A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Thursday, July 15, 2021

BENKI YA SERIKALI YA BIASHARA YAZINDULIWA RASMI

 25Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt.  Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).  wa pili (kushoto), akibonyeza ripoti kuashiria uzinduzi rasmi wa Muonekano  mpya wa jina na Nembo mpya ya Benki mpya ya  Serikali ya Biashara Tanzania Commercial Bank (TIB) ambayo ni muunganiko wa  Benki mbili TIB pamoja na  Benki ya Posta TPB zenye lengo la kuleta ushindani wa kibiashara. Wengine pichani ni Afisa Mtendaji Mkuu wa  Benki ya TCB  Sabasaba Moshingi, Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo  Edmund Mndolwa pamoja na viongozi wengine kutoka Serikalini.3Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt.  Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Muonekano  mpya wa jina na Nembo mpya ya Benki mpya ya  Serikali ya Biashara Tanzania Commercial Bank (TIB) ambayo ni muunganiko wa  Benki mbili TIB pamoja na  Benki ya Posta TPB zenye lengo la kuleta ushindani wa kibiashara.

31

 Afisa Mtendaji Mkuu wa  Benki ya TCB  Sabasaba Moshingi, akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Muonekano  mpya wa jina na Nembo mpya ya Benki mpya ya  Serikali ya Biashara Tanzania Commercial Bank (TIB) ambayo ni muunganiko wa  Benki mbili TIB pamoja na  Benki ya Posta TPB zenye lengo la kuleta ushindani wa kibiashara.

 

19

Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt.  Mwigulu Lameck Nchemba (watatu kushoto), akikabidhiwa mfano wa kadi zitakazotumika katika Benki hiyo na Afisa Mtendaji Mkuu wa  Benki ya TCB  Sabasaba Moshingi, wapili kulia20

Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt.  Mwigulu Lameck Nchwmba akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo  Edmund Mndolwa.23

Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo....... Picha zote na Brian Peter

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amezindua rasmi benki ya Serikali ya Biashara 'Tanzania Commercial Bank' (TCB,) ambayo ni muunganiko wa benki ya Maendeleo (TIB)na benki ya Posta (TPB) huku lengo kuu likielezwa ni kuundwa kwa benki kuu ya Serikali na ushindani ambayo itatoa huduma zote za kibenki na biashara kama benki nyingine za kibiashara duniani.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Waziri Nchemba amesema benki hizo zimeunganishwa kwa kuzingatia ushauri na matakwa ya kisheria hivyo wafanyakazi wa benki hiyo mpya hawana budi kulitendea haki kwa jina hilo kwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii, ushindani na ubunifu wa hali ya juu na kuleta mageuzi makubwa ya kiutendaji, kimfumo na taswira ya kuhimili ushindani wa kibiashara katika sekta ya fedha.

Amesema, benki hiyo itahudumia wateja wote na wafanyabashara waliokuwa TPB na TIB na itatoa huduma kwa viwango vya kuhakikisha mageuzi zaidi yanaendelea katika sekta ya fedha nchini ili kujenga uchumi imara na shindani katika viwango vya kimataifa.

"Hizi ni jitihada za Serikali katika kujenga uchumi wa taifa kwa kuzingatia uadlifu na ubunifu na sisi Wizara ya fedha na benki kuu tutatoa ushirikiano katika kuijenga benki ya biashara ya Serikali nchini TCB.'' Amesema Mwigulu.

Aidha Waziri Nchemba amezishauri benki zote nchini kushusha riba katika hatua zilizopo mikononi mwao na hiyo ni pamoja na kuangalia namna wanavyofilisi mali za wateja pindi wanaposhindwa kurejesha mikopo yao.

"Baadhi ya madalali wamekuwa wakiendesha minada ya dhamana za wateja kitapeli, mteja anaweza kuwa amelipa asilimia 95 ya mkopo na kubaki asilimia 5 pekee....hapa baadhi ya madalali wasio waaminifu wanauza dhamana kwa mnada ambao unazidi fedha iliyobaki, huu ni utapeli." Amesema.

Pia Mwigulu amewashauri wananchi kutumia fursa za uwepo wa mabenki na kuacha tabia ya kukwepa mifumo rasmi ya fedha na kutumia mifumo isiyo rasmi ikiwemo kukopa sehemu za riba ya juu pamoja na masharti magumu yasiyoweza kuhimili kupitia biashara.

Awali Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa benki TPB na sasa TCB Sabasaba Moshingi amesema kuanzishwa kwa benki hiyo ya biashara ya Serikali ni muhimu sana katika kujenga uchumi imara na shindani pamoja na kuimarisha sekta ya fedha.

Moshingi amesema, Benki kuu ya Tanzania (BOT,) pamoja na Wizara ya Fedha imesimamia mageuzi hayo na kuahidi kufanya kazi kwa uadilifu katika kujenga uchumi imara wa taifa.

Vilevile amesema, benki hiyo ikiwa taasisi ya umma itatoa huduma kwa wateja wote kuanzia ngazi ya chini kulingana na mahitaji yao.

Serikali imeendelea kuunganisha taasisi zake zinazofanya kazi zinazofanana ili kuimarisha ufanisi na ushindani zaidi, Benki ya Biashara ya Serikali (TCB,) ni zao la benki ya Posta (TPB) na benki ya Maendeleo (TIB.)
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive