A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Thursday, December 13, 2018

BENKI YA CBA NA VODACOM WATANGAZA MSHINDI MKUU WA KAMPENI YA M-PAWA NA WASHINDI WENGINE WATANO WALIOJISHINDIA BAJAJI KILA MMOJA.

Mkurugenzi  Idara  Usajili wa hazina wa Benki ya Biashara Afrika CBA Hakim Sheikh (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  kuchezesha  droo ya mwisho ya Promosheni iliyokuwa inakwenda kwa  jina la Shinda na  M-PAWA.  kushoto ni Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya pamoja na Sophet Mafuru hafla hiyo imefanyika leo kwenye ofisi za benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi  Idara  Usajili wa hazina wa Benki ya Biashara Afrika CBA Hakim Sheikh (kulia) akipiga simu kwa mmoja wa washindi wakati wa droo ya mwisho ya Promosheni iliyokuwa inakwenda kwa  jina la Shinda na  M-PAWA.  (Katikati)  ni Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya, pamoja na Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Abdallah Hemedy

Meneja Masoko wa Vodacom, Noel Mazoya  (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuchezesha  droo ya mwisho ya Promosheni iliyopewa jina la Shinda na  M-PAWA.  (wapilikushoto) ni Mkurugenzi  Idara  Wateja binafsi na Masoko wa Benki ya Biashara Afrika CBA Julius Konyani ambae amemuwakilisha Mkurugenzi  Mkuu wa Benki hiyo,   Wengine  ni Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha  Jehud Ngolo pamoja na Sophet Mafuru.  hafla hiyo imefanyika leo kwenye ofisi za benki hiyo jijini Dar es Salaam.


BENKI YA CBA NA VODACOM WATANGAZA MSHINDI MKUU WA KAMPENI
YA M-PAWA NA WASHINDI WENGINE WATANO WALIOJISHINDIA BAJAJI
KILA MMOJA.

Dar es Salaam, 13 Desemba 2018.

Benki ya CBA na Vodacom Tanzania waibua Mshindi Mkuu wa kampeni yao ya
‘‘SHINDA NA M-PAWA’’ iliyofikia tamati leo. Mshindi huyo aliyejinyakulia kitita cha
milioni kumi ni Sophia Sarapion wa Bukoba. Washindi wengine watano
waliopatikana kwenye droo hiyo kubwa waliojinyakulia bajaji moja moja ni Abeid
Abeid, Lucas Ngoye, Mariamu Barawa, Hassan Msabila na Hamisi Mpela.

Promosheni hii iliyowalenga, wateja wote wa M-PAWA nchini, imetengenezwa kwa
ajili ua kuwasaidia watumiaji kujiwezesha kifedha ili waweze kujiwekea utaratibu wa
kuweka akiba na kuwahimiza kurudisha mikopo mapema kwa riba za chini kabisa
kwa muda wa wiki 6 kuanzia tarehe 8 Novemba 2018 kukiwa na jumla ya wateja
1,296 wanaoshinda kwenye droo za kila wiki. Sambamba na draw ya washindi wa
mwisho droo hiyo imemalizia idadi ya wateja 200 waliongeza mara mbili ya amana
na wateja 15 walioweza kuchukua na kurejesha mikopo yao kabla ya wakati.

Wakizungumza kwenye muendelezo huo, washindi walitoa shukrani zao kwa Benki
ya CBA na Vodacom kwa kuwapa fursa hiyo ya kuwatuza na kuwawezesha wateja
kupitia kampeni ya “SHINDA NA M-PAWA’’.

Wakati akitoa tamko kwenye finali hizo za kampeni ya "SHINDA NA M-PAWA",
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CBA Bw. Hakim Sheikh alikiri
kwamba benki ya CBA imetimiza ahadi yao kwa wateja kwa kuwazawadia wote
walioshiriki na kufikia vigezo vya kampeni hiyo na wote walioshiriki katika droo zote
nne zilizopangwa wakati wa kampeni.

“Tunahimizwa na msisimko mkubwa wa ushiriki katika kampeni ya Shinda na MPAWA
na jinsi inavyoendelea kupokelea. Ukiacha zawadi mbalimbali walizoshinda
washiriki, ukweli ni kwamba kampeni hii imetupatia fursa kubwa ya kuwahamasisha
wateja wetu kuwa na utamaduni wa kujiweka akiba, ili kuwawezesha kifedha. Kwa
hiyo tunawahimiza Watanzania wasio wateja wa Benki ya CBA kujiunga na benki yetu
ili kufaidika na fursa mbalimbali za maendeleo zinazotolewa na Benki CBA”,
aliongeza Bw. Gift Shoko.

Katika maneno yake, Meneja Masoko wa M-PESA Vodacom, Bw. Noel Mazoya,
aliipongeza Benki ya CBA kwa kuendesha promosheni hiyo kwa uadilifu na uwazi.
Alithibitisha kuwa zoezi la kuchagua washindi hao lilifuata utaratibu toka mwanzo
wa kampeni Novemba 2018 hadi kuibuka kwa washindi mbalimbali. Aliwahimiza
wateja wenye bahati, hasa wale washindi, kutumia zawadi zao vizuri, na kusisitiza, ''
ni muhimu kuwekeza kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kukupa ushauri bure
unapohitaji''.

Commercial Bank of Africa (CBA) is a commercial bank in Tanzania. It is licensed by the Bank of Tanzania, the country's central bank and national banking regulator. The bank is a

subsidiary of the Commercial Bank of Africa Group.

Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive