A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Monday, March 8, 2021

AKIBA COMMERCIAL BANK YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KUCHAGUA CHANGAMOTO KULETA FIKRA MPYA KWA MAENDELEO

 
Meneja wa Benki ya Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Tawi la Kijitonyama Joachim Mowo (kulia), akikata keki pamoja na wateja wake kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambapo benki hiyo iliandaa hafla fupi kwaajili ya kuwashukuru wateja wake.
Meneja wa Benki ya Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Tawi la Kijitonyama Joachim Mowo (kulia), akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya futa vicoba endelevu ambae pia ni mteja wa Benki hiyo Hanipha Tarimo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo benki hiyo iliandaa hafla fupi kwaajili ya kuwashukuru wateja wake hafla hiyo imefanyika katika ofisi za benki ya ACB Tawi la Kijitonyama leo Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Dora Siria.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Dora Siria akimlisha keki Afisa wa Benki hiyo Tawi la Kijitonyama, Amani Mwakitalima wakati wa maadhimisho wa siku ya wanawake duniani ambapo Benki hiyo iliandaa hafla fupi kwaajili ya wateja wake.
Meneja wa Benki ya Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Tawi la Kijitonyama Joachim Mowo (katikati), akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani taasisi mbalimbali zimetakiwa kuhakikisha wanatoa huduma katika hali ya usawa bila kubagua jinsia.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Akiba commercial (ACB), Dora Siria Kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Hayo yamesemwa wakati wa Benki ya ACB kuwashukuru wateja wao waliokuwa nao kwa kipindi cha muda kirefu.

Amesema, kauli mbiu ya mwaka huu ni “Choose to Challenge" yaani Chagua Changamoto zaidi kwa maana kuwa changamoto maranyingi zinaleta fikrampya, mitazamomipya na mabadiliko.

Siria amesema, wanatambua mchango wa wanawake katika kujenga jamii bora ndio maana zaidi ya asilimia 50 ya wateja wanaopata huduma kwenye benki yao ni wanawake.

"Asilimia 50 ya wateja wetu ni wanawake ambao wamewezeshwa kwa kupewa huduma mbalimbali ambazo zimewasaidia kubadilisha hali zao za maisha kwa kuwa na maisha bora," amesema Dora.

Akiba Commercial Bank kama sehemu ya jamii pia inalichukulia swala hili kwa umakini na uzito wake tunaelewa na tunatambua na kuheshimu nafasi ya Mwanamke katika jamii.

Nae Mwenyekiti wa Taasisi ya Fata Vicoba Endelevu ambae pia ni mteja wa benki hiyo Hanipha Tarimo amesema amekuwa mteja wa ACB kwa kipindi cha muda wa miaka mitano na ameweza kujiendeleza kiuchumi kwa kufanya biashara yake ya kuuza nywele origino za kike, maduka ya Nguo yaliyopo karioo mtaa wa msimbazi, na ameendesha maisha yake vizuri tokea aanze kutumia Benki hiyo.

Amesema, anawasihi wanawake wengine wasisite kuchukua kuitumia Benki ya Akiba Commercial bank kwani inasaidia kuinua wanawake kiuchumi na pia ACB wamekuwa ni moja ya taasisi wasikivu hususani pale mteja anapokua amekwama.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive