
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere (Katikati), akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ambayo benki hiyo ilikabidhi zawadi za fedha taslimu kwa washindi 18 wa kila wiki wa kampeni inayoendelea ya ‘Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa’ jijini Dar es Salaam jana. Katika hafla hiyo, Absa ilitambulisha udhamini wa safari ya mtu na mwenza wake kushuhudia Tamasha la maarufu duniani la ‘Absa Champagne Afrika’ nchini Afrika Kusini na pia kuchezesha droo ya mwezi ya kampeni hiyo ya miezi mitatu iliyozinduliwa Septemba 30 mwaka huu ambayo kiasi cha shs milioni 120 zimetengwa kama zawadi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano, Bw. Aron Luhanga na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bi. Judith Wililo.
BENKI ya Absa Tanzania imesema imefanya uwekezaji mkubwa katika huduma zake za kibenki kwa njia ya kidigitali, hususani zinazohusisha matumizi ya kadi ili kuhakikisha watanzania wengi zaidi wanafikiwa na huduma za kibenki huku ikiwezesha wateja wake kunufaika na huduma hizo zenye ubora na gharama nafuu imeelezwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika hafla ya kuwazawadia washindi wa kampeni yake inayoendelea ya ‘Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa’ iliyozinduliwa Septemba 30 mwaka huu yenye lengo la kuhamasisha wateja kufanya miamala ya kibenki kwa kutumia kadi na huduma za kidigitali, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa benki hiyo, Bi. Ndabu Swere alisema kampeni hiyo inaenda sambamba na lengo kuu la benki hiyo la ‘Kuiwezesha Afrika ya kesho, pamoja, hatua moja baada ya nyingine.
‘Sisi kama Absa ni jambo la kujivunia kwa sababu tumefanya uwekezaji mkubwa katika mifumo ya huduma zetu za kidigitali ili kuwafanya wateja wetu kufurahia kufanya miamala hii ambayo ni rahisi, uhakika na salama hivyo kuwafanya waweze kutimiza malengo yao huku wakiepukana na majanga ambayo yangeweza kuwapata kwa kutembea na fedha taslimu.'
“Kama benki tunafanya haya kama sehemu ya kuwashukuru wateja wetu kwa kufanya miamala mingi kwetu, nasi tunahakikisha wateja wetu wanapata huduma bora zenye viwango vya hali ya juu na wanafanikiwa katika kila jambo”, alisema Bi. Ndabu.
Katika hafla hiyo washindi 18 wa kila wiki wa kampeni hiyo walizawadiwa kila mmoja shs 500,000, huku washindi watatu wa mwezi wakijishindia pesa taslimu jumla ya shs milioni 18, ambapo Bi. Flora Awur alishinda shs milioni 3, Bi. Stella Kahwa, shs milioni 5 na Bw. Tony Mushi alijishindia shs milioni 10.
Sambamba na hilo Meneja wa Bidhaa za Kadi na Malipo wa benki hiyo, Bi. Erica Mwaipopo, alizungumzia promosheni ya matumizi ya Kadi ya malipo ‘Absa Infinite card’ inayopatikana kwa Shilingi za kitanzania ama Dola ya Kimarekani kama kadi ya kawaida (debit) ama mkopo (credit) iliyokuwa ikifanyika pamoja na Kampeni ya ‘Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa’.
“Kwa kutambua thamani ya wateja wetu wanaotumia kadi hii tulifanya promosheni ambayo mteja atakayefanya miamala mingi zaidi atajishindia safari yeye na mwenza wake kushuhudia tamasha maarufu duniani la ‘Absa Champagne Afrika’ nchini Afrika Kusini linalotarajiwa kufanyika mwezi huu na ninayo furaha kumtangaza Bw. Felician Hechei kama mshindi wa promosheni hii."
“Infinite Credit Card ni kadi ya kifahari inayolenga kuhudumia wateja wa hadhi ya juu, kwa huduma za kifedha zilizoboreshwa, ni kadi iliyobuniwa kukidhi mahitaji ya wateja wanaotafuta ubora, usalama na upatikanaji wa huduma duniani kote”, alisema Bi. Erica.
Miongoni mwa faida zake ni bima ya safari za kimataifa, kupata huduma za chakula, vinywaji na mapumziko katika viwanja vya ndege zaidi ya 1,200, bei ya punguzo katika manunuzi, bima ya kufuta tiketi za safari, na udhamini wa bidhaa za muda mrefu.
Naye Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga akizungumza mahali hapo alisema tukio hilo linadhihirisha kwa vitendo kauli mbiu ya benki hiyo isemayo ‘Stori yako ina Thamani’ hivyo kwa kuwazawadia washindi hao inaonesha ni jinsi gani Benki ya Absa Tanzania inavyothamini stori za mafanikio ya wateja wao.
Mmoja wa washindi wa wiki, Dk Heri Marwa alisema kutokana na kusafiri sana nje ya nchi, kadi ya Absa Infinite Credit Card imemsaidia sana kupata huduma zikiwemo manunuzi ndani ya ndege na katika viwanja vya mbalimbali vya ndege ambazo hapo awali alishindwa kuzipata wakati akitumia kadi za kawaida.
Kampeni ya miezi mitatu ya ‘Ujanja ni Kuswipe na Benki ya Absa’ ilizinduliwa ilizinduliwa Septemba 30 mwaka huu ikiwa na washindi sita wa shs 500,000 kila wiki; mshindi wa shs milioni 3, shs milioni 5 na shs milioni 10 kila mwezi na mshindi mmoja wa mwisho wa shs milioni 10 ambapo benki hiyo imetenga jumla ya shs milioni 120 kama zawadi kwa washindi watakaopatikana katika kampeni yote.
.jpg)
Mmoja wa washindi wa kila wiki wa Kampeni ya ‘Ujanja ni Kuswipe na kadi ya Absa’, Dk. Heri Marwa, akichezesha droo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Benki ya Absa ilikabidhi zawadi za fedha taslimu kwa washindi 18 wa kila wiki wa kampeni inayoendelea jijini Dar es Salaam jana. Katika hafla hiyo, Absa ilitambulisha udhamini wa safari ya mtu na mwenza wake kushuhudia tamasha maarufu duniani la ‘Absa Champagne Afrika’ nchini Afrika Kusini na pia kuchezesha droo ya mwezi ya kampeni hiyo ya miezi mitatu iliyozinduliwa Septembapo 30 mwaka huu ambayo kiasi cha shs milioni 120 zimetengwa kama Zawadi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano, Bw. Aron Luhanga, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Swere na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bi. Judith Wililo.

Meneja wa Bidhaa za Kadi na Malipo wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Erica Mwaipopo (kulia), akizungumza kuhusu kampeni ya matumizi ya Kadi ya malipo ya ‘Absa Infinite credit card’ ambayo mshindi na mwenza wake watapata udhamini kushuhudia Tamasha maarufu duniani la ‘Absa Champagne Afrika’ nchini Afrika Kusini linalotarajiwa kufanyika mwezi huu. Katika hafla hiyo pia, Absa ilikabidhi zawadi za fedha taslimu kwa washindi 18 wa kila wiki wa kampeni nyingine inayoendelea ya ‘Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa’ na pia kuchezesha droo ya mwezi ya kampeni hiyo ya miezi mitatu iliyozinduliwa Septemba 30 mwaka huu ambayo kiasi cha shs milioni 120 zimetengwa kama zawadi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano, Bw. Aron Luhanga na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Swere.

Mmoja wa washindi wa wiki, wa Kampeni ya ‘Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa’ Bw. Felician Hechei (kushoto), akipokea mfano wa hundi ya malipo ya shs 500,000 kutoka kwa Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere, huku Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga akiangalia, jijini Dar es Salaam jana. Katika hafla hiyo washindi 18 wa kila wiki wa kampeni hiyo walizawadiwa kila mmoja shs 500,000, huku washindi watatu wa mwezi wakijishindia pesa taslimu jumla ya shs milioni 18. Absa pia ilitambulisha udhamini wa safari ya mtu na mwenza wake kushuhudia Tamasha la maarufu duniani la ‘Absa Champagne Afrika’ nchini Afrika Kusini na kuchezesha droo ya mwezi ya kampeni hiyo ya miezi mitatu iliyozinduliwa Septemba 30 mwaka huu ambayo kiasi cha shs milioni 120 zimetengwa kama zawadi.
.jpg)
Mmoja wa washindi wa wiki, wa Kampeni ya ‘Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa’ Dk. Heri Marwa (kushoto), akipokea mfano wa hundi ya malipo ya shs 500,000 kutoka kwa Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere, huku Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga akiangalia, jijini Dar es Salaam jana. Katika hafla hiyo washindi 18 wa kila wiki wa kampeni hiyo walizawadiwa kila mmoja shs 500,000 huku washindi watatu wa mwezi wakijishindia pesa taslimu jumla ya shs milioni 18. Absa pia ilitambulisha udhamini wa safari ya mtu na mwenza wake kushuhudia Tamasha la maarufu duniani la ‘Absa Champagne Afrika’ nchini Afrika Kusini na kuchezesha droo ya mwezi ya kampeni hiyo ya miezi mitatu iliyozinduliwa Septemba 30 mwaka huu ambayo kiasi cha shs milioni 120 zimetengwa kama zawadi.

Mmoja wa washindi wa wiki, wa Kampeni ya ‘Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa’ Bw. Bhavik Lwada (kushoto), akipokea mfano wa hundi ya malipo ya shs 500,000 kutoka kwa Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere, huku Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga akiangalia, jijini Dar es Salaam jana. Katika hafla hiyo washindi 18 wa kila wiki wa kampeni hiyo walizawadiwa kila mmoja shs 500,000, huku washindi watatu wa mwezi wakijishindia pesa taslimu jumla ya shs milioni 18. Absa pia ilitambulisha udhamini wa safari ya mtu na mwenza wake kushuhudia Tamasha la maarufu duniani la ‘Absa Champagne Afrika’ nchini Afrika Kusini na kuchezesha droo ya mwezi ya kampeni hiyo ya miezi mitatu iliyozinduliwa Septemba 30 mwaka huu ambayo kiasi cha shs milioni 120 zimetengwa kama zawadi.

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Beda Biswalo (kulia), akizungumza kwa simu, jijini Dar es Salaam jana, na baadhi ya washindi wa mwezi wa Kampeni ya ‘Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa’ ambapo wateja wa benki hiyo, Bi. Flora Awur alishinda shs milioni 3, Bi. Stella Kahwa, shs milioni 5 na Bw. Tony Mushi alijishindia shs milioni 10. Katika hafla hiyo washindi 18 wa kila wiki wa kampeni hiyo walizawadiwa shs 500,000 kila mmoja. Absa pia ilitambulisha udhamini wa safari ya mtu na mwenza wake kushuhudia Tamasha la maarufu duniani la ‘Absa Champagne Afrika’ nchini Afrika Kusini. Kampeni hiyo ya miezi mitatu ilizinduliwa Septemba 30 mwaka huu huku kiasi cha shs milioni 120 zikitengwa kama zawadi. Katika picha kutoka kushoto ni; Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano, Bw. Aron Luhanga, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Swere na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bi. Judith Wililo.

Baadhi ya washindi wa wiki wa Kampeni ya ‘Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa’ wakipozi mbele ya wapigapicha pamoja na baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Benki ya Absa Tanzania, mara baada ya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Washindi 18 wa kila wiki walikabidhiwa zawadi za pesa taslimu kila mmoja kiasi cha shs 500,000, huku washindi watatu wa mwezi wakijishindia pesa taslimu jumla ya shs milioni 18.










