A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Saturday, August 27, 2022

ZAIDI YA WAKAZI 500 KUNUFAIKA NA KAMBI YA MACHO BURE BAGAMOYO

 

Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo, Bw. Shauri Selenda, akiongea na wakazi wenye matatizo ya macho walijitokeza kupata matibabu ya macho bure katika kambi ya siku tatu ya huduma za macho bure iliyofadhiliwa na Lions Club ya Dar es Salaam-Mzizima—Kambi hiyo imezinduliwa Hospital ya Wilaya Bagamoyo jana--ambapo jumla ya wakazi 300 walipimwa na kati yao 50 walifanyiwa upasuaji. (picha na mpiga picha Wetu).
Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo, Bw. Shauri Selenda, (wapili kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Taasisi ya Lions Club , Dar es Salaam-Mzizima, wakati wa uzinduzi wa kambi maalum ya kutoa huduma za macho bure katika viwanja vya Hospital ya Wilaya Bagamoyo, iliyofadhiliwa na Lions Club—ambapo jumla ya wakazi 300 walipimwa na kati yao 50 walifanyiwa upasuaji. (picha na mpiga picha Wetu).

Mmoja wa Mjumbe wa Lions Club , Dar es Salaam-Mzizima akigawa zawadi mmoja wa wazazi waliojifungua katika Hospital ya Wilaya Bagamoyo, kama sehemu misaada inayotolewa na Taasisi hiyo kwa watu hahitaji





Zaidi ya wakazi 500 wa Bagamoyo wenye matatizo mbalimbali ya macho wanatarajia kupata matibabu bure katika kambi maalum ya matibabu ya macho Bure katika hospital ya Wilaya Bagamoyo, chini ya ufadhili wa Lions Club ya Dar es Salaam-Mzizima.

 

Kambi maalum ya kupima na kufanya upasuaji wa macho Bure imeanza jana katika hospitali ya wilaya bagamoyo na mpaka sasa zaidi ya wakazi 300 wamejitokeza kupima na 50 kati yao wamefanyiwa upasuaji.

 

“Tunashukuru sana watu wote waliofanyiwa upasuaji sasa hivi wanaona vizuri.  Kambi hii ni ukombozi mkubwa kwa wakazi wa Bagamoyo, hasa ukizingatia kuwa karibu asilimia 50 ya watu wa Bagamoyo wana matatizo ya mtoto wa jicho,” amesema Mkurugenzi wa Wilaya Bagamoyo, Bw. Shauri Selenda, wakati wa uzinduzi rasmi wa kambi ya   zaidi watu

 

Imefadhiliwa na Lions Club ya Dar es Salaam- Mzizima

 

Zaidi ya 300 wakazi bagamoyo wamejitokeza kufanyiwa vipimo vya matatizo ya macho na 50 kati yao wamefanyiwa operation na sasa wanaona vizuri.

 

"Wakazi wengi wenye matatizo ya macho wanaendelea kujitokeza, na katika zooezi lengo letu ni kifanya upasuaji kwa watu zaidi ya 200...." amesema Mkurugenzi wa Wilaya Bagamoyo , Shauri Selenda, wakati ufungizi rasmi wa kambi ya siku 3 ya kutuo huduma bure ya upimaji wa macho na upasuaji kwa wakazi wilayani huyo.

 

Mkurugenzi huyo ameishukuru Club ya Lions- Mzizima kwa kufadhili utoaji ya huduma hiyo bure, na kuwataka wadau wengine wa maendeleo kuiga mfano wa Lions Club mzizima, ili kuwakwamua watanzania wengi wanakabiliwa na matatizo ya macho—wilaya Bagamoyo na nchi nzima kwa ujumla.

 

Hata hivyo Mkurugenzi huyo, ametoa wito kwa Taasisi ya Lions Club Mzizima, awamu ijayo huduma hiyo ipanuliwe hadi katika mashule ya sekondari na msingi, ili kuwasaidia “watoto wetu wenye matatizo ya macho"

 

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Hospital ya Wilaya Bagamoyo, Bi. Kandi Lusingu, amesisitza kuwa awamu ijayo zoezi la upimaji wa macho liende sambamba na utoaji wa miwani kwa watu waliugulika kuwa na matatizo ya kuona, na kuongeza kuwa hatua hiyo itafanya zoezi hili kuwa na tija na manufaa kwa watu wenye matatizo hayo.

 

"Pia naunga mkono zooezi hili kufanyika mashuleni , kwani itasaidia sana kuboresha uwezo wa vijana wetu, kuongeza ufualu, na pia kuongeza nguvu kazi ambayo ni nguzo mihimu kwa maendeleo taifa letu,” amesema Bi. Lusingu.

 

Nae Raisi wa Lions Club Mzizima, Baruani Muslim  "Katika zoezi hili, taasisi yetu inalenga kuwasaidia wakazi zaidi 500 wa Bagamoyo wenye matatizo mbalimbali ya macho.. mbali na macho, Lions Club tunasaidia jamii katika maeneo mbalimbali—upimaji wa kisukari, utunzaji wa mazingira na mengine mengi."

 

"Lions Club Mzizima itaendelea kushirikiana na serikali, katika wasaidia watanzania wenye matatizo mbalibali, lengo kuu likiwa ni kuboresha maisha ya watanzania na kulewezesha Taifa kupiga hatua kubwa za maendeleo.

 

Mmoja wa wanufaika wa kambi ya macho Bagamoyo, Omary Shukuru amesema ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi wanasikia huduma kama hizi za bure, na kuongeza kuwa “katika hali ya kawaidia huduma hizi zina gharama kubwa ambazo mwananchi wa kawaidia hawezi kumudu.”

Share:

Thursday, August 11, 2022

WAZIRI BITEKO ATEMBELEA KIWANDA CHAKUZALISHA MKAA MBADALA

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi kutoka shirika la Madini la Taifa STAMICO Pili Athumani (wapili kushoto), alipotembelea kiwanda chakuzalisha mkaa mbadala kinachomilikiwa na Shirika hilo kilichopo jijini Dae es Salaam. kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse

Waziri wa Madini Doto Biteko akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse (kulia), wakati wa ziara ya waziri kutembelea kiwanda chakuzalisha mkaa mbadala kinachomilikiwa na Shirika hilo kilichopo jijini Dae es Salaam. 
Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza na wanahabari wakati alipotembelea kiwanda cha kuzalisha mkaa mbadalakinachimilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kilichopo nsasani Dar es Salaam.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse akizungumza na wanahari wakati wa ziara ya waziri wa Madini alipofanya ziara ya kikazi kutembelea kiwanda kiwanda chakuzalisha mkaa mbadala kinachomilikiwa na Shirika hilo kilichopo jijini Dae es Salaam.
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko (kushoto), akikabidhi zawadi ya mkaa mbadala kwa Mwaandishi wa Habari wa kituo cha Startv Piensia Rugarabamu mkaa huo unaozalishwa na kiwanda kinachomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa STAMIKO alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Msasani jijini Dar es Salaam. katika ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko (kushoto), akikabidhi zawadi ya mkaa mbadala kwa Mwaandishi wa Habari wa kituo cha GLOBALTV Denis Mtima, mkaa huo unaozalishwa na kiwanda kinachomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa STAMIKO alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Msasani jijini Dar es Salaam. katika ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dkt. Venance Mwasse.... Picha zote na Brian Peter



………………………………….


Katika kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amepongeza jitihada na ubunifu unaofanywa na shirika hilo.

Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha mkaa mbadala wa kupikia unaojulikana kama Rafiki Coal Briquettes unaotokana na makaa ya mawe kilichopo jijini Dar es Salaam.

Dkt. Biteko amesema, pamoja na Serikali kuendeleza juhudi za kupambana na matumizi ya mkaa utokanao na misitu na badala yake kutumia nishati mbadala, STAMICO imeunga mkono jitihada hizo kwa kuanzisha kiwanda cha kuzalisha mkaa wa mawe kwa ajili ya matumizi ya kupikia majumbani.

Aidha, Dkt. Biteko amesema kwa sasa STAMICO ina jumla ya uwekezaji wa zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 63.1 ukilinganisha na miaka michache iliyopita ambapo Shirika lilifisika na kutaka kufungwa.

Pia, Dkt. Biteko amesema STAMICO imeagiza mitambo mipya 11 kwa ajili ya uchorongaji na mitambo 4 kwa ajili ya kuzalisha makaa ya mawe ili kuongeza uzalishaji wa makaa hayo na kukidhi mahitaji ya watanzania ambapo mitambo hiyo itasimikwa jijini Dodoma, Songwe, Pwani na Kanda ya Ziwa.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse amesema, Shirika hilo lina mkakati wa kuhakikisha kunakuwa na uzalishaji wa kutosha ili kukidhi mahitaji ya watanzania ambapo limeagiza mitambo miwili yenye uwezo wa kuzalisha tani 20 za makaa hayo kwa saa.

Dkt. Mwasse amesema, mradi huo unatarajia kuwanufaisha watanzania kwa kutoa ajira na utapunguza janga la ukataji miti kwa ajili ya mkaa hivyo kuchangia kutunza mazingira.

Dkt. Mwasse amesema STAMICO imeanza kusambaza nishati hiyo ambayo ni nafuu zaidi na rafiki kwa mazingira baada ya kuidhinishwa na Shirika la Viwango la Taifa (TBS) tayari kwa matumizi baada ya uzalishaji wa majaribio kufanyika kwa ufanisi.

Aidha, Dkt. Mwasse amesema mkaa huo una faida lukuki na baadhi amezitaja kuwa ni pamoja na rafiki wa mazingira, kuokoa pesa nyingi zinazotumika kwenye nishati nyingine, mkaa wa mawe wakupikia unadumu jikoni kwa muda mrefu kuliko mkaa wa miti hivyo kuzidi kupunguza gharama za matumizi ya nishati hiyo, huboresha usafi wa jikoni na maeneo ya nyumbani yanayochafuliwa na mkaa wa miti.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mwasse amesema, misitu ni muhimu kwa maisha ya binadamu na viumbe hai kwa kuwa huifadhi vyanzo vya maji, kuboresha hali ya hewa, kuzuia mmomonyoko wa ardhi, malisho ya mifugo, kuboresha shughuli za kilimo na kuboresha mandhari ya nchi mijini na vijijini ambapo amewataka watanzania kuunga mkono matumizi ya makaa hayo ambayo matumizi yake ni rahisi na hupika kwa haraka zaidi na yana faida nyingi kuliko mkaa wa miti ambao athari zake kimazingira ni kubwa.

Dkt. ameongeza kuwa, kutokana na manufaa ya mkaa huo, tayari STAMICO inaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa jamii kubwa inanufaika na inatumia mkaa huo ambao ni wazi utasaidia kufanikisha kampeni ya utunzaji wa misitu ambapo kwa kuzingatia umuhimu wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isidor Mpango anatarajiwa kuuzindua rasmi mkaa huo Agost 12, 2022 ili uanze kutumika rasmi na watanzania wote.
Share:

Tuesday, August 9, 2022

BINTI FOUNDATION YATANGAZA NEEMA KWA VIJANA WA TANZANIA


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Binti Foundation, Johari Sadiq, akizungumza wakati wa hafla ya yakuwaaga vijana 16 waliokuwa wakipatiwa mafunzo ya ushonaji na ubunifu katika Taasisi hiyo mafunzo yaliyokuwa yakitolewa bure ikiwa ni muendelezo wa Taasisi hiyo kuwapatia nafasi vijana wa kitanzania ikiwa ni juhudi za Binti Binti foundation kuunga mkono serikali hasa katika soko la ajira.
Afisa Mtendaji wa kata ya Kunduchi Abel Silaa (kulia), akitoa cheti cha kuhitimu mafunzo ya ushonaji yaliyokuwa yakitolewa bure na Taasisi ya Binti Foundation wakati wa hafla ya yakuwaaga vijana 16 waliokuwa wakipatiwa mafunzo hayo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Johari Sadiq pamoja na mwalimu mkuu wa mafunzo hayo.
Picha ya pamoja

Share:

Thursday, August 4, 2022


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive