A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Sunday, June 27, 2021

Yara kushirikiana na serikali kuhamasisha matumizi bora ya mbolea na ukulima wa kisasa

 
Meneja Biashara wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Philipo Mwakipesile, akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkulima wa Pamba kuhusu faida ya mbolea ya kupanda na kukuzia ya Yara katika eneo lililowekwa mashamba darasa kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba katika Kata ya Miguwa, Wilaya ya Nzega, Mkoani Tabora jana.
Meneja Biashara wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Philipo Mwakipesile (katikati) akizungumza na baadhi ya wakulima wa pamba pamoja na waalikwa wengine wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkulima wa Pamba kuhusu faida ya mbolea ya kupanda na kukuzia ya Yara katika eneo walilowekamashamba darasa kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba katika Kata ya Miguwa, Wilaya ya Nzega, Mkoani Tabora jana. Wa tatu kushoto ni Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Bodi ya Pamba Tanzania, Jones Bwahama.
Meneja Biashara wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Philipo Mwakipesile (katikati, aliyevaa kofia), wakulima wa pamba na waalikwa wengine wakiangalia zao la pamba katika moja ya mashamba darasa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkulima wa Pamba kwenye eneo lililowekwa mashamba darasa hayo kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba katika Kata ya Miguwa, Wilaya ya Nzega, Mkoani Tabora jana.
Viongozi kutoka Kampuni ya Mbolea ya Yara na Bodi ya Pamba, viongozi wa kiserikali, wakuliwa na waalikwa wengine wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkulima wa Pamba katika Kata ya Miguwa, Nzega, Tabora jana.

KAMPUNI ya mbolea ya Yara Tanzania imesema itaendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa mkulima wa zao la pamba anaongeza uzalishaji na tija ili kuinua kipato chake na pia kuongeza malighafi ya pamba itakayotumika katika viwanda vya hapa nchini.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mkulima wa Pamba katika Kata ya Miguwa, Wilayani Nzega Mkoani Tabora jana, Meneja Biashara wa Yara Tanzania, Philipo Mwakipesile alisema mafanikio hayo yataweza kupatikana endapo wakulima wa zao hilo watatumia kwa ukamilifu matumizi ya mbolea na kufuata kanuzi zote za ukulima wa kisasa.

Alisema Yara kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba Tanzania waliweka mashamba darasa 124 katika mikoa minne ya Simiyu, Mwanza, Tabora na Geita na wilaya zake 12 kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2020/21 ili wakulima wa zao la pamba waweze kujifunza kwa vitendo namna bora ya matumizi ya mbolea ya Yara huku kampuni hiyo ikitoa mifuko 31 ya mbolea ya kupandia na mifuko 31 ya mbolea ya kukuzia kwa mashamba darasa yote.

Kampuni ya Yara ina furaha kubwa kuona kile ilichofanya kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba kimekamilika na ni matumaini yetu wakulima wamejifunza umuhimu wa kutumia mbolea ili kuupa mmea lishe linganifu hivyo kuongeza uzalishaji wa pamba kwa eneo."

Hapa Miguwa tuliweka shamba darasa ekari moja lililotumia mbolea ya kupandia ya YaraMila Otesha (NPK 13:24:12) mfuko 1(50kg) na ya kukuzia kwa mbolea ya YaraBela Sulfan (CAN 24%N+6%S) mfuko 1(50kg) na ekari nyingine haikuwekwa mbolea kama kilimo cha wakulima wengi wa pamba wafanyavyo, ni matumaini yetu matokeo yake kama inavyooneka hapa yataleta hamasa kubwa kwa wakulima kutumia mbolea”, alisema.

Akizungumza mahali hapo, Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Bodi ya Pamba, Jones Bwahama alisema bodi hiyo imepanga kuhamsisha ulimaji wa zao hilo la pamba kwa kutoa elimu ya wakulima juu ya kuzingatia kanuni bora za kilimo kwa kutumia mbolea na madawa vizuri na kupanda kwa nafasi zinazostahili ambapo itawawezesha wakulima kuvuna zaidi ya kilo 1000 kwa ekari moja.

Naye Ofisa kutoka katika Ofisi ya Kilimo Mkoa wa Tabora, Modest Kaijage alisema matumizi ya mbolea ni muhimu sana kwa mafanikio ya wakulima wa mkoa huo kwani utaleta tija kwa wakulima na kwa Taifa.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Miguwa, Anjelina Nyanda alisema mashamba darasa yaliyowekwa na Yara kwa kushirikiana na Bodi ya Pamba katika kata hiyo yamewanufaisha wakulima wa kata hiyo kuacha kilimo cha mazoea na sasa kufanya kilimo chanye tija.

Mmoja wa wakulima wa Kata ya Miguwa, Mariam Mashala alisema amefurahishwa na matumizi ya mbolea ya Yara ya kupandia na kukuzia mahindi kwa kupata mavuno mengi kuliko awali hivyo anaomba mbolea hiyo iongezwe katika msimu ujao wa kilimo.
Share:

Thursday, June 24, 2021

Wanafunzi wa Sekondari ya Sullivan wawakumbuka wenye mahitaji

3Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa (wa tatu kulia), akikabidhi baadhi ya misaada kwa Msimamizi wa Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Child in the Sun, Padri Paul Raj kinachoendeshwa chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi rasmi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kujitolea kusaidia jamii yenye mahitaji. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa Sullivan Provost, Fanuel Nashon, Meneja wa shule hiyo, Richard Samwel Mkami pamoja na baadhi ya watoto wanaolelewa kituoni hapo.1Mkuu wa Shule ya Wavulana ya Sullivan Provost, Fanuel Nashon, akikabidhi baadhi ya misaada kwa mmoja ya watoto wanaoelelewa katika Kituo cha Kulelea Watoto wenye Mahitaji cha Child in the Sun kinachoendeshwa na kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kusaidia jamii yenye mahitajii. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu. Wengine kutoka kulia ni msimamizi wa kituo hicho, Padri Paul Raj, Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Sekondari ya Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa pamoja na vijana wanaolelewa kituoni hapo.4Meneja wa shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost , Richard Samwel Mkami (kulia), akikabidhi baadhi ya misaada kwa Msimamizi wa Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Child in the Sun, Padri Paul Raj kinachoendeshwa chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi rasmi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kujitolea kusaidia jamii yenye mahitaji. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu. Wengine pichani ni vijana wanaolelewa katika kituo hicho.DSC_1323Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kujitolea kusaidia jamii yenye mahitaji. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu.waliohudhuriaBaadhi ya wadau waliohudhuria hafla ya uzinduzi rasmi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kujitolea kusaidia jamii yenye mahitaji. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu.04Baadhi ya wadau wa shule hiyo wakiendelea kujitolea kwaajili yakuunga mkono juhudi za uongozi wa shule ya ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost, wakati wa uzinduzi rasmi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kujitolea kusaidia jamii yenye mahitaji. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu.

mkuu%2Bwa%2BkituoMsimamizi wa Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji cha Child in the Sun, Padri Paul Raj akizungumza wakati wakati wa uzinduzi rasmi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kujitolea kusaidia jamii yenye mahitaji. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa pamoja na wafanya kazi wa kituo hicho.pongezi

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kuoka mikate cha Sands Bakery kilichopo Bunju, Sarah Makumbati (kushoto) akitoa mkono wa pongezi kwa mmoja ya wafanyakazi wa kituo cha kulelea watoto wenye Mahitaji cha Child in the Sun kinachoendeshwa na kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mpango maalumu wa shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost, wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kusaidia jamii yenye mahitajii. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu.DSC_1444

Baba wa Kiroho wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost, Mch: Tusimsahau Manoza akiendesha ibada fupi wakati wa uzinduzi rasmi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kujitolea kusaidia jamii yenye mahitaji. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami.


wakichezaMkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa pamoja na wadau wa shule hiyo na wananchi wakiserebuka wakati wa uzinduzi huo.7Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Sullivan Provost, Rachel Mwalukasa pamoja na Mkuu wa Shule hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na vijana wanaolelewa kwenye Kituo cha Kulelea Watoto wenye Mahitaji cha Child in the Sun kinachoendeshwa na kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mpango maalumu wa shule hiyo wenye lengo la kuwafundisha wanafunzi wake kuwa na utamaduni wa kusaidia jamii yenye mahitajii. Mpango huo uliasisiwa mwaka 2019 na aliyewahi kuwa Meneja wa Sekondari ya Sullivan, Mhandisi Eric Samwel Mkami ambaye sasa ni marehemu.
Share:

Sunday, June 20, 2021

Benki ya TPB Yapata faida ya Bilioni 21

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi, (kushoto), akizungumza na wanahabari wakati wa mkutano wa mwaka wa wanahisa uliofanyika  jijini Dar es Salaam leo kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi wa benki ya TPB, Dkt. Edmund B. Mndolwa.

Mwenyekiti wa Bodi wa benki ya TPB, Dkt. Edmund B. Mndolwa (kulia),  akizungumza na wanahabari wakati wa mkutano wa mwaka wa wanahisa uliofanyika  jijini Dar es Salaam leo kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB, Sabasaba Moshingi,

Picha ya pamoja. Picha na Brian peter

 

 

BENKI ya TPB imepata faida ya Shilingi bilioni 21 kabla ya kodi kwa mwaka 2020. Kiasi hicho ambacho kimepatikani kabla ya kodi, kinatajwa na uongozi wa benki kuwa ni kikubwa ukizingatia changamoto mbalimbali zilizojitokeza mwaka jana, hasa janga la Corona lililoathiri dunia nzima.

Akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa wanahisa jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo, Dkt. Edmund B. Mndolwa alisema benki hiyo inaendelea kufanya vizuri kwa kupata faida hiyo kabla ya kodi.

Utendaji kazi uliotukuka, ufanisi na umakini wa menejimeti ya benki huku wakisimamiwa kwa karibu na Bodi tumeweza kupata faida kubwa ambalo ni jambo la kujivunia sana kwa kufanya kazi kubwa kwa tija,’’ alisema Dkt. Mndolwa.

Alisema kwamba pamoja na kwamba benki hiyo ina mtaji mdogo, ikilinganishwa na benki nyingine, imeendelea kufanya vizuri katika nyanja zote kwa miaka takriban kumi.

Dkt. Mndolwa alisema kwamba benki hiyo itaendelea kujipanga na kupanua shughuli zake za kibenki nchini na kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto za kiuchumi kwa sasa katika sekta ya fedha nchini.

 

Benki ya TPB ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 11 ya mwaka 1991, kama ilivyofanyiwa mabadiliko mwaka 1992. Mwaka 2016 jina la Benki lilibadilishwa na kuwa Benki ya TPB badala ya Benki ya Posta Tanzania.

 

Katika kuendelea kuelezea matukio makubwa Kwa mwaka 2020, Dkt. Mndolwa alisema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
iliziunganisha Benki ya TPB na Benki ya Biashara ya TIB. Lengo likiwa kuunda benki kubwa ya serikali itakayo boresha huduma, kupanua wigo wa mtandao na kutengeneza faida kubwa.

Benki ya TPB itaendelea kuboresha huduma zake na kubuni huduma mpya zinazokidhi matarajio ya wateja na kuwafikia wateja wengi zaidi wa kipato cha chini. 

Miongoni mwa huduma kama hizo ni SONGESHA na M-KOBA ambazo zinatolewa na Benki ya TPB kwa kushirikiana na Kampuni ya simu ya Vodacom.

Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Edmund Mndolwa akimalizia taarifa yake amesema Benki ya TPB inafanya vizuri katika soko la mabenki na hivyo kutoa wito kwa wateja kuendelea kuiunga mkono Benki yao. Mwelekeo ni mzuri na ndiyo maana benki imeendelea kukua na hadi kufikisha thamani ya Mali za Shilingi trioni moja mwisho mwa mwaka 2020 ikishika nafasi ya Saba kati ya benki zaidi ya 50 kote nchini.

Share:

Tuesday, June 15, 2021

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA SGR MWANZA-ISAKA KM 341

6%2B%25281%2529

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho, Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine wa Chama, Serikali na Bunge, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka km 341


Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yuko ziarani mkoani Mwanza akikagua miradi ya maendeleo. Katika ziara hiyo Rais Samia amezindua rasmi ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga

 

Uzinduzi wa ujenzi wa kipande hicho cha reli ni ishara ya kuanza kwa ujenzi wa kipande hicho cha tano kinachojengwa ndani ya miezi 36 sawa na miaka mitatu.

 

Kukamilika kwa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa nchini Tanzania kutasaidia kutatua kero ya usafiri kwa kusafirisha mizigo na abiria kwa uharaka zaidi katika nchi za ukanda wa maziwa makuu.

 

Rais Samia  amezindua kipande hicho cha reli kutoka Mwanza hadi Shinyanga chenye urefu wa kilometa 341, ambapo kilometa 219 zitatumika kama njia kuu huku kilomita 122 zitatumika kama njia za kupishana  na vituo vya kushuka na kupanda abiria ni 9, huku idadi ya vivuko vya chini  vitakavyojengwa ni 44 na vya juu vitakuwa ni 23.

 

Mapema mwezi Januari mwaka huu, serikali za Tanzania na china zilitiliana saini za makubaliano ya ujenzi wa reli ya kisasa ambao utagharimu jumla ya shilingi za kitanzania  trilioni 3.1 sawa na zaidi ya dola za kimarekani bilioni 1.326.

 

Kuanza kwa ujenzi wa reli hiyo ya kisasa nchini Tanzania, kunatajwa kuwa na tija hasa kwa wananchi wa mikoa hiyo kwani zaidi ya ajira elfu 75 zinatajariwa kupatikana kwa miaka yote mitatu ya ujenzi wa reli hiyo.

 

Kuwekwa kwa jiwe la msingi ni kiashiria cha kuanza kujengwa kwa kipande cha tano, ambapo kipande cha kwanza ni kutoka dar es salaam hadi Morogoro, Morogoro hadi Makutupora, Makutoporakwenda Tabora, Tabora mpaka Isaka na Isaka hadi jijini Mwanza.


Akizungumza mkoani mwanza baada ya raisi kuzindua awamu ya tano ya  ujenzi wa reli ya kisasa kutoka mwanza hadi isaka Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Michael Zhang alisema kwasasa kampuni hiyo inashirikiana kwa ukaribu zaidi na Shirika la Reli Tanzania TRC kwa kutoa vifaa vya mawasiliano na huduma kwenye miradi ya SGR ikiwemo Mfumo wa  wa Teknolojia ya Mawasiliano-Reli (GSM-R) ambayo baadae itabadilika na kuwa mfumo wa LTE-R.


Niimani yetu kwamba chini ya uongozi mpya wa Rais Mama Samia Suluhu, Huawei itaendelea kujenga Miundombinu ya TEHAMA kulingana na Dira ya maemdeleo ya Tanzania 2025"  aliahidi

Share:

Friday, June 11, 2021

Benki ya Akiba yashiriki katika zoezi la kutoa na kuchangia damu

Kama sehemu ya jamii pamoja na kutambua umuhimu wa kuokoa maisha, Benki ya Akiba imeshiriki kikamilifu katika zoezi muhimu la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya siku ya maadhimisho ya siku ya kuchangia damu ambapo kilele cha maadhimisho yake ni June 14, 2021.


Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa zoezi hilo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Benki ya Akiba, Dora Saria amesema jumla ya wafanyakazi takribani 30 kutoka Benki hiyo wamejitolea kushiriki katika zoezi la kuchangia damu kutokana na umuhimu wa zoezi husika, ili kuunga mkono jamii.

“Benki ya Akiba imekuwa mshiriki mahiri katika masuala ya kijamii kwa kutoa misaada katika sekta za Elimu, Mazingira na Afya kama ambavyo siku ya leo tumeshiriki katika zoezi hili kuchangia damu”, amesema Dora.

Pia kwa niaba ya Benki hiyo, Dora amesema wanatoa rai kwa Taasisi nyingine mbalimbali na Watanzania wote kwa ujumla kushiriki katika zoezi hilo kwa ajili ya kuokoa maisha ya Watanzania wenye uhitaji wa damu.

Wafanyakazi wa Benki ya Akiba wakiwa kwenye maandalizi kabla ya kuanza zoezi la kuchangia damu lilofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi kuelekea maadhimisho yake June 14, 2021.



Baadhi ya Wananchi wakiendelea na Zoezi la kuchangia damu likiendelea jijini Dar es Saalam kuelekea kilele cha maadhimisho June 14, 2021.

Meneja Masoko wa Benki ya Akiba Commercial Bank PLC (ACB), Innocent Ishengoma akipima damu kabla ya kuanza zoezi la kuchangia damu lilofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi kuelekea maadhimisho yake June 14, 2021.

Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya Akiba wakipima kabla ya kuanza zoezi la kuchangia damu lilofanyika jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi kuelekea maadhimisho yake June 14, 2021.

Afisa Mauzo wa Benki ya Akiba Commercial Bank PLC ACB, Elizabeth Masolwa (kushoto), akiwa sehemu rasmi na mtaalam wa utoaji na uchangiaji damu
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Dora Siria (kushoto), akitambulishwa kwa mtaalamu wa kutoa damu na mchngiaji wa damu Masoud Kipanya wakati wa zoezi la kutoa na kuchangia damu iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Share:

BENKI YA NBC YASOGEA KARIBU ZAIDI KWA WAFANYABIASHARA WANAOCHIPUKIA

001Mkurugenzi wa Wateja wa Rejareja na Binafsi wa NBC, Nd Elibariki Masuke (Kulia) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo, Bi Neemarose Singo (Kushoto), wakipeperusha bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Twende Sawa na NBC inayolenga kuwafikia wafanyabiashara wanaochipukia nchi nzima na kuwasogezea akaunti ya Kua Nasi mahususi kwa wajasiriamali isiyo na gharama za uendeshaji pamoja na kuwapa elimu ya biashara wakiwa kwenye biashara zao.

002
Mkurugenzi wa Wateja wa Rejareja na Binafsi wa NBC, Nd Elibariki Masuke akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Twende Sawa na NBC inayolenga kuwafikia wafanyabiashara wanaochipukia nchi nzima na kuwasogezea akaunti ya Kua Nasi mahususi kwa wajasiriamali isiyo na gharama za uendeshaji pamoja na kuwapa elimu ya biashara wakiwa kwenye biashara zao.
003
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya NBC, Nd Raymond Urassa akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Twende Sawa na NBC inayolenga kuwafikia wafanyabiashara wanaochipukia nchi nzima na kuwasogezea akaunti ya Kua Nasi mahususi kwa wajasiriamali isiyo na gharama za uendeshaji pamoja na kuwapa elimu ya biashara wakiwa kwenye biashara zao.

 Benki ya Taifa ya Biashara leo imezindua kampeni yake ya Twende Sawa na NBC yenye lengo la kuwafuata na kuwapa elimu wafanyabiashara wanaochipukia katika maeneo yao ya kazi na biashara. Kampeni hiyo imezinduliwa leo katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wakiwemo wafanyakazi na baadhi ya wateja wa benki hiyo

Lengo kubwa la kampeni ya Twende Sawa na NBC ni kutoa elimu ya kuendesha biashara, usimamizi makini wa wapato, urasimishaji wa biashara pamoja na kuweka kumbukumbu za kifedha ili kumuwezesha mfanyabiashara anayechipukia kusimamia na kuendesha baishara yake kwa ufanisi zaidi. Pamoja na elimu itakayotolewa, kampeni ya Twende Sawa na NBC pia inatoa fursa kwa wafanyabiashara kufungua Akaunti ya Kua Nasi yenye masharti nafuu kufungua, inayotoa riba kwa amana za mteja pamoja na kutokuwa na gharama za uendeshaji za kila mwezi.

Akiongea katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Wateja wa Rejareja na Binafsi wa NBC, Nd Elibariki Masuke alisema kuwa lengo kubwa la Benki ya Taifa ya Biashara ni kuwa karibu zaidi na wafanyabiashara wadogo ili wawawezeshe kukuza biashara sambamba na benki hiyo. Aidha alisema kuna maboresho ambayo benki hiyo imekuwa ikifanya ili kutimiza lengo la kuwa karibu zaidi na wafanyabiashara wadogo.

“Tumeongeza wigo wa matawi ya benki yetu nchini kupitia NBC Wakala na tumeweka mfumo wa kidijitali wa kufungua akaunti, tumerahisisha ufunguaji wa akaunti ambapo mtu anahitaji kitambulisho chake cha NIDA tu hivyo tumejipanga kuwaifikia na kuwahudumia kikamilifu wafanyabisahara wa jiji la Dar es Salaam na na maeneno mengine ya nchi kote.” Alisema Nd. Masuke.

Aidha kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya NBC, Nd Raymond Urassa ambaye ndiyo msimamizi wa Akaunti ya Kua Nasi amasema akaunti hiyo ni mahususi na ni rafiki kwa wafanyabiashara wadogo.

“Sisi kama NBC tunatambua kwamba wafanyabiashara wadogo wanahitaji kukua kupitia benki yetu ndiyo maana tumeondoa makato ya uendeshaji ya kila mwezi, tunampa mjasiriamali faida kwa hela atakayokuwa ameweka, tunatoa vitabu vya hundi kwa gharama nafuu watakaohitaji lakini pia tumepunguza gharama za utoaji wa fedha kupitia akaunti hii ya Kua Nasi ili kumpa mjasiriamali fursa ya kukua zaidi.”

Akielezea akaunti hiyo, Nd Raymond Urassa alisema kwamba mfanyabiashara yeyote mdogo anaweza kufungua Akaunti ya Kua Nasi kupitia matawi yote ya Benki ya Taifa ya Biashara nchi nzima lakini pia kupitia mawakala wa benki hiyo ambao pia wanapatikana nchi nzima.


Share:

Saturday, June 5, 2021

KAMPUNI YA UNILEVER TANZANIA YATOA MKONO WA SHUKRANI KATIKA HOSPITALI MBALIMBALI DAR ES SALAAM

 

Kampuni ya Unilever Tanzania katika kuendeleza ushiriki wake kwa jamii, imetoa mkono wa shukrani kwa wateja wake kwa kuzihudumia hospitali tatu za jijini Dar es Salaam ambazo ni Mwananyamala, Amana pamoja na Muhimbili.


Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa mkono wa shukrani, Meneja Masoko wa Unilever kupitia sabuni ya Omo nchini Tanzania, Bi Upendo Mkusa alisema, “Tunawashukuru sana Uongozi wa Hospitali n Wauguzi kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya na kuhakikisha mnaendelea kutoa huduma bila kuchoka, sambamba na hilo tunatoa pole kwa wagonjwa wote kwa changamoto ya afya wanayopitia, tukiwaombea kwa Mwenyezi Mungu mpate nafuu na kupona kabisa.


Mwezi huu tumeamua kutoa Mkono wa Shukrani kwa kutoa Shuka pamoja na Sabuni za Omo kwaajili ya kusaidia waliopo na kuhudumiwa katika hospitali hizi” aliendelea Bi Upendo.


Upendo alimaliza kwa kusema, “Tunashukuru sana kwa ushirikiano wenu kwani hali hii ndiyo inatupa motisha ya kuendelea kuwapa huduma bora zaidi. Ningependa pia kuwahakikishia kuwa tutaendelea kuwapa bidhaa bora na kuhakikisha tunatimiza mahitaji ya kila Mtanzania.

HABARI PICHA






Share:

Thursday, June 3, 2021

SULLIVAN PROVOST BOYS’ SECONDARY SCHOOL COME WITH 'GIVEAWAY DAY TO THE NEEDY'

 
SULLIVAN PROVOST BOYS’ SECONDARY SCHOOL
GIVEAWAY DAY TO THE NEEDY
22ND JUNE EVERY YEAR



Background

In December 2019, our School Manager, the Late Eng. Eric Samwel Mkami initiated the program of having a ‘GIVEAWAY DAY’ for our school. The motive behind this program was to induce a giving culture to our students because he believed that when you give with love, you receive abundant blessings from GOD (2Corinthians 9:6-9).

His plan was to make students visit at least one orphanage centre or one hospital and/or Prison every year and give the needy ones some presents collected from themselves including Sports items, School Bags, Exercise books, clothes and shoes which they no longer use (but are still in good order), food and any valuable materials such as soaps, toothpaste, body lotion etc. This culture will make the students appreciate the fact that they are indeed privileged to have parents and/or guardians who have sacrificed their income and took them to Sullivan Provost Boys’ Secondary School where they are receiving quality education with good food on their tables, good shelter and good care.

Why ‘Giveaway Day’ on 22nd June Every year?

This is to make a dream come true of our very dear Son, Brother and Friend, Eng. Eric Samwel Mkami who passed away on 22nd June 2020 leaving behind this unfinished exercise to be progressed in his spiritual presence.

Who is to be part of this Dream come true?

All Sullivan Provost Boys’ Secondary School Stakeholders: Friends to Eric Samwel Mkami, Students, Teachers, Relatives, Neighbours and any good wishers to our School.

Mode of communication prior to the date: Radio/TV Adverts, Letters to the stakeholders, Social Media and Word of mouth.

When will this day be Launched and where?

This event will be launched on 22nd June 2021 when Eric will be turning 1 year since his passed away. The selected centre is ‘Child in the Sun’ at Mbezi Makabe where underprivileged boys coming from streets are being cared under the umbrella of Roman Catholic.

Who will present the collected Give Away items? - Few representative of Sullivan Provost Students, Appointed Teachers, Friends and any other stakeholders.

The Lord Jesus himself said: 'It is more blessed to give than to receive” Acts 20:35

For further details please contact: 0715210812/0754210812
Share:

Tuesday, June 1, 2021

Russia and Tanzania to create joint environmental projects

 IMG_4939

President of the Russian-Tanzanian Friendship Society, Mr Yuri Korobov (Left) speaks to African Diaspora Society President, Dr Zunebe Kinfu Tafesse (Right) during recent talks held in Russia to discuss Tanzania's participation in joint environmental projects.

Russia and Tanzania to create joint environmental projects

Dar es Salaam, June 2nd, 2021 – The Russian Society of Friendship that was formed in Russia by public figures and entrepreneurs will join forces with Tanzania to promote environmental and humanitarian projects at the international level.

The head of the Organisation, a member of the Russian Geographical Society Yuri Korobov said "Firstly, we plan to work on environmental projects. This is in both Russia and Tanzania, the problem of mass deforestation is the most acute. Because of the low cost, Tanzania is deforesting widespread rainforests, which are already few on the planet.

Tanzania is faced with a number of environmental problems. Resources are being

depleted, with major developmental and environmental implications. The major

environmental problems facing Tanzania are land degradation, lack of accessible, good

quality water for urban and rural inhabitants, environmental pollution, loss of wildlife

habitats and biological diversity, deterioration of aquatic systems and deforestation.

 

The Russian Society of Friendship plans on working with organisations in Tanzania such as The National Environmental Management Council (NEMC) which has the responsibility of advising the government on all matters related to the environment.

 

Korobov looked at other problems that are affecting the environment of which the society also plans on addressing in Tanzania. 

 

·         Looking at abandoned mines, which are not properly preserved after mining, releasing harmful chemical gases that lead to soil degradation,

·         Mass deforestation

·         Environmental pollution

 

“All of the above problems can be leveled at the expense of existing technologies in Russia. That's why we plan to conduct mutual training and exchange of specialists - environmentalists, engineers, chemists and volunteers," Korobov said.

The Russian Friendship Society and Tanzania are expected to sign their first agreement with the Tanzanian Friendship Society at the end of June 2021. As part of the agreement, the parties will create a business council, which will include members of the public and entrepreneurs.

 

"Together we will work together and implement an understanding of how projects should be implemented on the ground, so that everywhere, even in commercial projects, in which we will participate as consultants and give information support, there is an environmental focus," Korobov said.



In addition, the organization plans to implement a number of other projects. Among them are the creation of a platform of economic cooperation between the business of Tanzania and Russia, the holding of an economic forum with the theme of mutual investment attractiveness, the preparation of educational programs for students and young people of Russia and Tanzania, cooperation in the development of the agricultural sector of both countries, as well as the implementation of safe cognitive tourism programs, cultural exchange.



The Society of Friendship with Tanzania was established in Russia in April 2021 by an initiative group of public figures and entrepreneurs to promote environmental and humanitarian projects at the international level.



In 2019, Sochi hosted the first Russia-Africa economic summit, which resulted in a declaration containing the goals and objectives of further development of Russian-African cooperation in the fields of politics, security, economy, scientific, technical and cultural and humanitarian spheres. The second Russia-Africa summit is scheduled for 2022.

We look forward to a fruitful friendship between Russia and Tanzania towards an environmentally friendly country and continued partnership.

Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive