A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Sunday, May 6, 2018

Familia Moja jijini Dar es Salaam wapaza sauti na Kumlilia Rais Magufuli Pamoja na RC Makonda baada ya kuzulumiwa

Bi Edith Max akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Hi ndio nyumba ambayo tayari imeanza kubomolewa na taasisi hiyo.
Bi Edith akionyesha nyumba hiyo namba 868 iliyopo Mfaume Road Upanga mashariki 
Mwenekiti wa mtaa huo Abdulkarim Gulam Shmbe akizungumza na waandishi wa habari.

Familiya moja iliyokuwa ikiishi Mfaume Road, Kata ya Upanga Mashariki, jijini Dar es Salaam wamepaza sauti na kilio kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Mkuu wa mkoa wa Mkoa huo RC.Paul  Makonda kuwasaidia  kupata haki yao amabayo inaonekana kuporwa kwa nguvu na taasisi ya Khoja Shia ambayo ni ya kidini kwa kudai kuwa walinunua nyumba hiyo.


Akizungumza na wanahabari leo msemaji wa familiya hiyo Bi. Edith Max ameeleza kuwa awali mume wake ambaye anatambulika kwa jina la Emmanuel Max alikopa fedha katika benki ya Furaha ambapo benki hiyo ilibadilishwa jina kwa sasa inafahamika kama I &M Bank, ambapo kiasi cha fedha zilizokopwa ni shilling million 30 lakini walikatazwa kulipa kwanza na baada ya hapo kuwatoa katika nyumba hiyo kwa nguvu kwa kudai kuwa wameshindwa kulipa mkopo ambao ulipanda na kufikia deni la shilling million 120.


Ameendelea kusema kuwa walipotaka kulipa mkopo huo,waliambiwa wasubiri kwanza wataambiwa walipe baadae ya hapo walikwenda kwa ajili ya kulipa ndipo walipoambiwa kuwa Riba imeongezeka hivyo watatakiwa kulipa kiasi cha shilling million 90.


"Tulipoambiwa tulipe million 90, Mume wangu alikubali na akawa tayari kwa ajili ya kulipa lakini alipokwenda kulipa wakamwambia asubiri mwezi mmoja alafu watatuita baadae ya mwezi kwisha tukaenda kwa ajili ya kulipa wakasema Ribs imepanda Ivyo tunatakiwa kulipa million 120, tukawa tuko tayari kulipa na tunafanya mchakato wa kulipa" ameeleza.


Ameendelea kusema' Tukiwa tunafanya mchakato wa kulipa tukaja kutolewa katika hii nyumba mwaka 2014 na watu wakidai kuwa tumeshindwa kulipa mkopo huo jambo ambalo sio kweli kutokana na kuna kuondolewa kwa ghafla hali hiyo ilisababisha mama mkwe wangu kupata presha na kufariki na kupelekea mume wangu kupooza jambo lililopelekea Mimi kuahangaika na familia pekeangu na huku nina watoto wanne"

Amesema walibaini udanganyifu katika unaofanywa na Benki hiyo kwani kila wakitaka kulipa deni wanaambiwa wasubiri na baada ya hapo waligushi vyeti vya mirathi feki na hakuna mwanafamilia yeyote alietambulika katika mirathi hiyo.

Aidha Bi. Max amesema Familia  ili fungua Mirathi yake tarehe 17 Januari katika  Mahakama ya  mwanzo Kinondoni na Msimamizi wa Mirathi hiyo Max Edmund Kafipa.


Amwsema awali suala hili walilipeleka kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda katika Kampeni yake  ya kuwa sikiliza walidhulumiwa nyumba, viwanja na Mashamba  ambapo walifika katika ofisi hizo January 30, mwaka huu.ambapo pande zote ziliitwa na kujadiliana kwa wanasheria na maamuzi yao yanatarajiwa kutolewa  tarehe 7 May 2018.


Ameendelea kusema kufuatia kuendelea kwa kesi hiyo taasisi hiyo ilifika na kubomoa nyumba hiyo jambo ambalo ni kinyume na sheria na walipobaini waliomba zuio na wakabata barua ya kuzuia kuvunjwa kwa nyumba hiyo.


"Hii taasisi ambayo ni ya kidini wanasema ni watetezi wa wanyonge lakini si kweli kwani wamekuja na wanavunja nyumba yangu hii usiku wakidai kuwa wamenunua na ni Mali yao tulipewa zuio LA kutovunja lakini wanakuja kuvunja hata Jana usiku walikuja kuvunja kwa siri Mimi nalia naomba Rais wangu na Mkuu wa mkoa mnisikie kilio changu nipate haki yangu" Amesema Bi Edith.


Amesema kuwa hata hivyo taasisi hiyo jana waliamua Kuwaita ili waongee wakubaliane ili familia hiyo iseme inataka kiasi gani cha fedha ili wapatiwe wakasema wanataka Billion 2,ndipo wakasema watajadiliana badae watakuja na jibu ndipo walipochukua hatua ya kuvunja tena nyumba hiyo.
Edithi amebainisha kuwa 'Wakili wao alitamka wazi kwa Makonda hana Mamlaka ya kuingilia  mambo haya na hii nyumba tulikuwa tunaitaka muda mrefu'

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Abdulkarum Gulam Shambe, amesema ni kweli kuwa jambo hilo lipo na mgogoro huo kati yao na benki na kwamba taarifa za kuvunjwa kwa nyumba hiyo alipata  baada ya kuanza kuvunja ndipo walipopeleka taarifa hizo kwake.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive