A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


Monday, November 6, 2017

MAENDELEO BENKI YAENDELEA KUUZA HISA HADI DESEMBA 4, 2017

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Ibrahim Mwangalaba (kulia), akizungumza na waandishi wa habari katika hafla yakuongeza muda wa uuzwaji wa hisa katika benki hiyo hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkuu wa Idara ya fedha wa benki hiyo Peter Tarimo.

Maendeleo Benki imeongeza muda wa mwezi mmoja wa kufanya manunuzi ya hisa kwenye Benki hiyo ili kuwafikia watanzania wengi zaidi. 
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Ibrahim Mwangalaba ambapo amesema zoezi la uuzaji wa hisa litakamilika tar 4 Desemba 2017.
Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa watanzania kuchangamkia fursa ya ununuzi wa hisa ambapo hisa Moja inauzwa shilingi 600 na kiwango cha chini cha kununua hisa ni hisa 100 thamani yake ni shilingi 60000 na zinapatikana kwenye Matawi yote ya Benki ya Maendeleo. Crdb bank, Uchumi Commercial Bank Moshi na mawakala wa hisa waliohidhinishwa na mamlaka wa mitaji na viwango Tanzania
Share:

0 comments:

Post a Comment


Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive