A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Tuesday, May 14, 2019

BENKI YA DCB YAWASHUKURU WAHESHIMIWA WABUNGE NA SPIKA KWA KUFANIKISHA UUZWAJI WA HISA.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa pale ugeni kutoka benki hiyo ulipomtembelea  ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo, Prof. Lucian Msambichaka.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Kushoto), akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka (katikati) pale ugeni kutoka benki hiyo ulipomtembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Ndg. Godfrey Ndalahwa
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Katikati), akizungumza na ujumbe kutoka benki ya DCB ukiongozwa na  Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Lucian Msambichaka (kushoto kwake) ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma jana.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto), akisalimiana na Meneja wa Tawi la Benki ya DCB Dodoma, Joseph Njile wakati yeye na uongozi wa juu wa benki hiyo ukimtembelea spika, ofisini kwake, bungeni, Dodoma jana. Kutoka wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Lucian Msambichaka, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa na Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, James Ngaluko  wakati yeye Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Lucian Msambichaka na  Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa (kulia kwake), wakimtembelea mheshimiwa Spika, osifini kwake Dodoma jana.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto), akisalimiana na ofisa Uhusiano wa Benki ya Biashara ya DCB, Nuru Ashraf, wakati yeye na uongozi wa juu wa benki hiyo ukimtembelea spika, ofisini kwake, bungeni, Dodoma juzi. Kutoka wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Lucian Msambichaka, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa na Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha  Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa, wakati yeye na uongozi wa juu wa benki hiyo ukimtembelea spika, ofisini kwake, bungeni, Dodoma juzi. Kutoka wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Prof. Lucian Msambichaka, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa na Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Katikati), akiwa katika picha ya pamoja na ugeni kutoka Benki ya Biashara ya DCB ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo, Prof. Lucian Msambichaka (wa tatu kulia) walipomtembelea leo ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma jana.

Benki ya Biashara ya DCB imetoa shukurani kwa waheshimiwa wabunge pamoja na mheshimiwa spika kwa kufanikisha zoezi la uuzwaji wa hisa zao lililofanyika hivi karibuni kwa mafanikio. 


Akizungumza wakati wa mahojiano maalumu jijini Dodoma leo sambamba na ziara ya uongozi wa juu wa DCB ulioongozwa na Mwenyekiti wao wa Bodi bungeni juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa alisema wabunge kama wawakilishi wa wananchi wamesaidia sana kwa taarifa za uuzaji wa hisa zao kuwafikia wananchi wengi. 

Alisema mafanikio ya uuzaji wa hisa yaliyoifanya benki kuongeza mtaji wake yatasaidia mpango mkakati wao wa kutanua wigo wa huduma zao wakitarajia ndani ya miaka mitano kuwafikia watanzania wengi huku wakiwekeza zaidi katika huduma za kidigitali. 

“DCB ilianza mpango wake wa kujitanua kutoka jijini Dar es Salaam miaka miwili iliyopita, safari ya kujitanua inaendelea, tumeshafika Dodoma na maeneo ya karibu, mfumo wetu unaotusaidia ni kutoa huduma bora kwa bei nafuu tukiwekeza zaidi katika mfumo wa kidigatali hivyo kuwa na matawi machache na kuweka vituo vingi vya huduma sehemu mbalimbali nchini,” alisema. 






Zoezi la uuzwaji wa hisa za dcb lilizinduliwa Novemba 12,2018 na kuhitimishwa Januari 31, 2019 ambapo hisa 36,635,435 ziliuzwa ikivuka kiwango cha hisa 33,913,948 zilizopangwa awali. 
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive