A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Tuesday, February 27, 2018

GSM NA DANUBE KUJENGA KIWANDA NCHINI

Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM Farida Rubanza (kulia),  akizungumza na wandishi wa habari katika hafla  ya utiaji sahihi makubaliano kati ya kampuni hiyo na kampuni ya Danube Home  inayojishughulisha na  biashara ya kuuza samani ambapo kuptia makubaliano hayo watajenga kiwanda kikubwa cha  kutengeneza Samani za ndani  katika eneo la Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Wanne kushoto ni Waziri  wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji,   Charles  Mwijage  pamoja na maofisa wengine kutoka GSM na Danube.
Waziri  wa ,  Biashara na  Uwekezaji,   Charles  Mwijage (wa pili kushoto),  akizungumza katika hafla ya utiaji sahihi makubaliano kati ya kampuni za GSM na Danube Home  inayojishughulisha na  biashara ya kuuza samani ambapo kuptia makubaliano hayo watajenga kiwanda kikubwa cha  kutengeneza Samani za ndani  katika eneo la Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kushotoni Mkurugenzi Mtendaji  wa Danube Home,  Sayed Habib, wapili kulia ni Rais wa Danube Home Tanzania,  Ghalib Mohamed na Meneja Masoko wa GSM, Farida Rubanza. Hafla hiyo ilifanyika kwenye duka la Danube, Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Danube Home,   Sayed Habib (katikati),  akizungumza na wandishi wa habari katika ya utiaji sahihi makubaliano kati ya kampuni za GSM na Danube Home  inayojishughulisha na  biashara ya kuuza samani ambapo kuptia makubaliano hayo watajenga kiwanda kikubwa cha  kutengeneza samani za ndani  katika eneo la Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa GSM,  Fahad Ahmad pamoja na Waziri  wa Viwanda,  Biashara na  Uwekezaji,    Charles  Mwijage  ambae ndio alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Waziri  wa Viwanda  biashara na  uwekezaji   Charles  Mwijage ambae ndio alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo akisalimiana na mmoja ya wawekezaji kwenye Kampuni ya Danube Home Raymond Healy, wengine ni Maofisa wa Kampuni hiyo.

Waziri wa Viwanda amezipongeza kampuni za GSM na DANUBE Kuweza kuungana na kutaka kuanzisha kiwanda kitakachotengeneza samani mbalimbali hapa nchini. 


Waziri Mwaijage amezungumza leo katika tukio la makubaliano na kati ya kampuni zote mbili ambapo zimekubali kuungana na kuamua kutengeneza kiwanda kitakachozalisha samani mbalimbali ili kuwapa wananchi fursa ya kupata bidhaa kwa ukaribu na kwa bei nafuu  .

Amesema serikali ipo tayari kuwatoa sapoti katika kuhakikicha kiwanda hicho cha kuzalisha samani kinakuwepo nchini ambapo amesema kuanzishwa kwa kiwanda hicho kuyapeleka watanzania kupata ajira na kusaidia kukuza uchumi wa viwanda. 

"Nafahamu kyanzishwa kwa kiwanda hichi kwanza mmenisaidia mimi katika kutekeleza sera ya kukuza uchumi wa viwanda, pia itatengeneza ajira kwa wananchi wetu hivyo ni jambo jema na napenda kiwanda hichi kianzishwe" amesema Mwaijage. 

Aidha amebainisha kuwa kutengenezwa kwa samani katika nchi yetu kitasaidia kukuza soko la biashara na wateja kupata bidhaa kwa bei nafuu na kwa urahisi zaidi. 

 Kwa upande wake  Meneja masoko wa Kampuni ya GSM ,  Farida  Rubanza amesema wana tarajia kujenga kiwanda kikubwa kitakacho kuwa kina tengeneza samani za ndani  (Furniture)  kwa ajili ya kuuza nchini na kusafirisha nchi mbalimbali duniani.

‘’Sisi  GSM na DANUBE tumeona Nivema  tukaungana ilikujenga kiwanda hapahahapa na tutakuwa tuna pata malighafi hapahapa na kiwanda kikikamilika tuta kuwa na uwezo wa  kuuza Contener  500 kwa mwezi na tutauza masoko ya nje na ndani ‘’ alisema .

Rubanza pia ame mshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe. John P.Magufuli na serikali yake kwa  kwa kuweka mazingira Rafiki kwa wawekezaji wa ndani na wa kigeni na kuahidi  kuwa wao kama waekezaji wataendelea kutoa ajira kwa watanzania.


Katika muungano huu  amesema, wataanzisha  DUNUBE home  Academy   na watachukua wahitimu wa vyuo nchi na watawafundisha  na kuwapatia ajira ndani na nje ya nchi walikowekeza na wemgine watawa tafutia ajira sehemu mbalimbali

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya DANUBE Home Sayed Habib amesema wamewiwa kuja kuwekeza Tanzania kwani ina rasilimali za kuweza kusaidia uzalishaji wa samani hizo. 

Ameishukuru kampuni ya gsm kukubali kufanya muunganiko utakaosaidia kuanzishwa kwa kiwanda icho hapa nchini.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive