A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Monday, December 18, 2017

AIRTEL YAZIDI KUWANUFAISHA WATEJA WAKE

 Meneja Masoko Airtel Tanzania Aneth Muga, akitoa Maelezo wakati wa mkutano na watangazi wa radio mbalimbali  nchini  kuhusu ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti zinazotolewa na Airtel kupitia  bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ .
 Baadhi ya watangazaji wa radio mbalimbali nchini wakifuatilia mada kwa umakini wakati wa mkutano na watangazi wa radio mbalimbali  nchini  na Airtel kuhusu ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti zinazotolewa na Airtel kupitia  bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imekutana na watangazi wa radio mbalimbali  nchini  na kuongelea ongezeko la faida za mteja katika huduma za intaneti zinazotolewa na Airtel kupitia kuzinduliwa kwa  bando mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zilizozinduliwa  mwanzoni mwa wiki hii kwa lengo lengo la kuwapatia wateja na watumiaji wote wa intaneti bando nafuu zaidi.
Meneja Masoko Airtel Tanzania Anethy Muga alieleza kuwa bando Mpya ya ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja wote kujichagulia bando la intaneti KABAMBE wakati wowote, na kusisitiza kuwa mteja wa Airtel ataweza kunufaika na SMATIKA na Yatosha Intaneti kwa kujipatia bado za gharama nafuu ya hadi shilingi 200 na kupata MB 40. Vilevile ofa kabambe ya ‘SMATIKA Yatosha bando’ itamuwezesha mteja wa AirtelKUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu”
kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Yatosha mpya inakupa bado za siku, wik, mwezi gharama nafuu kuliko zote nchini, kwa mfano bado ya 5,000 zamani ilikuwa na GB 1,  kwa sasa Yatosha Intaneti Mpya unapata  GB 2 kwa siku 7, vile vile kwa shilingi 10,000 zamani ulikuwa unapata bando la GB 2.5 kwa siku 7 lakini sasa tumeliongeza zaidi unapata GB 6 zakutumia wiki nzima. Alieleza Muga
“SMATIKA na Yatosha Intaneti’ ni ishara ya Airtel kuanza vyema shamrashamra kusherehekea  sikukuu kwa kuwapatia uhakika wateja na watumiaji wa huduma ya intaneti wa kutoishiwa bando kwa muda mfupi,

Ukiwa na Airtel Yatosha Intaneti hainaga kuzima data tena!” Alisisitiza Mmbando.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive