A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Thursday, December 15, 2022

Wafanyakazi Wa Absa Wasaidia Madawati Kwa Watoto Wenye Mahitaji

Mkurugenzi wa Kitengo cha Utumishi na Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Patrick Foya (kushoto) akikabidhi madawati 37 yaliyowezeshwa kwa michango ya wafanyakazi wa benki hiyo kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Sezaria Kiwango ili kuwawezesha wanafunzi wenye uhitaji maalumu kupata mazingira bora ya mahali pa kujisomea. Madawati hayo yenye thamani ya sh milioni 10 yalikabidhiwa shuleni hapo, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kulia ni Ofisa Elimu Kata ya Gerezani, Mary Ruta na Ofisa Mauzo Absa, Jacqueline Asley.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Utumishi na Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Patrick Foya akishikana mikono na baadhi ya wanafunzi wenye uhitaji maalum wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhi msaada wa madawati 37 yenye thamani ya sh milioni 10 yaliyopatikana kwa michango ya wafanyakazi wa benki hiyo katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Kariakoo. madawati hayo yatawezesha wanafunzi wenye uhitaji maalumu kupata mazingira bora ya mahali pa kujisomea.
Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Benki ya Absa Tanzania, George Binde (kushoto) akikabidhi madawati 37 yenye thamani ya sh milioni 10 yaliyopatikana kwa michango ya wafanyakazi wa benki hiyo Kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Sezaria Kiwango Katika hafla iliyofanyika shuleni hapo, Kariakoo, Dar es Salaam. Madawati hayo yatawawezesha wanafunzi wenye uhitaji maalumu kupata mazingira bora ya mahali pa kujisomea.
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Hellen Siria (kulia) akisalimiana na Mwanafunzi.mwenye ualbino wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Mirfat Ibrahimu huku wenzake wakiangalia katika hafla ambayo wafanyakazi wa benki hiyo walikabidhi msaada wa madawati 37 yenye thamani ya sh milioni 10 shuleni hapo, Kariakoo, Dar es Salaam. Madawati hayo yatawawezesha wanafunzi wenye uhitaji maalumu kupata mazingira bora ya mahali pa kujisomea.
Wafanyakazi wa Benki ya Absa wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko baada kuwakabidhi msaada wa madawati 37 yenye thamni ya shilingi milioni 10 shuleni hapo, kariakoo, Dar es Salaam.
Share:

Thursday, December 8, 2022

Absa yazindua Ripoti ya Viashiria vya Masoko ya Fedha Afrika

Naibu Katibu Mkuu (Sera), wa Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru akihutubia kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba wakati akizindua ripoti ya Absa ya Viashiria vya Masoko ya Fedha Afrika, jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Absa, Simon Mponji, akitoa shukurani kwa Waziri wa Fedha pamoja na Naibu Katibu Mkuu kwa kukubali wito wa kufika katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Obedi Laiser, akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam hiyo akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, Abdi Mohamed.
Mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Absa kutoka ofisi ya Kanda, Jeff Gable akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Masoko ya Kifedha wa Absa Tanzania, Esther Maruma, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti hiyo jijini humo jana.
Naibu Katibu Mkuu (Sera), wa Wizara ya Fedha na Mipango, Lawrence Mafuru (wa tatu kulia),na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Absa Tanzania, Simon Mponji (wa nne kushoto), wakionyesha kitabu chenye ripoti ya Absa ya Viashiria vya Masoko ya Fedha Afrika,mara baada ya kuzinduliwa kwake jijini Dar es Salaam jana. Kushoto kwa Mafuru ni Mkurugenzi wa Fedha wa Absa, Obedi Laiser na Mkurugenzi wa Masoko ya Kifedha wa Absa Tanzania, Esther Maruma. Kushoto ni watoa mada, Anthony Kirui kutoka Absa Afrika, Abraham Byamungu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji (UNCDF), Charles Shirima kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) na Jeff Gable kutoka Absa Afrika.
Baadhi ya wageni waliolikwa katika hafla hiyo wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi naibu katibu mkuu sera wa wizara ya fedha jijini Dar es Salaam jana.
Share:

Monday, December 5, 2022

Benki ya DCB yafunga mwaka ikiendelea kubeba tuzo lukuki

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Jamali Kassim Ali (katikati), akikabidhi tuzo kwa Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya DCB, Costantine Mtumbuka jijini Dar es Salaam hivi karibuni baada ya benki hiyo kuibuka mshindi wa kwanza wa uandaaji bora wa hesabu kwa mwaka 2021 katika kundi la benki ndogo na za kati. Hii ni mara ya saba kwa DCB kushinda tuzo hizo za kila mwaka zinatolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA). Kulia ni Meneja Fedha wa DCB, Siriaki Surumbu na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA. Prof. Sylivia Temu. Hii ni mara ya saba kwa DCB kushinda tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na NBAA.

*Yanyakua tuzo ya NBAA kwa kuwasilisha mahesabu yaliyonyooka

Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya DCB, Costantine Mtumbuka (kushoto), Meneja Fedha, Siriaki Surumbu (katikati) na Ofisa Masoko na Mawasiliano Wa benki hiyo, Caroline Gabriel Nnko wakionyesha tuzo ya mshindi wa kwanza wa uandaaji bora wa hesabu kwa mwaka 2021 katika kundi la benki ndogo na za kati zinatolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Jamali Kassim Ali jijini Dar es Salaam. Hii ni mara ya saba kwa DCB kushinda tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na NBAA.
Maofisa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya DCB, Caroline Gabriel Nnko (kushoto), na Adelah Kaihula wakionyesha tuzo ya mshindi wa kwanza wa uandaaji bora wa hesabu kwa mwaka 2021 katika kundi la benki ndogo na za kati zinatolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Jamali Kassim Ali (hayupopichani), jijini Dar es Salaam.
Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya DCB, Costantine Mtumbuka (wa pili kulia waliosimama), akionyesha tuzo ya mshindi wa kwanza wa uandaaji bora wa hesabu kwa mwaka 2021 katika kundi la benki ndogo na za kati zinatolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Jamali Kassim Ali (katikati waliokaa), jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Share:

Monday, November 21, 2022

TANGA CEMENT YASHINDA TENA MZALISHAJI BORA TUZO ZA RAIS

guardian
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango akikabidhi Tuzo za 16 za Rais za wazalishaji bora wa Viwandani (PMAYA), kwa mshindi wa jumla ya wazalishaji bora wa mwaka 2021 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement wazalishaji wa Simba Cement (TCPLC), Reinhardt Swart,wakati wa hafla iliyoandaliwa na na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) jijini Dar es Salaam Tanga cement iliibuka kidedea kwa kuwa mshndi wa jumla na kuwa mzalishaji Bora wengine pichani ni Maofisa kutoka Tanga Cement.
1%20(136)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango akikabidhi Cheti cha Udhamini wa Tuzo za 16 za Rais za Wazalishaji Bora wa viwandani (PMAYA) kwa Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Kampuni ya Tanga Cement, Bi. Mtanga Noor pamoja na Ofisa Mawasiliano wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Helen Maleko ambapo Tanga cement waliibuka kidedea kwa kuwa mshndi wa jumla na kuwa mzalishaji Bora wa Makampuni.
1%20(127)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango, akizungumza wakati wa wa hafla ya utoaji Tuzo za Rais kwa wazalishaji bora wa viwandani.
1%20(79)
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement wazalishaji wa Simba Cement (TCPLC), Reinhardt Swart, pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Tanga Cement wakiwa katika hafla hiyo.
1%20(121)
1%20(3)
Picha ya Pamoja
Share:

Thursday, November 10, 2022

Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi yazinduliwa jijini Dar

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Angelina Ngalula (wa pili kushoto) na Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM, Rukia Yazid, wakizindua nembo kuashiria uzinduzi rasmi wa Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi 2022 jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Angelina Ngalula (wa tatu kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi wa Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi 2022. Wengine ni viongozi wa TPSF na wawakilishi wa makampuni wadhamini.
Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM, Rukia Yazid (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi wa Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi 2022. Wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa TPSF, Bi. Angelina Ngalula, viongozi wa TPSF na wawakilishi wa makampuni wadhamini.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bi. Angelina Ngalula, akipokea mfano wa hundi ya shs 58,300,000 kutoka kwa Mkuu Uendeshaji wa Kundi la Makampuni ya Bravo, Evarist Maganga (wa pili kulia) ikiwa ni udhamini wa kampuni hiyo katika maadhimisho ya Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi 2022 wakati wa hafla ya uzinduzi wake jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa Siku ya Taasisi ya Sekta Binafsi jijini Dar es Salaam leo.
Share:

Thursday, October 13, 2022

SWISSPORT YAKABIDHI MSAADA WA ULTRASOUND CCBRT

   IMG_7289

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi akipokea kifaa tiba - mashine ya Ultrasound kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania Mrisho Yassin katika hafka iliyofanyika leo Hospitalini hapo Jijini Dar es Salaam

 

WhatsApp%20Image%202022-10-13%20at%203.39.47%20PM

Muonekano wa kifaa tiba 'Ultrasound


IMG_7271

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi (kulia), akizungumza wakati wa hafla ya  makabidhiano  ya kifaa tiba cha Ultrasound kilichotolewa na Swissport kwa ajili ya Kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto  chenye thamani ya shilingi Milioni 68.

IMG_7259
Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania Mrisho Yassin akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kukabidhi kifaa tiba cha Ultrasound kwa ajili ya Kitengo cha Afya ya mama ma mtoto katika Hospitali ya CCBRT leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi


KATIKA kuhakikisha sekta ya afya inazidi kukua na jamii ya watanzania  inakuwa na afya bora kampuni ya Swissport Tanzania PLC  imeendelea kuwa karibu na jamii na kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Sama Suluhu Hassan kwa kutoa msaada wa kifaa tiba ‘Ultrasound’ chenye thamani ya shilingi milioni 68 katika taasisi ya CCBRT.



Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Swissport Tanzania PLC Mrisho Yassin amesema mchango huo umeelekezwa kuwasaidia akina Mama wajawazito.

‘’Tunatambua kuna changamoto ya vifaa tiba na sisi kama kampuni tumeliona hili na kuona kutoa mchango huu, kwa taarifa tuliyopewa kifaa hiki kitasaidia sana kutokana na uhiitaji wa mashine hii hapa CCBRT ili kusadia jamii ya watanzania  akina Mama wajawazito.’’ Amesema.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya CCBRT Brenda Msangi ameishukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kuchangia kifaa tiba hicho cha Ultrasound kitakachoongeza nguvu ya kuwahudumia akina Mama wajawazito wengi zaidi na kwa ufasaha.



‘’Sisi kama CCBRT asilimia 87 ya wagonjwa wanaokuja hapa ni aidha wanapata huduma za bure kabisa au wanachangia….Tunahitaji kushikwa mkono katika maeneo makuu matatu ya huduma za kibingwa na bobezi za afya, mafunzo kwa wafanyakazi na watoa huduma na eneo la vifaa na vifaa tiba na tunawashukuru Swissport na tuendeleze uhusiano huu.’’ Amesema.



Amesema, tangu kuanza kutolewa kwa huduma katika kitengo cha Mama na Mtoto mwezi Januari hadi Oktoba mwaka huu wamewahuduma akina Mama wapatao 225.



‘’CCBRT tunatoa shukrani zetu za dhati kwa SwissPort kwa kututembelea na kutoa kifaa hiki  kwa umoja huu iko siku ambayo tutaona kila mwanamke anayepata ujauzito anajifungua salama na kwa furaha….Tunashukuru sana kwa msaada wenu na ushirikiano wenye kwenye huduma hizi za kuokoa maisha ya watu.’’ Amesema.



Aidha amesema, mwezi Julai mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu alizindua rasmi kitengo cha Afya ya Mama na Mtoto ambacho kimepewa jina la ‘CCBRT- Samia Suluhu Hassan Maternity Wing’ kutokana na juhudi binafsi na Serikali anayoiongoza katika kupigania afya za akina Mama wajawazito na watoto wachanga pamoja na maboresho makubwa ya sekta ya afya nchini kote.



‘’Lengo la kuanzishwa kwa kitengo hiki ni cha uzazi ni kutaka kuwahakikishia akina Mama wote uzazi salama, kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi sambamba na kuzuia ulemavu….kitengo hiki kimedhamiria kuwahudumia akina Mama wajawazito wenye ulemavu, wenye historia hatarishi za uzazi, akina Mama wenye historia ya fistula na mabinti wanaopata mimba katika umri mdogo.’’ Amesema.

Share:

Monday, October 10, 2022

Benki ya Absa kutoa huduma bora zaidi zinazokidhi mahitaji ya wateja

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Melvin Saprapasen (wa tano kushoto), Meneja wa Absa Tawi la Ohio, Ally Janja (kushoto kwake), wafanyakazi wa Absa pamoja na Wateja wakigonganisha glasi kutakiana afya njema na mafanikio katika moja ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja ya benki hiyo jijini Dar es Salaam wiki iliyopita. Katika maadhimisho hayo viongozi wa ngazi za juu wa benki hiyo walitembelea matawi ya Absa nchini kote ili kuzungumza na wafanyakazi na pia Wateja wao ili kuweza kuona namna bora ya kuwahudumia na kushughulikia mahitaji yao.
Meneja wa Kitengo cha Bima wa Benki ya Absa Tanzania, Sandeep Chavda (kushoto), akimpa zawadi mmoja wa Wateja wa Absa Tawi la Dar City, huku Meneja wa tawi Hilo, Winford Mwang'onda akiangalia, katika hafla ya kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja tawini hapo, Dar es Salaam hivi karibuni.
Wafanyakazi wa Benki ya Absa Tawi la Alpha House pamoja na Wateja wao wakitakiana afya njema na mafanikio katika hafla iliyoandaliwa na tawi hilo kwa wateja wao, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.
Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Slipway, Veronica Okio (kulia), akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wateja wake katika hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, tawini hapo, Dar es Salaam hivi karibuni.
Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Pugu, Heri Sijaona (kushoto), akizungumza na wateja wa benki hiyo tawini hapo jijini Dar es Salaam hivi karibuni, katika
hafla ya kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Meneja wa Benki ya Absa Tawi la Zanzibar, Rabia Abood (katikati), akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wateja wake, Jabir Alfarsy katika hafla kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja katika tawi hilo visiwani humo hivi karibuni. Kushoto ni Meneja wa wateja Maalum katika tawi hi
lo, Salim Salum.
Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa Benki ya Absa Tanzania, John Beja (katikati, mwenye tai nyekundu) Mkurugenzi wa Fedha wa Absa Tanzania, Obedi Laiser (nyuma ya Beja), wakiselebuka pamoja na wafanyakazi na wateja wa Tawi la Absa Mikocheni, kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja tawini hapo, jijini Dar es Salaam wiki iliyopita
Mmoja wa watumishi waliofanyakazi kwa muda mrefu katika Benki ya Absa Tawi la Tanga, Mwanajumaa Darweshi (wa pili kulia), akionesha cheti cha shukurani muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Absa Tanzania, Ndabu Lilian Swere (kushoto), katika hafla iliyofanyika pamoja na maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja katika tawi hilo, mjini Tanga juma lililopita. Wa pili kushoto ni Meneja wa tawi hilo, Gloria Mallya.
Share:

Sunday, October 9, 2022

Benki ya DCB yang'ara ikiadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (katikati) akikata keki huku wafanyakazi na wateja wa Benki ya tawi la Victoria wakishangilia, wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, tawini hapo, Dar es Salaam wiki hii. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa.

Benki ya Biashara ya DCB imeendelea kung'ara wakati ikiadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mwaka huu huku ikianisha baadhi ya mafanikio iliyopata tangu ilipoanzishwa Mwaka 2000.
  • Benki ya kwanza kufuzu kutoka benki ya kijamii kwenda Benki ya Biashara.
  • Benki ya kwanza Tanzania kusajiliwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
  • Benki inayoongozwa na watanzania kuanzia Bodi ya Wakurugenzi hadi Menejimenti.
  • Benki imewanyanyua wajasiriamali wanawake zaidi ya 400,000 kupitia mikopo ya vikundi.
  • Benki inatoa huduma na bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wateja.
  • Benki ina Wateja kuanzia wajasiriamali wadogo, wafanyabiashara wa kati na wakubwa, wateja binafsi, waajiriwa, mashirika na makampuni.
  • Benki ipo sambamba na waajiriwa na inatoa mikopo yenye riba nafuu.
  • Benki ipo sambamba na wazazi kuwawezesha watoto elimu hadi chuo kikuu kupitia akaunti ya Skonga na mkopo wa ada.
  • Benki inatoa mikopo ya nyumba yenye masharti nafuu.
  • Fanya miamala na malipo mahali popote kupitia DCB Pesa, DCB Wakala, Visa, Master Card QR, DCB Malipo na Internet Banking.
  • Kufanya miamala nje ya nchi kupitia International money transfer na Western Union.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Bi. Zawadia Nanyaro (wa pili kulia), akikabidhi cheti cha shukurani kwa mmoja wa Wateja wa Tawi la DCB Victoria, Halima Iddi, katika hafla ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ya benki hiyo tawini hapo, jijini Dar es Salaam wiki hii. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya DCB, Nelson Swai (katikati), akikabidhi msaada wa viti, mashine ya kuchapia (printa) na mifuniko ya tairi za gari vilivyotolewa na DCB kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Magomeni, Mrakibu wa Polisi Edward Masunga, ikiwa ni sehemu ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, kituoni hapo, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Beki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (katikati), akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa benki katika moja ya shamrashamra wakiwapokea Wateja wao wajasiriamali wa mikopo ya vikundi waliofika katika hafla ya kuwapongeza katika makao makuu ya benki hiyo, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa akizungumza na wajasiriamali ambao kutoka vituo mbalimbali ambao ni wanufaika wa mikopo ya vikundi inayotokewa na DCB. Katika hafla hiyo DCB ilivitambua vituo bora na kukabidhi vyeti vya shukurani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto) akikabidhi cheti cha shukurani kwa baadhi ya wajasiriamali ambao kituo chao kufanya vizuri kwenye mikopo ya vikundi inayotolewa na benki hiyo. Hii ilikuwa ni moja ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, jijini Dar es Salaam wiki hii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto) akikabidhi cheti cha shukurani kwa baadhi ya wajasiriamali ambao kituo chao kufanya vizuri kwenye mikopo ya vikundi inayotolewa na benki hiyo. Hii ilikuwa ni moja ya matukio kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, jijini Dar es Salaam wiki hii.
Share:

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAJIVUNIA KUSHEREHEKEA HUDUMA BORA

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo Bi Janemary Rutahoile ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga, Mkurugenzi wa Teknohama na Uendeshaji wa benki hiyo Jema Msuya na kushoto ni Meneja wa TCB Tawi la Mlimani City Happy Ernest.Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo Bi Anna Philemoni ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga. Kushoto ni Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Mlimani City Happy ErnestAfisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga pamoja na wateja wa wa benki hiyoAfisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki Deodarus Nkeyera ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga na Kushoto ni Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Mlimani City Happy Ernest.


Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akimlisha keki Mteja wa Benki hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commecial Bank lililopo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu na utawala wa benki ya TCB Diana Myonga.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa benki hiyo.

Tanzania Commercial Bank (TCB)  imewahakikishia wateja wake kuwa inabuni mipango madhubuti ya kuzindua bidhaa mpya zinazoendana na mahitaji ya watumiaji wa huduma za kibenki kote nchini.

Akizungumza na wateja wake waalikwa wakati wa wiki ya Huduma kwa Wateja inayoendelea katika Tawi la Tanzania Commercial Bank lililopo Mlimani city jijini Dar es Salaam leo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank TCB Sabasaba Moshingi,  alisema  wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanatoa huduma bora na yenye kumdhamini mteja.

"Thamani yetu kuu iko katika uhakika kwamba tunamjali  na kuvutiwa na mteja, tunataka kuwahakikishia wateja wetu wapendwa kuwa tumejitolea kufanya uzoefu wako wa kibenki kuwa wa kufurahisha zaidi," alisema.

 

Anna Philemon, mteja wa Tanzania Commercial Bank alisema Benki ya TCB imeweka huduma zake na bidhaa ziko mikononi mwa mteja, na hivyo kuwasaidia wateja kufanya miamala kwa njia rahisi zaidi.

 

Anna alitoa wito kwa Watanzania kutoka nyanja mbalimbali kujiunga na Tanzania Commercial Bank na kufurahia baadhi ya huduma bora na bidhaa za kipekee zinazotolewa na benki hiyo.

Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive