A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Wednesday, August 21, 2019

Wateja wa kampuni ya nishati ya jua ya Mobisol wazidi kuongezeka

Meneja Mauzo wa Mobisol Kanda ya Pwani,  Wesley Muyenze (kulia), akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafaniko na mikakati ya kampuni hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa wa Kampuni ya Mobisol (kulia), wakitoa huduma kwa wateja wao  walipokwenda kufanya manunuzi ya bidhaa za Mobisol.

KAMPUNI ya usambazaji wa huduma  za vifaa vinavyotumia umeme unaotokana na nishati ya jua (Mobisol), imesema kuwa kwa sasa watanzania wengi wanauelewa juu ya matumizi ya umeme wa sola hali iliyochangia  kampuni hiyo kupata wateja zaidi 100,000 na kuwahudumia watu  500,000.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam jana na Meneja Mauzo wa Mobisol Kanda ya Pwani,  Wesley Muyenze wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafaniko na mikakati ya kampuni hiyo.

Alisema umeme wa jua ni chanzo kinachofaa cha nishati mbadala majumbani na nchi nyingi tayari zimegundua ukweli na zimeachana na vyanzo vya kuzalisha nishati ya
umeme vilivyozoeleka kama  makaa ya mawe.

Muyenze alisema anawashukuru watanzania ambao baadhi yao wameachana na nishati ya umeme inayotokana na vyanzo vilivyozoeleka na kutumia nishati ya jua inayouzwa na kampuni ya Mobisol.

"Hata hivyo kutokana na kuongezeka kwa wateja katika kampuni yetu,  tumeamua kutoa zawadi ambapo mteja akinunua mtambo wa W 40 anapata betri na paneli bure kabisa, kwahiyo niwaombe watanzania na wateja wetu wafike madukani kwetu ili waweze kununua bidhaa zetu na kujipatia zawadi hizo, " alisema.

Aidha alisema anatambua kuwa  kuwahudumia wateja zaidi ya 500,000 si kazi ndogo na kuongeza kuwa hali hiyo imetokana na kukua kwa uelewa wa wananchi juu ya matumizi hayo  ya nishati ya umeme unatokana na jua.

Hata hivyo alisema nchi haiwezi kufikia uchumi wa viwanda bila kuwa na umeme wa uhakika katika maeneo mengi ya nchi hivyo kama kampuni watahakikisha wanawafikia wananchi hasa waliopo vijijini.

Naye mteja wa mitambo ya umeme  inayouzwa katika kampuni hiyo kutoka Tarime,  Sophia Simon alisema mitambo inayouzwa na kampuni hiyo ni imara na tangu ainunue haijawahi kuzima hata kama mvua inyeshe wiki nzima.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive