A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Tuesday, December 12, 2017

Airtel yaja na bando mpya ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano (kulia) akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ mpya ambapo  itamuwezesha mteja wa Airtel KUSMATIKA NA GB 1  ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda Hafla ya uzinduzi huo umefanyika leo makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania Isack Nchunda  (kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ mpya ambapo  itamuwezesha mteja wa Airtel KUSMATIKA NA GB 1  ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu (kulia), ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano, Hafla ya uzinduzi huo umefanyika leo makao makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano, wakionyesha bango lemye aina mbalimbali za bando za huduma hiyo baada ya uzinduzi huo. Picha na Brian Peter

Airtel yaleta ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ SMATIKA NA 1GB  siku tatu kwa 2000 tu f
  • ‘SMATIKA NA 1GB Yatosha Intaneti inayokupa muda mrefu kwa gharama nafuu zaidi.
Airtel Tananzania Mtandao bora kwa Smartphone yako imewapatia wateja wake uhuru zaidi kwa kuwaletea  bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ maalum kwa watumiaji wa huduma za intaneti.   

Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Isack Nchuna wakati wa hafla ya kuzindua ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti, alisema “Airtel itaendelea kuleta huduma zenye ubora na ubunifu wa hali ya juu ili kuendelea kuwa  sambamba na mahitaji ya wateja katika huduma za intaneti ambapo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa Airtel imejiwekea mikakati endelevu mingi ili kukidhi uhitajika na wateja wote”

“Tuaendelea kudhihirisha dhamira yetu ya kutoa suluhisho la mawasiliano kupitia uzinduzi wa ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ kwa kutoa huduma nafuu ya Intaneti kwa watumiaji wote nchini  huku tukiweka kipaumbele zaidi katika ubora wa mtandao pamoja na kuwapatia  wateja uhuru zaidi” aliongeza Nchunda.
 
“SMATIKA na Yatosha Intaneti’ ni zawadi ya awali kabisa tunayowapatia watumiaji wa Airtel katika msimu huu wa sikukuu, tunaamini kuwa ndani ya msimu huu wa sikukuu wateja wanauhitaji mkubwa sana wa intaneti katika kukamilisha 

shamrasharna wakiwa wanawasiliana na ndugu, jamaa na marafiki  wakati wote!”
Akifafanua  zaidi Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi Beatrice Singano alisema Bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja wote wa airtel kujichagulia bando la intaneti KABAMBE wakati wowote.

“Mteja wa Airtel ataweza kunufaika na SMATIKA na Yatosha Intaneti kwa gharama nafuu ya hadi shilingi 200 na kujipatia MB 40, vilevlie mteja ataweza KUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu” alieleza Bi Singano.

“kujiunga na ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ unatakiwa kupiga *149*99# kisha chagua 5 Yatosha Intanet vilevile  unaweza kujiunga kupitia Airtel Money kwa kupiga *150*60# kisha chagua  Yatosha Intanet”.

Airtel Tanzania imekuwa katika programu ya uboreshaji wa miundombinu ya mawasiliano yake ili kukamilisha lengo lake la kutoa mawasiliano bora  na yenye uhakika kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya U900. Tayari Airtel imezindua maboresho ya mtandao wake kwa kutumia teknolojia hiyo ya U-900 kwenye mikoa ya Arusha, Dar es salaam, Dodoma, Morogoro na Mwanza huku ikiendelea kuwahakikishia wateja wake mawasiliano bora hasa katika maeneo ya nje na ndani ya majengo marefu au yenye uhitaji zaidi.

Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive