A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Wednesday, December 13, 2017

TMRC YATOA MSAADA WA SHILINGI MILIONI MBILI KITUO CHA KULELEA YATIMA KIWALANI

Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa mikopo kwa mabenki na Taasisi nyingine za kifedha kwaajili ya Ujenzi na ununuzi wa nyumba (TMRC),Oscar Mgaya (wapili kushoto) akikabidhi msaada wa vyakula pamoja na mahitaji muhimu ya kibinadamu kwa Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima Kiwalani Orphanage Centre,Elias Mwakalukwa, kushoto ni Mkurugenza wa Fedha wa Taasisi hiyo, Oswald Urassa.
Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa Mikopo kwa Mabenki na Taasisi nyingine za kifedha kwaajili ya Ujenzi na ununuzi wa nyumba (TMRC),Oscar Mgaya (wapili kushoto) akifafanua jambo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vyakula pamoja na mahitaji muhimu ya kibinadamu yenye thamani ya shilingi Milion 2  kwa Kituo cha kulea watoto yatima Kiwalani Orphanage Centre,kushoto ni Mlezi Mkuu wa Kituo hicho Elias Mwakalukwa wengine ni maofisa wa taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Taasisi inayotoa mikopo kwa mabenki na Taasisi nyingine za kifedha kwaajili ya Ujenzi na ununuzi wa nyumba (TMRC),Oscar Mgaya (wapili kushoto) akikabidhi zawadi ya Sikukuu ya Krismas kwa mwakilishi wa Wanafunzi wa Kituo hicho.
                              
                              



                                           TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TMRC YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA KIWALANI  

13, DESEMBA 2017 - (DAR ES SALAAM)Kampuni ya Tanzania Mortgage Refinance Company Limited (TMRC), imetoa zawadi ya Sikukuu ya Krismas zenye thamani ya Shilingi Milioni Mbili (Shilingi 2,000,000) kwa Kituo cha Watoto yatima cha Kiwalani (Kiwalani Orphanage Centre) kilichopo jijini Dar es Salaam.

Zawadi hizo zimekabidhiwa leo na Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Bw. Oscar P. Mgaya kwa Mkurugenzi wa Kituo hicho, Mchungaji   Elias Mwakalukwa -, katika ghafla iliyofanyika kwenye Kituo hicho kilichopo jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa zawadi zilizotolewa kwa kituo hicho cha watoto yatima ni pamoja na mchele, mafuta ya kupikia, unga wa sembe, maharage sabuni za kufulia na kuogea, sukari ,  chumvi,  dawa za meno, majani, kalamu na madaftari

“Kwa upendo wetu wa dhati kabisa tumeona umuhimu wa kushiriki pamoja na watoto yatima, ambao wapo katika mazingira magumu, katika kusherehekea Sikukuu ya Krimas mwaka 2017,” alisema Bw. Mgaya.

Bw. Mgaya, alisema kuwa taasisi yake imeamua kujumuika na watoto hawa yatima katika kuelekea kusherehekea Sikukuu ya Krismasi kwa kutoa zawadi mbalimbali za vyakula kama njia ya kuwafanya wajisikie furaha.

Hata hivyo, Mtendaji Mkuu huyo, amezitaka taasisi nyingine na watu binafsi kujitoa kwa dhati kuwasaidia watoto  walioko maeneo mbalimbali nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kituo hicho, Mchungaji   Elias Mwakalukwa, ameishukuru TMRC, kwa msaada huo na ameziomba taasisi nyingine kuiga mfano wao.
“Tunaishukuru sana TMRC, ninyi mmeonyesha mfano na hakika mmeonyesha upendo wa dhati kwa watoto hawa. Niziombe taasisi nyingine kuchukua mfano huu uliofanywa na taasisi yenu,” Mchungaji   Elias Mwakalukwa alisema.

Aliongeza kuwa uhitaji wa misaada kwa kituo chake ni mkubwa, lakini taasisi yao inapata faraja kupata wadau wanao ona umuhimu wa kusaidia watoto hao yatima.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive