A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Friday, July 7, 2023

MAKAMU WA RAIS DKT MPANGO APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA ELIMU KUTOKA TANZANIA COMMERCIAL BANK MKOANI KIGOMA

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Muyama mara baada ya gafla ya kupokea vyumba vitatu vya madarasani ofisi mbili za walimu na Samani mbalimbali za maofisini yaliokabidhiwa na Tanzania commercial Bank (TCB), katika Shule ya Msingi Muyama iliyopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango (wapili kulia), akikata utepe kuashiria kupokea Madarasa, Samani mbalimbali na Ofisi za Walimu yaliokarabatiwa na Tanzania Commercial Bank (TCB) katika Shule ya Msingi Muyama iliopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ikiwa ni utaratibu wa Benki hiyo kurudisha kwa kutoa msaada kwa jamii (CSR).

Hafla hiyo imefanyika katika shule hiyo hivi karibuni wengine pichani ni kutoka (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Sabasaba Moshingi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof Joyce Ndalichako na viongozi wengine wa serikalini pamoja na Maafisa wa Benki

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Philip Mpango, ameishukuru Tanzania Commercial Bank kwa kutoa msaada wa ukarabati wa Vyumba Vitatu vya Madarasa, Ofisi Mbili za Walimu madawati 50 pamoja na printer na vitu mbalimbali vya ofisini katika Shule ya Msingi Muyama iliopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma

Akipokea msaada huo aliushukuru ongozi mzima wa Benki ya TCB kwa kuendelea kusaidia jamii katika suala zima la Elimu Mkoa wa Kigoma na maeneo mengine hapa nchini.

Makamu wa Rais Philip Mpango alipokea msaada huo alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani humo na kutaka taasisi nyengine kuiga mfano mzuri unaofanywa na Tanzania commercial bank

Ameeleza kuwa Benk ya TCB imeonesha ukomavu wake hasa kwenye swala la elimu ya kifedha maana bila elimu hakuna chochote kwenye maendeleo ya nchi yetu.

Dkt Mpango ameongeza kuwa hata yeye amesoma katika shule hiyo ambayo leo Tanzania commercial bank wametoa msaada wa vitu hivi kwaajili ya kukuza elimu na maeneo mengine alisema mpango.

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw Sabasaba Moshingi alitoa shukrani za dhati kwa Mhe Mpango kwa kuweza kufika kwenye hafla fupi ya makabidhiano na kuhaidi kuwa benki itaendelea kusaidia jamii katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu. Vile vile alitoa rai kwa wananchi wa Buhigwe na maeneo ya karibu kuweza kujiunga na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka benki ya TCB mara baada ya hafla ya kupokea vyumba vitatu vya madarasa na ofisi mbili za walimu na Samani mbalimbali za maofisini yaliokabidhiwa na Tanzania commercial Bank (TCB), katika Shule ya Msingi Muyama iliyopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive