A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Monday, February 10, 2020

NBC yazindua kampeni ya Kijanisha Dodoma kwa kupanda miti 1000


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu (aliepiga magoti), akizindua rasmi zoezi la upandaji miti lililopewa jina la Kijanisha Dodoma na kudhaminiwa na Benki ya NBC katika mtaa wa Swaswa Halmashauri ya jiji la Dodoma likiwa na lengo la kutunza mazingira katika mkoa huo.  Nyuma ya mheshimiwa waziri ni Meneja wa Kanda ya kati wa NBC James Ndimbo, Afisa mauzo wa benki hiyo, Zachalia Lema (kushoto),  pamoja na Mkuu wa huduma kwa Wateja,  Anne Mwasaka. Upandaji miti huo umefanyika Dodoma hivi karibuni.
Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya NBC James Ndimbo, akipanda miti huku wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na na viongozi wa kata ya Swaswa wakiangalia wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti iliyopewa jina la Kijanisha Dodoma  uliofanyika mkoani humo kwa udhamini wa Benki ya NBC hivi karibuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu (kushoto), akishikana mikono na Afisa Mauzo wa Benki ya NBC, Dodoma, Zachalia Lema wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti iliyopewa jina la Kijanisha Dodoma  uliofanyika mkoani humo kwa udhamini wa Benki ya NBC hivi karibuni.
Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu Halmashauri ya jiji la Dodoma, Dickson Kimaro akipanda mti mara baada Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu kuzindua kampeni ya upandaji miti iliyopewa jina la Kijanisha Dodoma na kudhaminiwa na benki ya NBC katika mtaa wa Swaswa Halmashauri ya jiji la Dodoma hivi karibuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Azzan Zungu (katikati), akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi waa NBC, wakazi wa kitongoji cha Swaswa pamoja na wakai wengine wa Dodoma walishiriki hafla ya upandaji miti lililodhaminiwa na benki hiyo.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive