A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.

Thursday, September 28, 2017

Mahafali Ya 17 TIOB Yafana.Jijini Dar.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mabenki Tanzania (TIOB), Patrick Mususa (kushoto), akizungumza wakati wa sherehe ya mahafali ya 17 ya Taasisi hiyo  yaliyofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar es Salaam katikati ni Gavana wa Benki kuu ya Tanzania (BOT) Prof Benno Ndulu ambae alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo na (kulia) ni Msajili wa TIOB, Saad Banzi.
Gavana wa benki kuu ya Tanzania (BOT) Prof Benno Ndulu akizungumza katika mahafali ya 17 ya chuo cha The Tanzania Institute of bankers (TIOB) yaliyofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar.
Mkurugenzi mtendaji wa chuo cha The Tanzania Institute of bankers (TIOB) Bw. Patrck Mususa akifafanua jambo katika mahafali ya 17 ya chuo cha The Tanzania Institute of bankers (TIOB) yaliyofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar.
Wahitimu wa ngazi mbali mbali wakimsikiliza Gavana wa benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Benno Ndulu (hayupo pichani) katika mahafali ya 17 ya chuo cha The Tanzania Institute of bankers (TIOB) yaliyofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar.
Mshindi wa pili wa Banking Certificate Programme Bi Mariam H Mahige akipokea zawadi kutoka kwa Gavana wa BOT Profesa Benno Ndulu fedha taslimu Tsh Laki 4 katika mahafali ya 17 ya chuo cha The Tanzania Institute of bankers (TIOB) yaliyofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar.
 Mshindi wa wa Banking Certificate Programme Erick akipokea cheti katika mahafali ya 17 ya chuo cha The Tanzania Institute of bankers (TIOB) yaliyofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar.

THE TANZANIA INSTITUTE OF BANKERS (TIOB)
MAHAFALI YA 17 YA TAASISI YA MABENKI (THE TANZANIA INSTITUTE OF BANKERS -TIOB)

Taasisi ya Mabenki Tanzania - The Tanzania Institute of Bankers (TIOB) Inayofuraha kuwapa taarifa wanachama wote waTaasisi, wahitimu, na umma kwaujumla kwamba Shereheya Mahafaliya 17 ya Taasisi hiyo itafanyika Jumatano ya tarehe 27 Septemba, 2017  katika  Hoteliya Hyatt Regency Dar es Salaam – The Kilimanjaro, kuanzia saa 9:30 alasiri.

Katika mahafali haya, wahitimu 177 watatunukiwa vyeti vya uhitimu - 17 katika ngazi ya  cheti (Banking Certificate), 141 katika ngazi ya juu ya taaluma hii (Certified Professional Bankers) na 19 watakaopewa vyeti vya kubobea katika masomo maalum (Specialists).

Pia litakuwepo zoezi la utoaji zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri zaidi katika masomo yao (Prize awards). 

Wahitimu hawo, wengi wao ni wafanyakazi katika taasisi za fedha nchini na wengineni wale wanaojiandaa kuingia katika soko la ajira katika sekta hiyo.

Sherehe ya Mahafali itatanguliwa na Mkutano Mkuu wa Mwaka (Annual General Meeting) wa Taasisi hii (TIOB) utakaoanza saa 9.00 kamili alasiri hotelini hapo kabla ya Mahafali. 

Huu ni Mkutano wa 19 na unawahusu wanachama tu wataasisi ambao ni wanachama binafsi (Individual members) pamoja na Mabenki yote naTaasisi za Fedha zilizosajiliwa.

Agenda zitakazo wasilishwa katika Mkutano Mkuu ni pamoja na Ripoti ya Mwaka ya Ukaguzi kwa mwaka uliopita tarehe 31 Decemba, 2016; Mpango wa Mwaka 2017 wa TIOB; Uteuzi wa mkaguzi wa Hesabu kwa mwaka 2017 na Uteuzi wa Baraza la usimamizi wa Taasisi kwa miaka mitatu ijayo. Baraza lililopo linamaliza muda wake wakatiwa Mkutano huu.

TIOB ilianzishwa mwaka 1993 kwa sheria ya makampuni (Companies Ordinance- Cap 212) baada ya kuonekana umuhimu wa kuwa na chombo cha Kitaifa cha kusimamia taaluma ya kibenki hasa baada ya kufungua milango kwa taasisi za fedha za kimataifa kuwekeza Tanzania Hivyo basi, lengo kuu la Taasisi hii ni kusimamia na kuendeleza taaluma ya kibenki ili taasisi za fedha nchini ziweze kupata wataalam wenye elimu na ujuzi wa kuwawezesha kutoa huduma bora za kifedha kwa serikali, makampuni na jamii kwa ujumla katika kukuza uchumi wa nchi yetu.

Katika kusimamia na kuendeleza taaluma ya kibenki, Taasisi hii (TIOB) inatoa mitihani ya taaluma ambayo hufanyika mwezi Mei na Novemba kila mwaka katika vituo vya mafunzo na mitihani ambavyo kwasasa viko nane yaani Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Mbeya, Dodoma, Morogoro na Zanzibar.

Pamoja na mitihani hiyo, TIOB pia inatoa mafunzo endelevu kwa wafanyakazi wataasisi za fedha kwanjia ya kozi fupi, semina na makongamano ili kuhuisha na kukuza ujuzi wao.
 
Wakati TIOB inaanzishwa ili kuwa na wanachama waanzilishi 11 tu ambao ni taasisi za fedha zilizokuwepo nchini mwaka 1993. Leo hii kuna jumla ya taasisi wanachama (Taasisi za fedha) takribani hamsini na saba (57) na wanachama binafsi (Individual members) zaidi ya elfu saba (7,000).

TIOB inaushirikiano na taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi kwaajili ya kuendeleza taaluma ya kibenki ikiwa ni pamoja na kuwa miongoni mwa wanachama waanzilishi waushirika wataasisi za Mabenki katika Afrika(Alliance of African Institutes of bankers - AAIOB) ulioanzishwa mwaka 1997. AAIOB  hadi sasa inawanachama kumi na tatu (13) ikiwa ni pamoja na South Africa, Namibia, Botswana, Zimbabwe, Zambia, Msumbiji, Malawi, Tanzania, Kenya, Uganda, Nigeria, Ghana na Misri. 

Katika ushirika huu mtaala unaotumika katika mafunzo ni mmoja na hivyo cheti kinachotolewa katika ngazi ya juu ya utawala wa kibenki (Certified Proffessional Banker) kutokaTaasisi yoyote mwanachama kinatambuliwa na nchi zote wanachama wa AAIOB.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive