A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Tuesday, October 29, 2019

NBC YAENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIDIGITALI

Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslim na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati  wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize akizungumza na baadhi ya wateja wao wa makampuni wa jijini Mwanza, walipokutana na kufanya mazungumzo nao wakiwafahamisha huduma mbalimbali zitolewazo na NBC na pia kupata mrejesho kutoka kwao juu ya huduma hizo na jinsi wanaweza kuwahudumia vizuri zaidi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wa benki hiyo jijini humo hivi karibuni.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslim na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati  wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto), akiwasikiliza wateja wa benki hiyo Malesh Mathade (kulia), pamoja na Mitesh Metha, walipokutana na wateja wao wa makampuni mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho  ya mwezi wa huduma kwa wateja  wa NBC jijini humo hivi karibuni. NBC katika kipindi cha mwezi wa huduma kwa wateja imefanya mikutano kama hiyo kwa wateja wake sehemu mbalimbali nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslim na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (katikati),akishikana mikono na Mteja wa NBC kutoka kampuni ya Marine Services,  Erick Hamissi, walipokutana na wateja wao wa makampuni mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho  ya mwezi wa huduma kwa wateja  wa NBC jijini humo hivi karibuni.. Kulia ni Nelson Julius naye kutoka Marine Services.
Meneja wa Huduma kwa Wateja Wakubwa wa Benki ya NBC, Mary Opiyo (wa tatu kushoto), akishikana mikono na mteja wa benki hiyo, Mkurugenzi wa Bugando Medical Centre, Padre Engelbert Nyandwi, katika hafla waliyoiandaa kwa wateja wao wa makampuni ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja  jijini humo hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni maofisa uhusiano wateja wa benki hiyo, Abdallah Aruga na  Fainess Jeremiah.
Mkuu wa Kitengo cha wafanya biashara wa kati wa Benki ya NBC Moses Minja (kushoto), akishikana mikono na mteja wa NBC kutoka kampuni ya Marine Services, Erick Hamissi, walipokutana na wateja wao wa makampuni  mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho  ya mwezi wa huduma kwa wateja  wateja jijini humo  hivi karibuni. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslimu na Miamala kwa Wateja Wakubwa na wa Kati wa  NBC, Jimmy Myalize.

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), imeendelea kuongeza na kuimarisha huduma zake za kibenki kwa njia za kidigitali ili kuwawezesha wafanyabiashara na wateja wengine kufanya miamala mingi  ya kibenki mahali walipo imeelezwa jijini Mwanza hivi karibuni.

Akizungumza na wateja wa benki hiyo jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya mwezi wa huduma kwa wateja wa NBC, Meneja  Huduma katika  Kitengo cha Wateja wa Makampuni wa benki hiyo, Mary Opiyo alisema benki hiyo imerahisisha huduma zake nyingi kwenda  kidigitali ili kuwafanya wateja wao kupata muda zaidi wa kufanya biashara zao kuliko kupata huduma hizo katika matawi yao.

“Sasa mteja wetu anaweza kufanya malipo akiwa ofisini kwake kwa njia ya mtandao wa intaneti akatuma pesa kwa wateja wake ambao pengine ingebidi awapelekee au waje pale, NBC itaendelea kuboresha na pia imo mbioni kuongeza huduma nyingine bora zaidi hususan malipo kwa njia ya mtandao ili kutengeneza fursa mbalimbali za kibiashara kwa wateja wetu”, aliongeza meneja huyo.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Kitengo cha Fedha Taslimu na Miamala kwa wateja Wakubwa na wa Kati wa beni hiyo, Jimmy Myalize alisema mkutano huo una lengo la kuwashukuru wateja wao  kwa biashara wanayowapa na kuweza kuwaamini wakawa benki  waitumiayo  kwa ajili ya mambo yao ya kifedha.

Alisema pia katika kukutana kwao wameweza kuwafahamisha bidhaa zao mpya, benki ipo wapi na maendeleo ya benki kwa ujumla na pia kupata mrejesho kutoka kwao juu ya huduma za NBC na kama kuna maeneo wangependa yaboreshwe ili kuweza kuwahudumia vizuri zaidi.

“Pia tunawakutanisha wateja wetu ili kuweza kuongea biashara na  kutengeneza  fursa za kibiashara kati yao jambo litakalosaidia wateja wetu kukua kibiashara kwani mteja anapokua na sisi kama benki tunakua”

Benki ya NBC huadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wateja mwezi wa Oktoba kila mwaka kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kutoa misaada mbalimbali na kutoa elimu ya kifedha na ujasiriamali kwa makundi tofauti, kutembelea wateja wao mahali walipo na kufanya mikutano na wateja hao.

Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive