoa misaada mbalimbali hususani kwa wenye mahitaji maalum".
Ameeleza kuwa " Tanzania Commercial Bank (TCB) imetambua mchango wa mwanamke katika kuleta maendeleo"
Aliwahamasisha wanawake hao kuendelea kuiamini na kuitumia Benki hiyo kwani tumekuwa tukitoa misaada mbalimbali pale tunapohitajika.
mutta aliongeza kuwa benki ya TCB inatoa huduma nchi nzima ina matawi ambayo yanafanya kazi masaa 24 yote hayo ni kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata huduma muda wowote.
Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii Ocean Road Cancer Institute (ORCI) Devotha Kibanga ameishukuru benki hiyo na kusema kuwa imekuwa mstari wa mbele katika kutoa misaada kwa jamii inayotuzunguka hususani sekta ya afya
Wednesday, March 8, 2023
Benki Ya Absa Yawataka Wanawake Kujiamini
Thursday, March 2, 2023
TANGA CEMENT NA MIAKA 20 UDHAMINI WA KILIMARATHON
Akizungumza mara baada ya kumaliza kwa mbio hizo zilizofanyika 26 Februari 2023, katika Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Meneja wa Biashara wa Tanga Cement PLC, Peet Brits amesema, huu ni mwaka wa 20 wa ushiriki wao wakiwa wadhamini wakongwe na wakimbiaji kupitia timu za Simba katika mbio hizo ambazo Simba Cement na waandaaji wa Kili Marathon wamekuwa wakiziboresha hadi kufikia miaka 20 kwa mwaka 2023.
Amesema, udhamini wa mbio hizo ni kutokana na umuhimu wa michezo hasa Kili Marathoni ambayo huwakutanisha wafanyakazi wa Simba Cement na kufanya shughuli hii kwa umoja kama wanavyofanya viwandani pamoja kukutana na wadau pamoja na wateja wao.
"Katika ushiriki wetu hatukuangalia vyeo au nafasi zetu za kazi tuliona, Mkurugenzi Mtendaji akigawa maji kwa wakimbiaji, tulizungumza lugha moja kutoka langoni hadi kileleni kwa ushirikiano na wafanyakazi ambao ni wakimbiaji (Timu Simba) kwa pamoja na wakimbiaji wengine, wadau na wateja," alisema.
Pia alisema, wakati wa baada ya mbio hizo wafanyakazi ambao ni wakimbiaji wamekutana na wateja na wadau wao Kanda ya Kaskazini na kubadilishana mawazo ya uboreshaji katika huduma.
Kuhusiana na mafanikio kupitia mbio za Kili Marathon Peet amesema, wamefurahi kushirikiana katika mbio hizo zilizofanyika kwa mara ya 20 sasa na kufanya vizuri katika mbio hizo pamoja na kutoa huduma ya kugawa maji kwa wakimbiaji wa Kilometa 42 na 21 waliopita katika kituo chao cha kugawa maji.
"Tuna uhakika wakimbiaji wamefurahi kupita katika kituo chetu cha Point 8 wakati wa mbio hizi na kupata huduma, tutaendelea kushiriki katika tukio hili kila mwaka. Tunaipenda na kuithamini Kili Marathon na tunafurahi kudhamini kwa kugawa maji kwa wateja wetu na wadau wote waliopita katika 'Water Point' yetu na hawa ni kutoka katika mikoa ya Kaskazini ikiwemo Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga na mikoa mingine," alieleza.
Aidha amesema, kwa mwaka huu walijipanga kufanya vyema zaidi ikilinganishwa na mwaka uliopita kwa kuongeza idadi ya wakimbiaji kwa timu Simba pamoja na kuongeza nguvu baina yao kwa kuwapa moyo wakimbiaji na kumaliza kwa ushindi.
Vilevile amesema, wamekuwa na Timu hiyo inayojumuisha wafanyakazi si kwa mashindano ya Kili Marathon pekee na kampuni ilihakikisha gharama zote ikiwemo vifaa, malazi, usafiri na burudani zinatolewa kwa kila mshiriki ili waweze kupata ushindi na kueleza kuwa wamekuwa na mashindano mbalimbali katika idara ambayo yameleta chachu kwa kampuni kudhamini timu hiyo ya Simba.
Peet amesema kwa mwaka huu, wamevunja rekodi kwa kuwa na jumla ya washiriki 28 na kupitia Kili Marathon, wamesherehekea kwa upekee mafanikio ya mwaka 2022 wakiwa washindi wa jumla wa tuzo ya Rais kwa mzalishaji bora wa mwaka na mshindi wa jumla wa tuzo ya taarifa ya fedha iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA.)