A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Wednesday, July 3, 2019

Benki ya NBC yangara maonesho ya Sabasaba, yatwaa tuzo ya mshindi wa kwanza taasisi za kifedha

Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan (kushoto) akilakiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi kabla hajatembelea banda ya benki hiyo katika maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam Jana. Kulia ni Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe. 
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akikabidhi kikombe cha mshindi wa kwanza katika Kitengo cha Taasisi za Fedha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba,Dar es Salaam jana. NBC iliibuka na ushindi wa kwanza wa Muoneshaji Bora katika kundi la Taasisi za fedha.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (katikati) akisalimiana na baadhi ya watendaji wa NBC wakati alipotembelea banda ya benki hiyo katika maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam Jana. Kulia kwa Makamu wa Rais ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Thaobald Sabi. NBC iliibuka na ushindi wa kwanza wa Muoneshaji Bora katika kundi la Taasisi za Fedha. 
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo ya bidhaa zinazotengenezwa na mmoja wa wajasiriamali wakati akitembelea banda la Benki  ya NBC katika maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam Jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi na kulia kwake ni Waziri wa Viwanda na BIashara, Innocent Bashungwa. NBC ilitwaa tuzo ya mshindi wa kwanza ya Muoneshaji Bora katika kundi la Taasisi za Fedha.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia), akisikiliza maelezo ya bidhaa mbalimbali zinazoonyeshwa na mmoja wa wajasiriamali katikabanda la Benki ya NBC, wakati wa maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, Sabasaba, Dar es Salaam Jana. NBC iliibuka na ushindi wa kwanza wa Muoneshaji Bora katika kundi  la Taasisi za Fedha. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi na anayeangalia kwa karibu ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa.


BENKI ya NBC imeibuka kidedea kwa mwaka wa pili mfululizo katika maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar  es Salaam kwa kutwaa ushindi wa kwanza katika Kundi la Taasisi za  Fedha.

NBC inashiriki maonesho ya mwaka huu ikiongeza udhamini wake kwa kudhamini kliniki ya biashara ambapo watu wanaenda na kupata mafunzo, maelekezo na majibu toka kwa watalaamu waliobobea kutoka taasisi zinazohusika kwenye maswala ya biashara.

Akizungumza viwanjani hapo, jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo akisema NBC inasaidia usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda na wamewapa nafasi wajasiriamali ambao wananufaika na huduma za kibenki za NBC kuja kuuza bidhaa zao  na wapo kwenye banda la wajasiriamali la NBC hapo Sabasaba. 

"Tuna tawi na ATM, hivyo tunatoa huduma zote za kibenki. Tunafubgua Fasta Akaunti ambapo mteja anakuja na kitambulisho kimoja tu na anafunguliwa akaunti na kuanza kuitimia papo hapo na kuondoka na kadi yake ya ATM," Alina.  

Mbali na hilo pia wale watakaoingia katika banda la NBC wataweza kuunganishwa  kwenye huduma za NBC Kiganjani yaani Mobile Banking na Online Banking ambapo wateja wanaweza kulipa bili, kuweka na kutuma pesa moja kwa moja kutoka na kwenda kwenye akaunti zao za NBC.




Aidha  meneja huyo aliongeza kuwa huduma kama za kubadili fedha za kigeni, bima kwa ajili ya elimu na huduma nyingine za kibenki zinapatikana mahali hapo hivyo akatoa wito kwa watu wote wanaotembelea maonesho hayo kufika katika banda la NBC.
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive