A blog that gives out financial institutions news on time with accurate informations.


  • CRDB Bank Share up 16PC in three weeks

    CRDB bank share price has made an abrupt U-turn after appreciating by 16 per cent in the last three weeks.

  • TIB slashes losses, bad loans up!

    TIB Development Bank has considerably reduced its net loss 17 times to 582m/- in this year quarter two (Q2) after cutting expenses.

  • MALINZI blesses TFF elections

    THE ousted Tanzania Football Federation (TFF) President Jamal Malinzi has expressed gratitude to the government, sponsors and football stakeholders in the country for their massive support.

  • Barrick, government talks next week

    BARRICK Gold will begin discussions with the government on the concentrate export ban and other issues next week

Friday, April 18, 2025

WATU 12,000 WAHOFIWA KUUGUA UGONJWA WA HIMOFILIA NCHINI

Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (katikati), akika utepe kuashiria uzinduzi wa kliniki ya himofilia, sambamba na maadhimisho ya Siku ya Himofilia Duniani katika hafla iliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, Visiwani Zanzibar, jana. Pamoja naye ni wawakilishi kutoka Chama cha Himofilia Tanzania (HST), Taasisi ya himofilia ya novo nordisk, Wizara za afya kutoka Tanzania na Zanzibar, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Chama cha Himofilia Duniani na wadau wengine.

Na mwandishi wetu, Zanzibar.

TAKWIMU zinaonyesha kati ya watu elfu sita hadi elfu 12, wanahofiwa kuugua ugonjwa wa himofilia nchini huku idadi ya watu waliogundulika kuwa na ugonjwa huo hadi sasa wakiwa ni 451 pekee.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Himofilia Duniani iliyofanyika pamoja na uzinduzi wa Kliniki ya Himofilia, katika Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, Visiwani humo jana.

Hafla hiyo iliandaliwa na Chama cha Himofilia Tanzania (HST), kwa uwezeshaji kutoka Taasisi ya himofilia ya novo nordisk na Chama cha Himofilia Duniani kwa ushirikiano kutoka Serikali ya Tanzania na ya Zanzibar, wizara za afya kutoka pande zote mbili, Hospitali ya Taifa Muhimbili na wadau wengine.

Mheshimiwa waziri alisema takwimu za kidunia zinaonesha mtu mmoja kati ya 10 anapatikana na ugonjwa huo, hii ikimanisha kuwa Tanzania yenye watu takribani milioni 61 inaweza kuwa na wagonjwa elfu 6 hadi elfu 12, huku ikielezwa 97% ya watu wenye ugonjwa huu duniani kote hawajagundulika, ambapo kwa upande wa Tanzania waliogundulika mpaka sasa ni 451 tu.

Kama tunavyofahamu himofilia ni ugonjwa wa damu kukosa uwezo wa kuganda unaosababishwa na ukosefu wa kiwango cha chembechembe za protini zinazotakiwa kugandisha damu hivyo kusababisha damu kuvuja kwa mda mrefu pindi mtu anavyopata jeraha hivyo kuhatarisha maisha yake."

Maisha ya watu wenye matatizo haya yanahitaji uangalizi mkubwa na tahadhari kubwa ili kuzuia uvujaji wa damu, ulemavu na vifo hivyo kuwepo na hitaji la kubaini aina ya himofilia na kupata matibabu ya kuchomwa sindano yenye chembechembe za protini zinazokosekana mwilini ili kusaidia kuzalisha damu”, alisema Waziri Mazrui.

Alisema Mwaka 2020 Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikishirikiana na Taasisi ya himofilia ya Novo Nordisk ilianzisha mradi wa kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma kwa watu wenye magonjwa ya damu lengo kuu ikiwa ni kuunga mkono serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya afya katika kupunguza madhara ya vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyo ambukiza ikiwemo himofilia na selimundu.

Pamoja na hayo alisema, lengo kubwa la mradi huu ni kuwezesha upatikanaji wa vipimo vya wagonjwa wa damu, seli mundu, na himofilia katika hospitali za rufaa nchini sambamba na kuanzisha kliniki za magonjwa hayo, kuwezesha mafunzo na upatikanaji wataalamu wa afya waliobobea kwenye hospitali hizo pamoja na upatikanaji wa miundo mbinu sahihi, vipimo na dawa ili wagonjwa wahudumiwe mahali popote nchini bila kulazimika kufika Muhimbili.

Katika maadhimisho haya leo nina furaha kubwa kuwaambia kuwa mradi huu katika kipindi cha uhai wake kuanzia kipindi cha kwanza hadi kipindi cha pili tayari umefanikisha kukamilisha ukarabati wa kliniki za himofilia katika hospitali 13 zikiwemo hospitali za Muhimbili, KCMC, mbeya na Bugando."

Tunawashukuru pia wafadhili wetu kwa msaada wa dawa zenye thamani ya shs milioni 500, kwa kweli mmetusaidia sana na vifaa nyenye gharama kubwa, chini ya uongozi wa maraisi wetu, Samia Suluhu Hassan na Hussein Ali Mwinyi, tunaendelea kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kila mtanzania anapata matibabu kwa usahihi na kwa wakati, hivyo juhudi zenu hizi zinatufanya twende sambamba na juhudi za viongozi wetu hawa”, aliongeza waziri huyo.

Akizungumzia zaidi kuhusu himofilia, Mwenyekiti wa Chama cha Himofilia Tanzania (HST), Dk. Stella Rwezaura alisema, asilimia 70 ya wagonjwa wa himofilia wanarithi na inabebwa katika kinasaba cha kike, kwani mwanamke ana ‘x’ mbili na mwanaume ana ‘xy’, hivyo endapo mwanamke ana ‘x’ yenye vinasaba vya himofilia, asilimia 50 ya watoto wake wa kiume watakuwa na tatizo hilo hivyo kufanya asilimia 99 ya wagonjwa wa himofilia kuwa wanaume.

Tunaposherehea Siku ya Himofilia Duniani, sambamba na Kauli Mbiu ya Mwaka 2025 isemayo, ‘Wanawake na Wasichana pia wanakumbwa na tatizo la kuvuja damu, licha ya himofilia kuwapata zaidi wanaume, tuwaite wanawake waje kupima, waweze kutambulika mapema hivyo kupata matibabu sahihi."

Lengo la mradi huu ni kuwatambua wagonjwa wengi zaidi na kupata huduma kwani wapo wengi wenye tatizo hili na hii ilitokana na changamoto ya uhaba wa vifaa, mashine na vitendanishi vya kutambua ugonjwa huu, hivyo kwa msaada wa wafadhili, vyama vya wagonjwa pamoja na serikali yetu sikivu ya Tanzania, ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, wizara yake ya afya na wadau wengine, huduma hizi sasa zinafika karibu kwa wananchi kwa usahihi zaidi”, aliongeza Dk. Stella.

Naye mmoja wa wagonjwa wa Himofilia ambaye pia anauguza watoto wawili wenye ugonjwa huo, Regina Shirima alisema anakabiliwa na changamoto kubwa ya hali duni ya kiuchumi baada ya kutumia muda wake mwingi katika kuhudumia watoto hivyo kutokuwa na muda kabisa wa kujishughulisha na kazi za kujitafutia kipato.

changamoto nyingine ni kwa watoto wenyewe hawapati muda wa kusoma, kucheza na wenzao ama kuwa na furaha kwani muda mwingi wanakuwa wagonjwa, lakini ni ukweli kuwa wanawake ndio wanabeba vinasaba vya himofilia, lawama nyingi zinakuja kwetu kwa kuzaa watoto wenye changamoto hii, hivyo unajikuta familia imekuacha”. Akiongeza kuwa kuna wakati kulikuwa na changamoo ya upatikanaji wa dawa ukizingatia kuwa mgonjwa wa himofilia akikosa dawa tu anaweza uhai wake unakuwa hatarini.

Natoa wito kwa jamii kuwa gonjwa hili la himofilia lipo na mama sio anayesababisha mtoto kuzaliwa na ugonjwa huu, kwani huwezi kupata mtoto bila ya baba”, aliongeza Bi. Regina kwa mshangao.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Himofilia Tanzania (HST), Dk. Lawrence Museru alisema HST imekuwa sauti ya wenye ugonjwa wa himofilia katika kuangalia changamoto wanazopitia katika kutafuta tiba, moja ya changaoto ni utambuzi wa ugonjwa huu katika jamii.

Wagojwa wamekuja kutambulika baada ya kupoteza maisha ama kupata ulemavu wa kudumu kwasababu ugonjwa huo haukutambulika hivyo tunaokoa sauti yao kuona jamii na watoa huduma za afya wanatambua ugonjwa huo na wagonjwa wanapata tiba sahihi."

Tiba sahihi ni ghali sana na serikali haiwezi peke yake, hivyo lazima uwepo ushirikiano kutoka kwa sisi chama ambacho kina wataalamu na wadau wengine ili kuusemea ugonjwa huu, na tunaimani uwepo wako mheshimiwa waziri unafanya ugonjwa huu usemeke katika vyombo vya maaumuzi”, alisema Prof. Museru.

Akimkaribisha Mheshimiwa Waziri, Mkurugenzi wa Tiba na Elimu ya Afya Zanzibar, Dk. Marijani Msafiri alisema katika kipindi cha miaka minne, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wa Dr. Hussein Ali Mwinyi imefanya mapinduzi makubwa katika kuboresha huduma za afya, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa hospitali 10 za wilaya na hospitali moja kubwa ya kisasa ya mkoa ya Lumumba.

Ndani ya hospitali hizi sasa tumeimarisha miundombinu na huduma, serikali yetu ya awamu na nane pia imeamua kufanya kazi na sekta binafsi ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa wote ikiwa ni pamoja na wagonjwa wa himofilia, zikiwemo huduma za maabara, utoaji wa dawa na uendeshaji wa hospitali”, alisema Dk. Msafiri.
Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (katikati), akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Himofilia Tanzania (HST), Dk. Stella Rwezaura, mara baada ya maadhimisho ya Siku ya Himofilia Duniani iliyofanyika pamoja na uzinduzi wa Kliniki ya Himofilia, katika Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, Visiwani Zanzibar jana. Mstari wa chini ni baadhi ya watoto wanaougua ugonjwa wa himofilia.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Himofilia Tanzania (HST), Prof. Lawrence Museru (katikati), akiongoza maandamano kuadhimisha Siku ya Himofilia Duniani, Visiwani Zanzibar jana. Maadhimisho hayo yalifanyika pamoja na uzinduzi wa kliniki ya Himofilia katika Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, visiwani humo.
Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (kushoto), akipokea cheti cha shukurani, kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Himofilia Tanzania (HST), Dk. Stella Rwezaura, mara baada ya maadhimisho ya Siku ya Himofilia Duniani, pamoja na uzinduzi wa Kliniki ya Himofilia, katika hafla iliyofanyika kwenye Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, Visiwani Zanzibar, jana.
Mkazi wa Zanzibar, Baba mwenye watoto wawili wanaougua himofilia, Suleiman Ali Seif, akishiriki matembezi akiwa na watoto wake wenye ugonjwa huo, Murshin Ali (kulia), na Sahir Ali, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Himofilia Duniani, mjini Zanzibar jana. Maadhimisho hayo yaliyofanyika pamoja na uzinduzi wa Kliniki ya Himofilia, yaliandaliwa na Chama cha Himofilia Tanzania (HST), kwa uwezeshaji kutoka Taasisi ya himofilia ya novo nordisk na Chama cha Himofilia Duniani. Himofilia ni ugonjwa wa damu kukosa uwezo wa kuganda unaosababishwa na ukosefu wa kiwango cha chembechembe za protini zinazotakiwa kugandisha damu hivyo kusababisha damu kuvuja kwa mda mrefu pindi mtu anavyopata jeraha hivyo kuhatarisha maisha yake.
Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (kushoto), akisalimiana na Mwenykiti wa Bodi ya Chama cha Himofilia Tanzania, Prof. Lawrence Museru, wakati akipokea maandamano, yaliyokuwa sehemu ya shamrashamra za maadhinisho ya Siku ya Homifilia Duniani, sambamba na uzinduzi wa Kliniki ya Himofilia, katika Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, mjini Zanzibar, jana.
Mmoja wa wadau wa himofilia, akipokea cheti cha shukurani, mara baada ya kukamilika kwa hafla ya maadhimisho Siku ya Homifilia Duniani, sambamba na uzinduzi wa Kliniki ya Himofilia, katika Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, mjini Zanzibar, jana.
Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (katikati), akiwa na wawakilishi kutoka Chama cha Himofilia Tanzania (HST), Taasisi ya himofilia ya novo nordisk, Wizara za afya kutoka Tanzania na Zanzibar, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Chama cha Himofilia Duniani na wadau wengine katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Himofilia Duniani iliyofanyika pamoja na uzinduzi wa Kliniki ya Himofilia, katika Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, Visiwani Zanzibar jana.
Share:

Sunday, April 13, 2025

AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YATOA ELIMU YA KIFEDHA KWA WATEJA WAKE KARIAKOO

Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Silvest Arumasi (kushoto), akiwa Kwenye kikao na wateja na wajasiriamali (SMEs) kutoka Kariakoo, katikati ya kitovu cha biashara Afrika Mashariki, ili kujadili changamoto zao na kushirikiana mawazo kuhusu masuluhisho yanayoweza kukuza biashara zao hafla hiyo imefanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya hiyo Bi Wesi Olivia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Silvest Arumasi (katikati), akiwabkatika picha ya pamoja wateja na wajasiriamali (SMEs) kutoka Kariakoo, katikati ya kitovu cha biashara Afrika Mashariki, ili kujadili changamoto zao na kushirikiana mawazo kuhusu masuluhisho yanayoweza kukuza biashara zao


Mnamo tarehe 12/04/2025 Benki ya Akiba  ilifanya kikao na wateja wake na wajasiriamali (SMEs) kutoka Kariakoo, katikati ya kitovu cha biashara Afrika Mashariki, ili kujadili changamoto zao na kushirikiana mawazo kuhusu masuluhisho yanayoweza kukuza biashara zao. Hii ni sehemu ya juhudi zetu za kuwa karibu na wateja na kutekeleza dhamira yetu ya kuwawezesha wajasiriamali na kuimarisha elimu ya fedha, alisema Bi. Dora Saria Mkuu wa Kitengo cha masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bwana Silvest Arumasi, alielezea furaha yake kwa kushirikiana moja kwa moja na wateja, akisema, "katika Benki yetu , tunaamini kwamba mafanikio ya wateja wetu ni mafanikio yetu. Tunajivunia sana kushirikiana na wajasiriamali wote nchini  katika  kusaidia  kukuza biashara zao kupitia elimu ya fedha, mikopo, na huduma za kidijitali."


Akizungumza katika tukio hilo, Bi. Wezi Olivia Mwazani, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya Akiba, alisisitiza umuhimu wa kujenga uhusiano ya kudumu na wateja kwa kutoa huduma za kifedha zinazolingana na mahitaji yao.


 "Tunafurahi kuwa na fursa ya kuzungumza na wateja wetu moja kwa moja, kuelewa changamoto zao na kutoa masuluhisho ya kifedha ambayo yatasaidia katika mafanikio yao ya muda mrefu."


Wateja waliokuwepo waliotoa  shukrani zao kwa juhudi hizo,  wakielezea jinsi fursa ya kushirikiana na Benki hiyo  ilivyo muhimu kwa ukuaji wa biashara zao. Wengi walielezea kuwa mpango huu wa elimu ya fedha na huduma za kidijitali utawawezesha kufanya biashara zao kwa ufanisi zaidi.


Bw. Silvest Arumasi, Mkurugenzi Mtendaji wa ACB aliwashukuru wateja kwa uaminifu wao na ushirikiano wa muda mrefu, akiongeza, "Tunapenda kuwashukuru wateja wetu wa Kariakoo na maeneo mengine kwa ushirikiano wao ikiwa ni pamoja na kutuchagua na kutuamini. Pamoja, tutaendelea kuleta mabadiliko katika sekta ya SMEs na kusaidia katika maendeleo endelevu ya kiuchumi."


Benki ya Akiba  inaendelea  kutoa huduma za kibenki zinazolenga mahitaji ya wateja na kusaidia ukuaji wa biashara za watu binafsi, SMEs pamoja na makampuni makubwa na taasisi mbalimbali  kupitia huduma zinazokidhi mahitaji yao  na matumizi ya teknolojia ya kidijitali.
Share:

Friday, April 11, 2025

WADAU ZAIDI YA 500 KUSHIRIKI WIKI YA AZAKI 2025 MWEZI JULAI ARUSHA

Kuelekea katika wiki hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge amewahimiza wananchi kupaza sauti zao kwa kutoa maoni yatakayopelekea kupata dira bora kwa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Rutenge amesema hayo Dar es Saalam wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) 2025, ambapo zaidi ya washiriki 500 wanatarajiwa kushiriki na kutoa wito kwa watanzania kushiriki kwa wingi.

Wiki ya Azaki imefanyika kwa miaka sita mfululizo na sasa ni mwaka wa Saba lengo likiwa kuwaleta pamoja wadau wa sekta ya Azaki kufanya mijadala mbalimbali ya maendeleo kwa mustakabali wa nchi yetu Tanzania,"

Kila mwaka tuna utaratibu wa kuangazia mambo mbalimbali na kuweka sawa Mahudhui ya wiki ya Azaki na mwaka huu tutaangazia mchakato mzima wa dira ya Taifa."

Watanzania wengi wanatambua kuwa mwaka huu tumeshiriki kwa kina kwenye mchakato wa kutengeneza dira yetu ya maendeleo ya mwaka 2050 ambayo ni fursa inayokujaga mara chache mara moja kwa miongo miwili au miwili na nusu."
Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi, CBM International ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati za Asasi za Kiraia Nesia Mahenge amesema wiki hiyo inalenga kutatua changamoto ambazo zipo katika azaki za kiraia na kuona ni namna gani zinatatuliwa.

Azaki kutoka nchi za Tanzania bara, Zanzibar wanaangalia ni namna gani kila mwaka ndani ya wiki moja tunakutana na kutathimini kazi za mashirika yasio ya kiserikali kuangalia maendeleo ambayo tumeyaleta katika nchi yetu."

Kwa mwaka huu itakuwa tofauti tulizoea kufanya mwezi wa kumi mkoani Dodoma lakini kwa sasa ni Arusha kutokana na mapendekezo ya jamii hatutafanya mkoa mmoja."

Tujumuike kuangalia jinsi ya kupanga mikakati na kutenga fedha za kuleta maendeleo kwenye jamii na pia mataifa mengine kuangalia maendeleo yetu na kuyapeleka kwenye nchi zao."
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkaazi wa Trademark Africa Elibariki Shami, amesema kuwa FCS imeonesha jitihada kubwa katika kuimarisha utetezi wa AZAKi kwa kuhakikisha haki za walaji zinapatikana na kuongeza uelewa katika ulinzi wa watumiaji.

FCS inalenga kuhakikisha kuwa ifikapo 2026, AZAKi zinashiriki kikamilifu katika mipango ya ulinzi wa watumiaji na kuwepo kwa ongezeko la uelewa wa jamii juu ya ulinzi wa walaji” amesema.

Ameongeza kuwa kushiriki wa moja kwa moja wa FCS katika kushughulikia masuala ya kijamii, sambamba na utaalamu wa utetezi na kujitolea, unawakilisha maslahi ya raia na walaji, nakwamba AZAKi huziba pengo kati ya sera na hatua za msingi za kuhakikisha ulinzi thabiti wa walaji unakuwepo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Association NGoS Adamsoni Nsimba amesema wamefurahi kujumuika katika uzinduzi wa wiki za Azaki itakayomsaidia na kumlinda mlaji na kujenga uwezo kwa jamii na kumpa mlaji haki tofauti na mfanya biashara kuchagiza sera na sheria.
Share:

Propellerads

Search Brazuka Kibenki

FOLLOW US ON FACEBOOK

  • ()
  • ()
Show more

Labels

Blog Archive