A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Wednesday, August 2, 2023

Airtel yazindua Airtel Vikoba Kidigitali

    
*Inapatikana kwa wateja wote wa Airtel Money

*ni kwa kushirikiana na Benki ya TCB kupitia kauli mbiu isemayo ‘Tubebane Pamoja’.

Meneja Mahusiano wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kulia), akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya Airtel Vikoba kwa kutumia njia ya Airtel Money kwa kushirikiana na Benki ya TCB kupitia kauli mbiu yao ya ‘Tubebane Pamoja’ jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Masoko wa TCB, Deo Kwiyukwa, Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba na Mkuu wa Tehema na Uendeshaji wa TCB, Jema Msuya.
Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba (wa pili kushoto), akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya Airtel Vikoba kwa kutumia njia ya Airtel Money kwa kushirikiana na Benki ya TCB kupitia kauli mbiu yao ya ‘Tubebane Pamoja’ jijini Dar es Salaam leo. Pamoja naye kutoka kushoto ni, Mkuu wa Tehama na Uendeshaji wa TCB, Jema Msuya, Mkuu wa Masoko wa TCB, Deo Kwiyukwa na Meneja Mahusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.
Mkuu wa Tehama na Uendeshaji wa Benki ya TCB, Jema Msuya (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba na Mkurugenzi wa Masoko wa TCB, Deo Kwiyukwa.
Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba (kulia), na Mkuu wa Tehama na Uendeshaji wa Benki ya TCB, Jema Msuya wakionesha mfano wa kadi ikiwa ni ishara ya ushirikiano kati yao wakati wa uzinduzi wa huduma ya Airtel Vikoba kwa kutumia njia ya Airtel Money kwa kushirikiana na Benki ya TCB kupitia kauli mbiu yao ya ‘Tubebane Pamoja’ jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni, Mkuu wa Masoko wa TCB, Deo Kwiyukwa na Meneja Huduma za Airtel Money, Hellen Lyimo.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive