A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Friday, October 24, 2025

Benki ya Absa Tanzania na ASA Microfinance Yaadhimisha Miaka Minne ya Mafanikio katika Kuwawezesha Wanawake na Kubadilisha Jamii

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (Katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati akitangaza mafanikio ya ushirikiano wa kibiashara kati ya benki hiyo na taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance kwa kipindi cha miaka minne. Kupitia ushirikiano huo, Benki ya Absa imeikopesha ASA kiasi cha shs billioni 40 zilizoiwezesha taasisi hiyo kutoa mikopo kwa wanawake wajasiriamali zaidi ya 50,000 kutoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa, Bi. Abigail Lukuvi, Mkurugenzi wa wateja wa Makampuni wa Absa, Nellyana Mmanyi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa ASA Microfinance Tanzania, Bw. Muhammad Shah Newaj na Meneja Mahusiano ya Jamii na Utawala wa ASA, Bi. Veneranda Francis.

Benki ya Absa Tanzania, kwa ushirikiano na taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance, inajivunia kuadhimisha mwaka wa nne wa ushirikiano wa kipekee ambao umewezesha zaidi ya wanawake wajasiriamali 50,000 nchini Tanzania kupata mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 40 za Kitanzania.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2022, ushirikiano huu wa muda mrefu umeenda zaidi ya kutoa mikopo pekee, kila mwanamke mjasiriamali aliyewezeshwa si tu anabadilisha maisha yake binafsi, bali pia anagusa maisha ya familia yake, wafanyakazi, wasambazaji, na jamii pana inayomzunguka. Utafiti wa maendeleo unaonyesha kwamba kumwezesha mjasiriamali mmoja mwanamke nchini Tanzania kunaweza kuinua maisha ya watu 15 hadi 20 walioko karibu naye, hii inamaanisha kwamba ushirikiano kati ya Benki ya Absa na ASA Microfinance umegusa maisha ya karibu watanzania milioni moja, ukiimarisha familia na kuchochea ukuaji jumuishi wa kiuchumi.

Akizungumza kuhusu mafanikio haya jijini Dar es Salaam leo katika mkutano na waandishi wa habari, Obedi Laiser, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, alisema: “Taasisi nyingi huzingatia uwezeshaji wa wanawake kama mradi wa muda mfupi, kwa Absa, hili ni jukumu lenye kusukumwa na dhamira ya kweli. Kwa kuwawezesha zaidi ya wanawake 50,000 kupata mitaji na kukuza biashara zao, tunaona athari chanya zinazopanuka, zinazobadilisha familia, kuelimisha watoto, kuunda ajira, na kujenga ustahimilivu katika jamii. Hivi ndivyo tunavyoishi kauli mbiu yetu ya Kuiwezesha Afrika ya kesho, pamoja… hatua moja baada ya nyingine, kwa sababu kwetu Absa, Stori yako ina thamani.

Kwa upande wake, Muhammad Shah Newaj, Ofisa Mtendaji kuu wa ASA Microfinance Tanzania, aliongeza:

Ushirikiano wetu na Benki ya Absa Tanzania umeleta mageuzi makubwa. Kupitia msaada wa Absa, ASA imeweza kupanua huduma za mikopo midogo kwa maelfu ya wanawake wajasiriamali ambao wangeachwa nje ya mfumo rasmi wa kifedha. Pamoja, hatufadhili biashara pekee , tunafadhili heshima, matumaini, na fursa zinazoinua vizazi.

Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, ushirikiano huu umeunganisha utoaji wa mitaji na mafunzo ya elimu ya kifedha, kuhakikisha kwamba wanawake wajasiriamali hawapati mikopo tu bali pia maarifa ya kuiendesha kwa uendelevu. Mapema mwezi huu, wanawake 50 kutoka Dar es Salaam walishiriki katika programu ya elimu ya kifedha iliyojumuisha mada za upangaji bajetiakibauwekezaji, na utunzaji wa kumbukumbu, hatua muhimu katika kubadilisha mikopo kuwa uwezeshaji endelevu wa kiuchumi.

Mpango huu unaonyesha mkakati wa Uwajibikaji wa Kijamii wa Absa, unaolenga ujumuishaji wa kifedha, ujasiriamali, na maendeleo endelevu. Pia unaendana na ajenda ya kitaifa ya ujumuishaji wa kifedha nchini Tanzania kwa kupanua huduma za mikopo na elimu kwa makundi yasiyohudumiwa ipasavyo, hivyo kuleta mabadiliko ya kudumu ya ustahimilivu wa kiuchumi.

Kupitia ushirikiano huu endelevu, Benki ya Absa Tanzania na ASA Microfinance zinaendelea kuandika simulizi za mabadiliko , simulizi ambazo mwanamke mmoja aliyewezeshwa hubadilisha si maisha yake tu, bali pia maisha ya wengi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa tatu kushoto), akikabidhi tuzo kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, Bw. Muhammad Shah Newaj, kwa kutambua mchango wa taasisi hiyo, katika kuwawezesha wanawake wajasiriamali nchini, kwa kupitia masuluhisho mbalimbali ya kifedha. Ilikuwa ni katika hafla ambayo Absa ilitangaza mafanikio ya ushirikiano wa kibiashara kati ya benki na taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka minne. Kupitia ushirikiano huo, Benki ya Absa imeikopesha ASA kiasi cha shs billioni 40 zilizoiwezesha taasisi hiyo kutoa mikopo kwa wanawake wajasiriamali zaidi ya 50,000 kutoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa, Bi. Abigail Lukuvi, Mkurugenzi wa wateja wa Makampuni wa Absa, Bi. Nellyana Mmanyi, na Meneja Mahusiano ya Jamii na Utawala wa ASA Microfinance, Bi. Veneranda Francis.
Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigal Lukuvi (kushoto), akizungumza katika hafla ambayo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Obedi Laiser (wa tatu kushoto), akitangaza mafanikio ya ushirikiano wa kibiashara kati ya benki hiyo na taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance kwa kipindi cha miaka minne. Kupitia ushirikiano huo, Benki ya Absa imeikopesha ASA kiasi cha shs billioni 40 zilizoiwezesha taasisi hiyo kutoa mikopo kwa wanawake wajasiriamali zaidi ya 50,000 kutoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania. Wengine kutoka kushoto kwake ni, Mkurugenzi wa wateja wa Makampuni, Bi. Nellyana Mmanyi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa ASA Microfinance Tanzania, Bw. Muhammad Shah na Meneja Mahusiano ya Jamii na Utawala wa ASA, Bi. Veneranda Francis.
Share:

Saturday, October 18, 2025

BENKI YA ABSA TANZANIA YAZINDUA KLABU YA MATEMBEZI NA MBIO FUPI IKIHAMASISHA UMUHIMU WA MAZOEZI KWA AFYA YA MWILI NA AKILI

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Melvin Saprapasen (katikati) na Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha wa Absa Tanzania, Bi.Irene Rwegalulira (kushoto) wakizindua rasmi Klabu ya matembezi na mbio fupi ya benki hiyo itakayoshirikisha wafanyakazi wa kitengo hicho na wateja wao. Hafla hii ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Klabu hiyo itaendesha matembezi hayo mara mbili kwa mwezi ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano kati ya benki na wateja na pia kuhamasisha umuhimu wa mazoezi ya mwili kwa ustawi wa afya ya mwili na akili.
Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (kulia) akiwatangulia baadhi ya wafanyakazi na wateja wa kitengo cha biashar, wakati wa uzinduzi rasmi wa Klabu ya matembezi na mbio fupi ya benki hiyo itakayoshirikisha wafanyakazi wa kitengo hicho na wateja. Hafla hii ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Klabu hiyo itaendesha matembezi hayo mara mbili kwa mwezi ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano kati ya benki na wateja na pia kuhamasisha umuhimu wa mazoezi ya mwili kwa ustawi wa afya ya mwili na akili.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Absa Tanzania kitengo cha biashara pamoja na wateja wao, wakishiriki matembezi na mbio fupi jijini Dar es Salaam leo katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Klabu ya matembezi na mbio fupi ya benki hiyo itakayoshirikisha wafanyakazi wa kitengo hicho na wateja. Klabu hiyo itaendesha matembezi hayo mara mbili kwa mwezi ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano kati ya benki na wateja na pia kuhamasisha umuhimu wa mazoezi ya mwili kwa ustawi wa afya ya mwili na akili.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Absa Tanzania kitengo cha biashara pamoja na wateja, wakipiga picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi rasmi wa Klabu ya matembezi na mbio fupi ya benki hiyo itakayoshirikisha wafanyakazi wa kitengo hicho na wateja. Klabu hiyo itaendesha matembezi hayo mara mbili kwa mwezi ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano kati ya benki na wateja na pia kuhamasisha umuhimu wa mazoezi ya mwili kwa ustawi wa afya ya mwili na akili.
Share:

Tuesday, October 14, 2025

Absa Tanzania Celebrates Innovation and Inclusion at GirlCode Hackathon 2025

Absa Bank Tanzania Director of Technology, Mr. Emanuel Mwinuka (fourth from left), speaks with participants of the program titled “Absa GirlCode Hackathon 2025,” in which female university students were required to develop digital codes that provide solutions to support the banking sector and other industries. The event took place in Dar es Salaam over the weekend.

Absa Bank Tanzania has reaffirmed its commitment to empowering women in technology with the successful conclusion of the GirlCode Hackathon 2025, a high-energy, 36-hour innovation challenge that brought together young women coders, developers, and entrepreneurs from across the country.

The event, held in partnership with the Women in Tech Centre and Girl Code Africa, provided a platform for participants to develop digital solutions addressing real-world challenges in Fintech, Artificial Intelligence, and Cybersecurity.

In her closing address in Dar es Salaam over the weekend, the Director of Human Resources at Absa Bank Tanzania, Mr Patrick Foya commended the participants for their creativity, determination, and problem-solving spirit.

Your solutions stood out not only for their technical excellence but also for their potential to make a real difference, you’ve tackled complex challenges with boldness and brilliance, you’ve proven that innovation knows no gender, and that the future of technology is brighter because of you”, he said.

The HR Director also emphasized that the hackathon was more than a competition-it was a platform for learning, growth, and transformation where participants collaborated to design solutions ranging from ecosystem banking platforms to AI-powered optimization engines, demonstrating that young Tanzanian women are ready to lead the next wave of technological innovation.

When women are given the opportunity, they don’t just participate, they lead,” he added. “The next generation of tech leaders is already here.

Highlighting Absa’s role in nurturing female talent, the Director reiterated the bank’s commitment to creating inclusive pathways for women in technology in line with Absa’s purpose of Empowering Africa’s Tomorrow, Together, One Story at a Time, under the brand message “Your Story Matters.”.

Events like this are not just about coding, they’re about creating pipelines,” he said. “We are identifying talent, nurturing potential, and opening doors, Absa Bank Tanzania is committed to ensuring that young women who participated here today have access to opportunities such as internships, mentorships, and future employment.

Addressing those who did not win awards, the HR Director offered a message of encouragement; “Every great technologist has faced setbacks,” he reminded them. “What matters is how you respond, take what you’ve learned here and keep building, keep dreaming, and keep pushing boundaries.

One of the participants in the challenge, Mariam Saidi Mohammed, a computer software developer, expressed her gratitude to Absa Bank together with the GirlCode Hackathon for organizing the event, saying that it had helped her build confidence in finding solutions to various challenges through technology.

I would like to encourage all women with ideas not to be afraid, come forward, you can solve many problems through technology,” said Ms. Mariam.

Speaking at the event, the Bank’s Director of Technology, Mr. Emanuel Mwinuka, said that the Absa GirlCode Hackathon will help address the gender imbalance among computer systems professionals in the country, which has been a major challenge in many workplaces.

This challenge is not only in banks but also in other industries. That is why we at Absa decided to encourage young women from universities and workplaces to take advantage of opportunities in the world of technology and also provide solutions through technology."

Today’s event has been very successful, we have had three winners, since this event is also taking place in other countries, the first-place winner will have the opportunity to compete with winners from other nations through their solutions, and the best solution will receive another award,” said Mr. Mwinuka.

The Girl Code Hackathon 2025 was concluded with award presentations, networking sessions, and a shared commitment to sustaining the momentum of empowering women in the tech ecosystem.
The Director of Human Resources at Absa Bank Tanzania, Mr. Patrick Foya (second from right), presents a certificate to the first-place winners, the Tokiva Sisters team, during the “Absa GirlCode Hackathon 2025” program, where female university students were required to create digital codes offering solutions beneficial to the banking sector and other industries. The event was held in Dar es Salaam over the weekend. From right: Absa Bank’s Director of Operations, Mr. Oscar Mwamfwagasi, and Director of Technology, Mr. Emanuel Mwinuka.
The Director of Operations at Absa Bank Tanzania, Mr. Oscar Mwamfwagasi (right), presents a certificate to the third-place winners, the Tech Divas team, during the “Absa GirlCode Hackathon 2025” program, where female university students were required to design digital codes offering solutions to support the banking sector and other industries. The event was held in Dar es Salaam over the weekend.
Absa Bank Tanzania Citizenship and Events Manager, Abigail Lukuvi (centre), speaks with some of the participants of the “Absa GirlCode Hackathon 2025” program, where female university students were required to create digital codes that provide solutions to benefit the banking sector and the broader community. The event took place in Dar es Salaam over the weekend.
Share:

Monday, October 13, 2025

TANZANIA KUSHINDANA VIPENGELE 20 TUZO ZA UTALII DUNIANI

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru (katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini  Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upigaji kura wa tuzo  za kimataifa zinazotambua na kuthamini ubora, ubunifu na huduma bora katika sekta ya utalii na usafiri duniani. Wengine pichani kutoka (kushoto), ni Meneja Mawasiliano wa Bodi hiyo Paulina Mkama pamoja na Meneja Masoko wa Vivian Temi,


‎Meneja Mawasiliano wa Bodi yaUtaliiTanzania(TTB), hiyo Paulina Mkama (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini  Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upigaji kura wa tuzo  za kimataifa zinazotambua na kuthamini ubora, ubunifu na huduma bora katika sekta ya utalii na usafiri duniani. (Katikati), ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru pamoja na Meneja Masoko wa wa bodi hiyo  Vivian Temi

.com/img/a/

Na Mwandishi Wetu 

Tanzania imeingia kwenye kinyang’anyiro cha  Tuzo za Dunia za Utalii ( World Travel Award 2025) baada ya kuteuliwa kushiriki katika vipengele 20  vyenye  wagombea 24 vikiwemo taasisi na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii.


Akizungumza Oktoba 13, 2025 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upigaji kura, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru, amesema  hatua hiyo ni ya kihistoria kwani inaonyesha jinsi Tanzania inavyozidi kutambulika kimataifa.


“Kwa kawaida Tanzania imekuwa ikishinda katika tuzo za ngazi ya Afrika , lakini mwaka huu tumeingia katika mashindano ya dunia, mwaka  jana tulichaguliwa kama nchi bora kwa safari za utalii, jambo ambalo limeendelea kuitangaza nchi yetu zaidi,” amesema  Mafuru.


Ameeleza kuwa  World Travel Award( WTA) ni tuzo za kimataifa zinazotambua na kuthamini ubora, ubunifu na huduma bora katika sekta ya utalii na usafiri duniani.


“Tuzo hizi zilianzishwa mwaka 1993, na kwa sasa zinajulikana kama, Oscars za sekta za Utalii , kutokana na heshima na ushawishi wake katika kuonyesha viwango vya juu vya ubora duniani,” amefafanua  Mafuru.


Mafuru amesema  lengo la tuzo hizo ni kutambua na kuhamasisha ubora katika nyanja zote za utalii, ikiwemo mashirika ya ndege, hifadhi za taifa, hoteli, miji ya kitalii, kampuni za usafiri na taasisi za utalii za kitaifa kama TTB.


Amewahamasisha watanzania wote kujitokeza kupiga kura kupitia simu zao na mitandao ya kijamii katika kampeni iliyoanza  oktoba 6 hadi  oktoba 16,2025 , ili Tanzania iweze kushinda katika vipengele mbalimbali ikiwemo Nchi bora ya Utalii, Bodi Bora ya Utalii, Hifadhi Bora, Kivutio Bora na Uwanja bora wa ndege.


“Ushindi katika tuzo hizi utaongeza hadhi ya Tanzania katika sekta ya utalii duniani, kuongeza idadi ya watalii na kuimarisha juhudi za kulinda rasilimali na urithi wa taifa,” amesema .


Aidha, Mafuru amesisitiza  kuwa mafanikio yanayoonekana sasa ni matokeo ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa kinara katika kutangaza vivutio vya utalii kupitia ziara na filamu ya Royal Tour pamoja na hotuba zake

Share:

Sunday, October 5, 2025

BENKI YA ABSA TANZANIA KUENDELEA KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI WENGI ZAIDI NCHINI

Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (kulia), akizungumza na baadhi ya wanawake wajasiriamali, wanachama wa taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, katika semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa uwezeshaji wa benki hiyo ikihusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo haya ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo ya kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la Benki ya Absa la Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, Mr. Muhammed Shah Newaj (kulia), akizungumza kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya taasisi hiyo na Benki ya Absa Tanzania, wakati wa semina ya wanawake wajasiriamali wanachama wa taasisi hiyo kuhusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo haya ni sehemu ya mikakati ya Benki ya Absa katika kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la benki hiyo la 'Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine', kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Mkufunzi wa masuala ya kifedha, Bw. Edmund Munyagi (kulia), akifundisha kuhusu 'Usimamizi Binafsi wa Fedha' wakati wa semina iliyoandaliwa na Taasisi ya huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania na kuwezeshwa na Benki ya Absa Tanzania, ikishirikisha wanawake wajasiriamali wanachama wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana. Semina hiyo iliyohusu elimu ya kifedha na usimamizi wa biashara wenye tija ni sehemu ya mikakati ya Benki ya Absa nchini ya kuwawezesha wajasiriamali sambamba na Lengo la benki hiyo la Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Mmoja wa wanawake wajasiariamali mwanachama wa Taasisi ya huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, akichangia hoja wakati wa semina kuhusu elimu ya kifedha na usimamizi wa biashara wenye tija, iliyoandaliwa na taasisi hiyo ikiwezeshwa na Benki ya Absa Tanzania, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo haya ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo katika kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la benki hiyo la 'Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine', kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Baadhi ya wanawake wajasiriamali wanachama wa Taasisi ya huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, wakishagilia wakati Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi akizungumza nao wakati wa semina kuhusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, iliyoandaliwa na Taasisi ya ASA Microfinance Tanzania kwa uwezeshaji wa benki hiyo, jijini Dar es Salaam jana. Semina hiyo ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo katika kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la benki hiyo la 'Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine', kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (katikati), baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania na wanachama wao, wakionesha alama ya ushindi mara baada ya semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa uwezeshaji wa benki hiyo ikihusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo hayo ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo ya kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la Benki ya Absa la Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.

Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive