A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Monday, May 21, 2018

Balozi Ambokile kutangaza chakula cha Kitanzania Afrika Kusini


01
Balozi wa Tanzania  nchini  Afrika Kusini, SylvesterAmbokile , (kulia) akifurahia jambo pamoja na Mmiliki wa mgahawa huo.
02
Msanii wa bongo fleva sheta akipiga msosi katika Mgahawa huo.

BALOZI wa Tanzania  nchini  Afrika Kusini,Sylvester Ambokile ,  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mgahawa wa kisasa  wa chakula cha Kitanzania uitwao  Grill House Take Away  jijini Johanesburg nchini humo.

Mgahawa huo unalengo la kutangaza chakula asili cha kitanzania  kimataifa  pamoja na kuwapa huduma hiyo watanzania waishio nchini humo.

Akizungumza  na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, jana kwa niaba ya Mmiliki wa Mgahawa huo ,  Christopher Robert, mwakilishi wa mkurugenzi huyo hapa nchini, Frank Koko alisema sherehe za ufunguzi rasmi zimepangwa kufanyika  Juni 21 mwaka huu.

“Dhima yetu ni kukitangaza chakula asilia cha kitanzania kimataifa. Wapishi wote ni kutoka Tanzania na chakula kinasafirishwa kutoka Tanzania hadi nchini humo,”alisema Koko.

Alisema, kwa miaka mingi chakula cha kitanzania hakijapewa nafasi kubwa katika soko la  hoteli na migahawa duniani  kiasi cha kuwafanya hata watanzania wakiwa nje ya nchi kulazimika kula chakula ambacho si asili yao.

“Tuliona kwamba hata hoteli za kitanzania zinapika zaidi  chakula cha  utamaduni wa nje, watu wanalazimika kula tu.Ukifika Johanesburg ni changamoto kubwa kupata chakula cha nyumbani.

Watanzania wanahangaika kupata chakula cha asili yao jambo ambalo lilitusukuma kuja na wazo hili la kuwa na sehemu ambayo mtanzania akitua Johanesburg atapata huduma zote kama za nyumbani,”alisema.

Aliongeza; “ Tunaomba watanzania watakaotembelea Johanesburg watemelee Grill House Take Away , Mtaa wa 
51 Regent ili  waweze kutuunga mkono,”alisema Koko.

Picha mbalimbali muonekano wa Mgahawa huo.
IMG-20180521-WA0041

IMG-20180521-WA0036

IMG-20180521-WA0042

IMG-20180521-WA0043%2B%25281%2529

IMG-20180521-WA0037%2B%25281%2529
IMG-20180521-WA0036

IMG-20180521-WA0038

IMG-20180521-WA0045

IMG-20180521-WA0048

IMG-20180521-WA0038

sssss

IMG-20180521-WA0050
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive