
DAR ES SALAAM: WATANZANIA watapata fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali ambazo zitabadili maisha yao msimu huu wa sikukuu baada ya Benki ya Akiba Commercial Bank Plc kuzindua kampeni maalumu ya kufanikisha hilo.
Leo Desemba 22, ACB imezindua kampeni ya msimu wa sikukuu ijulikanayo kama ‘Twende Kidijitali, Miamala Yako, Ushindi Wako’yenye lengo la kuhamasisha matumizi ya huduma za kibenki kidijitali.

Kampeni hiyo inawahamasisha wateja kuongeza miamala kupitia huduma za VISA, Mobile Banking na Internet Banking za ACB, huku ikichochea ujumuishaji wa kifedha na kuimarisha uhusiano na wateja katika kipindi cha sikukuu na kuendelea hadi mwaka mpya.
Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Magreth Mwasumbi, Meneja Mwandamizi wa Huduma za Kifedha Kidijitali, alisisitiza umuhimu wa huduma za kibenki kidijitali katika kutoa suluhisho rahisi na salama za miamala kwa Watanzania wote.

Alieleza kuwa kampeni hiyo imelenga kuwazawadia wateja wanaotumia huduma hizo mara kwa mara na kuimarisha imani kwa huduma za kidijitali za benki.
Kwa upande wake, Dora Saria, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano, aliwahimiza wateja kushiriki kikamilifu na kutumia fursa hiyo kujishindia zawadi.
Alieleza kuwa kampeni hiyo itakuwa na droo tatu: droo ya mwisho wa Desemba, droo ya katikati ya Januari, na Droo Kuu itakayofanyika mwishoni mwa Januari 2026, ili kuhakikisha ushiriki endelevu na kutambua wateja waaminifu.
Akiba Commercial Bank Plc inawahamasisha wateja wote kukumbatia huduma za kibenki kidijitali na kushiriki katika kampeni ya “Twende Kidijitali Miamala Yako, Ushindi Wako!” ili kufurahia huduma za kibenki zilizo rahisi na za kisasa, huku wakipata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali kulingana na masharti na vigezo vya kampeni.
Akiba Commercial Bank Plc inaendelea kujitolea kutoa suluhisho bunifu za kibenki zinazochochea ujumuishaji wa kifedha, kuhimiza mageuzi ya kidijitali, na kuunga mkono maendeleo ya jamii ya Tanzania







0 comments:
Post a Comment