A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Thursday, June 13, 2019

BENKI YA KCB KUTOA RUZUKU YA MILIONI 85 /-KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI.


Mkuu Wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya  KCB, Christine Manyenye (katikati) akizungumza na waaandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa programu ya 2jiajiri ambapo jumla ya sh.milioni 85 zinatarajiwa kutolewa kwa wanawake 17 ili kukuza biashara zao, aliyekaa kushoto kwake ni  Mnufaika wa mafunzo hayo pia ni Mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya East Coast ya Kibaha,Bhoke Mhini,  kulia kwake ni Rojas Mdoe, Mkuu wa kitengo cha uendeshaji na technology na mwishoni Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa hafla hiyo imefanyika leo Makao makuu ya Benki hiyo
Mkuu Wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya  KCB, Christine Manyenye (katikati), akizungumza na waaandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa programu ya 2jiajiri ambapo jumla ya sh.milioni 85 zinatarajiwa kutolewa kwa wanawake 17 ili kukuza biashara zao, aliyekaa kushoto kwake ni  Mnufaika wa mafunzo hayo pia ni Mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya East Coast ya Kibaha,Bhoke Mhini,  kulia kwake ni Rojas Mdoe, Mkuu wa kitengo cha uendeshaji na technology na mwishoni Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa hafla hiyo imefanyika leo Makao makuu ya Benki hiyo
Mkuu Wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya  KCB, Christine Manyenye, akizungumza wakati wa hafla hiyo  wengine ni Maofisa wa Benki hiyo pamoja na waandishi wa habari


Mnufaika wa Mafunzo hayo na Mkurugenzi wa shule ya Sekondari ya East Coast ya Kibaha,Bhoke Mhini, akizungumza wakati wa hafla hiyo, kulia ni Mkuu Wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya  KCB, Christine Manyenye pamoja na Maofisa kutoka Benki hiyo

Benki ya KCB Tanzania leo imezindua awamu ya pili ya programu yake ya 2jiajiri katika warsha iliyofanyika katika makao makuu yabenki hiyo jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo iliyohudhuriwa na baadhi ya walengwa wa programu ya 2jiajiri, wafanyakazi wa Benki ya KCB, waandishi wa habari na wadau mbali mbali umeendelea kuonyesha dhamira ya dhati ya benki hiyo katika kumnyanyua mwanamke wa Kitanzania.

Tangu kuzinduliwa kwake mwaka 2016, programu ya 2jiajiri imefanikiwa kuwawezesha wanawake 256 wa Kitanzania katika sekta ya biashara kwa kuwapa mafunzo mbali mbali na kuwapanulia wigo wa masoko ili kukuza mitaji na uwezo wa kibiashara.

2jiajiri kwa Mwaka 2019 inafanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ililenga katika kutoa mafunzo nadharia kwa wanawake 256 katika nyanja za kurasimisha biashara, usimamizi wa fedha na mafunzo ya kuongeza mauzo na kukuza soko la biashara zao.

 Aidha wanawake 115 kati ya 256 walipitia mafunzo kwa vitendo katika nyanja mbali mbali. Awamu ya pili ambayo imezinduliwa leo tarehe 12 Juni 2019 inatarajia kutoa ruzuku ya TSH 5,000,000.00 kwa washiriki wa programu hiyo ambao wamekamilisha na kufuzu awamu ya kwanza ya programu ya 2jiajiri.

Jumla ya walengwa 17 watapitia mchujo ili kuhakikisha ustahili wa na matumizi sahihi ya ruzuku hiyo ili kukuza biashara zao. Akiongea katika uzinduzi huo, Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Bi. Christine Manyenye alisema japo ruzuku hiyo haina marejesho, Benki ya KCB itaendelea kufuatilia kwa karibu maendeleo ya wapokeaji ili kuhakikisha wanawake hao wanafikia malengo yao ya kibiashara.

Aidha Bi. Manyeye aliainisha vigezo ambavyo wapokeaji wanatakiwa kukidhi vikiwemo kujaza fomu inayopatikana katika tovuti ya Benki ya KCB na matawi yake nchi nzima, lazima mpokeaji awe amekamilisha mafunzo ya kinadharia na vitendo katika awamu ya kwanza, awe muendesha akaunti ya 2jiajiri iliyo hai na awe mwenye cheti na leseni halali ya usajili wa biashara.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Bi. Bhoke Mukoji Mhini, Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Sekondari ya East Coast iliyo Kibaha ambaye ni mmoja wa walengwa wa programu ya 2jiajiri alisema kwamba hajawahi kuona dhamira ya dhati katika kumuwezesha wanawake wa Kitanzania na kuwa Benki ya KCB na 2jiajiri ni mfano wa kuigwa na taasisi nyingine.

“KCB Bank na mpango wa 2jiajiri umenyanyua ufito wa uwekezaji kwa jamii. Kuhusu Benki ya KCB Benki ya KCB ni benki kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Toka hapo benki imekua na kuenea katika nchi 6 za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia.

 Leo hii ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 262, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 15,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki Afrika Mashariki. Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation.

Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Benki ya KCB Tanzania ni mlipa kodi mzuri, mwajiri wa watanzania zaidi ya 300, inafundisha wafanyakazi wake weledi wa kikazi na pia pale inapotokea nafasi inapeleka wafanyakazi katika soko la Afrika

Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive