A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Monday, August 14, 2017

BARCELONA YACHEZEA KICHAPO KWA REAL MADRID

Barcelona wamepoteza mchezo wa kwanza wa fainali ya Super Cup baada ya kuruhusu magoli matatu dhidi ya mahasimu wao wakubwa Real Madrid katika uwanja wa Camp Nou.



Real walianza kupata bao la kwanza ambalo beki Gerard Pique wa Barcelona alijifunga baada ya kumalizia pasi iliyopigwa na mlizni Mbrazili, Marcelo na kumhadaa golikipa wake.

Barcelona walirudisha goli la kwanza kupitia kwa Mesi ambaye alifunga kwa mkwaju wa penalti baada ya Luis Suarez kuangushwa kwenye eneo la hatari la Real Madrid, penalti ambayo hata hivyo ilizua utataa kuwa amejirusha.


Real walipata goli la pili kupitia Cristiano Ronaldo aliyeingia kuchukua nafasi ya Karim Benzema baada ya kupiga shuti kali nje kidogo ya eneo la hatari la Barca.


Ronaldo alipewa kadi ya njano kwa kuvua shati wakati akishangilia mbele ya washabiki wa Barcelona, na dakika tatu baadae alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kujiangusha baada ya kushindana na Umtiti katika kuwania mpira.


Real walifunga goli la tatu kupitia kwa Marco Asencio aliemalizia vizuri kazi ya Lucas Vazquez nje ya box la hatari umbali wa mita 25.


Ushindi huu unawapa Real nafasi kubwa ya kunyakua kombe hili wakirudi Bernabeu na akiba ya magoli mawili waliyopata leo ugenini Camp Nou.


Zifuatazo ni baadhi ya picha za mtanange huo.







Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive